Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Nne-04)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tatu-03)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Pili-02)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Nne-04)
    Hadithi

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Nne-04)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 15, 20253 Comments9 Mins Read545 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Tatu 

    “Ndio ishakuwa hiyo hairudi nyuma, akitaka unampa atakavyo” 

    Tulicheka kwa pamoja kuashiria tulikuwa tumefurahi wote kwa  kilichotokea. Nikawa nahisi raha ile ya kusex na Jonas hata  nikiwa darasani nililoa kila nilipomtazama, naye alihisi  hilo. Endelea 

    SEHEMU YA NNE

    Nilipotoka darasani alinifuata na kunipa mate na kunipapasa  lakini hofu yangu ikawa kwenye kukeketwa, nikasema sitampa  mapenzi Jonas hadi tulewe. 

    Ikawa ndio mchezo, tunapiga pombe kwanza ndio tunaenda kusex  akawa ananipa pesa za matumizi mara mbili ya mwanzo, nikawa  namtumia Mama zimsaidie hata hivyo baadae alizikataa huku  akiniambia kuwa hakuwa na shida ya pesa.

    Nilihisi ni vile aliona aibu tu kupokea zile pesa, nikawa  nazitumia tu, hata zile Elfu 50 alizonipa Anko Sanga  nilizitumbua chuoni mpaka marafiki zangu walishangaa,  nilianza kuipenda pombe maana nilikuwa nikiitegemea kwenye  kusex. 

    “Siku hizi Veronica yupo vizuri anapiga maji hatari,  anatupita hata sisi wazoefu” yalikuwa ni maneno ya Sofia  akimwambia Konzo. 

    Nilianza kuhisi nina ujauzito, nilitapika hovyo hata Wanachuo  wengine walishtuka na minong’ono ikawa mingi kuwa nina mimba 

    “Chuo kizima wanajua una mimba Veronica, hukuwa muangalifu” “Wanasema nina mimba?” 

    “Ndio, tena taarifa zipo kila kona. Sijui kama Jonas  hazijamfikia” 

    “Unasema sikuwa mwangalifu hivi nasex nikiwa nimelewa huo  uangalifu unatokea wapi?” 

    “Itabidi umueleze mapema Jonas au unataka kuitoa juu juu?” “Kutoa mimba naogopa Konzo, ngoja niongee na Jonas kwanza” 

    Nilimtafuta Jonas na niliongea nae akaniuliza ninawaza nini  kuhusu ujauzito,nilimueleza kuwa sikufikiria kuhusu kuitoa  ile mimba maana nilikuwa muoga, alifurahi kisha akaniambia  atailea 

    “Kuhusu kusoma Jonas?” 

    “Utasomaje na mimba my love?” 

    “Itakuwaje Naogopa Mama akijua nina mimba jonas” 

    “Twende kwenu kwa Mama yako mengine niachie mimi” Alisema, na  kunihakikishia kuwa haitakuwa tatizo, nilimjua jinsi Mama  yangu alivyonisihi kusoma. 

    Kila nilipo ongea nae aliniuliza jinsi masomo yalivyokuwa  yakiendelea, nilimuhakikishia kuwa nitatimiza ndoto zangu na  za kwake, sasa akisikia nina mimba sijui itakuwaje. 

    Nilianza kuwaza, sikuwa tena na muda wa kufuatilia masomo,  Jonas alinichukua nikawa naishi kwake, alikuwa na nyumba  aliyojengewa na Baba yake! Wazazi wake walikuwa huko Tabora baada ya kustaafu kazi ya Kuitumikia nchi kwenye vitengo  nyeti vya Serikali, wakamjengea nyumba na kumpa uhuru wa  kubakia Dar. 

    “Nyumba yenu ni nzuri Jonas, wazazi wako wakijua unakaa na  Mwanamke watakuelewa?” 

    “Achana na hofu zisizo na msingi Veronica, nimeamua kuwa na  wewe hivyo hakuna atakaye nipinga kwenye maamuzi yangu!”  Jonas alikuwa ni Mwanaume mwenye misimamo yake, alitaka niwe  huru kwenye kila jambo! 

