Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Nneย
“Lengo la kuja huku ni kumpa taarifa Mama lakini hatuweziย kuondoka bila yeye kiridhia, Veronica mpenzi tuvumilie tuย hadi pale hasira zake zitakapoisha”ย
“Kwanini Mama ananifanyia hivi mimi, kama hakunizaa yeye?”ย nilijiuliza baada ya kukumbuka tukio la kubakwa na Anko Sangaย ambapo Kwa maelezo ya Mama ilionesha kuwa alikuwa akijua kilaย kitu . Endeleaย
SEHEMU YA TANO
“Usiseme hivyo Veronica, Mama amechukia tu kwasababu taarifaย hii siyo njema kwa Mzazi yeyote yule….fikiria ingelikuwa niย wewe ndio Mzazi unamsomesha Mtoto kwa gharama kubwa alafuย anaishia kupata mimba? Inaumiza ndio maana nakwambiaย tusiondoke hadi tupate radhi zake” Yalikuwa ni maneno yaย Jonas yaliyojaa busara na hekimaย
“Nifanye kuwa Mkeo Jonas”ย
“Wewe tayari ni Mke wangu, tusubirie tu baraka za Mama yako”ย Kutokana na maneno mazuri ya Jonas nilijikuta nikitakaย kumwambia ukweli kuhusu kukeketwa lakini nikaona sio mudaย sahihi.ย
Ulipita mwezi mmoja Mama hakuonekana nyumbani na simu yakeย ikawa haipatikani, hofu ilianza kuniingia nikahisi labdaย amepatwa na tatizo. Nilimfuata yule jirani aliyenipa taarifaย kuwa Mama alichukuliwa na gari ndogo ile siku, nilichotakaย kujua ni nani alimchukuaย
“Jirani samahani, ni mwezi sasa Mama haonekani mpaka naanzaย kuingiwa na wasiwasi”ย
Nilimwambia baada ya kinipa nafasi ya kuzungumza nae “Ina maana tokea siku ile hadi leo hajarudi?”ย
“Ndio Jirani napata mashaka ni wapi alipo, hivi umemtambuaย aliyekuja kumchukua hapa?” Jirani alionekana kutafakari kablaย ya kunijibu ni wazi alikuwa akimtambuaย
“Sura yake sio ngeni sana”ย
“Anaonekanaje”ย
“Mweusi, sijui kuhusu urefu sababu alikuwa ndani ya gari” “Itakuwa Anko Sanga huyo”ย
Nilimuonesha picha ya Anko Sanga kupitia simu yangu iliย amtambue kama ni yeye au ni Mtu mwingineย
“Eeeh! ni huyu hapa, hata hivyo hupaswi kuwa na wasiwasi sanaย kwasababu huyu alikuwa akija hapa mara kwa mara, amesimamiaย ukarabati wa nyumba yenu mpaka ulipoisha”ย
“Oooopsss” Nilivuta pumzi na kuzitoaย
“Ahsante sana jirani”
Uvumilivu wa kuendelea kumsubiria Mama ulinishindaย nikamueleza Jonas kuwa nimechoka ikiwezekana tuondoke, mimbaย ilifikia miezi minne, hata upande wa Jonas vivyo hivyoย alianza kuchoka licha ya ujasiri wake wa kila siku kusemaย tuendelee kumsubiria.ย
Tulikusanya mabegi yetu ili tuondoke, tulipofika mlangoniย tulisikia Mlio wa gari, nilipochungulia nilimuona Mama akiwaย anashuka kwenye gari ya Anko Sanga.ย
Tukayarudisha yale mabegi kusudi asijue kama tulikusudiaย kuondoka. wote waliingia ndani na kutukuta tumekaa paleย sebleni. Anko Sanga alitusalimia na kuketi pamoja na sisiย lakini Mama alipita zake na kuingia chumbani kwakeย
“Hivi Mama yangu amepatwa na nini?” nilimuuliza Anko Sangaย maana ndiye aliyekuwa karibu zaidi na Mamaย
