Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 02
“Kumwambia Ukweli Zahoro kua Adui Kimya ni wewe, kilicho mbele ni kumpata Binti yetu Moana Kisha kutafuta njia ya kuelekea Duniani. Baada ya Kisasi sitawalazimiaha Zahoro na Moana kuishi Kuzimu. Watachagua wapi wanataka kuishi” Alisema Anna, Alice alifuta chozi lake Kisha akamwambia Anna
“Kama ni hivyo basi tunaweza kua kitu kimoja lakini sitakusaidia kuelekea Duniani ikiwa Kuna njia, Mimi nitaitawala Patiosa Milele kuenzi Wazazi wetu. Kwasasa nitaungana nawe kurejea Patiosa kwa ajili ya kumpata Mtoto na kupambana Mfalme Selasi. Wote wakatabasamu.
SEHEMU YA NNE
Dunia Halisi.
Miaka Mingi ilikua imepita, yalifanyika majaribio mengi ya kukitafuta Kijiji Cha Nzena bila mafanikio. Wanasayansi wakubwa walishindwa kutatua Fumbo Hilo, isipokua Mwanasayansi Mmoja aliyejizolea umaarufu Kila kona ya Dunia.
Alikua na ushawishi Mkubwa sana, alikua tajiri na mwenye nguvu. Aliweza kufanya tafsiri zilizoonekana kua ngumu, yeye aliweza kupata majibu ndani ya muda mfupi sana. Alipoulizwa kuhusu Nzena alionesha Kigugumizi, hakua na jibu lolote lile.
Eneo ambalo Kijiji kilipotelea palijengwa Makumbusho ya Nchi ya Ganza. Makumbusho ambayo yalikua maarufu sana Kila kona ya Dunia, historia ya kilichotokea Nzena kilitokea Miaka Mingi iliyopita huko Mashariki ya mbali, zaidi ya Miaka Miatatu.
Siku Moja, taarifa mbaya zilianza kusambaa zikimhusu Mwanasayansi Steve Mbasa, Mwanasayansi anayetumainiwa. Taarifa zilisambaa kwa Kasi sana kwenye Mitandao mbali mbali ya Kijamii kua umashuhuri wote alionao Steve Mbasa hautokani na Sayansi ya kawaida isipokua Pete ya kifalme kutoka Mji wa Patiosa.
Taarifa ilieleza kua, hata Umri wa Steve Mbasa unasogea taratibu sana ukilinganisha na Watu aliozaliwa nao Mwaka mmoja, taarifa iliendelea mbali zaidi na kusema kua Steve Mbasa ana Miaka 93 lakini anaonekana kama mwenye Miaka 50 kutokana na Pete hiyo ya Miujiza.
Taarifa hii ilimfikia Steve Mbasa mwenyewe akiwa kwenye Moja ya nyumba zake za kifahari, kilicho mchukiza zaidi ni Mtu aliyeibua taarifa hizo alikua ni rafiki yake wa karibu aliyeitwa GGB. Hawa wote ni Wanasayansi Mashuhuri sana Duniani, lakini GGB aliibua skendo hiyo kwa nia Fulani.
Taarifa hii ilizua taharuki kote Duniani, ilimchafua sana Steve Mbasa, akatupa glasi yenye waini ndani yake Kisha akampigia simu GGB. Lakini simu ya GGB haikupatikana, taarifa ziliendelea kutoka, pamoja na Vipande vya video vilivyomwonesha GGB mwenye Miaka 93 akieleza Siri ya Sayansi ya Steve Mbasa.
GGB aliwaeleza Watu kua yeye na Steve Mbasa walifanikiwa kufika Kuzimu kupitia Pango Moja la Siri sana ambalo kwasasa limejifunga. Akasema walipitia kwenye Pango Moja wakajikuta wapo Kuzimu kwenye Mji mmoja uitwao Patiosa. Mji uliokua ukiongozwa na Mfalme mmoja aitwaye Munis.
GGB na Steve Mbasa walifanikiwa kumfikia Mfalme na kumwahidi kua wangemwonesha lango la kuelekea Duniani, akasema Mfalme aliwapenda sana GGB na mwenzake Steve Mbasa. Walijitambulisha wao ni Wanasayansi Wanaokua kwa Kasi sana.
