Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Kuhusu Aziz KI Msimamo Wangu Ni Huu Hapa
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Kuhusu Aziz KI Msimamo Wangu Ni Huu Hapa

    MhaririBy MhaririMay 21, 2024Updated:May 22, 202419 Comments2 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Aziz Ki
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kote duniani biashara ya mpira ndivyo ilivyo mchezaji ni kama mfanya biashara tu siku bidhaa yake ikiwa poa ndio nyakati ambayo hua anatafuta mteja ambaye ataifikia gharama ya bei yake.

    Kinachoendelea hivi sasa kwa mchezaji Stephanie Aziz Ki ni yeye kutoongeza mkataba MPYA ndani ya Yanga SC, siyo habari nzuri sana kuzisikia kutoka klabuni hapo na mchezaji wao. Aziz ni moyo wa timu kwasasa hilo halina ubishi, mabao yake mengi yaliifanya Yanga kufikia baadhi ya malengo ya Klabu.

    Boss anakuna kichwa kuhusu wino mpya wa mfanyakazi wake, ni wakati mgumu kwake kwani anafahamu namna alivyowahi kuinasa saini hiyo hakuwa kazi rahisi kuipata vita ilikuwa tena dhidi ya Mtani wao Simba SC. Leo linapokuja jambo kama hili mchezaji anapata kigugumuzi cha kuongeza mkataba wala hatupaswi kuanza kumshangaa mchezaji, tumuelewe kuwa hii ndio kazi yake, hayo ni maisha yake kaja Tanzania kutengeza kipato.

    Inaarifiwa kuwa STEPHEN AZIZ KI ana ofa mbili kutoka Al Ahly na Orlando Pirates, amewapa Yanga unafuu wa offer ili aweze kusaini kwao na mahitaji yake kutoka kwa vyanzo vyangu anahitaji kiasi cha dola 500,000 ili aweze kusaini ikiwa ni sawa na BILLION 1.2 za Kitanzania.

    Mpaka hivi sasa Wananchi hawana kiasi hicho na klabu kwa mujibu wa vyanzo imejipiga mpaka Dola 350,000 za Kimarekani wapo tayari kumpa ila Aziz ameshikilia zifike 500,000 ili asaini, jitihada zinaendelea ila kinachohitajika ni huo mzigo.

    Mpaka hivi sasa Aziz hajasaini KARATASI yoyote ndani ya Jangwani.

    Kinachobaki kwenye timu na klabuni milele ni Mwanachama na Shabiki pekee yao, wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Viongozi wa timu hua siyo watu wa kudumu kwaiyo tukiyajua hayo wala hatuingii kwenye kumshangaa mchezaji. Ikitokea wameelewana katika ya boss na mchezaji ili aendelee kusalia, basi itakuwa poa sana na kama ikitokea imeshindikana ni kumtakia kheri mchezaji popote aendako.
    Maoni Yako Ni Yapi? Tuambie Kwenye Comments

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]  

    AZIZ KI Aziz Ki Yanga

    19 Comments

    1. Junias Pontion Frugens on May 21, 2024 2:58 pm

      Akiondoka ndo atakuwa anapoteza kipaji chake Bora angebaki asikimbilie pesa

      Reply
      • Haruni on May 22, 2024 8:11 am

        Akiondoka anaweza asipotee yeye Cha muhimu aangalie sehemu ambayo haitauwa kipaji chake aend kwenye timu itakayokuwa na combination nzuri Kama alionayo yanga hicho ndo Cha muhimu kwake asiangaloe mkwanja

        Reply
      • Rifati on June 10, 2024 8:30 am

        Kuondoka kwa azizi ki kunaumiza sana mashabik lakin ndo utalatibu wa mchezaji, chakuzingatia yeye n kwamba akitoka yanga aendelee kupambana asishuke kiwango akawa namajin kama mayele

        Reply
    2. Ismaily Mourlyd on May 21, 2024 2:59 pm

      star mwingne ata rise sabab tz kwanza huwa tunatamaduni ya promoshen then performance maana yake aende sababu ndiye anaelisha familia yake ila star mpya tutamuandaa kuanzia promo mpaka ajiamin na kuperform

