Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 01
Hapakua na sauti yoyote iliyosikika, hapakua na Ndege wala wadudu waliopiga kelele. Ghafla Zahoro alisimama, akatoa ishara kwa Anna kusimama pia
Sauti ya ajabu ilianza kusikika kama kuna kitu kikubwa kinakaribia kutokea juu. Zahoro, aliyekuwa ni mtu wa tahadhari, hakutaka kugeuka haraka. Badala yake, alivuta hisia zake kwa umakini zaidi. Taratibu, aligeuka na kutazama juu— palikuwa na nyoka mkubwa mweusi aliyekuwa akishuka kwa taratibu, kwa mtindo wa kuvizia.
Endelea
SEHEMU YA PILI
Mlilio wa ajabu wa nyoka huyo ulizidi kuongezeka. Kwa tahadhari kubwa, Zahoro alianza kuuchomoa upanga wake aliouweka nyuma ya kiuno. Alijua fika kuwa yule nyoka alikuwa mwindaji hatari. Taratibu, nyoka alianza kuishusha shingo yake, akielekea kwao.
Ghafla, kwa kasi ya ajabu, Anna alichomoa upanga wake na kukata kichwa cha nyoka huyo kwa kishindo.
“Tukimbie!” alisikika Anna akipiga kelele kwa sauti ya juu. Hakukuwa na siri tena kuhusu adui yao—Kimya.
Papo hapo, nuru nyekundu ikaja kwa kasi ya ajabu kutoka nyuma yao. Zahoro alimwongoza Anna mbele, na wote wakaanza kukimbia kwa kasi kuelekea mtoni. Nuru hiyo haikuacha—iliendelea kuwafuata kwa kasi isiyo ya kawaida.
Mara ghafla, wote walisimama. Ile nuru nyekundu ilikuwa tayari mbele yao. Wote walibaki kimya, wakifunika macho yao kwa kutumia vitambaa vyeusi.
Taswira ya jicho Moja kubwa ilionekana kwenye ule mwanga mwekundu, hakuna walichokiona kwasababu walikua wamefunga macho Yao.
“Mko wapi?” ilisikika sauti iliyotoka kwa kunong’ona pole pole. Ilizidi kuwaonesha kua walikua kwenye hatari kubwa sana. Kwa mbali pia walikua wakiisikia sauti ya Maji ya Mto yakitiririka, lile jicho lilizidi kusogea huku likiwatazama kama masanamu yaliyo tengwa. Moana alikua ametulia tulii Mgongoni kwa Anna, yeye alikua amefundishwa Kila kitu kuhusu Adui Yao aitwaye KIMYA.
Upepo wa taratibu uliendelea kuvuma na kusukuma majani, sauti ilizidi kuuliza. Ilikua ni sauti ya Kike Iliyo hatari zaidi tena ilitoka kwa vitisho vikubwa sana
“Nataka niwaone, mko wapi?” iliendelea kuuliza, ilikua ni sauti yenye nguvu za ajabu, ilisikika zaidi kwenye vichwa vyao. Walisimama kama askari, wakiwa kimya kuliko kawaida.
Walijizuia hata kupumua kwa nguvu maana Adui Yao aliweza kusikia sauti Kisha macho Ndiyo huona. Anapokutazama usoni, basi safari ya Maisha Yako huishia hapo
Zilipita dakika tano za ukimya Kisha lile jicho lilijifunga, papo hapo ule mwanga mwekundu nao ulitoweka. Kisha Hali ya Ukimya iliendelea, Angalau sasa walishusha pumzi zao, wakaondoa vitambaa usoni mwao. Hali ilionekana kua shwari, kwa mbali kidogo sauti ya kutiririka kwa Maji ilisikika
Zahoro akamwuliza Anna kwa ishara kama alikua yupo salama, Anna aliitikia pia kwa kutumia ishara ya kichwa, Kisha safari Yao iliendelea kwa kuuruka kidogo mwili wa nyoka mkubwa. Walitembea taratibu sana na kwa tahadhari kubwa, sasa walikua na kiu ya kuufikia Mto ambao waliamini ungewapeleka mbali zaidi kuliko kutembea kwa Miguu.
Jua lilipofika utosini liliwakuta wakiwa wamesimama wakiutazama Mto mbele Yao, walikua wakitabasamu kwa Uchungu. Bado palikua kimya sana. Zahoro akampa Anna ishara kua wamsubirie hapo, taratibu alishuka Hadi Mtoni, Kisha aligeuka na kumtazama Anna pamoja na Mtoto.
Kimya kilikua kimetawala sana, aliyatumia macho yake kuangaza huku na kule kwa tahadhari zaidi lakini pia alihitaji kutafuta kitu ambacho kingeweza kuwasafirisha. Aliangaza zaidi na zaidi Kisha aliuwona Mtumbwi mmoja uliojificha kwenye miti midogo kando ya Mto, alisogea hapo haraka Kisha aliupapasa Mtumbwi kwa kutumia vidole vyake.
