Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 06
Walipofika shangwe liliibuka kwa Wananchi waliamini kua kumwaga Damu kutawasaidia Mji wao kuendelea kua na nguvu zaidi. Miongoni mwa Walioletwa
mbele ya Mfalme alikuwepo Mtoto Moana. Chozi lilimtoka Anna alipomwona Moana akiwa amefungwa minyororo.
“Moana” aliita Anna kwa sauti ya Juu, Moana alimtazama Mama yake Kisha alimpa tabasamu la matumaini.
Mfalme akawaambia walinzi kua Watu watatu watakua wa mwisho kuuawa Asubuhi hiyo, Watu hao ni Moana, Anna na Zahoro. Walitengwa huku wakishuhudia namna Watu wengine wakiuawa kwa kuchinjwa kama Kuku Kisha Damu kutiwa kwenye chombo maalumu kwa ajili ya sadaka. Endelea
SEHEMU YA SABA
Walikua wanauawa kikatili sana Kisha miili Yao kutupwa kwenye tanuli la moto, ilikua ni kama Ibada kwao wakiaminishwa na Mganga Segebuka kua Damu hizo zitafanya Mji wao kua na nguvu zaidi.
Mfalme alikuwa ameketi akivalia mavazi yenye kung’aa, mkononi alikua ameshikilia kitu Fulani. Mtoto Moana alikua akilia Kila alivyoona Mtu akiuawa mbele yake, ilikua kadhia kwake ila kwa Mfalme Selasi ilikua ni furaha kuona anatowesha maono ya Segebuka kua atakuja Mtu kutoka kwenye Damu ya Mfalme wa zamani kuchukua Ufalme.
Walipomaliza kuwaua wale wengine ilikua ni zamu ya akina Zahoro. Walisogezwa wote watatu kwa pamoja, kabla zoezi halijaanza Mfalme akalisimamisha Kisha akasema
“Nitaondoa Maisha Yao kwa Mikono yangu” Kisha akageuka kumtazama Segebuka, ni kama walikua wamepanga jambo Fulani kwa pamoja. Shangwe na vifijo viliendelea, wakifurahia kumwaga Damu walizoamini zimebeba Matumaini.
Mfalme Selasi akaagiza akina Zahoro wafungwe kwanza vitambaa vyeusi usoni ili hukumu Yao ipite gizani mbele Yao. Mara Moja walifungwa vitambaa usoni ili kuzuia macho Yao yasione chochote, katikati ya hofu na Mashaka ukimya ulitawala kwa kiasi kikubwa, Kila mmoja alishangaa.
Mfalme Selasi alipanga Kuwauwa kwa kutumia Bastola lakini ilianza kusikika sauti ya Kutisha iliyosambaa Kila kona, sauti hiyo ilikua ikisema
“Mwisho Umefika, mwisho Umefika, mwisho Umefika” Kila mmoja alijitahidi kutafuta kwa macho ilipotokea sauti hiyo, lakini ilikua Kila Sehemu ya Mji wa Patiosa
Sauti hiyo ilisambaza woga, baadhi ya Watu walianza kukimbia kurejea Makwao, Mfalme Selasi akachomoa Bastola na kumweka usoni Segebuka
“Ni sauti ya nini?” aliuliza Mfalme. Japo alikua anafanya yote lakini aliamini anaweza kubadilisha hatima iliyosemwa na Mganga wake Segebuka. Jasho likimbubujika, Segebuka akamwambia Mfalme Selasi
“Kama unaweza kunimaliza itakua vyema Mfalme kuliko kushuhudia Mapinduzi, hatma haiko tena Upande wako. Unaangushwa” alisema Segebuka akiwa anaonekana kukata tamaa na kua tayari kwa lolote lile litakalo tokea, hakukwepesha macho yake Bali alikua akimtazama Mfalme tofauti na siku zote alivyokua akimpa heshima ya Juu sana Mfalme kwa kutomtazama usoni.
