Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Saba
Ile simu ilikuwa ndogo tu yaani ya kitochi, hivyo ilikuwaย ngumu kwangu japo kupata namba za Jonas wala za marafikiย zangu niliosoma nao kama Konzo, Siku moja alirudi akiwaย amelewa, alikuwa na Mwanamke mmoja ambaye jinsiย alivyozungumza alikuwa hajalewa kabisa.ย
Siku zote kila alipoleta Mtu alikuwa akinifungia chumbani naย kustarehe chumba Kingine, nikiwa mle chumbani nilipata harufuย ya Sigara alafu nikasikia sauti ya Mwanamke akiongea kuwaย
“Nalala huku huku asubuhi anipe changu, kalewa chakali”ย nilisikia sauti hii niliita . Endelea
SEHEMU YA SABA
“Dada! Dada!” ilikuwa majira ya usiku sana kama saa sabaย hivi, nilisikia ukimya baada ya kuita alafu nikaanza kusikiaย sauti ya kiatu kuja nilipo.ย
“Nani anaita?” aliuliza yule Mdada, pale pale Mtoto akaanzaย kuliaย
“Ni mimi hapa, Naitwa Veronica”
“Nikusaidie nini?”ย
“Naomba nifungulie tafadhari nina shida kidogo” “Nakufungulia vipi kwani umeingiaje humo”ย
“Nitakuelezea, naomba unifungulie tafadhari” Yule Mdadaย alinifungulia maana alikuwa akifunga kwa nje kwa kutumiaย komeo za kisasa!ย
“Ahsante sana Dada”ย
“Vipi huyo Mtoto ni wa kwako?”ย
“Ndio wa kwangu”ย
“Sasa ilikuaje ukajifungia humo tena, kama nisingepita hukuย ingekuwaje?”ย
“Mimi ni msichana wa kazi, nina shida ya simu” Ilibidiย nimdanganye yule mdada ambaye alinipa tumaini laย kunisikiliza, nilitamani kumwambia anitoroshe usiku uleย lakini niliogopa kuhusu Afya ya Mtoto wangu na ile baridi yaย Usiku niliona nitahatarisha zaidi Maisha yake.ย
“Hii hapa” alinipatia Simu yake kubwa na ndichoย nilichokitaka, haraka haraka niliingia facebook nikamtafutaย Konzo, nikamtumia meseji iliyoambatana na namba yangu!ย
“Ahsante!” nilimpatia simu yake baada ya kufuta mesejiย niliyoitumaย
“Usimueleze Anko Sanga tafadhari, nifungie kwa nje” nilisemaย na kurudi ndani, hapana shaka yule mdada alinisikiliza naย kuelewa nilichotaka, kilichobakia kwangu ni dua na sala iliย Konzo azione meseji zangu.ย
Asubuhi, yule mdada alikuja kuniaga akaondoka zake. Masaaย mawili baadaye Anko Sanga alinifungulia, ndio hivyo niliishiย kama Mtumwa kwenye maisha yangu. Mtoto alipoumwa alimchukuaย na kwenda nae Hospitali, chakula na vitu vingine alivifanyaย mwenyewe, Jukumu langu likawa kupika, kula na kumpa penzi.ย
Kama bahati tu baada ya siku tatu Konzo alinipigia, sikuaminiย kabisa. Nilizungumza nae na kumueleza hali halisi ya maishaย yangu kwa kipindi kile, alisikitika sana pia hakuamini kamaย Mama yangu alikuwa akinitumikisha namna ile, akaniambiaย atamtafuta Jonas ili azungumze nae, kwakuwa Anko Sangaย aliiunganisha ile simu na simu yake alifanikiwa kujuaย nilikuwa nikiongea na Mtu. Ilipokata alinipigia na kunifokeaย sana.ย
Aliporudi aliichukua ile simu na kuniambia sitaweza kuongeaย na yeyote yule, Akanipa na mkwara mzito kuwa endapo nitaendaย kinyume atamuua Mtoto wangu!ย
