Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Tatuย
“Ndio ishakuwa hiyo hairudi nyuma, akitaka unampa atakavyo”ย
Tulicheka kwa pamoja kuashiria tulikuwa tumefurahi wote kwaย kilichotokea. Nikawa nahisi raha ile ya kusex na Jonas hataย nikiwa darasani nililoa kila nilipomtazama, naye alihisiย hilo. Endeleaย
SEHEMU YA NNE
Nilipotoka darasani alinifuata na kunipa mate na kunipapasaย lakini hofu yangu ikawa kwenye kukeketwa, nikasema sitampaย mapenzi Jonas hadi tulewe.ย
Ikawa ndio mchezo, tunapiga pombe kwanza ndio tunaenda kusexย akawa ananipa pesa za matumizi mara mbili ya mwanzo, nikawaย namtumia Mama zimsaidie hata hivyo baadae alizikataa hukuย akiniambia kuwa hakuwa na shida ya pesa.
Nilihisi ni vile aliona aibu tu kupokea zile pesa, nikawaย nazitumia tu, hata zile Elfu 50 alizonipa Anko Sangaย nilizitumbua chuoni mpaka marafiki zangu walishangaa,ย nilianza kuipenda pombe maana nilikuwa nikiitegemea kwenyeย kusex.ย
“Siku hizi Veronica yupo vizuri anapiga maji hatari,ย anatupita hata sisi wazoefu” yalikuwa ni maneno ya Sofiaย akimwambia Konzo.ย
Nilianza kuhisi nina ujauzito, nilitapika hovyo hata Wanachuoย wengine walishtuka na minong’ono ikawa mingi kuwa nina mimbaย
“Chuo kizima wanajua una mimba Veronica, hukuwa muangalifu” “Wanasema nina mimba?”ย
“Ndio, tena taarifa zipo kila kona. Sijui kama Jonasย hazijamfikia”ย
“Unasema sikuwa mwangalifu hivi nasex nikiwa nimelewa huoย uangalifu unatokea wapi?”ย
“Itabidi umueleze mapema Jonas au unataka kuitoa juu juu?” “Kutoa mimba naogopa Konzo, ngoja niongee na Jonas kwanza”ย
Nilimtafuta Jonas na niliongea nae akaniuliza ninawaza niniย kuhusu ujauzito,nilimueleza kuwa sikufikiria kuhusu kuitoaย ile mimba maana nilikuwa muoga, alifurahi kisha akaniambiaย ataileaย
“Kuhusu kusoma Jonas?”ย
“Utasomaje na mimba my love?”ย
“Itakuwaje Naogopa Mama akijua nina mimba jonas”ย
“Twende kwenu kwa Mama yako mengine niachie mimi” Alisema, naย kunihakikishia kuwa haitakuwa tatizo, nilimjua jinsi Mamaย yangu alivyonisihi kusoma.ย
Kila nilipo ongea nae aliniuliza jinsi masomo yalivyokuwaย yakiendelea, nilimuhakikishia kuwa nitatimiza ndoto zangu naย za kwake, sasa akisikia nina mimba sijui itakuwaje.ย
Nilianza kuwaza, sikuwa tena na muda wa kufuatilia masomo,ย Jonas alinichukua nikawa naishi kwake, alikuwa na nyumbaย aliyojengewa na Baba yake! Wazazi wake walikuwa huko Taboraย baada ya kustaafu kazi ya Kuitumikia nchi kwenye vitengoย nyeti vya Serikali, wakamjengea nyumba na kumpa uhuru waย kubakia Dar.ย
“Nyumba yenu ni nzuri Jonas, wazazi wako wakijua unakaa naย Mwanamke watakuelewa?”ย
“Achana na hofu zisizo na msingi Veronica, nimeamua kuwa naย wewe hivyo hakuna atakaye nipinga kwenye maamuzi yangu!”ย Jonas alikuwa ni Mwanaume mwenye misimamo yake, alitaka niweย huru kwenye kila jambo!ย
“Kuanzia leo sitaki unywe pombe, Utaharibu ujauzito” Alisema,ย nikaacha kabisa kunywa pombe, bado hofu yangu ya kukeketwaย ilinitesa sana hadi nikamwambia Mama kuwa najihisi nikoย tofauti na Wanawake wengine, Mama akaniambia Wao ndio wakoย tofauti na mimi kwasababu mimi nipo kamili.ย