      Reply
    3. calix on May 21, 2024 3:02 pm

      dah asalie tu apa ndo nyumban

      Reply
    4. Chard michael on May 21, 2024 3:03 pm

      Oya admin utaweka fungate sehemu ya tisa, au tukufuate hukohuko😠😠😠

      Reply
    5. Shaban on May 21, 2024 3:04 pm

      Hapo asijalibu kabisa maana yatamtokea kama luis mwisho wa siku kipaji chake kinapotea ni bora atulie tu

      Reply
    6. Manyusi on May 21, 2024 3:04 pm

      Admin umeongea jambo muhimu sana siku zote kinachobaki milele kwenye timu ni mashabiki hivyo kama Aziz ki akiamua kuondoka kila la kheri 🙌🙌🙌

      Reply
    7. Sensible on May 21, 2024 3:09 pm

      Hii ni ajira kama ajira nyengine tuu ni wajibu kwake kuchagua kiasi anachokihitaji. Na inakubidi wewe ndo uridhike na pesa ambayo unaipata sehemu ulipoajiriwa. Familia inamuangalia yeye kama anaona anapoenda matunda ni mazuri zaid kuliko alipo ni kheri aende tuu. 🔜🔜

      Reply
    8. Chard michael on May 21, 2024 3:10 pm

      Admin unataka dola 500,000 kama aziz ili utuletee fungate sehemu ya 9 au vepe!?

      Reply
    9. Henderson Didas on May 21, 2024 3:11 pm

      Pesa ni muhimu kuliko vyote apo afate mahali kuna michongo mikubwa zaid .Maan izo timu zinamuhitaji ni timu kubwa mno ina maan atazidi kukuwa na kufahamika na kupata michongo mikubwa zaidi kuliko kubaki sehemu moja

      Reply
    10. Richard on May 21, 2024 3:18 pm

      Some time life ndivyo ilivyo huwezi kupambana ukiwa sehem mmoja hii nikama challenge ya maish ya soka ilitokea kwawanasoka wengi tu so yot kwa yot tunamtakia Kila la kher

      Reply
    11. Joseph Jackson on May 21, 2024 3:30 pm

      Hakika kinachobaki kwenye klabu mpaka kifo ni sisi mashabiki, lakin wachezaji na staff nzima yaweza kubadilika Kila msimu, mwaka Jana waliondoka most important people who was the part of the team kama mayele, pro. Nabi na benchi lake la ufundi mpaka kocha wa viungo lakin still maisha yaliendelea, hivyo akisema bhana pesa anayopata haitoshi aende tunamtakia Kila lakheri ila kama ataamua kubaki tutazidi kumpenda.

      Reply
    12. Josiah on May 21, 2024 3:38 pm

      Hivi hukuna mchezaji anae penda team kweli anayo tumikia..

      Au ndo ile money first 🤔🤔

      Reply
    13. VALENCE on May 21, 2024 4:16 pm

      Kama hataki kubaki aondoke tu,,, maana wapo watakuja na anaweza kuja mzuri zaidi yake!

      Reply
    14. Barcowinya on May 21, 2024 6:08 pm

      Yanga imekua chimbo Kwa wachezaji wenye juhudi haya ni maisha wamuache akapambane ili na sisi TUJITAFAKARI kama alivyoondoka mayele
      Wampe na baraka zooote

      Reply
    15. Jeyb on May 27, 2024 3:23 pm

      Ni vigumu sana master ki kubak jagwan kutokana na kiasi anachokihitaji

      Reply
    16. Pingback: Funga Kazi Ligi Kuu Iko Hivi | Vita Ya Nafasi Ya Pili Na Kiatu

    17. Abby boy on May 27, 2024 4:09 pm

      Mi nashauli kwamba ackimbilie kwend all ahly maan wanatabia ya kupoteza vipaji vya wa2 weusi mfano Luis miqson so ni Bora akaze 2 hapo au kam vp aende hata simba sio mbaya

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.