Kwa kipindi hiki sikumsikia wala kumuona Mama yangu kabisa,ย nikawa mfungwa kwenye nyumba ya Anko Sanga.ย
Upande wa Konzo alifanya jitihada za kumtafuta Jonasย akamuelezea changamoto nilizokuwa nazipitia, pamoja na hasiraย za Jonas alijikuta akinionea huruma, akasafiri kuja Arushaย kunitafuta.ย
Kibaya zaidi ni kuwa Mama alihama pale alipokuwa anaishiย hivyo alipoenda pale aliambiwa kuwa mwenye ile nyumba aliuzaย na kuondoka pale Arusha.ย
Yule jirani alipomuona Jonas alimsimulia kilichotokea kwaย upande wa Mama maana hakujuwa kilichotokea upande wangu,ย kipindi yale mambo yanatendeka pale alikuwa Hospitaliย kutokana na kuanguka ghaflaย
“Kuhusu Veronica sijui alipo, labda Mama yake ameondoka naye” “Na Mjomba wake unaweza ukapafahamu anapoishi?”ย
“Kiukweli sijui anaishi wapi Kaka yangu!” Jonas alikuwaย kwenye nyakati ngumu za kunipata mimi.ย
Baada ya Anko Sanga kuichukua ile simu haikupatikana tena,ย Jonas alipojaribu kuipiga ile namba aliyopewa na Konzoย haikuita kabisaย
Ilikua ngumu kwa Jonas kupafahamu nilipokuwa ninaishi, Mtotoย wangu aliendelea kukua hatimae miaka miwili ilipita, Moyoย alianza kuongea na kukimbia, hakupata nafasi ya kucheza walaย kujumuika na watu wengine, alinifahamu mimi na Anko Sangaย Pekee, kila nilipomtazama Mwanangu niliiona kabisa taswira yaย Jonas, alifanana sana na Baba yake!ย
“Utakua huru Moyo” nilimwambia Mwanangu nikiwa ninalia wakatiย huo akiwa amelala, hata kama angelikuwa macho asingeliwezaย kutambua nilichomwambia, miaka miwili haikitosha kuwa naย ufahamu kwake.ย
Nilimpiga busu la upendo binti yangu kisha nilimlaza, Ankoย Sanga alipoingia alinikuta nikiwa namfunika vizuri maanaย baridi la Arusha wakati huo lilikuwa juu sana.
“Nakuhitaji Chumbani” Alisema, nilijuwa tu alikua akihitajiย penzi ili azidi kupata pesaย
“Nakuja” Nilimjibu, alikua akimchukia sana binti yangu baadaย ya kugundua kuwa ujauzito haukua wake maana mwanzo alikuwaย akidai kuwa Mimba ni yake lakini alipozaliwa Moyo akiwa naย sura ya Jonas alianza kumchukia.ย
Siku moja aliniambia tumtenge Mtoto kwenye chumba kingine,ย tena wakati huo Moyo akiwa na mwaka mmoja tuu, ilikua ngumuย kwangu lakini ililazimika kuwa hivyo japo roho iliniumaย kumuacha Mtoto wangu kwenye chumba kingine.ย
Basi, baada ya kumaliza kumlaza Moyo nilienda chumbani kwaย Anko Sanga, wakati huu tukiwa Mke na Mume, niliufunga uleย Mlango vizuri kisha funguo niliondoka nayo, nilikuwaย nikihofia sana juu ya Usalama wa binti yangu maana Anko Sangaย alikuwa hamtaki pale nyumbani.ย
Nilimkuta akiwa amekasirika, alinitaka nikae kitandani namiย nilifanya hivyo, nilishamzoea na hasira zake za mara kwaย mara.ย
“Miaka Mitatu kasoro sasa tokea tumefunga ndoa, sijawahiย kumuona Mama akija hapa, sipati mawasiliano naye. Napataย wakati mgumu sana kujua kama yupo hai au amekufa” Nilisemaย ili tu kumhamisha kwenye kile alichokuwa anataka kuniambiaย maana nikitaka kumkera basi nimuulize kuhusu Mamaย
“Hicho sio nilicho kuitia hapa Veronica, usinihamishe kwenyeย reli”ย