Kumbe nyakati zote hizi, Mama na Anko Sanga walikuwaย wamekamilisha mambo yao, ile shuka yenye damu ilikuwa kamaย sadaka ya mambo ya Anko Sanga kufanikiwa, aliipeleka ileย shuka kwa mganga wakapata pesa na akabadirisha Maisha ya Mamaย hata wakati namwambia nimtumie pesa zimsaidie hakuzihitajiย sababu alikuwa nazo tena za kutosha tuu!ย
Tulipanga safari ya kwenda Arusha, Ili kumtambulisha Jonasย kwa Mama yangu Mzazi,ย
Tulipofika Arusha nilijuwa naenda kwenye Uwanja wa vita yaย pili ya Dunia, ningefanyaje na nina mimba? ilikuwa ni lazimaย nimueleze Mama, aliponiona alifurahi kuniona lakini ujioย wangu ulimtatanisha baada ya Kumuona Jonasย
“Huyu ni nani?” aliniuliza kwa Kilugha cha kwetu, lengo lakeย Jonas asijue ameuliza niniย
“Ni mgeni Mama nitakutambulisha nyumbani”ย
“Veronica! Veronica! haya” Alisema, Mama huku tukiongozaย kuelekea nyumbani, Mama alihisi tu kuwa niliyekuja nae hakuwaย mgeni wa kawaida.ย
Tuliongea mambo machache kabla ya kuniuliza kuhusu chuo, badoย nilimsistiza kuwa tutaongea nyumbani. Tulipofika nyumbaniย nilishangaa mazingira jinsi yalivyo badirika, Nyumbaย ilifanyiwa ukarabati, ilikuwa imeng’ara sana, sikutakaย kumuuliza Mama japo kulikuwa na mabadiriko mengi sana.
“Karibu Jonas!” Nilimkaribisha kipenzi changu, Mamaย alinitazama kwa jicho la husuda hadi nikajiuliza maraย mbilimbili.ย
“Mh! sio kwa mabadiliko haya Mama”ย
Hakunijibu, nafikiri alisubiria kuona utambulisho wa Jonas,ย nilianza kumtambulisha yule Mwanaume kwa Mama, alinisikilizaย nilipomaliza aliniita njeย
“Umesema yule ni nani?” Aliniuliza Mama baada ya kuniita nje,ย ni kama hakufurahishwa na utambulisho ule. Alionekana kuwa naย hasiraย
“Ni mume wangu mtarajiwa Mama” nilisema kwa kutimiza wajibuย tu wa kumjibu Mama yangu lakini alikuwa kwenye hasiraย
“Veronica nilikupeleka chuo ukasome na sio kuhangaika naย wanaume, kwahiyo hakuna chuo tena?”ย
“Ndio Mama, sasa ni Mjamzito?”ย
“Unasemaje? Mja nini? Gharama zote ni kazi bure” aliongeaย Mama kisha alinivuta nyweleย
“Mama unaniumiza Aaaah”ย
“Mjinga wewe! Veronica umefanya nini”ย
Alinisema sana yaani hadi nilijisikia hovyo nikaanzaย kutapika, Jonas alivyosikia natapika alinifuata iliย kunihudumia, Mama akampiga kikumbo wakati wanapishanaย Mlangoni, Jonas akamuomba msamaha Mama kwa kitendo kileย lakini Mama hakujibu aliingia ndani.ย
“Upo salama Veronica?” alinishika huku nikiendelea kutapika,ย uwepo wa Jonas ulinifanya nijisikie vizuri kila nilipomtazamaย nilijihisi ni mwenye bahati, alikuwa akijua jinsi ya kumjaliย Mwanamke.ย
Alikaa na mimi hadi nilipomaliza kutapika, alinipelekaย sebleni kisha akanilaza kwenye kochi, akaelekea Jikoni ambakoย alisikia purukushani, alipofika alimkuta Mama yanguย
“Samahani Mama, naweza kupata Uji na limao?” alimuuliza Mamaย kwa heshima zoteย