“Ulisena tunaweza kubadilisha hatima, imekuaje?” Aliuliza Mfalme, sura yake ilionesha ni namna gani alivyokua amechanganikiwa. Aliamini ana nguvu za kupambana na yeyote atakayejitokeza mbele yake lakini Mtu pekee aliyempa tumaini aliimaliza tumaini hiyo, mkono alioshikilia Bastola ulikua unatetemeka sana.
Ile sauti ya ajabu ilizidi kusogea, haikua sauti ngeni kwa Zahoro na Anna, ilikua ni sauti ya Alice pacha wa Anna. Alikua na nguvu ya kuitumia sauti yake kuangamiza maadui zake. Kwa namna sauti ilivyokua inazidi kusogea karibu zaidi ilionesha Alice alikua ameshafika ndani ya Mji wa Patiosa
Mfalme alishusha Bastola yake, Zahoro na Anna walitazamana Kisha Zahoro alikubali kumpokea Alice kwa mara ya kwanza licha ya kua aliuwa Watu wengi sana. Chozi lilimbubujika Zahoro, Mtoto wao alikua amefungwa na mnyororo, hakuna aliyeweza kumsaidia mwenzake isipokua kutazama mambo yalivyokua yakiendelea.
Mfalme Selasi baada ya kuona mambo sio mazuri, akakimbilia ndani ili kuangalia afanye nini. Upepo ulianza kuvuma kuashiria Alice alikua amefika, katikati ya Upepo mkali akatokea Alice.
Askari wa Mfalme Selasi wakajaribu kupambana na Alice lakini ilikua ni mpambano wa kujidanganya, Alice alikua na nguvu za ajabu, aliweza kuamrisha jambo likatokea papo hapo. Kila askari aliyekutana na macho ya Alice aliugeuza Upanga na kujimaliza.
Watu waliobakia walianza kukimbia, Segebuka alisimama akimtazama Alice. Kisha alipiga goti na kusema
“Sijawahi kupata kushuhudia Binadamu mwenye nguvu kama wewe.” Akainamisha kichwa chake kumpa heshima, Alice hakuona kama ilikua ni sawa kummaliza Segebuka, alimtazama tu Kisha aliikata minyororo iliyowashikilia Anna, Zahoro na Moana Kisha akawaambia
“Tazameni nyuma yenu” walimwona Mfalme Selasi akiondoka kwa farasi kisha lango la kuingilia Mji wa Patiosa lilifungwa.
“Tokeni hapa, Mimi nitapambana na hila zote za Mji huu, hakikisheni mnampata Mfalme” alipomaliza kuongea walisikia sauti za Askari wakija Upande wao, halikua kundi dogo Bali ni Maelfu ya Askari wa Mji wa Patiosa wakiwa na Mapanga na Mikuki.
Anna na Zahoro kitu Cha kwanza kilikua kuhakiki kuhusu Hali ya Moana, walimkumbatia kwa furaha sana Kisha Zahoro akasema
“Inabidi tulipate jicho la Mfalme Selasi, jicho pekee Ndilo ufunguo wa Lango la Kuzimu” kwakua alikua na ramani ya Ufalme wote kutokana na maono ya ndoto alizoota, alijua ni wapi kilipo chumba kilichohifadhi jicho Hilo la ajabu.
Zahoro alielekea ndani ya Jumba la Kifalme, alikutana na walinzi kadhaa lakini alikua na mazoezi ya kupambana nao bila kupepesa macho, alikua fundi wa kutumia Upanga. Alipopata nafasi ya kushikilia Upanga alihakikisha anamwaga Damu Hadi kukifikia chumba Cha Mfalme Selasi. Alipofika hapo, aligundua sanduku lilikua tupu
“Mfalme amechukua jicho, anaelekea kulifungua lango Kisha aondoke” alisema Zahoro kwa sauti ya chini Kisha haraka alirudi alipomwacha Anna na Mtoto Moana, wakati huo Alice alikua ameshikilia Upanga akipambana na Maelfu ya Askari wa Patiosa.