“Kuna ubaya gani ukinijibu? sijatoka ndani kwa miaka hiyoย yote, siwasiliani na yeyote kwa kipindi hicho chote zaidi yaย Wewe”ย
“Sikia Veronica, nataka unipatie Mtoto wako nimpeleke kwaย Bibi yake, siwezi kukaa na damu ya Mtu mwingine” Alisema hukuย akiweka sura ya Ukauzu, alikua ameniingizia kitu kipya kabisaย kwenye kichwa changu.ย
“Umchukue Moyo?”ย
“Ndio!”ย
“Bado hujaongea sawa sawa! Nikupe binti yangu? hiloย haliwezekani Sanga…nimefanya kila ulichotaka lakini kwaย binti yangu unavuka mipaka kabisa, siwezi kukupa binti yanguย hata siku moja na nisisikie unaongelea hilo jambo tena”
Nilijikuta nikimkalipia Anko Sanga, ndio ilikua ni mara yanguย ya Kwanza kufanya hivyo, siku zote nilikuwa mtiifu kwakeย lakini alipomgusia Mtoto wangu alinigusa pabaya sana.ย
“Unanipandishia sauti mimi?”ย
“Sikupi Mtoto Sanga labda uniuwe kwanza ndipo umchukue lakiniย sio kwa hidhini yangu, hata Moyo akijua ulimchukua kutokaย kwangu atanilaani sana” Nilipomaliza hii kauli nilikutana naย kibao cha nguvu upande wa kushoto wa Shavu langu!ย
“Mpumbavu Mkubwa hivi unaniona mimi poyoyo kama huyo uliyezaaย nae? sasa nisikilize kwa makini umetaka hujataka Mtotoย ataondoka hapa full Stop”ย
“Endelea kunipiga hadi uniuwe lakini Kukupa Mtoto haiwezekaniย kabisa Sanga” niliongea nikiwa ninalia, alinipiga kibaoย kingine akanitupa chini kisha alianza kunikanyagaย
“Shenzi taipu! Ujinga…wafanyie….wajinga wenzio…”ย alinipiga sana siku hiyo tena bila kupumzika akawaย amenivimbisha jicho la upande wa kulia, alinisababishiaย maumivu makali kwenye kiuno changu kutokana na kunikanyaga!ย
Nililia sana, nikiwa kama Mama sikutaka kabisa kutengana naย binti yangu alafu nisijuwe yuko wapi? Ushirikina wao sikutakaย wamuingizie Mwanangu, japo alisema anampeleka kwa Mama lakiniย niliishiwa nguvu ya kuruhusu hilo kwanza Mama mwenyeweย alishakuwa adui yangu, kingine sikujua anaishi wapi naย sikupata kumuona kwa miaka hiyo yote. Alinipokonya funguo waย chumba ambacho Moyo alikuwa amelala, nilijitahidi sanaย kupambana na Sanga asimchukue Mtoto lakini sikuwa na mabavuย ya kupimana nae.ย
Niliishia kulia kwa uchungu, hii nyumba ya Anko Sanga ilikuwaย ya kifahari kubwa sana kiasi hata nifanyaje ilikuwa ni ngumuย kutoa sauti nje, ilikuwa imejitenga nje ya mji wa Arushaย ambako kulikuwa na mashamba yake. Usiku huo huo Anko Sangaย alimchukua Moyo, alinifungia kule chumbani nilipiga sanaย kelele aniachie japo Binti yangu nipate kukaa nae lakiniย haikusaidia kwani alidhamiria kuniumiza, kunitia kovu ndaniย ya moyo wangu!ย
Nilimsikia Moyo akiwa analia ni wazi kuwa Sanga alimbebaย vibaya Moyo bila hata kujali kama alikuwa Mtoto mdogoย anayehitaji kunyenyekewa istoshe alikuwa usingizini, aliliaย huku akiita ‘Mamaa! ‘Mamaaa!’ Alinitia Uchungu sana, baadayeย ukimya ulitawala nikaliona gari la Sanga likiwa linatokaย maana nyumba ilikuwa ya ghorofa hivyo nilipata nafasi yaย kuchunguza kutokea juu!
