Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Saba-07)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Sita-06)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tano-05)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Saba-07)
    Hadithi

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Saba-07)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 19, 2025Updated:May 19, 20256 Comments9 Mins Read802 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Saba

    Ile simu ilikuwa ndogo tu yaani ya kitochi, hivyo ilikuwa  ngumu kwangu japo kupata namba za Jonas wala za marafiki  zangu niliosoma nao kama Konzo, Siku moja alirudi akiwa  amelewa, alikuwa na Mwanamke mmoja ambaye jinsi  alivyozungumza alikuwa hajalewa kabisa. 

    Siku zote kila alipoleta Mtu alikuwa akinifungia chumbani na  kustarehe chumba Kingine, nikiwa mle chumbani nilipata harufu  ya Sigara alafu nikasikia sauti ya Mwanamke akiongea kuwa 

    “Nalala huku huku asubuhi anipe changu, kalewa chakali”  nilisikia sauti hii niliita . Endelea

    SEHEMU YA SABA

    “Dada! Dada!” ilikuwa majira ya usiku sana kama saa saba  hivi, nilisikia ukimya baada ya kuita alafu nikaanza kusikia  sauti ya kiatu kuja nilipo. 

    “Nani anaita?” aliuliza yule Mdada, pale pale Mtoto akaanza  kulia 

    “Ni mimi hapa, Naitwa Veronica”

    “Nikusaidie nini?” 

    “Naomba nifungulie tafadhari nina shida kidogo” “Nakufungulia vipi kwani umeingiaje humo” 

    “Nitakuelezea, naomba unifungulie tafadhari” Yule Mdada  alinifungulia maana alikuwa akifunga kwa nje kwa kutumia  komeo za kisasa! 

    “Ahsante sana Dada” 

    “Vipi huyo Mtoto ni wa kwako?” 

    “Ndio wa kwangu” 

    “Sasa ilikuaje ukajifungia humo tena, kama nisingepita huku  ingekuwaje?” 

    “Mimi ni msichana wa kazi, nina shida ya simu” Ilibidi  nimdanganye yule mdada ambaye alinipa tumaini la  kunisikiliza, nilitamani kumwambia anitoroshe usiku ule  lakini niliogopa kuhusu Afya ya Mtoto wangu na ile baridi ya  Usiku niliona nitahatarisha zaidi Maisha yake. 

    “Hii hapa” alinipatia Simu yake kubwa na ndicho  nilichokitaka, haraka haraka niliingia facebook nikamtafuta  Konzo, nikamtumia meseji iliyoambatana na namba yangu! 

    “Ahsante!” nilimpatia simu yake baada ya kufuta meseji  niliyoituma 

    “Usimueleze Anko Sanga tafadhari, nifungie kwa nje” nilisema  na kurudi ndani, hapana shaka yule mdada alinisikiliza na  kuelewa nilichotaka, kilichobakia kwangu ni dua na sala ili  Konzo azione meseji zangu. 

    Asubuhi, yule mdada alikuja kuniaga akaondoka zake. Masaa  mawili baadaye Anko Sanga alinifungulia, ndio hivyo niliishi  kama Mtumwa kwenye maisha yangu. Mtoto alipoumwa alimchukua  na kwenda nae Hospitali, chakula na vitu vingine alivifanya  mwenyewe, Jukumu langu likawa kupika, kula na kumpa penzi. 

    Kama bahati tu baada ya siku tatu Konzo alinipigia, sikuamini  kabisa. Nilizungumza nae na kumueleza hali halisi ya maisha  yangu kwa kipindi kile, alisikitika sana pia hakuamini kama  Mama yangu alikuwa akinitumikisha namna ile, akaniambia  atamtafuta Jonas ili azungumze nae, kwakuwa Anko Sanga  aliiunganisha ile simu na simu yake alifanikiwa kujua nilikuwa nikiongea na Mtu. Ilipokata alinipigia na kunifokea  sana. 

    Aliporudi aliichukua ile simu na kuniambia sitaweza kuongea  na yeyote yule, Akanipa na mkwara mzito kuwa endapo nitaenda  kinyume atamuua Mtoto wangu! 

    Kwa kipindi hiki sikumsikia wala kumuona Mama yangu kabisa,  nikawa mfungwa kwenye nyumba ya Anko Sanga. 