Mfalme Munis akawaeleza kua angewapa nguvu za Miujiza kidogo kutoka kwenye Pete yake ili wawe Wanasayansi hatari zaidi lakini kwa sharti la kumwonesha
Lango la Kuelekea Duniani. Mfalme Munis alikua na kiu kubwa ya kwenda Duniani, lakini GGB anasema. Siku Moja Steve Mbasa alimwambia Mfalme kua wafanye safari ya Siri kuelekea Langoni kwani wao wanategemea kurudi Duniani.
Walimwambia kua safari hiyo isihusishe mlinzi yeyote wa Mji wa Patiosa. Wala familia ya Mfalme Munis, lakini Mfalme akafikiria kidogo Kisha akawaambia kua ili aweze kutoa nguvu kutoka kwenye Pete ni lazima Mke wake awepo pamoja na Watoto wao wawili Mapacha ambao ni Anna na Alice.
GGB anasema alishangaa sana kuona Steve akisema mambo ambayo hawakukubaliana, Kisha akamwita Steve chemba na kumuuliza ni kwanini alimwambia hivyo Mfalme Munis. Steve akamwambia GGB kua anaitaka Pete ya Mfalme Munis kwani ni ya Miujiza mikubwa sana, GGB anasema wakaingia kwenye mzozano baina Yao lakini Steve Mbasa akamwambia GGB kua wangeitumia pamoja Pete hiyo kua matajiri, Wanasayansi Mashuhuri zaidi Duniani.
GGB anasema alikubali kwa shingo upande huku akijua fika kua wanafanya Kosa kubwa kwa kupanga njama za kuiba Pete hiyo kutoka kwa Mfalme. Basi, walikubaliana na Mashariti ya Mfalme Munis.
Usiku wa siku hiyo, Mfalme aliondoka jumba la Kifalme na familia yake kwa Siri sana, waliongozana na GGB na Steve Mbasa Hadi nje kabisa ya Mji wa Patiosa. Walipofika huko walimwambia Mfalme aiache familia yake kwanza ili akalione lango peke yake Kisha warudi ili wakabidhiane nguvu.
Walianza safari nyingine ndefu kwa kutumia farasi huku Mfalme Munis akiwauliza ni kwanini wameiacha familia yake mbali kiasi kile. Baadaye Mfalme alisimamisha Farasi na kudai kua hawezi kwenda mbali kiasi hicho na kuiacha Familia yake eneo la Msitu lenye Wanyama wakali.
GGB anasema alishangaa uamuzi wa ghafla na wa tamaa wa Steve Mbasa wa kuuchomoa Upanga wa Mfalme Kisha kumlazimisha ashuke kwenye farasi. Kisha haraka Steve Mbasa alimuuwa Mfalme kwa kumkata na Upanga shingoni, akaichukua Pete wakaondoka hapo kwa Mguu na kurejea pangoni Kisha kurudi Duniani.
GGB anasema walipofika nyumbani, Steve Mbasa alimwambia GGB waiamuru hiyo Pete kama ambavyo Mfalme alikua alifanya Kisha Miujiza hutokea. Kitu Cha Kwanza waliamuru kiasi kikubwa Cha pesa kitokee, wote walistaajabu kilitokea kiasi kikubwa Cha pesa, Kila walichosema kilifanyika haraka sana.
Wakakubaliana kua Pete hiyo itakua Yao wote lakini baadaye Steve alimgeuka GGB na kuamua kujimilikisha nguvu zote peke yake. Kwa hasira GGB alifunga safari ya Siri kurudi Kuzimu kupitia pangoni ili akawaambie familia ya Mfalme kua aliyemuuwa Mfalme ni Steve Mbasa, awaambie ndiye anayeimiliki Pete lakini alipofika pangoni hakukuta njia ya Kuzimu isipokua Pango lisilo na chochote.
GGB alilia sana baada ya kutambua kua asingeweza kurudi Kuzimu kwani lango lilikua limejifunga. Aliishi na Siri hiyo kwa Miaka Mingi tokea wakiwa vijana, alizitumia pesa zake alizozipata kwa kufanya tafiti mbalimbali kama Mwanasayansi.
Taarifa ya GGB ilimgadhibisha sana Steve Mbasa. Simu za Waandishi wa Habari na viongozi mbalimbali zilizidi kumtia hasira Steve Mbasa, Kila Mtu alimwona GGB kama Mtu aliyekosa hoja za Msingi za Kisayansi, hakuna Mwanasayansi aliyeamini alichokua anakizungumza lakini alifanikiwa kumchafua Steve Mbasa kwa baadhi ya Watu ambao waliamini hakua Mwanasayansi wa kawaida.