“Uji na Limao? ulipokuwa unampachika ujauzito uliniombaย ruhusa?” Mama alijibu kwa jaziba sana nilikuwa nikisikiaย maongezi yao, sikuwa na nguvu ya kuongea kabisa, nilimjuaย Mama yangu jinsi alivyo Mkaksiย
“Hapana Mama, Veronica hajisikii vizuri ndio maanaย nimekuuliza hivyo. Nisamehe kama nimekukwaza hata hivyoย ninaweza nikatengeneza mwenyewe”ย
“Hivi ndivyo ambavyo watoto wajeuri huongea, utengeneze ujiย kwenye nyumba za watu ndio adabu uliyofundishwa? Huyuย Veronica anakupa jeuri sana sasa tutaona Kama kunaย kitakachoendelea”ย
“Unamaanisha nini Mama?”ย
“Utanielewa taratibu” Mama aliondoka, Jonas alibakia akiwaย haelewi yale Maneno ya Mama yalitokana na nini, basiย alipoangaza aliona jiko la gesi akaliwasha na kuweka Maji,ย akatafuta unga akaweka kwenye Maji kisha akaanza mapishiย yake.ย
Akaenda kununua Limao gengeni akaweka kwenye uji kishaย akaniletea, nilimuonea huruma jinsi alivyonijali, alikuwaย akivuja jasho, rangi yake nyeupe iligeuka kuwa nyekundu.ย
“Hujazoea haya Maisha Jonas?” Nilimuuliza baada ya kupataย nguvu, uji ulinisaidia maana nilitapika sana na kupoteza majiย na chakula nilichokuwa nimekula.ย
“Hata kama sijazoea napaswa kuzoea sababu ndio mazingiraย niliyopo Veronica”ย
“Unateseka kisa mimi Jonas?”ย
“Sio wewe tu, bali na Mtoto aliye tumboni” Tulijikutaย tukicheka na kufurahi hadi usiku ulipoingia, Umeme ulizimikaย usiku kukawa na giza, Mama alikuwa amejifungia chumbaniย kwake.ย
“Hatuwezi kulala hapa na mbu hivi Veronica, utaugua Malari naย Mama mjamzito hapaswi kung’atwa na Mbu” alisema Jonas hukuย akinishauri nikagonge kwenye mlango wa Mamaย
“Unapenda kusikia maneno yake ya kukera?”ย
“Hata kama ana maneno kiasi gani, ni lazima ulale ndani yaย chandarua. Kama itawezekana ukalale nae alafu mimi nitalalaย hapa”
“Oooooh Mungu wangu” nilinyanyuka na kuelekea kugonga Mlango,ย vyumba vingine vilikuwa vimefungwa.ย
Nilimgongea Mama zaidi ya mara tatu, mara ya nne alifunguaย mlangoย
“Unasemaje?” aliuliza kwa kisirani hadi nikaogopa. “Mama naomba funguo ya chumba kimoja ili nilale na Jonas”ย
“Ulale na Jonas? hivi una akili wewe? nyumba yangu ulale naย Mwanaume?” Nilikaa kimya kumsikiliza maana ningemjibuย angeweza hata kutufukuza. Alipomaliza kuongea aliingiaย chumbani kwake, nilisimama hadi nikakata tamaa ila wakatiย naondoka nilisikia mlango ukifunguliwa na ufunguo ukatupwaย chini kisha Mlango ukafungwa tena.ย
Niliwasha tochi ya simu na kuuokota bila kujua utakuwaย unafungua mlango gani kati ya Milango ile minne, Jonasย alinisaidia kujaribu hadi tulipopata chumba husika.ย
Mle kulikuwa na kitanda nilichokuwa nakilalia zamani, vituย vingi vilikuwa ni vile nilivyo viacha. Kulikuwa na vumbi,ย tulifanya usafi mdogo usiku uleule, tulipomaliza tukawa hoiย tumechoka.ย
“Inabidi tukaoge” Alisema Jonas, ni kweli maana jashoย lilikuwa limetutapakaa mnoย
“Sasa inabidi nikaanze ndipo ukaoge wewe maana Mamaย akitusikia itakuwa shida”ย