    “Kuanzia leo sitaki unywe pombe, Utaharibu ujauzito” Alisema,  nikaacha kabisa kunywa pombe, bado hofu yangu ya kukeketwa  ilinitesa sana hadi nikamwambia Mama kuwa najihisi niko  tofauti na Wanawake wengine, Mama akaniambia Wao ndio wako  tofauti na mimi kwasababu mimi nipo kamili. 

    Kumbe nyakati zote hizi, Mama na Anko Sanga walikuwa  wamekamilisha mambo yao, ile shuka yenye damu ilikuwa kama  sadaka ya mambo ya Anko Sanga kufanikiwa, aliipeleka ile  shuka kwa mganga wakapata pesa na akabadirisha Maisha ya Mama  hata wakati namwambia nimtumie pesa zimsaidie hakuzihitaji  sababu alikuwa nazo tena za kutosha tuu! 

    Tulipanga safari ya kwenda Arusha, Ili kumtambulisha Jonas  kwa Mama yangu Mzazi, 

    Tulipofika Arusha nilijuwa naenda kwenye Uwanja wa vita ya  pili ya Dunia, ningefanyaje na nina mimba? ilikuwa ni lazima  nimueleze Mama, aliponiona alifurahi kuniona lakini ujio  wangu ulimtatanisha baada ya Kumuona Jonas 

    “Huyu ni nani?” aliniuliza kwa Kilugha cha kwetu, lengo lake  Jonas asijue ameuliza nini 

    “Ni mgeni Mama nitakutambulisha nyumbani” 

    “Veronica! Veronica! haya” Alisema, Mama huku tukiongoza  kuelekea nyumbani, Mama alihisi tu kuwa niliyekuja nae hakuwa  mgeni wa kawaida. 

    Tuliongea mambo machache kabla ya kuniuliza kuhusu chuo, bado  nilimsistiza kuwa tutaongea nyumbani. Tulipofika nyumbani  nilishangaa mazingira jinsi yalivyo badirika, Nyumba  ilifanyiwa ukarabati, ilikuwa imeng’ara sana, sikutaka  kumuuliza Mama japo kulikuwa na mabadiriko mengi sana.

    “Karibu Jonas!” Nilimkaribisha kipenzi changu, Mama  alinitazama kwa jicho la husuda hadi nikajiuliza mara  mbilimbili. 

    “Mh! sio kwa mabadiliko haya Mama” 

    Hakunijibu, nafikiri alisubiria kuona utambulisho wa Jonas,  nilianza kumtambulisha yule Mwanaume kwa Mama, alinisikiliza  nilipomaliza aliniita nje 

    “Umesema yule ni nani?” Aliniuliza Mama baada ya kuniita nje,  ni kama hakufurahishwa na utambulisho ule. Alionekana kuwa na  hasira 

    “Ni mume wangu mtarajiwa Mama” nilisema kwa kutimiza wajibu  tu wa kumjibu Mama yangu lakini alikuwa kwenye hasira 

    “Veronica nilikupeleka chuo ukasome na sio kuhangaika na  wanaume, kwahiyo hakuna chuo tena?” 

    “Ndio Mama, sasa ni Mjamzito?” 

    “Unasemaje? Mja nini? Gharama zote ni kazi bure” aliongea  Mama kisha alinivuta nywele 

    “Mama unaniumiza Aaaah” 

    “Mjinga wewe! Veronica umefanya nini” 

    Alinisema sana yaani hadi nilijisikia hovyo nikaanza  kutapika, Jonas alivyosikia natapika alinifuata ili  kunihudumia, Mama akampiga kikumbo wakati wanapishana  Mlangoni, Jonas akamuomba msamaha Mama kwa kitendo kile  lakini Mama hakujibu aliingia ndani. 

    “Upo salama Veronica?” alinishika huku nikiendelea kutapika,  uwepo wa Jonas ulinifanya nijisikie vizuri kila nilipomtazama  nilijihisi ni mwenye bahati, alikuwa akijua jinsi ya kumjali  Mwanamke. 

