Mvua kubwa ilikua ikinyesha, baridi Kali lilikua limekivamia Kijiji Cha Nzena.  Giza nalo tayari lilikua limeshatua, palikua Kimya. Pazia la chumbani kwa Zahoro lilifunuliwa, Mzee Miroshi alikua amesimama akimtazama Zahoro aliyekua  Usingizini. 

Mwanga hafifu wa kibatari ulikua ukiendelea kukifanya chumba Kiwe na Nuru  kidogo, Mzee Miroshi aliingia chumbani Kisha aliketi juu ya kitandan Cha Kamba  alicholala Mwanaye 

Aliutazama uso wa mwanawe kwa muda mrefu, kana kwamba alikuwa akijifunza  kitu kutoka katika kila mstari wa uso wake. Pumzi yake ilikuwa nzito, macho yake  yakionesha huzuni iliyojificha kwa miaka mingi. 

“Zahoro…” aliita kwa sauti ya chini sana, karibu kama mnong’ono, lakini kijana  huyo hakuamka. Mvua iliendelea kupiga dari ya nyasi kwa nguvu, kila tone  likiambatana na sauti kama ya dondosha ya mshituko. 

Mzee Miroshi alinyosha mkono wake polepole, akaushika mkono wa Zahoro.  Mikono ya kijana huyo ilikuwa baridi—baridi isiyo ya kawaida, kana kwamba  mwili wake haukuwa na uhai. 

“Samahani, mwanangu,” alizungumza tena kwa sauti ya chini, “lakini kuna jambo  lazima lifanyike kabla ya alfajiri.” 

Ghafla, nje ya chumba, paka mweusi alilia kwa sauti ya kutisha. Mbwa wa jirani  wakaanza kubweka kwa hofu. Ndani ya chumba, mwanga wa kibatari ulianza 

kuyumba-yumba, kana kwamba ulikuwa ukipigana na upepo wenye nguvu isiyo onekana. 

Mzee Miroshi alisimama, akafungua mfuko mdogo wa ngozi alioubeba tangu  asubuhi. Ndani yake kulikuwa na kitu kilichofunikwa kwa vitambaa vitakatifu vya  miaka mingi. Alikitoa kwa hofu na kumtazama mwanawe kwa mara ya mwisho  kabla ya kuanza kulia kimya kimya. 

Kimya cha kijiji kilikatizwa na mlio wa radi kali—na hapo ndipo kila kitu kilianza  kubadilika… 

Radi ilipopiga, mwanga wake uliangaza kwa sekunde chache chumba cha Zahoro,  na kwa mara ya kwanza, Mzee Miroshi aliona kivuli kikisimama pembeni ya  mlango wa chumba hicho. Moyo wake uliruka. Hakuweza kusogea. Kivuli hicho  hakikusogea pia, kilionekana tu kama kimya kilicho hai—kikitazama. 

Alifumba macho, akavuta pumzi ndefu, kisha akakifunika tena kile kitu alichokitoa  kwenye mfuko wake wa ngozi. Alijua hakikuwa wakati wa kukikabidhi bado, japo  ndicho kitu pekee kinachoweza kumlinda Zahoro na kuvunja kile alichoamini  kuwa ni laana ya Bi. Lugumi. 

“Usiingilie muda,” sauti ya kike ilisikika ikinong’ona karibu na sikio lake.  Aligeuka kwa haraka, lakini hakuona mtu. Jasho lilianza kumtoka. Alijua alikuwa  amechelewa. Alijua macho ya kale yanamtazama, yakihoji, yakimlaumu. 

Zahoro alianza kuhema kwa nguvu, uso wake ukionekana kuteseka na ndoto nzito.  Alipiga kelele moja, kisha akanyamaza tena ghafla—kimya kama kifo. Mzee  Miroshi alinyanyuka haraka na kumtikisa, “Zahoro! Mwanangu, amka!  Usimruhusu akuone!”

Lakini Razaro hakuamka. Badala yake, midomo yake ilianza kunong’ona maneno  yasiyoeleweka—lugha ya kale, isiyo ya kawaida. Mwanga wa kibatari ukazima  ghafla. Giza likatawala. 

Ndani ya giza hilo, sauti ya mtoto ikasikika kutoka kona ya chumba. “Mbona mmechelewa tena…?” 

Sauti hiyo ilimfanya Mzee Miroshi asimame barabara, uso wake ukiwa mweupe  kama karatasi. Alijua sauti hiyo. Ilikuwa ya Masumbuko—mtoto wa kwanza wa  kijiji aliyechukuliwa miaka mingi iliyopita, usiku kama huo. 

Papo hapo, Zahoro alishtuka kutoka Usingizini na kugundua ilikua ni ndoto mbaya  iliyomshtua. Jasho lilikua likimtoka, ndevu nyingi zilikua zimemwota. Umri wake  haukua ule wa awali, Miaka Thelathini ilikua imepita tayari 

Alikua ndani ya pango, Miaka yote hakufanikiwa kutoka ndani ya Kijiji Cha  Nzena, Kijiji kilicholaaniwa. Aliishikilia Sehemu ya kifua ambayo moyo hukaa  hapo, alihisi mapigo yasiyo ya kawaida. Aliitazama Kando yake, palikua na  Mwanamke aliyelala pamoja na Mtoto wa Miaka mitano. 

