Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Kuhusu Aziz KI Msimamo Wangu Ni Huu Hapa
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Kuhusu Aziz KI Msimamo Wangu Ni Huu Hapa

    MhaririBy MhaririMay 21, 2024Updated:May 22, 202419 Comments2 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Aziz Ki
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kote duniani biashara ya mpira ndivyo ilivyo mchezaji ni kama mfanya biashara tu siku bidhaa yake ikiwa poa ndio nyakati ambayo hua anatafuta mteja ambaye ataifikia gharama ya bei yake.

    Kinachoendelea hivi sasa kwa mchezaji Stephanie Aziz Ki ni yeye kutoongeza mkataba MPYA ndani ya Yanga SC, siyo habari nzuri sana kuzisikia kutoka klabuni hapo na mchezaji wao. Aziz ni moyo wa timu kwasasa hilo halina ubishi, mabao yake mengi yaliifanya Yanga kufikia baadhi ya malengo ya Klabu.

    Boss anakuna kichwa kuhusu wino mpya wa mfanyakazi wake, ni wakati mgumu kwake kwani anafahamu namna alivyowahi kuinasa saini hiyo hakuwa kazi rahisi kuipata vita ilikuwa tena dhidi ya Mtani wao Simba SC. Leo linapokuja jambo kama hili mchezaji anapata kigugumuzi cha kuongeza mkataba wala hatupaswi kuanza kumshangaa mchezaji, tumuelewe kuwa hii ndio kazi yake, hayo ni maisha yake kaja Tanzania kutengeza kipato.

    Inaarifiwa kuwa STEPHEN AZIZ KI ana ofa mbili kutoka Al Ahly na Orlando Pirates, amewapa Yanga unafuu wa offer ili aweze kusaini kwao na mahitaji yake kutoka kwa vyanzo vyangu anahitaji kiasi cha dola 500,000 ili aweze kusaini ikiwa ni sawa na BILLION 1.2 za Kitanzania.

    Mpaka hivi sasa Wananchi hawana kiasi hicho na klabu kwa mujibu wa vyanzo imejipiga mpaka Dola 350,000 za Kimarekani wapo tayari kumpa ila Aziz ameshikilia zifike 500,000 ili asaini, jitihada zinaendelea ila kinachohitajika ni huo mzigo.

    Mpaka hivi sasa Aziz hajasaini KARATASI yoyote ndani ya Jangwani.

    Kinachobaki kwenye timu na klabuni milele ni Mwanachama na Shabiki pekee yao, wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Viongozi wa timu hua siyo watu wa kudumu kwaiyo tukiyajua hayo wala hatuingii kwenye kumshangaa mchezaji. Ikitokea wameelewana katika ya boss na mchezaji ili aendelee kusalia, basi itakuwa poa sana na kama ikitokea imeshindikana ni kumtakia kheri mchezaji popote aendako.
    Maoni Yako Ni Yapi? Tuambie Kwenye Comments

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]  

    AZIZ KI Aziz Ki Yanga
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.