    Alikaa na mimi hadi nilipomaliza kutapika, alinipeleka  sebleni kisha akanilaza kwenye kochi, akaelekea Jikoni ambako  alisikia purukushani, alipofika alimkuta Mama yangu 

    “Samahani Mama, naweza kupata Uji na limao?” alimuuliza Mama  kwa heshima zote 

    “Uji na Limao? ulipokuwa unampachika ujauzito uliniomba  ruhusa?” Mama alijibu kwa jaziba sana nilikuwa nikisikia maongezi yao, sikuwa na nguvu ya kuongea kabisa, nilimjua  Mama yangu jinsi alivyo Mkaksi 

    “Hapana Mama, Veronica hajisikii vizuri ndio maana  nimekuuliza hivyo. Nisamehe kama nimekukwaza hata hivyo  ninaweza nikatengeneza mwenyewe” 

    “Hivi ndivyo ambavyo watoto wajeuri huongea, utengeneze uji  kwenye nyumba za watu ndio adabu uliyofundishwa? Huyu  Veronica anakupa jeuri sana sasa tutaona Kama kuna  kitakachoendelea” 

    “Unamaanisha nini Mama?” 

    “Utanielewa taratibu” Mama aliondoka, Jonas alibakia akiwa  haelewi yale Maneno ya Mama yalitokana na nini, basi  alipoangaza aliona jiko la gesi akaliwasha na kuweka Maji,  akatafuta unga akaweka kwenye Maji kisha akaanza mapishi  yake. 

    Akaenda kununua Limao gengeni akaweka kwenye uji kisha  akaniletea, nilimuonea huruma jinsi alivyonijali, alikuwa  akivuja jasho, rangi yake nyeupe iligeuka kuwa nyekundu. 

    “Hujazoea haya Maisha Jonas?” Nilimuuliza baada ya kupata  nguvu, uji ulinisaidia maana nilitapika sana na kupoteza maji  na chakula nilichokuwa nimekula. 

    “Hata kama sijazoea napaswa kuzoea sababu ndio mazingira  niliyopo Veronica” 

    “Unateseka kisa mimi Jonas?” 

    “Sio wewe tu, bali na Mtoto aliye tumboni” Tulijikuta  tukicheka na kufurahi hadi usiku ulipoingia, Umeme ulizimika  usiku kukawa na giza, Mama alikuwa amejifungia chumbani  kwake. 

    “Hatuwezi kulala hapa na mbu hivi Veronica, utaugua Malari na  Mama mjamzito hapaswi kung’atwa na Mbu” alisema Jonas huku  akinishauri nikagonge kwenye mlango wa Mama 

    “Unapenda kusikia maneno yake ya kukera?” 

    “Hata kama ana maneno kiasi gani, ni lazima ulale ndani ya  chandarua. Kama itawezekana ukalale nae alafu mimi nitalala  hapa”

    “Oooooh Mungu wangu” nilinyanyuka na kuelekea kugonga Mlango,  vyumba vingine vilikuwa vimefungwa. 

    Nilimgongea Mama zaidi ya mara tatu, mara ya nne alifungua  mlango 

    “Unasemaje?” aliuliza kwa kisirani hadi nikaogopa. “Mama naomba funguo ya chumba kimoja ili nilale na Jonas” 

    “Ulale na Jonas? hivi una akili wewe? nyumba yangu ulale na  Mwanaume?” Nilikaa kimya kumsikiliza maana ningemjibu  angeweza hata kutufukuza. Alipomaliza kuongea aliingia  chumbani kwake, nilisimama hadi nikakata tamaa ila wakati  naondoka nilisikia mlango ukifunguliwa na ufunguo ukatupwa  chini kisha Mlango ukafungwa tena. 

    Niliwasha tochi ya simu na kuuokota bila kujua utakuwa  unafungua mlango gani kati ya Milango ile minne, Jonas  alinisaidia kujaribu hadi tulipopata chumba husika. 

    Mle kulikuwa na kitanda nilichokuwa nakilalia zamani, vitu  vingi vilikuwa ni vile nilivyo viacha. Kulikuwa na vumbi,  tulifanya usafi mdogo usiku uleule, tulipomaliza tukawa hoi  tumechoka. 

    “Inabidi tukaoge” Alisema Jonas, ni kweli maana jasho  lilikuwa limetutapakaa mno 

    “Sasa inabidi nikaanze ndipo ukaoge wewe maana Mama  akitusikia itakuwa shida” 

    “Sawa nakusubiria” Nilianza kwenda kuoga, niliporudi naye  alielekea kuoga. Kutokana na uchovu wa safari na ile mimba  nilijikuta nikizama usingizini, Jonas hakurudi kabisa hadi  majira ya saa 8 usiku niliposhtuka. 