Chozi lilimtoka, alitamani asiamini kama alikua amepata usafiri. Aliuvuta taratibu Hadi kwenye Ukingo wa Mto. Aliutazama ulikua ni Mtumbwi uliokaribia kuoza lakini angalau ungeweza kuwasogeza mbali kidogo, aligeuka kumtazama Anna.
Anna hakuwepo eneo alilomwacha, mara ya Kwanza alihisi labda macho yake yalimdanganya lakini alipoangalia vizuri palikua patupu. Moyo ulianza kumwenda mbio, haraka Alikimbilia juu alipomwacha Anna na Mtoto.
Alimkuta Anna akiwa ameshikiliwa na Mwanaume Mmoja mweusi, mnene mwenye tumbo kubwa. Alikua ameshikilia kisu Kisha alimpa ishara Zahoro asifanye chochote vinginevyo angemuuwa Anna. Mikono ya Zahoro ilitetemeka kwa hasira, alitamani kupambana lakini eneo Hilo lilipaswa kua Kimya zaidi. Akamuuliza yule Mwanaume kwa sauti ya kunong’ona
“Unataka nini?” swali hili lilijibiwa na Kicheko Cha Mwanaume huyo, Kicheko Cha chini chini kilichojaa daharau za kutosha.
“Nataka mfe badala yetu, Kisha sisi tuondoke hapa kwa kutumia Ule Mtumbwi kule chini” aliposema hivi, Zahoro aligeuka. Akamwona Mwanaume mwingine aliyevalia nguo zilizo loa Damu akiuburuza Mtumbwi ndani ya Maji.
“Washenzi….” Alisema kwa hasira ya chini Zahoro, ule Mtumbwi Ndiyo tumaini pekee kwao. Aligundua kua huwenda Kuna Watu wengi walionasa kwa Miaka Mingi kama wao.
“Sawa, unataka tufanye nini?” aliuliza Zahoro kwa sauti ile ile ya chini lakini iliyojaa hasira isiyovumilika, alikunja mikono yake lakini hakuwa na la kufanya.
“Sawa. Nataka msimame hapa juu mpige kelele, wakati sisi tunaondoka na Mtumbwi” alisema yule Mwanaume, lengo lake likiwa zisikike kelele ili Adui Kimya akisikia basi apoteze muda kuwadhuru akina Zahoro ili wao waondoke hapo. Wakati anaongea hivi, kule chini mwenzie alikua akimsubiria.
Anna alikua akitetemeka, Mtoto alikuwa Mgongoni Kisha yule Mwanaume akawaambia
“Nitamchukua Mtoto, msipofanya hivyo basi sisi na Mtoto tutakufa. Lakini mkitii, Mtoto ataishi nasi” alisema kwa dharau tena kwa sauti ile ile ya chini, hapakua na chaguo Bali kuwasikiliza.
“Mpatie” alisema Zahoro, Anna alibubujisha machozi. Hakutegemea kama angetengana na Moana kwa staili hii katili sana. Alimshusha Moana taratibu huku akiwa anatokwa na machozi
“Utakua salama Moana” Anna alimwambia Moana aliyekua Bado angali na kitambaa usoni pake kumkinga na Macho ya Adui Kimya.
“Mama‼” aliita Moana kwa sauti ya chini, haraka yule Mwanaume akamkwapua Moana kutoka chini, akamwekea kisu kidogo shingoni Kisha akasema
“Fuateni nitakacho kisema” alisema kwa tahadhari sana, Kisha aliachia tabasamu. Hakuonekana kua Mtu mwema kabisa na wala Zahoro hakumtambua Mtu huyo kama alitoka Kijijini kwao Nzena lakini pengine labda ni miongoni mwa wageni waliopotea na Kijiji.
Taratibu alishuka na Moana Hadi chini, Kisha aligeuka na kuwatazama akawapa ishara ya tusi kwa kutumia kidole, chozi lilimbubujika sana Anna. Kilio Cha ndani Cha Kiume kilimshika Zahoro.
Moana alikua ni zaidi ya Mtoto kwao, walimfundisha Ujasiri, walimpa mbinu nyingi za kukabiliana na Adui Yao Kimya. Hawakua na namna ya kufanya isipokua kufanya kama walivyoambiwa ili kumlinda Moana. Hata wao waliamini upande wa pili wa Mto huo kulikua na Maisha ya Watu wengine, pengine palikua salama zaidi ya hapo walipo.
Walimsindikiza Mwanaume yule Hadi alipopanda kwenye Mtumbwi, Kisha walianza kuyakata Maji ya Mto taratibu kuondoka hapo huku chozi la huzuni na maumivu likiwa linamtoka Moana. Bado alikua na kitambaa usoni lakini aliweza kupata hisia Kali ya maumivu isiyostahimilika.
