Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Makocha 5 Wanaolipwa Pesa Ndefu Zaidi AFCON
    Africa | CAF

    Makocha 5 Wanaolipwa Pesa Ndefu Zaidi AFCON

    MhaririBy MhaririJanuary 8, 2024No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    DJAMEL BELMADI (ALGERIA) Miongoni makocha wanaolipwa pesa nyingi zaidi
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Tarehe 13/01/2024 bila shaka ni siku inayosubiriwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa soka barani Afrika kwa lengo kubwa la kutazama timu zao za Taifa zikimenyana kumtafuta bingwa wa kombe la mataifa barani Afrika (AFCON) kwa msimu wa mwaka 2023 itakayofanyika nchini Ivory Coast huku kila timu ya taifa ina kocha ambaye anaandaa mbinu zake kwa ajili ya kuchukua ubingwa huu na hapa tutazame orodha ya makocha watano bora wanaopokea pesa ndefu zaidi kufundisha timu za taifa katika michuano ya AFCON msimu huu.

    1. HUGO BROOS (AFRICA KUSINI)

    Kocha huyu kutoka Ubelgiji aliwahi kushinda AFCON akiwa na kikosi cha Cameroon mwaka 2017 na amekuwa akihudumu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini tangu 2021 huku mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, lakini hajawahi  kuipatia timu hiyo taji lolote.

    1. WALID REGRAGUI (MOROCCO)

    Ni miongoni mwa makocha bora barani Afrika kati ya makocha waliofanya vizuri kwenye Kombe la Dunia

    mwaka juzi nchini Qatar akiifikisha nusu fainali Morocco, Walid anakunja Euro 60,000 kwa mwezi na ana mkataba wa kuifundisha Morocco hadi 2025.Mbali ya fedha pia ni mmoja kati ya makocha tishio wanaotarajiwa kuwepo kwenye mashindano ya mwaka huu.

    1. RUI VITORIA (MISRI)

    Huyu ni mmoja kati ya makocha bora kutoka Ureno ambaye mfukoni mwake ana medali za ubingwa wa ligi nchini humo mara mbili. Kocha huyu ana mkataba wa kuitumikia Misri hadi  mwaka 2026, na aliajiriwa mwaka 2022. Analipwa Euro 200, 000 kwa mwezi

    1. JEAN-LOUIS GASSET (IVORY COAST)

    Wenyeji wa michuano hii nao si haba kwani kocha wao wanamlipa kiasi cha Euro 108,00 kwa mwezi akiwa na rekodi ya kushinda mechi 9 akisare michezo 3 na kufungwa mechi 2 kati ya mechi 14 alizoisimiamia timu hiyo toka mwaka 2022.

    1. DJAMEL BELMADI (ALGERIA)

    Kocha huyu ambaye ni raia wa Algeria ndiye anaongoza kwa kuwa na mshahara mkubwa zaidi kwenye mashindano hayo. Mshahara wake wa Euro 208,000 kwa mwezi ameanza kuupokea tangu 2018 alipochukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo. Belmadi ameisaidia nchi hiyo kushinda taji moja la Afcon mwaka 2019 na pia aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Qatar. Pia aliwahi kuchukua tuzo ya kocha bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) 2019.

    Endelea kusoma zaidi kuhusu AFCON kwa kugusa hapa.

    AFCON 2023
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.