“Sijui nikuulize wewe Veronica umemfanya nini Mama yako?”ย
“Mimi Anko Sanga? Mama simuelewi naona ameninunia tu,ย ameondoka bila kusema anaenda wapi!”ย
“Mama yako amechukizwa na ulichokifanya unapaswa kumuombaย sana msamaha Veronica, amekupigania sana lakini umemlipaย asichostahili”ย
“Anko! makosa hayarekebishwi kwa hasira bali busara zilizoย njema lakini kwa staili hii hapa anajenga au anabomoa?”ย alidakia Jonasย
“Kijana hata Kama ungelikuwa wewe ndio Mzazi wa Veronica kwaย kilichotokea ungelitumia busara gani? Tunu ya Mama ni kuonaย Mtoto anafikia malengo aliyoyaweka Mzazi sasa kama Mtotoย anafikia hatua ya kuharibu Maisha yake, Unafikiria Mzaziย atakuwa kwenye wakati gani?”ย
“Imeshatokea na tumekiri Makosa, kinachotakiwa Kama Mzaziย akubali kuwa Maji yameshamwagika, tuangalie kinachofuataย baada ya hapa….Ujauzito wake unakaribia miezi mitano,ย tukiendelea hivi atakonda kwa mawazo” Alisema tena Jonas,ย Dhahiri nilimuona Anko Sanga akimtazama kwa jicho la ubayaย Jonas.ย
Alikuwa akimtazama kama Mwanaume wangu au adui aliyekatizaย ndoto zangu? Mbona yeye aliutumia mwili wangu kwa stareheย zake tena akishirikiana na Mama yangu Mzazi? Nilijiulizaย nikiendelea kumtazama
“Chakufanya hapa ni nyie kuongea na Mama Veronica, hakunaย njia nyingine” Alisema kikaksi akafunga mazungumzoย
“Anko Sanga…kama hatufikii makubaliano hapa nitaondoka,ย nitakuwa tayari kuishi bila baraka zenu”ย
Yalikuwa ndio maamuzi yangu na sikutaka Mtu anipinge, hataย nilipoongea na Mama nilimwambia hivyo hivyo ndipo nilipomuonaย akianza kulegeza hasira zakeย
“Kwahiyo unataka nifanye nini?” Aliniuliza baada ya kunisikiaย nilikuwa tayari kufanya maamuzi yangu binafsiย
“Kubali niolewe na Jonas”ย
“Unataka awe Mumeo?”ย
“Ndio Mama, hata ukisema hapana sitarudi nyuma. Mtoto aliyeย tumboni anatakiwa kulelewa na Baba yake Mzazi” Mama hakuwa naย Jinsi alikubali nifunge ndoa na Jonas, ruhusa ilienda sawa naย mipango ya haraka. Hatimaye tulifunga ndoa Arusha kwenye lileย Kanisa nililokiwa nikisali siku zote.ย
Tukarudi Dar tukiwa Mke na Mume Maisha ya ndoa yalianza naย furaha iliyatawala maisha yetu, tukaenda kuishi Mbezi na hukuย ndiko nilikokutana na Mama Sofia, alikuwa jirani yetu sikuย moja alinisaidia nilipokuwa najisikia vibaya ndio ukawaย mwanzo wa kufahamiana kwetu.ย
Tulijenga urafiki na huyu Mama mfanya biashara, alitokeaย kunipenda mno kwa jinsi nilivyokuwa na moyo wa ujasiri naย kujali,ย
“Jonas Mkeo ni Mtu wa pekee sana, ana moyo wa dhahabu”ย Alisema Mama Sofia, nikaona nimueleze kuwa nilikuwaย nimekeketwa na jambo hili lilikuwa siri kwanguย
“Mume wako anajua?”ย
“Hapana nimemficha kwa kitambo sasa”ย
“Hupaswi kumficha, atajua tu ni vema ukamueleza” “Nahofia ataniacha Mama Sofia”ย
“Usikubali roho ya uwoga ikutawale Veronica, mueleze ajue”ย Alinishauri hivyo, jinsi ya kumueleza Jonas ilikuwa ngumuย sana.
