Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Saba
Vishindo vya miguu vilikoma kwenye mlango wa Chumba nilichopo kisha funguo ilianza kufungua kitasa taratibu, nilifumba macho yangu ili nisione kitakacho fanyika pale, niliivuta ile chupa sawa sawa, mlango ulipofunguliwa nikawa nyuma ya Mlango, niliposikia akitembea kuingia ndani basi nikaiachia ile chupa nikiwa nimefumba macho yangu ikatua kwenye kichwa chake, nikasikia sauti iliyoshindwa kutoka sawa sawa kisha nilisikia kitu kikianguka kama mzigo, Yes! nilikuwa nimelenga shabaha yangu vizuri, ikabidi sasa nifumbue macho yangu. Endelea
SEHEMU YA NANE
Kumbe wakati Jonas ananitafuta mimi, Anko Sanga na Mama walikuwa wakimfwatilia pia wakiamini ndio tatizo kwenye mipango yao, kupitia simu ya Konzo aliyonipigia walifanikiwa kumkamata Konzo, walimtumia kama Mtego ili wamnase Jonas.
Mama nae alikuwa akiishi nje ya Mji kama ambavyo Anko Sanga alikuwa akiishi tena kwenye jumba la kifahari sana, walimchukua Konzo na kwenda nae huko nje ya mji ambako Mama alikuwa akiishi. Konzo alilazimishwa kuwa mtego wa kumnasa Jonas ambaye kwa kipindi hicho alikuwa Ndani ya Jiji la Arusha kunitafuta mimi na Mtoto.
Konzo alifanya kama ambavyo alilazimishwa, alimpigia simu Jonas wakutane nje ya Mji akimwambia kuwa ana taarifa zinazonihusu, hivyo wakafanikiwa kumpata Jonas, walitumia nguvu zao za kishirikina na kuwapumbaza Konzo na Jonas, Mama akamchukua Konzo na kwenda kumtupa huko Porini, Jonas akamfanya kuwa Mwanaume wake.
Hivyo, Jonas na Mama yangu Mzazi wakawa wanaishi kama Mume na Mke kama ambavyo Mimi na Anko Sanga tulikuwa tukiishi, wazo la Jonas la kunitafuta lilifutika kabisa akawa mtumwa kwenye penzi la Mama yangu, walifanya hivi ili waendelee kuvuna pesa na kuishi maisha ya kitajiri, mimi ndio nilikuwa mtaji wao Mkubwa.
Hakukuwa na Mtu mwingine ambaye angeliweza kunikomboa au kumkomboa Jonas kutoka kwa Mama yangu, ushetani wao ulikuwa mbaya sana, tamaa ya pesa iliwafanya wageuke kuwa Wanyama.
NYUMBANI KWA ANKO SANGA
Nilikuwa nikihema juu juu kama Mbwa aliyepona kutoka kwenye umauti, chupa kilikuwa sakafuni kikiwa kimevunjika, woga ulinijaa na kilichonishangaza zaidi ni Mtu aliye chini pale, nilimgeuza.
Hakuwa Anko Sanga bali ni dereva wake aliyeitwa James, ndiye aliyekuwa akimtuma mara nyingi aje nyumbani anapokuwa amesafiri
“OHHH! Mungu wangu” nilisema nikiwa nimeweka Kiganja changu mdomoni wakati mkono mwingine ukiwa kichwani, nilianza kumuamsha James ili aamke maana kama Anko Sanga atakuja akimuona James yupo katika hali ile pengine angenifungia kabisa chumbani, nilimwamsha kwa muda mrefu lakini hakuamka, nilianza kuhofia kwa kujua nimemuuwa.
Nilienda dirishani kuchungulia kama Anko Sanga alikuwa akija au Mtu nwingine yeyote lakini hakukuwa hata na dalili ya Mtu kuja pale nyumbani. Nilimburuza James hadi bafuni, nilirudi na kufuta damu iliyokuwa sakafuni, niliondoa vipande vya vyupa pale sakafuni kisha nilienda bafuni.
Nilimmwagia maji ya baridi ili aamke, sikuwa na tatizo na James kabisa, alikuwa akiongea na mimi vizuri hivyo kumsababishia umauti lilikuwa jambo baya kwangu, ndipo nilipogundua kuwa James alikuwa amepoteza maisha.
Niliwaza nifanye nini, nikapata wazo la kutoroka pale ndani, sijui hata nilikuwa nikichelewa nini wakati lengo langu miaka yote nitoroke, leo nilikuwa nimeipata hiyo nafasi. Nilikuwa ninevalia pajama la kulalia, nilimpapasa James na kuchukua rundo la funguo, sasa mtiti ulikuwa ni kufahamu funguo zilikuwa zikifungua wapi na wapi maana zilikuwa nyingi.
