Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Nne 

“Lengo la kuja huku ni kumpa taarifa Mama lakini hatuwezi  kuondoka bila yeye kiridhia, Veronica mpenzi tuvumilie tu  hadi pale hasira zake zitakapoisha” 

“Kwanini Mama ananifanyia hivi mimi, kama hakunizaa yeye?”  nilijiuliza baada ya kukumbuka tukio la kubakwa na Anko Sanga  ambapo Kwa maelezo ya Mama ilionesha kuwa alikuwa akijua kila  kitu . Endelea 

SEHEMU YA TANO

“Usiseme hivyo Veronica, Mama amechukia tu kwasababu taarifa  hii siyo njema kwa Mzazi yeyote yule….fikiria ingelikuwa ni  wewe ndio Mzazi unamsomesha Mtoto kwa gharama kubwa alafu  anaishia kupata mimba? Inaumiza ndio maana nakwambia  tusiondoke hadi tupate radhi zake” Yalikuwa ni maneno ya  Jonas yaliyojaa busara na hekima 

“Nifanye kuwa Mkeo Jonas” 

“Wewe tayari ni Mke wangu, tusubirie tu baraka za Mama yako”  Kutokana na maneno mazuri ya Jonas nilijikuta nikitaka  kumwambia ukweli kuhusu kukeketwa lakini nikaona sio muda  sahihi. 

Ulipita mwezi mmoja Mama hakuonekana nyumbani na simu yake  ikawa haipatikani, hofu ilianza kuniingia nikahisi labda  amepatwa na tatizo. Nilimfuata yule jirani aliyenipa taarifa  kuwa Mama alichukuliwa na gari ndogo ile siku, nilichotaka  kujua ni nani alimchukua 

“Jirani samahani, ni mwezi sasa Mama haonekani mpaka naanza  kuingiwa na wasiwasi” 

Nilimwambia baada ya kinipa nafasi ya kuzungumza nae “Ina maana tokea siku ile hadi leo hajarudi?” 

“Ndio Jirani napata mashaka ni wapi alipo, hivi umemtambua  aliyekuja kumchukua hapa?” Jirani alionekana kutafakari kabla  ya kunijibu ni wazi alikuwa akimtambua 

“Sura yake sio ngeni sana” 

“Anaonekanaje” 

“Mweusi, sijui kuhusu urefu sababu alikuwa ndani ya gari” “Itakuwa Anko Sanga huyo” 

Nilimuonesha picha ya Anko Sanga kupitia simu yangu ili  amtambue kama ni yeye au ni Mtu mwingine 

“Eeeh! ni huyu hapa, hata hivyo hupaswi kuwa na wasiwasi sana  kwasababu huyu alikuwa akija hapa mara kwa mara, amesimamia  ukarabati wa nyumba yenu mpaka ulipoisha” 

“Oooopsss” Nilivuta pumzi na kuzitoa 

“Ahsante sana jirani”

Uvumilivu wa kuendelea kumsubiria Mama ulinishinda  nikamueleza Jonas kuwa nimechoka ikiwezekana tuondoke, mimba  ilifikia miezi minne, hata upande wa Jonas vivyo hivyo  alianza kuchoka licha ya ujasiri wake wa kila siku kusema  tuendelee kumsubiria. 

Tulikusanya mabegi yetu ili tuondoke, tulipofika mlangoni  tulisikia Mlio wa gari, nilipochungulia nilimuona Mama akiwa  anashuka kwenye gari ya Anko Sanga. 

Tukayarudisha yale mabegi kusudi asijue kama tulikusudia  kuondoka. wote waliingia ndani na kutukuta tumekaa pale  sebleni. Anko Sanga alitusalimia na kuketi pamoja na sisi  lakini Mama alipita zake na kuingia chumbani kwake 

“Hivi Mama yangu amepatwa na nini?” nilimuuliza Anko Sanga  maana ndiye aliyekuwa karibu zaidi na Mama 

“Sijui nikuulize wewe Veronica umemfanya nini Mama yako?” 

“Mimi Anko Sanga? Mama simuelewi naona ameninunia tu,  ameondoka bila kusema anaenda wapi!” 

