Ilipoishia “Benjamin akamsogelea Malkia Zandawe na kumtuliza kwa kumshika bega, hata yule rubaniย wa Helkopta ya Kijeshi aliona wazi kua Binti huyo alikua akizungumza kwa hisia kali iliyomuumiza. Malkia Zandawe akafuta chozi lake kisha akamwambia ndege wake mweupeย aongoze njia, akamtaka na Benjamin aingie ndani ya Helkopta hiyo pamoja na sokwe wakeย ampendaye.ย
Kitendo cha ndege kuruka kiliwafanya na Popo kuzama Msituni zaidi kwa kukimbia kwaย spidi kali kisha Benjamin, rubani, Malkia Zandawe na Sokwe wakaingia ndani ya Helkoptaย hiyo tayari kuelekea ndani ya Black Site kuikomboa familia ya Benjamin Kingai. Dakikaย tano baadaye Helkopta ikawa angani ikimfuata ndege mkubwa mpelelezi aitwaye Gola. Endeleaย
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
โBado nipo ndani ya Msitu, naandamwa kila kona Mkuu. Nipo na Msichana lakini hali niย ngumuโ ilikua ni sauti ya Muuwaji akizungumza na Mtoa kazi ambaye ni Waziri Mkuu Hajiย Babi kwa njia ya simu. Alikua ameketi juu ya jiwe moja, Elizabeth Kimaro akiwa hajitambuiย yupo chini, pembeni palikua na Mkondo mdogo wa Maji uliokua umekatiza msituni, maweย kadhaa yalikua yamelizunguka eneo hilo.ย
โSawa Mkuuโ alisema tena baada ya kusikiliza kwa Makini simu hiyo, Waziri Mkuuย akaagiza kikosi kazi cha kuhakikisha Muuwaji anatoka salama ndani ya Msiitu akiwa naย Msichana Elizabeth.ย
Hekaheka ilikua nzito ndani ya Ikulu, Ugeni mzito wa Mwanasheria Mkuu wa Serikaliย uliingia Ikulu kwa simu ya haraka kutoka kwa Waziri Mkuu, Haji Babi alihitaji uhakika zaidiย wa Nani atakua Mrithi wa Urais endapo Rais atafia Madarakani.ย
โKwanini umeniita hapa?โ akauliza Mwanasheria Mkuu, walikua kwenye chumba maalumย cha wageni hapo Ikulu, Mwanasheria alianza kuhisia jambo fulani baya limemfika Rais, Waziri Mkuu akakuna kidevu chake kisha akamwambia Mwanasheria Mkuu.ย
โNataka ushirika baina yetu, ushirika wenye tija hapo baadayeโ akasema Waziri Mkuu, tayariย alishaanza kukusanya viongozi wa Serikali ili kusiwe na Mgongano endapo atatangaza kifoย cha Rais, japo palikua na Makamu wa Rais lakini hakua na nguvu mbele ya Waziri Mkuuย ambaye ni Mtendaji Mkuu wa shughuli zote za Serikali.ย
โUshirika?โย
โNdiyoโ
โKwanini umeniita Ikulu, Rais limemfika jambo?โ akauliza Mwanasheria mkuu huku akikazaย macho yake madogo yenye makunyanzi kutokana na Uzee wake, Waziri Mkuu akanyanyukaย na kusogea alipoketi Mwanasheria Mkuu.ย
โHatuna Rais kwasasa, sheria inasemaje?โ akahoji Waziri Mkuu wakati huo Mwanasheriaย Mkuu wa Serikali akisimama kwa mshitukoย
โUnamaanisha nini?โย
Waziri Mkuu akamnyuka Mwanasheria Mkuu kisha akamuuliza kwa Jazba nzito โRais asipokuwepo nini kinafuata?โย
โUnataka kulihasi Taifa lako?โ akahoji Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku mawani yakeย ikianguka chini kutokana na purukushani, pale pale Waziri Mkuu akamnyooshea Bastolaย Mwanasheria Mkuuย
โUnatakiwa kuamua jambo moja, kushiriki au kutoshiriki. Sihitaji maswali mengi kutokaย kwako Mzeeโ alisema Waziri Mkuu, jasho likiwa linamtoka. Hadi kufikia hapo Mwanashriaย Mkuu akaingiwa na woga akajikuta akiketi. Kicheko cha juu kikamtoka Waziri Mkuu hukuย akiwa anahema, Halafu akarudi kuketi kitini.ย
โUmemuuwa Rais?โ akauliza Mwanasheria kwa sauti ya unyonge ili athibitishe.ย
โSiyo Rais peke yake, hata wewe unaweza ukamfwata endapo utakataa kutia saini nyaraka zaย uthibitisho mbele ya kadamnasiโ alisema Waziri Mkuu akijua fika Kua Mtu wa Mwishoย kuthibitisha madaraka hayo atakua ni Mwanasheria Mkuu tena atatia saini mbele yaย Kadamnasi mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha Rais Lucas mbelwa.ย