Nilirudi haraka kule chumbani ambako nilimpiga chupa James, kisha nilichungulia dirishani bado hali ilikuwa shwari kabisa nikaona ndio wakati wangu wa kwenda kukomboa maisha yangu na ya binti yangu Moyo.
Nilianza kufungua milango ya ile nyumba, nilikuwa nikihangaika na kuchukua muda mrefu kufungua mlango mmoja, yaani nilijawa na woga kupitiliza, mikono ilikuwa ikikosa nguvu hadi nilikuwa nikidondosha funguo mara kadhaa, nilifanikiwa kufungua milango miwili ambayo James alipokuwa akiingia alifungua na kuifunga.
Wakati namalizia mlango wa mwisho nilisikia mlio wa gari, ilinibidi nirudi chumbani kuchungulia dirishani maana kile ndio chumba pekee kilichokuwa kikionyesha sehemu ya mbele yaani geti na barabara, nilimuona Anko Sanga akishuka kwenye gari, alienda kuangalia gari yake Rav4 kisha alichukua simu na kupiga, niliisikia ikiita bafuni, ilikuwa ni simu ya James
Haraka nilikimbilia bafuni na kuichukua simu ya James, ilipomaliza kuita niliizima kisha niliipeleka kwenye chumba kingine, nikaweka mazingira ya Bafu vizuri, maana niliupeleka mwili wa James kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa na bafu ndani. Haraka nilikimbilia mlangoni na kufunga milango yote, wakati huo Anko Sanga alikuwa akipandisha ngazi kuja juu. Nilielekea bafuni kuzuga, nilianza kuoga ili tu kutengeneza mazingira wakati huo mwili wa James ukiwa kwenye chumba kingine kabisa tena chumba ambacho kilikuwa hakilaliwi na Mtu.
“James yuko wapi?” aliingia hadi bafuni na kuniuliza
“Sijamuona” nilimjibu kwa mkato tu, bado nilikuwa na kisirani nae kwa kitendo cha kumchukua Binti yangu Moyo
“Hujamuona wakati gari iko pale nje? nilimtuma mzigo chumbani kwangu,”
“Sasa sijamuona nikwambie nimemwona?”
“Oky!” alielekea chumbani akiwa na funguo za ziada, zile funguo zingine nilikuwa nazo mimi sikutaka kabisa kuziachia.
Alipofika chumbani alianza kupatwa na wasiwasi alipiga tena simu ya James haikupatikana na kibaya zaidi viatu vya James vilikuwa pale nje, akarudi tena kwangu akiwa na sura ya kikauzu!
“James yupo wapi?” aliniuliza lakini nilimkatalia kabisa, moyoni nilijua kuwa James alikuwa amekufa
“Sijamuona akiingia humu ndani” nilimjibu, kilichokuwa kinampa tumaini ni milango kuikuta ikiwa imefungwa vilevile, alinitazama kisha alinifungia chumbani, wakati huu nilikuwa nimemaliza kuoga na nilikuwa na zile funguo.
Nilimsikia akifunga milango kisha aliondoka zake, chumba nilichokuwa nimefungiwa hakikunipa nafasi ya kumuona akiwa anatoka getini, ghafla akarudi na kufungua mlango, nilimuona akivua nguo zake na kubakia kama alivyozaliwa nilijua tu alitaka penzi, nilimvulia nguo akanifanya hadi alipomaliza kisha aliondoka zake.
Nilirudi bafuni kuoga, kisha nilianza harakati za kutaka kutoroka pale ndani, nilichukua funguo mahali ambapo nilikuwa nimezificha kisha nilivaa nguo sikuhitaji hata begi lolote maana ile nafasi pekee niliitafuta kwa kitambo sana.
Nilifungua milango haraka haraka ili niweze kutoroka pale nyumbani kwa Anko Sanga, nilifanikiwa kufungua milango yote hadi wa mwisho ambao ndio ulikuwa ukitazamana na geti kubwa la kutoka pale kwa Anko Sanga.
Niliitazama ile nyumba jinsi ilivyogeuka kuwa jela ya Mateso kwa zaidi ya Miaka mitatu, nilijikuta nikiangusha chozi. Mateso niliyoyapata pale hayakupata kuelezeka kabisa, moyo wangu uliteketea kwa maumivu makali zaidi hata ya sindano izamapo ndani ya jicho, nilipiga magoti nikiwa ninalia.
Katika hali isiyo ya kufikirika nilihisi kuguswa kwenye bega langu, hali ya kulia ilikata mara moja huku kiu ya kumjua aliyenishika bega alikuwa nani ilinijia, nilipogeuka nilikutana na sura kavu ya Anko Sanga ikiwa inanitazama, wakati namtazama nilijisemea kuwa sitakiwi kuichezea ile nafasi, nilijifanya naendelea kujawa na woga huku nikimlia taiming jinsi ya kumkwepa pale ili niweze kutoroka!