Sikupata Usingizi, nilikesha ninalia na kusali ili Munguย anitoe kwenye ile mitihani mizito iliyo migumu kwangu,ย
“Mungu nimekukosea nini mimi? kwanini unaniadhibu namna hii,ย kwanini yote ya kwangu mimi tuu?” Nilijikuta nikipaza sautiย yangu ili kama Mungu amesinzia basi aamke aone jinsiย ninavyoteseka, Maisha yangu yote niliishi kwa kumtegemea yeyeย na kuamiani lakini kwa kipindi kile niliona amenisahauย kabisa.ย
Sanga hakurudi hadi kulipo pambazuka, nilikuwa nimesimamaย nikichungulia nje hadi jua lilipotoka, nilikuwa nikitazamaย geti pamoja na barabara ili kuona kama kuna Mtu au gariย ilikuwa ikija, ndipo nilipoiona gari ndogo ya Anko Sanga ainaย ya Rav4 New Model, nikasema ni lazima nilipize kwaย alichokifanya kwa binti yangu, kunitenga nae ni adhabu kubwaย sana kwangu!ย
Nilipata wazo la kumpiga na kitu kizito kichwani ili nimuuweย kabisa maana nilikuwa nafanya kila kitu kwa ajili ya Mtotoย wangu lakini walishamchukua, nilifunga dirisha baada ya kuonaย gari limeingia ndani, nilitafuta kitu kizito pale chumbani,ย niliiona chupa ya soda niliichukuwa na kujificha nyuma yaย mlango ili akifungua tu nimtandike nayo, nilishajipanga kuwaย liwalo na liwe siwezi kuendelea kuwa Mtumwa.ย
Nilijibanza vizuri sana huku nikiamini kuwa ilikuwa ndioย nafasi yangu ya mwisho, nikiikosa hiyo nafasi nawezaย nisiipate tena maana nikimkosa hapo anaweza akanigeuza kuwaย Mtumwa nisiye na uhuru tena, angeniona adui yake kwasababuย ningemlipiza kwa kumchukua Mtoto wangu.ย
Nilikaa kwa kitambo kidogo kabla ya kuanza kusikia milangoย ikifunguliwa, kawaida alikuwa akitembea na rundo la funguo zaย milango, nilikuwa nikizisikia kila alipokuwa akitembea,ย nilisikia akija upande wangu ni wazi kuwa alikuwa akijaย chumbani, nilivuta pumzi za kutosha kisha nilijiweka sawaย kumshambulia. Sikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo lakiniย ilinibidi maana bila hivyo ningelikuwa kwenye wakati mgumuย sana.ย
Vishindo vya miguu vilikoma kwenye mlango wa Chumba nilichopoย kisha funguo ilianza kufungua kitasa taratibu, nilifumbaย macho yangu ili nisione kitakacho fanyika pale, niliivuta ileย chupa sawa sawa, mlango ulipofunguliwa nikawa nyuma yaย Mlango, niliposikia akitembea kuingia ndani basi nikaiachiaย ile chupa nikiwa nimefumba macho yangu ikatua kwenye kichwaย chake, nikasikia sauti iliyoshindwa kutoka sawa sawa kishaย nilisikia kitu kikianguka kama mzigo, Yes! nilikuwa nimelengaย shabaha yangu vizuri, ikabidi sasa nifumbue macho yangu!
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA NANE
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
32 Comments
Sasa weka ya 8 tuendelee ma huondo
That is how ,,unatakiwa uwe binti vero๐
Yaani admin fanya kututunuku ya 8 please na mvua hizi mambo yaende mukidemukide
Uncle Sanga Mnyakyusa sio ahahahaha
Ni mkinga Hilo jina lake ni mkinga halisi
Angalau Ningejua aliyedondoka Alikuwa Anko Sanga au Mama Yake Sema Na Ya Nane Naiomba Leoeo
Good story
Tuendele na story nzuri sna part 8
Jana ujaeka endelea plz jmn
Afuuu y 7 mbn ilichelewa kutoka kwann
Aya mambo ayatakiwi kuchelewa admin tupe ya nane tupate uhondo
Cool partnership https://shorturl.fm/XIZGD
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/FIJkD
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/j3kEj
https://shorturl.fm/9fnIC
https://shorturl.fm/N6nl1
https://shorturl.fm/6539m
https://shorturl.fm/m8ueY
https://shorturl.fm/N6nl1
https://shorturl.fm/a0B2m
https://shorturl.fm/A5ni8
https://shorturl.fm/TbTre
https://shorturl.fm/j3kEj
https://shorturl.fm/XIZGD
https://shorturl.fm/uyMvT
https://shorturl.fm/IPXDm
https://shorturl.fm/ypgnt
https://shorturl.fm/retLL