    Upande wa Konzo alifanya jitihada za kumtafuta Jonas  akamuelezea changamoto nilizokuwa nazipitia, pamoja na hasira  za Jonas alijikuta akinionea huruma, akasafiri kuja Arusha  kunitafuta. 

    Kibaya zaidi ni kuwa Mama alihama pale alipokuwa anaishi  hivyo alipoenda pale aliambiwa kuwa mwenye ile nyumba aliuza  na kuondoka pale Arusha. 

    Yule jirani alipomuona Jonas alimsimulia kilichotokea kwa  upande wa Mama maana hakujuwa kilichotokea upande wangu,  kipindi yale mambo yanatendeka pale alikuwa Hospitali  kutokana na kuanguka ghafla 

    “Kuhusu Veronica sijui alipo, labda Mama yake ameondoka naye” “Na Mjomba wake unaweza ukapafahamu anapoishi?” 

    “Kiukweli sijui anaishi wapi Kaka yangu!” Jonas alikuwa  kwenye nyakati ngumu za kunipata mimi. 

    Baada ya Anko Sanga kuichukua ile simu haikupatikana tena,  Jonas alipojaribu kuipiga ile namba aliyopewa na Konzo  haikuita kabisa 

    Ilikua ngumu kwa Jonas kupafahamu nilipokuwa ninaishi, Mtoto  wangu aliendelea kukua hatimae miaka miwili ilipita, Moyo  alianza kuongea na kukimbia, hakupata nafasi ya kucheza wala  kujumuika na watu wengine, alinifahamu mimi na Anko Sanga  Pekee, kila nilipomtazama Mwanangu niliiona kabisa taswira ya  Jonas, alifanana sana na Baba yake! 

    “Utakua huru Moyo” nilimwambia Mwanangu nikiwa ninalia wakati  huo akiwa amelala, hata kama angelikuwa macho asingeliweza  kutambua nilichomwambia, miaka miwili haikitosha kuwa na  ufahamu kwake. 

    Nilimpiga busu la upendo binti yangu kisha nilimlaza, Anko  Sanga alipoingia alinikuta nikiwa namfunika vizuri maana  baridi la Arusha wakati huo lilikuwa juu sana.

    “Nakuhitaji Chumbani” Alisema, nilijuwa tu alikua akihitaji  penzi ili azidi kupata pesa 

    “Nakuja” Nilimjibu, alikua akimchukia sana binti yangu baada  ya kugundua kuwa ujauzito haukua wake maana mwanzo alikuwa  akidai kuwa Mimba ni yake lakini alipozaliwa Moyo akiwa na  sura ya Jonas alianza kumchukia. 

    Siku moja aliniambia tumtenge Mtoto kwenye chumba kingine,  tena wakati huo Moyo akiwa na mwaka mmoja tuu, ilikua ngumu  kwangu lakini ililazimika kuwa hivyo japo roho iliniuma  kumuacha Mtoto wangu kwenye chumba kingine. 

    Basi, baada ya kumaliza kumlaza Moyo nilienda chumbani kwa  Anko Sanga, wakati huu tukiwa Mke na Mume, niliufunga ule  Mlango vizuri kisha funguo niliondoka nayo, nilikuwa  nikihofia sana juu ya Usalama wa binti yangu maana Anko Sanga  alikuwa hamtaki pale nyumbani. 

    Nilimkuta akiwa amekasirika, alinitaka nikae kitandani nami  nilifanya hivyo, nilishamzoea na hasira zake za mara kwa  mara. 

    “Miaka Mitatu kasoro sasa tokea tumefunga ndoa, sijawahi  kumuona Mama akija hapa, sipati mawasiliano naye. Napata  wakati mgumu sana kujua kama yupo hai au amekufa” Nilisema  ili tu kumhamisha kwenye kile alichokuwa anataka kuniambia  maana nikitaka kumkera basi nimuulize kuhusu Mama 

    “Hicho sio nilicho kuitia hapa Veronica, usinihamishe kwenye  reli” 

    “Kuna ubaya gani ukinijibu? sijatoka ndani kwa miaka hiyo  yote, siwasiliani na yeyote kwa kipindi hicho chote zaidi ya  Wewe” 

    “Sikia Veronica, nataka unipatie Mtoto wako nimpeleke kwa  Bibi yake, siwezi kukaa na damu ya Mtu mwingine” Alisema huku  akiweka sura ya Ukauzu, alikua ameniingizia kitu kipya kabisa  kwenye kichwa changu. 