Hesabu zangu zilienda sawa kabisa, alipokuwa akinisogelea niliachia teke hadi kwenye zizi lake, akaanza kulalamika huku akiwa amejishika, nilijua ile sehemu ingemsababishia maumivu ambayo yangenifanya nikimbie haraka kuelekea getini ili niweze kutoka nje kabisa ya ile nyumba.
Nilimtazama jinsi alivyokuwa akiugulia maumivu makali ambayo yalimpeleka hadi chini, akawa ana galagala chini huku akipiga ukunga wa maumivu. Nilimeza mate kisha nilitoka mbio kuelekea getini, wakati niko bize pale kufungua geti nilihisi ubaridi sehemu ya shingo, ghafla maumivu makali yaliyoambata na kuishiwa nguvu yalianza, nilijikuta nikilegea.
Nilijitahidi kujishikiza kwenye lile geti ili nisidondoke, giza zito liliyakumba macho yangu, nilianza kupoteza uwezo wa kufikiria, nilijikuta hata uwezo wa kusikia ukipotea. Nguvu kidogo iliyobakia niliitumia kugeuka nyuma, kwa nuru kidogo ilibakia ndani ya macho yangu nilifanikiwa kumuona Mama yangu Mzazi, kabla sijapoteza ufahamu wangu nilifanikiwa kugundua kuwa Mama yangu ndiye aliyesababisha niwe katika hali ile, mkononi alishikilia kipande cha Mti, Palepale nilidondoka na kupoteza fahamu zangu!
Nikiwa kwenye giza zito ndani ya ufahamu wangu nilimkumbuka Mwanangu Moyo, sikujua Mtoto wangu alikuwa wapi licha ya Anko Sanga kusema alikuwa kwa Mama yangu, nilihisi uwepo wa Jonas mbele ya Macho yangu, nilijikuta nikitabasamu!! Ubaridi ulinifanya nirudishe ufahamu wangu ulionitoroka kwa takribani masaa matatu.
Niliiona Sura ya Anko Sanga na Mama yangu wakiwa wananitazama, sura zao zilijaa uzito wa hali ya juu, pale pale nikakumbuka kilichotokea masaa kadhaa yaliyopita, nilijikusanya na kuketi, wakati nakaa vizuri nilihisi kugusa kitu na nilipogeuka niliuona mwili wa James pale Sakafuni. Nilianza kufikiria nje ya Box
“Veronica huwezi kutoroka hapa, hilo kamwe haliwezi kutokea! Wewe ni adhina muhimu sana kwetu istoshe tuna Mtoto wako, nadhani huwezi kufanya upuuzi wowote ule kwani kwa kufanya hivyo utamuacha Binti yako mikononi mwetu” Yalikuwa ni maneno makali ya Anko Sanga, maneno haya yaliibua hisia nzito sana, yalinifanya nianze kutokwa na machozi.
“Kwasababu ulitaka kutoroka hapa, nakupa adhabu ya kuishi na maiti ya James, nilijuwa uwepo wa jambo hili nilipoingia bafuni na kuuona mwili wa James, hivyo niliweka mtego makusudi ili nikunase” Aliongeza
“Mama! Mama! Umenizaa wewe mwenyewe kweli? Unyama gani huu unanifanyia Veronica wako? Ulinizaa peke yangu na huna binti mwingine” Nilisema nikiwa ninalia, nilikuwa nimejikunyata, tatizo kwangu halikuwa Anko Sanga bali ni Mama yangu Mzazi, nilijiuliza alikuwa ameingiwa na shetani gani hadi anifanyie yote yale?
“Nisingekuzaa nisingefanya hivi, kwani Wazazi wako wangepiga sana kelele…leo nimeamua kufanya kwasababu hakuna wa kupiga kelele”
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TISA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
11 Comments
Riwaya tamu sana hii sema shida inatola Ep chache alafu Kwa kuchelewa
Riway nzuri San ila inachelewa kutok itoen kila siku jmn
Riwaya Ni Nzuri Mnoo Changamoto Unakuja kwa Kuchelewa saana
Mmh jaman wamama wa hivo wapo sayari hii ya Dunia au??
Tatizo ni nzul alafu saiv imekuwa fup admin
🔥
Request;mtume hata mbilii kwa siku tafadhalii
Maestro05
Imekuwa fupi Sana Admn saiv hta vibe la kusoma linakata kbs pia inachelewa kutoka
Nzur sana jmn
Ya 9 bila kuchelewa please
Kazi mzuri