Kila alipotaka kusex na mimi nilimwambia nasikia maumivu yaย tumbo, kwakuwa nilikuwa mjamzito ilimfanya anihurumie japoย niliona kama alikuwa anakosa raha.ย
Tulikaa miezi mitano bila kufanya mapenzi, mara ya mwishoย ilikuwa wakati tuko Chuo ambapo nilikuwa nahakikisha tumelewaย ndipo tunafanya hata hivyo alinikataza kutumia kilevi baadaย ya kuwa Mjamzito.ย
Nilijua tu ipo siku atajua lakini nilijipa muda ili akijuaย niwe nimejitayarisha kwa kila kitu, Nilipoanza Klinikiย daktari aligundua hili jambo na kibaya zaidi alikuwa niย rafiki wa Jonasย
“Shem kumbe umekeketwa?” aliniuliza akiwa ananifanyia vipimoย kadhaa ikiwemo Ultra Sound ili kugundua Mtoto amekaaje naย jinsia yake.ย
“Ndio Shem” nilimjibu kwa wasiwasiย
“Mh!”ย
“Mbona unaguna?”ย
“Hapana” Nilijua tu atamwambia Jonas lile jambo,ย
“Najua umeshtuka sana lakini ndio ukweli huo, Jonas hajuiย hili jambo nakuomba usimueleze nitakaa naye chini nitaongeaย nae” Hakunijibu, aliendelea na vipimoย
Suala lile lilizidi kunipa mawazo sana na kunifanya nikumbukeย zamani nilipokeketwa, Mama ndiye aliyenilazimisha kufanyiwaย vile akisema ni mila zao na kama nitakataa nitatengwa.ย
Mimba ilipofika miezi 6, yule Daktari alinipigia simu naย kunitaka niende tena Hospitali, baada ya kumaliza vipimoย aliniulizaย
“Umeshaongea na Mumeo?”ย
“Hapana sijaongea naye, nitaongea naye siku za hivi karibuni”ย
“Ina maana hamkutani kimwili? ilikuwaje asilijuwe hiliย jambo?”ย
“Ni stori ndefu sana Dokta”ย
“Kuwa makini sana hili jambo halipaswi kuwa siri kabisa,ย mueleze ukweli” Alinipa tena mtihani wa kuongea na Jonas,
Nilipanga nizungumze naye niliporudi, kabla hata sijaongeaย naye Mama alinipigia simu na kunitaka niende Arusha, nilianzaย kumkatalia sababu alisema niende mwenyeweย
“Nenda Veronica” Jonas alisemaย
“Naendaje bila wewe Mume wangu?”ย
“Kitakachojiri huko utaniambia”ย
Moyo wangu ulisita sana kelekea Arusha tena bila Jonas, Mamaย yangu nilianza kutomuelewa kwa kauli zake tata kilaย alipozungumza na mimi.ย
Sikuwa na budi bali kuondoka na kwenda Arusha kuitikia witoย wa Mama. Mimba ilifika miezi 7 kasoro, Mama alitaka nikaeย Arusha hadi nitakapo Jifunguaย
“Mama hilo halitawezekana, nitajifungua vipi bila Jonasย kuwepo?”ย
“Veronica usiwe mbishi, unatakiwa kujifungua kwa mila naย tamaduni za kabila letu” Alisema Mama kwa msistizo,ย nikakumbuka maneno ya daktari kuwa nilikuwa nina ujauzito waย Mtoto wa Kike, hofu ya mtoto wangu kufanyiwa kamaย nilivyofanyiwa ilinijia nikamwambia Mamaย
“Mtoto wangu hawezi kufanyiwa kama mlivyonifanyia mimi” “Unamaanisha nini?”ย
“Hawezi kukeketwa kama mnavyotaka”ย
“Nani amekwambia tunataka kumkeketa Mtoto wako? na kama niย wakike ni lazima afanyiwe hivyo Veronica”ย
“Sitakubali Mama, nitapingana na wewe hadi naingia kuburini”ย
“Anhaa! Huyo Jonas anakupa kiburi sana, tutaona” Alisema Mamaย kisha alicheka na kujifanya ameongea utani ila kwa akiliย zangu na jinsi nilivyomtafsiri niligundua kuwa alimaanishaย alichokisema.ย
Nilijawa na hofu kila nilipomfikiria Mwanangu, Yule jiraniย alinifuata na kunipongeza kutokana na ujauzito wanguย
“Ahsante Jirani, ndio ukubwa huu”ย
“Lakini Veronica unatakiwa kuwa makini sana na Mama yako!”
“Kwanini?”ย
“Mama yako ana sifa mbaya hapa mtaani, inasemekana yeye naย Kaka yake wanashiriki ushirikina”ย
“Unamaanisha Mama yangu ni Mchawi?”ย
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
27 Comments
Huyu veronica nae kama hana akili….anapekekeshwa sna an mamake
Hii kalii๐ฅ๐ฅ kesho zitoke mbili Admin.๐
Aah hiki kipande ni. Shidaa,, admin tunaomba utuwahishie mwendelezo kwa wakati ๐
Kesho Fanya Utoa Double Mr Admin
Aah hiki kipande ni. Shidaa,, admin tunaomba utuwahishie mwendelezo kwa wakati ๐
Unachelewa Kutuma mwendelezo
Mzuri
mu34jk
Super https://shorturl.fm/6539m
https://shorturl.fm/j3kEj
https://shorturl.fm/j3kEj
https://shorturl.fm/XIZGD
https://shorturl.fm/TbTre
https://shorturl.fm/TbTre
https://shorturl.fm/FIJkD
https://shorturl.fm/68Y8V
https://shorturl.fm/FIJkD
https://shorturl.fm/6539m
https://shorturl.fm/TbTre
https://shorturl.fm/XIZGD
https://shorturl.fm/9fnIC
https://shorturl.fm/oYjg5
https://shorturl.fm/9fnIC
https://shorturl.fm/N6nl1
https://shorturl.fm/A5ni8
https://shorturl.fm/FIJkD
bcmxao