    Nilipoangaza sikumuona kabisa Jonas, nilipapasa bahati nzuri  umeme ulikuwa umerudi niliamka na kuwasha taa. 

    Sikupata kumuona wala kumsikia, nilichanganikiwa, ikabidi  nikamuangalie sebleni, nilimkuta akiwa amelala sebleni.  Nilimuamsha kisha tulielekea Chumbani 

    “Unalala pale na mbu wale Jonas?” 

    “sijui hata nimewezaje kulala pale Veronica, nakumbuka mara  ya mwisho nilienda bafuni kuoga, nilijikuta nikipata  kizunguzungu tu sikujua kilichoendelea hadi nimekuta pale”

    “Mh! kutoka bafuni hadi Sebleni?” kiukweli ilichekesha Mtu  atoke Bafuni ambapo ilikuwa ikitazamana na chumba chetu  aelekee Sebleni ambako ni mbali 

    “Usinichekeshe Usiku huu” Nilisema 

    “Ni kweli Veronica sijui nimefikaje kule” ilikuwa kama  hadithi iliyosadikiwa tu huku ukweli wa tukio ukibakia kuwa  wa kuchekesha. 

    Basi tulilala hadi asubuhi kulipo pambazuka, mimi niliamka  kwasababu nililala vizuri lakini Jonas nilimuacha akiwa bado  amelala, nilimgongea Mama mara kadhaa lakini sikusikia majibu  kutoka kwake, ndipo nikaelekea nje. Kulikuwa na jirani mmoja  alikuwa akifanya usafi nje, alikuwa akinifahamu maana  nimeishi pale kwa miaka mingi sana. Aliponiona alifurahi  alafu akanisalimia kwa mbwembwe zote. 

    “Nimekusikia ukimuita Mama yako!” 

    “Ndio, lakini sipati majibu” 

    “Ametoka mapema sana, gari ndogo imemchukua Alfajiri” “Eeh! ameenda wapi tena?” 

    “Ina maana ametoka bila kukuaga binti yake?” Nilipoona  ananiuliza maswali ya kimbea nilimuaga na kuelekea ndani. 

    Niliandaa chai ili Jonas akiamka ale maana tulilala bila kula  alafu nilikuwa nikihisi njaa sana, nilipomuangalia nilimkuta  akiwa amelala sikutaka kumuamsha, alipoamka alinikuta sebleni  nikiwa nimekaa. Tulijumuika kunywa chai pamoja baada ya  kumaliza tulirudi chumbani kwetu, hatukumuona Mama kwa zaidi  ya siku saba pasipo kujua alienda wapi, hakutaka kabisa  kupokea simu 

    “Ni mtu mzima huyo anajua anachokifanya” Alisema Jonas “Sikatai lakini ni maisha gani haya? tuondoke basi” 

    “Lengo la kuja huku ni kumpa taarifa Mama lakini hatuwezi  kuondoka bila yeye kiridhia, Veronica mpenzi tuvumilie tu  hadi pale hasira zake zitakapoisha” 

    “Kwanini Mama ananifanyia hivi mimi, kama hakunizaa yeye?”  nilijiuliza baada ya kukumbuka tukio la kubakwa na Anko Sanga  ambapo Kwa maelezo ya Mama ilionesha kuwa alikuwa akijua kila  kitu .

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    riwaya za kuvutia simulizi kijiweni simulizi za kijasusi simulizi za mapenzi soma riwaya bure

    3 Comments

    1. G shirima on May 15, 2025 6:42 pm

      Fupii

      Reply
    2. Rahim Rashid yusuph on May 15, 2025 7:14 pm

      Nzuri Ila fupi

      Reply
    3. Adam on May 15, 2025 7:36 pm

      Ya leo Ni Fupi Saana

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi May 15, 2025

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Nne-04)

    Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Tatu  “Ndio ishakuwa hiyo hairudi nyuma, akitaka unampa…

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tatu-03)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Pili-02)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Kwanza-01)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.