“Inabidi tumfuate Mfalme” alisema Zahoro Kisha haraka walianza kukimbia kuelekea eneo ambalo Farasi walikua wamefungiwa Kisha walichukua farasi wawili, Anna na Mtoto walikwea farasi mmoja, Zahoro naye alikua juu ya Farasi mwingine.
Waliondoka kulielekea lango ambalo lilikua na askari wa kutosha kwa ajili ya kuwazuia.
Zahoro alining’inia kwenye farasi mithiri ya digidigi mwenye hasira Kisha alianza kukata shingo za Askari kama feni, alipoinuka Upanga wake ulikua unamwagika Damu. Moana alitabasamu akimwona Baba yake akipambana kwenye Uwanja wa vita.
Kisha akiteremeka kwa Kasi na kumwachia farasi, alianza mapigano ya Upanga kwa Kasi sana alihakikisha anaharakisha mpambano ili wamwahi Mfalme Selasi aliyekua akikimbia.
Ndani ya dakika tatu zilitosha kwa Zahoro kumaliza kazi Kisha alilifungua lango Kisha alimkwea farasi, wakaongoza njia pekee iliyokua ikitoka ndani ya Mji huo, upande mwingine yalijaa Maji hivyo walikua na uhakika kua Mfalme aliitumia njia hiyo kutokomea.
Aliongoza safari kwa kumliza farasi atembee kwa Kasi sana, nyuma yake Anna pamoja na Moana walikua wakifuatia, Upanga uliendelea kusikika ndani ya Mji wa Patiosa, Alice alikua akipambana na Maelfu ya Askari wa Mji huo.
Askari walikua wengi sana kiasi kwamba Alice alianza kuzidiwa, lakini Kila alipokumbuka kuhusu kifo Cha Baba Yao na Mama yao ilimlazimu kuendelea kupiga Upanga.
Upande wa pili, Zahoro alikua akikimbia na farasi kwa Kasi ya ajabu sana. Alijua kama watamkosa Mfalme Selasi basi njia ya kuelekea Duniani isingelikuwepo tena na pengine wangelisubiria kwa Miaka Mingi.
Farasi aliendelea kupiga kelele huku akikita kwato zake ardhini kwa kishindo kizito sana, Kila hatua ilimfanya Zahoro avute Upepo mkali uliombatana na baridi Kali la Msituni, Giza lilikua limetanda lakini macho makali ya Farasi yalikua yakimulika mbele.
Baada ya kitambo kirefu, Farasi wa Zahoro aligoma kusonga mbele. Alikita miguu yake na kufunga breki katikati ya Msitu ulio Kimya sana huku sauti pekee iliyosikika baada ya Farasi kutulia ilikua ni sauti ya kusukumwa kwa majani makavu.
Palikua kimya huku pakiwa na ishara ya jambo lisilo la kawaida, kusimama kwa farasi kuliashiria jambo Fulani, Zahoro akashuka kutoka juu ya Farasi. Kisha Upanga ukawa mkononi ili kujikinga na Adui atakaye jitokeza mbele yake.
Aliyalazimisha macho yake kutazama katikati ya Giza nene, hisia isiyo ya kawaida ilimwambia asogee mbele zaidi kwa hatua takribani tano.
Aliposogea kidogo mbele akamwona Farasi akiwa amesimama kando ya njia. Akajua sasa kua Mfalme Selasi hakua mbali na eneo Hilo, akatazama kulia Kisha kushoto asijuwe Mfalme atakuwa ameelekea wapi.
Akajiuliza “Atakua upande upi?” akatikisa kope za macho yake kama aliyeingiwa na mdudu hivi Kisha akaamua kuelekea Upande wa kulia ambako yule Farasi alikuwepo, alizama Msituni huku akipapasia. Palikua Giza sana, alisonga mbele huku akiamini kua Mfalme Selasi asingeliweza kujificha Bali aliingia Msituni hapo kwa ajili ya jambo Fulani la Siri.