โHata hivyo nina kazi ya kuifanya kabla ya kutangaza Kifo cha Raisโ alisema Waziri Mkuuย Haji Babi. Hadi kufikia hapo taarifa ya kifo cha Rais Mbelwa ilianza kutoka kwa Watuย wakubwa wa Serikali.ย
Mate ya hofu yalipita kwa Mwanasheria wa Serikali, alitupa macho yake mezani kishaย akayarudisha kwa Waziri Mkuu Haji Babi.ย
โUtanihakikishia Usalama wangu?โ akauliza, Waziri Mkuu akatabasamu kwasababu alijuaย amefanikiwa kumtetemesha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.ย
**ย
Ndege Gola aliwaongoza kufika Black Site akiwa Mstari wa mbele, hakuna aliyeitiliaย Mashaka Helkopta hiyo sababu ilikua ya jeshi pia palikua na Helkopta nyingine juu zikirandaย randa juu ya Msitu kumsaka Muuwaji. Yule rubani alikua akiifahamu vyema kambi hiyo,ย moja kwa moja alienda kutua ndani ya Jengo la Black Site.ย
Wakati Helkopta inashuka kwa ajili ya kutua ikazingirwa na Walinzi wa Black Site, wakatiย huo Malkia Zandawe alikua amesha chomoa Bunduki kutoka kwenye begi. Moja akampaย Benjamin, machoni pa Benjamin tukio kama hili lilikua likijirudia, alishawahi kupewaย Bunduki na Elizabeth Mlacha
โUlinzi wako huo Benโ akasema Malkia Zandawe nyingine akampa Sokwe wake Mkubwa,ย ambaye alitoa tabasamu baada ya kupewa Bunduki hiyo. Akaunguruma kidogo kisha Rubaniย akawaambiaย
โSiwezi kutua, tunahatarisha Maishaโ alipayuka akionekana mwenye Hofu lakini Malkiaย Zandawe akamwambia huku akiwa amemnyooshea Bundukiย
โShusha Helkopta chini kama bado unahitaji kuishiโ alisema kwa Msistizo mkubwa, Rubaniย akatii maagizo ya Zandawe, akaishusha Helkopta Chiniย
โUtakua ngao yanguโ alisema Malkia Zandawe, kisha akashuka akiwa amemteka yuleย Rubani, wale Walinzi wapatao zaidi ya ishirini wakiwa ndani ya sare nyeusi kama mafundiย Bomba walishapata taarifa ya moja kwa moja kua Helkopta hiyo ilibeba Watu wasio sahihiย kuingia ndani ya Black Siteย
Panga Boi ilikua ikimaliza Mzunguko wa mwisho wakati huo Malkia Zandawe alikuaย amesimama mbele ya Walinzi akiwaambiaย
โOle wake Mtu afanye Ujanja, mtampoteza huyu Rubaniโ alisema Malkia Zandawe kwaย kujiamini sana huku akiikaza Bunduki kuelekea kwa Rubani aliyemkamata vizuri, sare zaย Rubani zilionesha wazi kua alikua ni mmoja wa Marubaji wa Helkopta za Black Site.ย
Hatua za taratibu zilizojaa umakini zilisikika kutoka kwa Zandawe, akawavuka walinziย waliokua mbele yake wote wakampisha, sasa macho yake akayaelekeza lango kuu laย kuingilia Black Site, akalisogelea akiwa na mateka wake. Wakati walinzi wakiwa bize sanaย kumtazama Zandawe, nyuma yao Benjamin na Sokwe walitoka kwenye Helkopta naย kutafuta uchochoro wa kuingilia, Zandawe akalifikia lango kisha akalifungua.ย
Akawatisha kidogo wale walinzi kisha haraka akaingia ndani na mateka wake kisha akufungaย mlango Mkuu wa kuingilia Black Site, walipofika ndani Zandawe akamwacha yule Rubaniย kisha akamuulizaย
โNi wapi wanapohifadhiwa mateka?โ akauliza kwa haraka huku kupitia kioo akiwaonaย walinzi walivyokua wakifanya jitihada za kutaka kuingia ndaniย
โNi hukuโ Rubani akasema kisha akaongoza mbele kuelekea sehemu wanapohifadhiwaย mateka wa Black Site, aliamini huko angeipata familia ya Benjamin Kingai, wakakimbiaย haraka wakati huo walinzi wakizidi kuuvunja mlango waingie ndani kumdhibiti Malkiaย Zandawe.ย
Jengo hilo lilikua la siri sana kiasi kwamba palikua na ofisi nyingine zilizo chini ya jengo,ย wakashuka hadi huko na kuanza kukagua chumba kimoja baada ya kingine, vyumba vingiย vilikua vitupu, palikua na vyumba vingi sana huko chini, nyingi zilikua ofisi zenye kompyutaย nyingi.ย
Wakazidi kudhurura bila mafanikio, vyumba vyote vilikua tayari vimepekuliwa na hapakuaย na Mtu yeyote yule, wakaziona ngazi zilizokua zikieleke juu, haraka wakazitumia wakiaminiย zitawafikisha mahali walipo mateka wa eneo hilo.