    “Umchukue Moyo?” 

    “Ndio!” 

    “Bado hujaongea sawa sawa! Nikupe binti yangu? hilo  haliwezekani Sanga…nimefanya kila ulichotaka lakini kwa  binti yangu unavuka mipaka kabisa, siwezi kukupa binti yangu  hata siku moja na nisisikie unaongelea hilo jambo tena”

    Nilijikuta nikimkalipia Anko Sanga, ndio ilikua ni mara yangu  ya Kwanza kufanya hivyo, siku zote nilikuwa mtiifu kwake  lakini alipomgusia Mtoto wangu alinigusa pabaya sana. 

    “Unanipandishia sauti mimi?” 

    “Sikupi Mtoto Sanga labda uniuwe kwanza ndipo umchukue lakini  sio kwa hidhini yangu, hata Moyo akijua ulimchukua kutoka  kwangu atanilaani sana” Nilipomaliza hii kauli nilikutana na  kibao cha nguvu upande wa kushoto wa Shavu langu! 

    “Mpumbavu Mkubwa hivi unaniona mimi poyoyo kama huyo uliyezaa  nae? sasa nisikilize kwa makini umetaka hujataka Mtoto  ataondoka hapa full Stop” 

    “Endelea kunipiga hadi uniuwe lakini Kukupa Mtoto haiwezekani  kabisa Sanga” niliongea nikiwa ninalia, alinipiga kibao  kingine akanitupa chini kisha alianza kunikanyaga 

    “Shenzi taipu! Ujinga…wafanyie….wajinga wenzio…”  alinipiga sana siku hiyo tena bila kupumzika akawa  amenivimbisha jicho la upande wa kulia, alinisababishia  maumivu makali kwenye kiuno changu kutokana na kunikanyaga! 

    Nililia sana, nikiwa kama Mama sikutaka kabisa kutengana na  binti yangu alafu nisijuwe yuko wapi? Ushirikina wao sikutaka  wamuingizie Mwanangu, japo alisema anampeleka kwa Mama lakini  niliishiwa nguvu ya kuruhusu hilo kwanza Mama mwenyewe  alishakuwa adui yangu, kingine sikujua anaishi wapi na  sikupata kumuona kwa miaka hiyo yote. Alinipokonya funguo wa  chumba ambacho Moyo alikuwa amelala, nilijitahidi sana  kupambana na Sanga asimchukue Mtoto lakini sikuwa na mabavu  ya kupimana nae. 

    Niliishia kulia kwa uchungu, hii nyumba ya Anko Sanga ilikuwa  ya kifahari kubwa sana kiasi hata nifanyaje ilikuwa ni ngumu  kutoa sauti nje, ilikuwa imejitenga nje ya mji wa Arusha  ambako kulikuwa na mashamba yake. Usiku huo huo Anko Sanga  alimchukua Moyo, alinifungia kule chumbani nilipiga sana  kelele aniachie japo Binti yangu nipate kukaa nae lakini  haikusaidia kwani alidhamiria kuniumiza, kunitia kovu ndani  ya moyo wangu! 

    Nilimsikia Moyo akiwa analia ni wazi kuwa Sanga alimbeba  vibaya Moyo bila hata kujali kama alikuwa Mtoto mdogo  anayehitaji kunyenyekewa istoshe alikuwa usingizini, alilia  huku akiita ‘Mamaa! ‘Mamaaa!’ Alinitia Uchungu sana, baadaye  ukimya ulitawala nikaliona gari la Sanga likiwa linatoka  maana nyumba ilikuwa ya ghorofa hivyo nilipata nafasi ya  kuchunguza kutokea juu!