“Sawa nakusubiria” Nilianza kwenda kuoga, niliporudi nayeย alielekea kuoga. Kutokana na uchovu wa safari na ile mimbaย nilijikuta nikizama usingizini, Jonas hakurudi kabisa hadiย majira ya saa 8 usiku niliposhtuka.ย
Nilipoangaza sikumuona kabisa Jonas, nilipapasa bahati nzuriย umeme ulikuwa umerudi niliamka na kuwasha taa.ย
Sikupata kumuona wala kumsikia, nilichanganikiwa, ikabidiย nikamuangalie sebleni, nilimkuta akiwa amelala sebleni.ย Nilimuamsha kisha tulielekea Chumbaniย
“Unalala pale na mbu wale Jonas?”ย
“sijui hata nimewezaje kulala pale Veronica, nakumbuka maraย ya mwisho nilienda bafuni kuoga, nilijikuta nikipataย kizunguzungu tu sikujua kilichoendelea hadi nimekuta pale”
“Mh! kutoka bafuni hadi Sebleni?” kiukweli ilichekesha Mtuย atoke Bafuni ambapo ilikuwa ikitazamana na chumba chetuย aelekee Sebleni ambako ni mbaliย
“Usinichekeshe Usiku huu” Nilisemaย
“Ni kweli Veronica sijui nimefikaje kule” ilikuwa kamaย hadithi iliyosadikiwa tu huku ukweli wa tukio ukibakia kuwaย wa kuchekesha.ย
Basi tulilala hadi asubuhi kulipo pambazuka, mimi niliamkaย kwasababu nililala vizuri lakini Jonas nilimuacha akiwa badoย amelala, nilimgongea Mama mara kadhaa lakini sikusikia majibuย kutoka kwake, ndipo nikaelekea nje. Kulikuwa na jirani mmojaย alikuwa akifanya usafi nje, alikuwa akinifahamu maanaย nimeishi pale kwa miaka mingi sana. Aliponiona alifurahiย alafu akanisalimia kwa mbwembwe zote.ย
“Nimekusikia ukimuita Mama yako!”ย
“Ndio, lakini sipati majibu”ย
“Ametoka mapema sana, gari ndogo imemchukua Alfajiri” “Eeh! ameenda wapi tena?”ย
“Ina maana ametoka bila kukuaga binti yake?” Nilipoonaย ananiuliza maswali ya kimbea nilimuaga na kuelekea ndani.ย
Niliandaa chai ili Jonas akiamka ale maana tulilala bila kulaย alafu nilikuwa nikihisi njaa sana, nilipomuangalia nilimkutaย akiwa amelala sikutaka kumuamsha, alipoamka alinikuta sebleniย nikiwa nimekaa. Tulijumuika kunywa chai pamoja baada yaย kumaliza tulirudi chumbani kwetu, hatukumuona Mama kwa zaidiย ya siku saba pasipo kujua alienda wapi, hakutaka kabisaย kupokea simuย
“Ni mtu mzima huyo anajua anachokifanya” Alisema Jonas “Sikatai lakini ni maisha gani haya? tuondoke basi”ย
“Lengo la kuja huku ni kumpa taarifa Mama lakini hatuweziย kuondoka bila yeye kiridhia, Veronica mpenzi tuvumilie tuย hadi pale hasira zake zitakapoisha”ย
“Kwanini Mama ananifanyia hivi mimi, kama hakunizaa yeye?”ย nilijiuliza baada ya kukumbuka tukio la kubakwa na Anko Sangaย ambapo Kwa maelezo ya Mama ilionesha kuwa alikuwa akijua kilaย kitu .
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
17 Comments
Fupii
Nzuri Ila fupi
Ya leo Ni Fupi Saana
Too short๐๐ฅฒ
https://shorturl.fm/a0B2m
https://shorturl.fm/j3kEj
https://shorturl.fm/A5ni8
https://shorturl.fm/68Y8V
https://shorturl.fm/bODKa
https://shorturl.fm/m8ueY
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/FIJkD
https://shorturl.fm/a0B2m
https://shorturl.fm/6539m
https://shorturl.fm/68Y8V
https://shorturl.fm/FIJkD
https://shorturl.fm/j3kEj