“Mama yako amechukizwa na ulichokifanya unapaswa kumuomba  sana msamaha Veronica, amekupigania sana lakini umemlipa  asichostahili” 

“Anko! makosa hayarekebishwi kwa hasira bali busara zilizo  njema lakini kwa staili hii hapa anajenga au anabomoa?”  alidakia Jonas 

“Kijana hata Kama ungelikuwa wewe ndio Mzazi wa Veronica kwa  kilichotokea ungelitumia busara gani? Tunu ya Mama ni kuona  Mtoto anafikia malengo aliyoyaweka Mzazi sasa kama Mtoto  anafikia hatua ya kuharibu Maisha yake, Unafikiria Mzazi  atakuwa kwenye wakati gani?” 

“Imeshatokea na tumekiri Makosa, kinachotakiwa Kama Mzazi  akubali kuwa Maji yameshamwagika, tuangalie kinachofuata  baada ya hapa….Ujauzito wake unakaribia miezi mitano,  tukiendelea hivi atakonda kwa mawazo” Alisema tena Jonas,  Dhahiri nilimuona Anko Sanga akimtazama kwa jicho la ubaya  Jonas. 

Alikuwa akimtazama kama Mwanaume wangu au adui aliyekatiza  ndoto zangu? Mbona yeye aliutumia mwili wangu kwa starehe  zake tena akishirikiana na Mama yangu Mzazi? Nilijiuliza  nikiendelea kumtazama

“Chakufanya hapa ni nyie kuongea na Mama Veronica, hakuna  njia nyingine” Alisema kikaksi akafunga mazungumzo 

“Anko Sanga…kama hatufikii makubaliano hapa nitaondoka,  nitakuwa tayari kuishi bila baraka zenu” 

Yalikuwa ndio maamuzi yangu na sikutaka Mtu anipinge, hata  nilipoongea na Mama nilimwambia hivyo hivyo ndipo nilipomuona  akianza kulegeza hasira zake 

“Kwahiyo unataka nifanye nini?” Aliniuliza baada ya kunisikia  nilikuwa tayari kufanya maamuzi yangu binafsi 

“Kubali niolewe na Jonas” 

“Unataka awe Mumeo?” 

“Ndio Mama, hata ukisema hapana sitarudi nyuma. Mtoto aliye  tumboni anatakiwa kulelewa na Baba yake Mzazi” Mama hakuwa na  Jinsi alikubali nifunge ndoa na Jonas, ruhusa ilienda sawa na  mipango ya haraka. Hatimaye tulifunga ndoa Arusha kwenye lile  Kanisa nililokiwa nikisali siku zote. 

Tukarudi Dar tukiwa Mke na Mume Maisha ya ndoa yalianza na  furaha iliyatawala maisha yetu, tukaenda kuishi Mbezi na huku  ndiko nilikokutana na Mama Sofia, alikuwa jirani yetu siku  moja alinisaidia nilipokuwa najisikia vibaya ndio ukawa  mwanzo wa kufahamiana kwetu. 

Tulijenga urafiki na huyu Mama mfanya biashara, alitokea  kunipenda mno kwa jinsi nilivyokuwa na moyo wa ujasiri na  kujali, 

“Jonas Mkeo ni Mtu wa pekee sana, ana moyo wa dhahabu”  Alisema Mama Sofia, nikaona nimueleze kuwa nilikuwa  nimekeketwa na jambo hili lilikuwa siri kwangu 

“Mume wako anajua?” 

“Hapana nimemficha kwa kitambo sasa” 

“Hupaswi kumficha, atajua tu ni vema ukamueleza” “Nahofia ataniacha Mama Sofia” 

“Usikubali roho ya uwoga ikutawale Veronica, mueleze ajue”  Alinishauri hivyo, jinsi ya kumueleza Jonas ilikuwa ngumu  sana.

Kila alipotaka kusex na mimi nilimwambia nasikia maumivu ya  tumbo, kwakuwa nilikuwa mjamzito ilimfanya anihurumie japo  niliona kama alikuwa anakosa raha. 

Tulikaa miezi mitano bila kufanya mapenzi, mara ya mwisho  ilikuwa wakati tuko Chuo ambapo nilikuwa nahakikisha tumelewa  ndipo tunafanya hata hivyo alinikataza kutumia kilevi baada  ya kuwa Mjamzito. 