    Sikupata Usingizi, nilikesha ninalia na kusali ili Mungu  anitoe kwenye ile mitihani mizito iliyo migumu kwangu, 

    “Mungu nimekukosea nini mimi? kwanini unaniadhibu namna hii,  kwanini yote ya kwangu mimi tuu?” Nilijikuta nikipaza sauti  yangu ili kama Mungu amesinzia basi aamke aone jinsi  ninavyoteseka, Maisha yangu yote niliishi kwa kumtegemea yeye  na kuamiani lakini kwa kipindi kile niliona amenisahau  kabisa. 

    Sanga hakurudi hadi kulipo pambazuka, nilikuwa nimesimama  nikichungulia nje hadi jua lilipotoka, nilikuwa nikitazama  geti pamoja na barabara ili kuona kama kuna Mtu au gari  ilikuwa ikija, ndipo nilipoiona gari ndogo ya Anko Sanga aina  ya Rav4 New Model, nikasema ni lazima nilipize kwa  alichokifanya kwa binti yangu, kunitenga nae ni adhabu kubwa  sana kwangu! 

    Nilipata wazo la kumpiga na kitu kizito kichwani ili nimuuwe  kabisa maana nilikuwa nafanya kila kitu kwa ajili ya Mtoto  wangu lakini walishamchukua, nilifunga dirisha baada ya kuona  gari limeingia ndani, nilitafuta kitu kizito pale chumbani,  niliiona chupa ya soda niliichukuwa na kujificha nyuma ya  mlango ili akifungua tu nimtandike nayo, nilishajipanga kuwa  liwalo na liwe siwezi kuendelea kuwa Mtumwa. 

    Nilijibanza vizuri sana huku nikiamini kuwa ilikuwa ndio  nafasi yangu ya mwisho, nikiikosa hiyo nafasi naweza  nisiipate tena maana nikimkosa hapo anaweza akanigeuza kuwa  Mtumwa nisiye na uhuru tena, angeniona adui yake kwasababu  ningemlipiza kwa kumchukua Mtoto wangu. 

    Nilikaa kwa kitambo kidogo kabla ya kuanza kusikia milango  ikifunguliwa, kawaida alikuwa akitembea na rundo la funguo za  milango, nilikuwa nikizisikia kila alipokuwa akitembea,  nilisikia akija upande wangu ni wazi kuwa alikuwa akija  chumbani, nilivuta pumzi za kutosha kisha nilijiweka sawa  kumshambulia. Sikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo lakini  ilinibidi maana bila hivyo ningelikuwa kwenye wakati mgumu  sana. 

    Vishindo vya miguu vilikoma kwenye mlango wa Chumba nilichopo  kisha funguo ilianza kufungua kitasa taratibu, nilifumba  macho yangu ili nisione kitakacho fanyika pale, niliivuta ile  chupa sawa sawa, mlango ulipofunguliwa nikawa nyuma ya  Mlango, niliposikia akitembea kuingia ndani basi nikaiachia  ile chupa nikiwa nimefumba macho yangu ikatua kwenye kichwa  chake, nikasikia sauti iliyoshindwa kutoka sawa sawa kisha  nilisikia kitu kikianguka kama mzigo, Yes! nilikuwa nimelenga  shabaha yangu vizuri, ikabidi sasa nifumbue macho yangu!

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA NANE

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni riwaya za kuvutia soma riwaya bure

    6 Comments

    1. G shirima on May 19, 2025 11:54 am

      Sasa weka ya 8 tuendelee ma huondo

      Reply
    2. Warda on May 19, 2025 3:37 pm

      That is how ,,unatakiwa uwe binti vero😊

      Reply
      • Salma Ibrahim on May 19, 2025 5:39 pm

        Yaani admin fanya kututunuku ya 8 please na mvua hizi mambo yaende mukidemukide

        Reply
    3. Wallace on May 19, 2025 5:08 pm

      Uncle Sanga Mnyakyusa sio ahahahaha

      Reply
      • Salma Ibrahim on May 19, 2025 5:40 pm

        Ni mkinga Hilo jina lake ni mkinga halisi

        Reply
    4. Adam on May 19, 2025 5:44 pm

      Angalau Ningejua aliyedondoka Alikuwa Anko Sanga au Mama Yake Sema Na Ya Nane Naiomba Leoeo

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi May 19, 2025

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Saba-07)

    Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Saba Ile simu ilikuwa ndogo tu yaani ya…

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Sita-06)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tano-05)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Nne-04)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.