Taratibu alianza kuhisi Nuru machoni pake, alianza kuona mwangaza mkali sana. Aliamua kuufuata mwanga ulio mbele yake, sasa alikua akiona Kila kitu hivyo hata mwendo wake haukua mdogo. Alijua mwanga huo ulikua na uhusiano wa moja kwa Moja na Mfalme Selasi.
Alikatiza Msitu, aliyapita Majani na nyasi kuufuata ule Mwanga. Hatimaye alifika mahali ambapo palikua Ndiyo chanzo Cha huo mwanga, alimwona Mfalme Selasi kwa mbali aliwa amesimama kando ya Mwanga kwenye Mti mkubwa wenye Pango, Naam! Hapa ndipo ilipo njia ya kuelekea Duniani.
Mfalme Selasi alikuwa mwingi wa kuangalia huku na kule akionekana kusubiria jambo Fulani hapo, Kisha Zahoro akakatiza bwawa dogo kwa haraka na kutokea upande wa pili, akabakiza hatua chache kufika alipo Mfalme.
Aliushuhudia Upepo mkali sana ukitoka kwenye lile Pango, kiasi kwamba hata kofia ya Kifalme ilimtoka Mfalme Selasi.
Zahoro akatambua sasa huwenda hiyo njia ilikua ikifunguka, lengo la Mfalme lilikua ni Kukimbia kuelekea Duniani.
Haraka Zahoro akaanza kukimbia kwa Kasi kumfuata Mfalme ambaye alikua akipiga hatua kuzama ndani ya Pango Hilo, kitendo bila kukawia haraka Zahoro akamfikia Mfalme na kumvuta Mkono, akamtoa ndani ya Pango
Mkononi Mfalme Selasi alikua ameshikilia Bastola, akaielekeza kwa Zahoro
“Usijaribu kunizuia Kijana, nitakuuwa hapa na maiti Yako haitapatikana” alisema Mfalme, akionekana kuvizia taratibu kwa jicho lake la kushoto akiangalia njia. Zahoro akatazama namna Mlango ulivyokua ukifunguka
Wakati ambapo Kuzimu ilikua Usiku, upande wa Duniani ilikua ni Mchana. Aliona Mabdhari ya kupendeza sana, lakini kizuizi kilikua ni Mfalme Selasi aliyeshikilia Bastola.
Mfalme Selasi akaanza kurudi nyuma nyuma ili kuingia pangoni, Zahoro akapiga mahesabu afanye nini ili amzuie Mfalme asiingia humo maana alijua fika kua kama Mfalme ataingia na mlango utajifunga.
Licha ya kushikilia Bastola, mkono mwingine aliishikilia mfuko Fulani mweusi, humo ndimo lilimo jicho la Mfalme lenye ufunguo wa kufunga na kufungua Njia ya kuelekea Duniani, kutokana na papara na wasiwasi akajikuta akidondosha mfuko huo
Akakaza Bastola kuelekea kwa Zahoro huku akipiga hesabu ya namna gani ataokota Mfuko Kila hatua aliyoipiga, taratibu Zahoro naye alisogea.
“Usisogee Kijana nitakuuwa” akasema Mfalme Selasi, lakini Zahoro hakuacha kupiga hatua za mgando. Kitendo Cha Mfalme Selasi kuinama aokote mfuko akampa mwanya Zahoro kumfikia, papo hapo kabla hata Zahoro hajamgusa Mfalme, akapigwa Risasi ya Bega. Kisha Mfalme akafyatua nyingine lakini bahati mbaya kwake risasi zilikua zimeisha.
Zahoro alipoligundua Hilo akamvaa Mfalme na kuanza kumshushia kipigo kizito, Kisha akauokota ule mfuko. Pale pale taratibu Lango la Kuzimu likaanza kujifunga kwasababu hapakua na Mtu anayeingia humo.