Kelele za Kasia zilianza kusababisha Hali ya Upepo wa ajabu sana huku mwanga mwekundu ukija kwa Kasi kutokea Msituni. Anna akamwambia Zahoro
“Lazima tumsaidie Moana, hawezi kufa machoni mwetu” alisema kwa hasira huku akiwa anabubujisha chozi lake, akawa wa kwanza kupanda juu ya Jiwe kubwa, akahakikisha Buti zake zikikamata vizuri. Kisha alimeza funda zito la mate akiwa anatazama Mtumbwi uliokua ukizidi kusonga mbele kwa Kasi sana.
Razaro naye akapanda juu ya jiwe, kazi ikawa Moja tu kuhakikisha Moana anaondoka salama japo na Watu ambao hata wao hawawajui kabisa. Iliwalazimu kupiga kelele ili ule mwanga mwekundu usiufikie Mtumbwi, walipiga yowe. Ule Mwanga pamoja na Upepo vilisimama mahali Kisha vikageuza uelekeo na kuanza kuwafuata wao.
Wakaruka kutoka juu ya jiwe Kisha wakazama Msituni na kuanza kukimbia kwa Kasi sana, waliamua kurejea kule pangoni. Mahali ambako waliishi kwa Usalama kwa Miaka Mingi. Walikua ni Watu wa mazoezi waliozoea Maisha ya Hela heka, ikawa mfukuzano wa Kasi sana baina Yao na ule Mwanga.
Walipoona ule mwanga unakaribia kuwafikia, waliamua kujificha nyuma ya jiwe Moja. Walikua kimya huku wakiwa wameshajifunga vitambaa usoni mwao, walihakikisha hawawezi kuona mbele. Upepo mkali ulisogea taratibu Hadi walipo, matawi ya Miti yalikua yakichezacheza kwa Kasi kutokana na ule Upepo.
Walibana pumzi zao vizuri, walianza kuisikia sauti ya Mwanamke. Sauti iliyowauliza
“Mko wapi?” ilikua ni ile sauti ya ajabu ya kunong’ona. Ikiambatana na Kicheko Cha chini chini.
“Nawaona” iliendelea sauti hiyo huku Zahoro akiwa amejikausha kimya, ile sauti Ikawa inakuja karibu na walipo kwa juu, Zahoro akampa ishara Anna kua wanapaswa kutengana kwa muda ikiwezekana wakutane pangoni. Mwanga ulizidi kusogea huku Upepo ukiwa unakaribia walipokua wamejificha.
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
38 Comments
https://shorturl.fm/q23OW
Usually I do not read article on blogs however I would like to say that this writeup very compelled me to take a look at and do so Your writing taste has been amazed me Thanks quite nice post
https://shorturl.fm/crtVY
https://shorturl.fm/BcZBF
Your blog is a true hidden gem on the internet. Your thoughtful analysis and engaging writing style set you apart from the crowd. Keep up the excellent work!
https://shorturl.fm/nZte4
5c49fh
My brother suggested I might like this website He was totally right This post actually made my day You cannt imagine just how much time I had spent for this information Thanks
zpj39h
https://shorturl.fm/YcKMb
Every time I visit your website, I’m greeted with thought-provoking content and impeccable writing. You truly have a gift for articulating complex ideas in a clear and engaging manner.
https://shorturl.fm/ibnTo
https://shorturl.fm/eteJG
I’ve been following your blog for quite some time now, and I’m continually impressed by the quality of your content. Your ability to blend information with entertainment is truly commendable.
https://shorturl.fm/Y7G0W
https://shorturl.fm/COCIP
https://shorturl.fm/5ExgC
https://shorturl.fm/jArrd
https://shorturl.fm/2DX0v
https://shorturl.fm/aBp59
https://shorturl.fm/K7Cr5
Its like you read my mind You appear to know a lot about this like you wrote the book in it or something I think that you could do with some pics to drive the message home a little bit but instead of that this is fantastic blog An excellent read I will certainly be back
https://shorturl.fm/NdTC7
I do believe all the ideas youve presented for your post They are really convincing and will certainly work Nonetheless the posts are too short for novices May just you please lengthen them a little from subsequent time Thanks for the post
https://shorturl.fm/CoyEJ
https://shorturl.fm/LrTYW
p532z7
https://shorturl.fm/cTI6B
https://shorturl.fm/JcpPg
mqrgj7
1zw4pu
https://shorturl.fm/MIDeY
https://shorturl.fm/EnkTw
https://shorturl.fm/2nCzT
https://shorturl.fm/NKWXw
https://shorturl.fm/SdR2Z
https://shorturl.fm/rJNDq
https://shorturl.fm/RMmnC