Nilijua tu ipo siku atajua lakini nilijipa muda ili akijua  niwe nimejitayarisha kwa kila kitu, Nilipoanza Kliniki  daktari aligundua hili jambo na kibaya zaidi alikuwa ni  rafiki wa Jonas 

“Shem kumbe umekeketwa?” aliniuliza akiwa ananifanyia vipimo  kadhaa ikiwemo Ultra Sound ili kugundua Mtoto amekaaje na  jinsia yake. 

“Ndio Shem” nilimjibu kwa wasiwasi 

“Mh!” 

“Mbona unaguna?” 

“Hapana” Nilijua tu atamwambia Jonas lile jambo, 

“Najua umeshtuka sana lakini ndio ukweli huo, Jonas hajui  hili jambo nakuomba usimueleze nitakaa naye chini nitaongea  nae” Hakunijibu, aliendelea na vipimo 

Suala lile lilizidi kunipa mawazo sana na kunifanya nikumbuke  zamani nilipokeketwa, Mama ndiye aliyenilazimisha kufanyiwa  vile akisema ni mila zao na kama nitakataa nitatengwa. 

Mimba ilipofika miezi 6, yule Daktari alinipigia simu na  kunitaka niende tena Hospitali, baada ya kumaliza vipimo  aliniuliza 

“Umeshaongea na Mumeo?” 

“Hapana sijaongea naye, nitaongea naye siku za hivi karibuni” 

“Ina maana hamkutani kimwili? ilikuwaje asilijuwe hili  jambo?” 

“Ni stori ndefu sana Dokta” 

“Kuwa makini sana hili jambo halipaswi kuwa siri kabisa,  mueleze ukweli” Alinipa tena mtihani wa kuongea na Jonas,

Nilipanga nizungumze naye niliporudi, kabla hata sijaongea  naye Mama alinipigia simu na kunitaka niende Arusha, nilianza  kumkatalia sababu alisema niende mwenyewe 

“Nenda Veronica” Jonas alisema 

“Naendaje bila wewe Mume wangu?” 

“Kitakachojiri huko utaniambia” 

Moyo wangu ulisita sana kelekea Arusha tena bila Jonas, Mama  yangu nilianza kutomuelewa kwa kauli zake tata kila  alipozungumza na mimi. 

Sikuwa na budi bali kuondoka na kwenda Arusha kuitikia wito  wa Mama. Mimba ilifika miezi 7 kasoro, Mama alitaka nikae  Arusha hadi nitakapo Jifungua 

“Mama hilo halitawezekana, nitajifungua vipi bila Jonas  kuwepo?” 

“Veronica usiwe mbishi, unatakiwa kujifungua kwa mila na  tamaduni za kabila letu” Alisema Mama kwa msistizo,  nikakumbuka maneno ya daktari kuwa nilikuwa nina ujauzito wa  Mtoto wa Kike, hofu ya mtoto wangu kufanyiwa kama  nilivyofanyiwa ilinijia nikamwambia Mama 

“Mtoto wangu hawezi kufanyiwa kama mlivyonifanyia mimi” “Unamaanisha nini?” 

“Hawezi kukeketwa kama mnavyotaka” 

“Nani amekwambia tunataka kumkeketa Mtoto wako? na kama ni  wakike ni lazima afanyiwe hivyo Veronica” 

“Sitakubali Mama, nitapingana na wewe hadi naingia kuburini” 

“Anhaa! Huyo Jonas anakupa kiburi sana, tutaona” Alisema Mama  kisha alicheka na kujifanya ameongea utani ila kwa akili  zangu na jinsi nilivyomtafsiri niligundua kuwa alimaanisha  alichokisema. 

Nilijawa na hofu kila nilipomfikiria Mwanangu, Yule jirani  alinifuata na kunipongeza kutokana na ujauzito wangu 

“Ahsante Jirani, ndio ukubwa huu” 

“Lakini Veronica unatakiwa kuwa makini sana na Mama yako!”

“Kwanini?” 

“Mama yako ana sifa mbaya hapa mtaani, inasemekana yeye na  Kaka yake wanashiriki ushirikina” 

“Unamaanisha Mama yangu ni Mchawi?” 

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

8 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version