Mfalme Selasi akiwa chini, Zahoro akiwa juu yake. Taratibu mkono wa Mfalme Selasi ukapapasa pembeni na kuokota jiwe, Kisha akalipeleka usoni kwa Zahoro kwa nguvu. Akafanikiwa kumsukumiza Zahoro pembeni, Giza likaanza kuingia hapo sababu mlango wa kutoka kuzimu ulishaanza kujifunga
Haraka Mfalme Selasi akiwa na wenge akaanza kutafuta ule mfuko wenye jicho lake lenye Miujiza. Bahati nzuri kwake akafanikiwa kuupata, wakati huo Zahoro akiwa chini akigaa gaa kwa maumivu makali ya kupigwa na jiwe
“Aaggghh‼” Mfalme Selasi akagugumia kidogo, akasogea kwenye mlango wa kutokea Kuzimu Kisha akalitoa lile jicho kwenye mfuko, akalionyeshea kwenye mlango
Lile jicho likawaka mwanga mwekundu, Kisha pole pole mlango wa Kuzimu ukaanza kufunguka upya. Mfalme Selasi akaanza kufurahi, wakati huo mwanga ulikua ukianza kutawala eneo lote kwasababu Mlango ulikua unafunguka.
Zahoro Kila alivyojaribu kunyanyuka alihisi kizungu-zungu, maumivu ya kichwa. Ulikua ni wakati wa Mfalme Selasi kuondoka. Akageuka kumtazama Zahoro Kisha akamwambia
“Utaishi Kuzimu Milele” akamalizia kwa Kicheko kikubwa, Ghafla Mfalme Selasi akapigwa Mshale Mgongoni, akapigwa na Mshale mwingine bega la kulia na mwingine bega la Kushoto.
Zahoro alipoangalia ni Nani aliyemshambulia alimwona Anna akiwa ameshikilia Mshale, kando yake yupo Moana. Alijikuta akiachia tabasamu la furaha na maumivu
Mfalme Selasi licha ya kupigwa Mshale na kuanguka chini, Bado alianza kujiburuza ili atoke Kuzimu, lakini Zahoro alimzuia kwa kumvuta nyuma Kisha akamwambia
“Wewe ndiye utakayeishi Kuzimu Milele” mara Anna na Moana walifika na kulichukua jicho kutoka kwa Mfalme Selasi.
“Utalipa kwa kifo Cha Wazazi Wangu, kama ulivyofanya kwetu ndivyo tutakavyofanya kwako pia.” Alisema Anna, Mfalme Selasi akamwambia Anna
“Najua unachokitafuta ni Nini Ndiyo maana unataka kwenda Duniani, lakini wewe si wa huko. Wewe ni Mali ya Kuzimu” Anna alikunja uso wake Kisha akamuuliza
“Unajua nini wewe?” Wakati huo Damu nyingi zilikua zikimtoka Mfalme Selasi, akamwambia Anna
“Unaenda kutafuta Pete ya Baba Yako, Mimi naijua ilipo. Namjua anayeitumia huko Duniani, bila Mimi kamwe hutoipata” Anna aligeuka akamtazama Zahoro Kisha Zahoro akamuuliza Mfalme Selasi
“Kama utasema ilipo basi nitakupatia jicho lako. Utajitibia na kupona, ipo kwa Nani?” Mfalme Selasi akaachia Kicheko Cha maumivu huku Damu ikimtoka Mdomoni.
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya NANE
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx
3 Comments
https://shorturl.fm/ptAnw
Your blog is a beacon of light in the often murky waters of online content. Your thoughtful analysis and insightful commentary never fail to leave a lasting impression. Keep up the amazing work!
Wonderful web site Lots of useful info here Im sending it to a few friends ans additionally sharing in delicious And obviously thanks to your effort