Kuzimu.
Zahoro alifanikiwa kufika pangoni akiwa na maumivu makali sana ya Mguu. Aliugulia maumivu huku akiwaza ni wapi alipo Anna, alijiegemza kwenye jiwe kubwa akiendelea na tafakari.
Mara alisikia kishindo, Kisha alimwona Anna akiingia Pangoni.
“Anna” aliita Zahoro akiwa ameushikilia Mguu wake unaovuja Damu. Taratibu Anna alisogea karibu na Zahoro Kisha alimwambia
“Pole kwa maumivu Zahoro, nilifanya Kila jitihada kuhakikisha unajua salama” alisema Anna huku akihangaika kuwasha moto ili amtibie Zahoro kwa dawa za Mitishamba. Alice alisimama lango la Pango kwa Siri sana akimtazama Zahoro Kisha aliondoka zake.
Basi, Anna aliitumia Mitishamba aliyoifahamu kumtibia Zahoro. Kisha baada ya Dakika kadhaa za kumaliza kumtibia waliketi wakizungumza mawili matatu, Razaro alimuuliza Anna ni wapi wangempata Moana.
Anna alikua akiijua Kuzimu vizuri sana sababu alizaliwa na kukulia Kuzimu, aliujua Mji wa kutisha wa Patiosa unaoongozwa na Mfalme Selasi. Alikaa kimya kidogo, hakutaka kumweleza Zahoro juu ya Siri ya Adui Kimya.
“Wanaweza kua Upande wa pili wa Mto, pengine tunaweza kumpata huko. Unapaswa kupona haraka Zahoro.”
“Ni sawa, siwezi kuruhusu Moana apotee mbele ya Macho yangu.” Alisema Zahoro.
Aliendelea na matibabu ya Mitishamba na mazoezi ya Hapa na pale, Anna alikua akitoka kwenda kuchukua chakula nje, huko alikua akikutana na Pacha wake Alice, walipanga mipango Mingi ya Siri ya Namna ya kuingia Patiosa. Lakini Anna alimweleza Alice kua, Zahoro ni Mwanaume wa maono. Siku Moja kupitia ndoto zake atagundua Siri ya kutoka Kuzimu na kuelekea Duniani.
Maisha yaliendelea, siku zilizogea kwa Kasi huku Zahoro akiendelea kupona majeraha ya Mguu wake. Mara nyingi Zahoro alipokua amelala, Anna alikaa macho ili kumtazama Zahoro kama alikua akiota ndoto ya matumaini.
Usiku mmoja, wakiwa wamelala. Zahoro alianza kutaja jina la Selasi, Mfalme katili wa Mji wa Patiosa, wakati anaiota ndoto hiyo alikua akitokwa na jasho Kali sana. Anna hakujua ni kwanini Zahoro Zahorita Mfalme huyo asiyemjua wala hata kusikia kuhusu habari zake.
Zahoro aliendelea kumtaja Selasi pamoja na Mji wa Patiosa. Kisha alizinduka kutoka Usingizini, akikutana na macho makavu ya Anna.
Alikua mchovu na mwenye wasiwasi sana, aligundua Anna alikua akimfuatilia. Alimtazama Kisha alimwambia
“Nimeuona Mji uitwao Patiosa ukiongozwa na Mfalme mwenye jicho Moja aitwaye Selasi.” Alisema, Anna alistaajabu kwa namna ambavyo Zahoro aliyapatia maelezo hayo kuhusu Mfalme na huo Mji.
“Huo Mji upo hapa Kuzimu, ndiko aliko Moana.” Alisema Zahoro Kisha aliketi sawa sawa halafu akaendelea
“Huko Kuna Siri ya njia ya kuelekea Duniani.” Anna alishtuka, akamuuliza “Siri ipi hiyo” Zahoro alimtazama Anna Kisha akamjibu kwa utaratibu “Jicho la Mfalme Selasi Ndiyo Njia ya kurejea Duniani.”
“Jicho?”
“Ndiyo, hilo ni funguo ya kufungua lango. Jicho lake Hilo amelihifadhi kwa Siri kwenye Gaston maalum. Ni jicho lenye maana Ndiyo maana alilitoa na kulificha, Ndiyo Siri ya yeye kua na jicho Moja” Anna alipoyasikia maelezo haya hakujua afurahi au alie maana yalikua ni maelezo yaliyoshiba haswa.