โUna hakika? Kumbuka sikufahamu hivyo siyo rahisi nikakuaminiโ alisema Zandawe baadaย ya kuona palikua na mzunguko mrefu bila dalili yoyote ile ya kuipata familia ya Benjaminย Kingai.ย ย
โNami nataka kua salama dhidi yako ndiyo maana nahakikisha nakusaidia ili uniache, siweziย kukuingiza chakaโ akasema yule Rubani kisha akaongoza mbele zaidi, lakini huko alikokuaย akimpeleka Zandawe hapakuonekana kua na dalili ya kuwepo wa mateka, hisia mbayaย ikaanza kumcheza Malkia Zandaweย
โSikia siwezi kwenda zaidi ya hapa, hakuna dalili ya kuwepo kwa Watu ninaowataka hukuย unakozidi kunipelekaโ alisema Zandawe kisha alisimama, Bunduki akaielekeza kwa yuleย Rubani.ย
โChumba namba 303, nina hakika na kumbukumbu zangu niliiyona familia moja huko sikuย chache zilizopita, korido ya Pili kutoka hapaโ alisema yule Rubani akiwa anajianda kuzidiย kusonga mbele.ย
โHebu subiri, mwanzo ulisema hujui walipo. Sasa hivi unasema wapo Chumba namba 303.ย Una mpango gani?โ akauliza Malkia Zandawe akiwa ameyasimamisha masikio yake,ย akihesabu pumzi zake kwa uzuri kabisa.ย
โAaah unajua mwanzo niliamini hutoweza kuwapita wale Walinzi hivyo sikutaka kupotezaย muda kukueleza mengi, ila kwasasa naona tumaini langu ni kusema ukweli wa yaleย uyatakayoโ akajitetea huku akihema, Zandawe akatafakari kauli ya Rubani yule kishaย akamwambiaย
โUkifanya mchezo wowote ule nakumaliza huku huku, sishindwiโ alisema kwa Msisitizoย Mkubwa sana Malkia Zandawe, sura yake ikakazia uhalisia wa yale ayasemayo. Yule Rubaniย akajibaraguza kidogo kisha akasonga mbele kwa spidi huku akimwambia Zandawe kuaย anaijua njia ya siri ya kutoka ndani ya jengo hilo kwa usalama kabisa.ย
Wakazidi kusonga huku nyuma yao wale Walinzi wakisaidiana na Makomandooย walifanikiwa kuvunja Mlango, sasa wakawaandama Rubani na Zandawe popote walipo tenaย kwa Msako mkali sana ulioanzia kwenye chumba cha Mawasiliano ya Black Site.ย
Kupitia Kamera zilizotegwa kwenye korido zote walifanikiwa kuona mahali walipokuaย wakielekea, ikawa rahisi kwao kuwafwatilia.ย
**ย
Nje ya Jengo la Black Site Palikua na heka heka nzito ya Kumsaka Muuwaji aliyemtoroshaย Elizabeth ndani ya jengo la Black Site, Makomandoo walizidi kusonga Msituni wakisaidiwaย na Mbwa ili kuhakikisha Mlengwa ananaswa haraka sana. Muuwaji naye alizidi kukimbiaย akiwa amembeba Elizabeth aliyepoteza fahamu, nguvu zilianza kumwisha hasa baada yaย kudondoka wakati ule kutoka juu hadi chini ya korongo na kuumiza Bega lake.ย
Akafika mahali akahitaji kupumzika, vinasa mawasiliano viliacha kufanya kazi na hiiย ilimwonesha kua mahali alipokua akielekea ni ndani zaidi, kifupi alikua akizidi kupoteaย Msituni bila kujua, hata Msaada aliouomba isingelikua rahisi kumfikia tena.