“Zahoro, natamani wewe na Moana muende Duniani. Munastahili kuishi Sehemu nzuri na salama kuliko hapa” alisema Anna Kisha taratibu alijiegemza kwenye bega la Zahoro.
***
Asubuhi ya Siku iliyofuata, Anna alijikuta akiamka peke yake. Alipoangaza hakumwona Zahoro, alijiweka sawa kiakili kabla ya kutoka ndani ya Pango na kuelekea juu ya Mlima. Alimwona Zahoro akifanya mazoezi ya Upanga, aliachia tabasamu sababu alijua tayari Zahoro alikua ameshapona kwa ajili ya safari ya kuelekea upande wa pili wa Mto.
Pamoja na yote, Bado Anna aliamini siyo muda muafaka wa kumweleza ukweli Zahoro. Japo nafsi yake ilikua ikimsuta lakini aliamini wakati ukifika atamweleza ukweli Zahoro, aliamini kua kwa kuujua ukweli kutabadilisha Imani ya Zahoro juu yake.
Baada ya mazoezi Zahoro alirejea pangoni akiwa imara kuliko wakati wowote huku moyo wake ukimsukuma kuelekea Upande wa pili wa Mto kwa ajili ya kumtafuta Moana. Anna aliendelea kuitafakari ndoto ya Zahoro, aliijua njia mpya ya kupata lango la kuelekea Duniani, ni kwa kuiba jicho la Mfalme Selasi wa Patiosa.
Alishusha pumzi zake Kisha alimuuliza Zahoro.
“Unajisikia kua imara sasa?” Zahoro alimtazama Anna Kisha akamwambia
“Kuliko wakati wowote ule katika Maisha yangu. Nahitaji kufika Patiosa sasa” alisema kwa Ujasiri na kujiamini sana.
“Unapajua?”
“Nina hakika na nilichokiota wakati huu, tuuvuke Mto kwanza kwa mara ya Kwanza” alisema Zahoro, Anna alishusha pumzi zake. Alijua asingeliweza kuizima ndoto ya Zahoro. Akamsogelea Kisha akamwambia
“Kwa ajili ya Moana, nipo tayari kwa lolote. Lakini tunapaswa kua makini sana, pengine si Mji wa kawaida kama unavyoweza kufikiria” alisema Anna, ilibidi watoke waelekee juu ya Mlima. Huko walipata nafasi nzuri ya kuzungumza na kupanga mipango Yao.
Mchana wa siku hiyo walianza safari ya kuelekea Mji wa Patiosa. Anna alikua akiufahamu vyema Mji huo lakini hakutaka kumwambia Zahoro, alijua ni hatari kiasi gani walikua wakiifuata.
Basi, ili asionekane anajua chochote aliigiza kua mwoga kwa Kila hatua huku wakiwa kimya. Walitembea taratibu Hadi walipofika kwenye Kingo ya Mto, mahali ambapo walitengana na Mtoto wao Moana. Walisimama kwa majonzi Kisha Zahoro aliongea kwa sauti ya chini akamwambia Anna
“Nina amini, Mji wa Patiosa una majibu ya maswali mengi. Siri nyingi zitafunguka” alisema akimtazama Anna ambaye alianza kuonesha Mashaka huku akijiuliza kama Zahoro aliota jambo lingine aliloamua kulifanya Siri. Wakati wakiwa hapo wanazungumza, Alice alikua amesimama kwa mbali akiwatazama.
“Kuna jambo lingine uliliota?” akauliza Anna. Zahoro akamjibu
“Hakuna zaidi ya nilicho kusimulia. Lakini Nina uhakika na Mji wa Patiosa, utaenda kutegua kitendawili” Alisema Zahoro Kisha alimshika mkono Anna wakashuka taratibu Hadi chini, Zahoro alionekana kua makini sana, aliangaza huku na kule kabla ya kuanza kutafuta Mtumbwi.
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx
4 Comments
I loved as much as youll receive carried out right here The sketch is attractive your authored material stylish nonetheless you command get bought an nervousness over that you wish be delivering the following unwell unquestionably come more formerly again as exactly the same nearly a lot often inside case you shield this hike
https://shorturl.fm/jXcQc
Adimin unachelewa sana adi tunasahau
Thanks I have recently been looking for info about this subject for a while and yours is the greatest I have discovered so far However what in regards to the bottom line Are you certain in regards to the supply