Akamweka Elizabeth kando ya fukutu moja lililoshiba nyasi za kutosha, jua lilikua likipataย shida sana kuangaza sehemu kubwa ya Msitu huo kutokana na miti ilivyokua imeuzongaย Msitu mzima na kufanya sehemu kubwa kua Giza. Dakika kadhaa za kua hapo alianzaย kusikia sauti za Mbwa wakibweka, haraka akamchukua Elizabeth akasonga naye mbele kwaย kasi ya Kipanga, lakini kadili alivyozidi kwenda alianza kusikia sauti kubwa ya Maji iliyoashilia kua alikua amefika mwisho wa safari yake.ย
NDANI YA BLACK SITEย
Zandawe na Rubani walifika mbele ya chumba namba 303, kidogo ikamfanya Zandaweย aingiwe na imani ya kumwamini Mtu huyo kua alikua akiijua vizuri Black Site. Macho yaoย yalitazamaย
โUna hakika?โ akahoji Zandaweย
โNina hakika niliwaona huku mara ya mwisho, Mimi ndiye niliyewaleta hapa kwa Helkoptaโย akazidi kusema Rubani, Zandawe akausukuma mlango kwa tahadhari kubwa sana akijua fikaย uzembe wowote utagharinu Maisha yao, akajikuta akiwa mbele ya Rubani asiye mfahamuย vizuri, ghafla akapigwa teke na kuangukia ndani ya chumba kisha Rubani akaufunga uleย mlango kwa nje, kisha akaanza safari ya Mbio kurudi nyuma walipotoka.ย
Zandawe akajaribu kuusukuma mlango lakini aligundua ulikua umefungwa vyema, akiwaย anafikiria kuuvunja kwa kutumia Bunduki alipata wazo la kuangalia ndani ya chumba hichoย mlikua na Nini, akiwa ametuliza hisia zake vyema alianza kusikia sauti ikitoka nyuma yaย pipa moja.ย
Chumba hicho kilikua kama stoo hivi, sauti aliyoisikia ilimueleza vyema kua ilikua ni sauitiย ya Mtu aliyezuiwa kusema chochote mdomoni mwake, wazo la kutaka kuvunja Mlangoย lilimwisha Zandawe, akainyoosha Bunduki kuelekea huko, kadili alivyosogea ndivyoย alivyoanza kuona kitu kikifurukuta. Akanyoosha vyema Bunduki, akamkuta Mwanamkeย mmoja nyuma ya Pipa akiwa amefungwa mikono, miguu pia alikua na plasta ngumuย mdomoni mwakeย
Zandawe akaiegemeza Bunduki haraka ukutani ili amsaidie, kitu cha kwanza kufanya alimtoaย plasta ngumu mdomoni ili amsikilize.ย
โWewe ni Mke wa Benjamin?โ akauliza Zandawe wakati huo Mwanamke yule akitaabikiaย kuhema vizuri, alipotulia akaitikia kwa kichwaย
โMtoto yupo wapi nimekuja kuwasaidiaโ alisema Malkia Zandaweย
โSijui kuhusu Mtoto, mimi ni mpenzi tu wa Benjamin. Yeye yupo wapi kwani?โ alihoji,ย Malkia Zandawe akagundua kua Mwanamke huyo ndiye Suzan, haraka akamsaidiaย kumfungua kamba ili watoke. Alipomaliza akamwambiaย
โBenjamin yuko nje anatusubiriaโ kabla hata hajamaliza kusema alichokua amekikusudia,ย zikasikika buti mlangoni, kisha Sauti ya risasi ikasikika, damu ikamwagika ikapenya chini yaย Mlango. Malkia Zandawe akaivuta bunduki yake na kuanza kujibu mashambulizi ya Risasiย za mfululizo.
Alipiga risasi nyingi mlangoni ili awatishe waliokua hapo waone sasa kua aliye ndani alikuaย amejipanga, Malikia Zandawe hakujua nje kwenye korido palikua na Walinzi naย Makomandoo wa kutosha.ย
Mwili wa rubani ulikua ni miongoni mwa miili iliyolala kando ya Mlango, Suzan alikuaย mwingi wa kugumia kila aliposikia risasi zikilia…ย
Nini kitaendelea?ย
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย 
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
 
		
 
									 
					
11 Comments
Woyooo msalaaa me WA kwanza
Duuuh
Asa huyo malikia zandawe amekaribishwa RASMI kwenye msala๐๐๐
Msala umekuwa msala kwelikweli!
Big up Admin.
Malkia ameyakanyaga ya Kandonga mtu kazi๐๐
Kwan ni mimi pekeangu cjaiona msala sehem ya 26
Sema kimeumanaaa ๐คฃ
Good ila kuanzia sehem ya kwanza cjapat sas sjui ntazupataj kweny Hadith hii
Hii movie ni kali sana aiseeee
Huwa mizigo ya kijasusi kama hii naielewa sana..
Hivi ndio hatuipati tena, maana naona Pigo Takatifu on the air…..
Kisa cha hii adisi inasisimua na nimependa uwandishi wake na alie andaa anajua
0zgv7v