Taratibu Zahoro alinyanyuka. Alishafikisha Miaka 52, alikua Mwanaume  aliyekamilika lakini aliyechoka Maisha ya kutisha. Alisogea taratibu Hadi nje ya  Pango, akasimama juu ya Mlima na kulitazama jua likiwa linazama.  

Macho yake yalikua mazito sana, yalijaa uzito usio wa kawaida. Alijilazimisha  kulitazama jua Kisha akauliza 

“Kanakwamba unanitazama na huwezi kunisaidia?” jua liliendelea na safari yake  kama vile halikusikia swali lililoulizwa, Zahoro alikohoa kidogo kabla ya kuisikia  sauti nyuma yake 

“Hujachoka?” ilikua ni sauti ya Kike, nyuma yake alisimama Mwanamke  aliyemtazama Zahoro kwa jicho kavu. Zahoro alipogeuka akasema

“Anna, aliyechoka ni yule aliyepata. Nafikiria kuhusu Binti yetu Moana, bahati  mbaya kwake hajawahi kumwona Binadamu tofauti na Mimi na wewe” alisema  kwa huzuni sana Zahoro. 

“Mh! Nani angefika Kuzimu Baba Moana, tumesubiria sababu ya kurudi Duniani  kwa Miaka yote Hadi tumepata Mtoto huku. Wote wamekufa, ni sisi pekee Ndiyo  tunaishi huku” alisema Kisha akamsogelea karibu Zahoro. 

“Tuna Kila sababu ya kufanya safari kutoka hapa. Tukatafute Sehemu nyingine ya  Kuzimu, pengine Kuna Mji mwingine uliopotea kama Kijiji Cha Nzena” alisema  Zahoro. 

“Sawa, lakini sasa Adui yetu ni Kimya. Ni ngumu sana kupambana na Adui  anayewinda Sauti Zahoro, lakini kuendelea kuishi pangoni hakutasaidia, ni Bora  tufanye safari kama ulivyosema”Alisema Anna. Taratibu aliondoka na kurejea  pangoni. 

Razaro hakuacha kulisindikiza jua likizama mbele ya macho yake, Kisha Nuru ya  Giza iliingia, alitembea Kurudi ndani ya Pango. 

*** 

Siku iliyofuata, Zahoro, Mtoto Moana pamoja na Anna. Walikua tayari kwa ajili ya  kuondoka ndani ya Pango ili kutafuta Makazi mengine. Ilikua ni huzuni kuondoka  ndani ya Pango Hilo salama ambalo waliishi kwa Miaka Thelathini. 

“Baba, tunaenda wapi?” aliuliza Moana, alikua amevalia nguo chakavu. Zahoro alichuchumaa na kumwambia Moana kwa sauti ya utaratibu sana. 

“Tunaenda kuishi Sehemu nyingine salama zaidi. Usijali” Moana aliachia  tabasamu, sura yake ya mviringo na macho ya kudumbukia ndani vilimfanya  aonekane ni Mtoto mzuri sana, bila kujalisha wanaishi Maisha gani alikubaliana na  Hali halisi licha ya kuisikia TU Hadithi ya Dunia ilivyo. 

Walibeba chakula kidogo walichobakiwa nacho, mizizi na baadhi ya mabaki ya  nyama. Kisha Zahoro akamfunga kitambaa usoni Moana, halafu wao wakajiweka  sawa kwa kulegeza vitambaa kichwani.

Adui Yao Mpya alikua ni KIMYA. Yeye ni Adui waliyemwogopa sana kuliko sauti  ya Bibi Lugumi. Waligeuka kulitazama Pango kwa huzuni sana, waliishi hapo kwa  usalama kwa Miaka Mingi.  

Taratibu Anna alimtazama Zahoro, ulikua ni wakati wao wa kuondoka. Walianza  safari taratibu, kwa utulivu wa Hali ya Juu sana. Walishuka kutoka Kilimani Kisha  waliupa mgongo. 

Taratibu wakaingia Msituni huku lengo lao likiwa ni kuelekea Mtoni, wasafiri  kupitia Maji ya Mto huo.  

Msitu ulikua kimya na wenye kutisha sana, palikua na kinvuli Kila walipopita  kutokana na Kua na miti mingi mikubwa. Majani mengi yaliyooza yalikua aridhini,  hapakua na njia rasmi isipokua vichochoro. 

Anna alikua amembeba Moana Mgongoni, Zahoro alikua ameshikilia kifurushi  Cha chakula. Mioyoni Yao ilizungumza zaidi, huku lugha pekee waliyokua  wakiitumia ilikua ni ishara. 

Zahoro alikua ndiye kiongozi wa msafara, alihakikisha anafanya awezalo waufikie  Upande wa Pili wa Mto. Wakiamini pengine wangeliweza kupata msaada huko,  anga lilikua la kahawia, huku jua Kali likiendelea kuwaka. 

Hapakua na sauti yoyote iliyosikika, hapakua na Ndege wala wadudu waliopiga  kelele. Ghafla Zahoro alisimama, akatoa ishara kwa Anna kusimama pia 

Sauti ya ajabu ilianza kusikika kama kuna kitu kikubwa kinakaribia kutokea juu.  Zahoro, aliyekuwa ni mtu wa tahadhari, hakutaka kugeuka haraka. Badala yake,  alivuta hisia zake kwa umakini zaidi. Taratibu, aligeuka na kutazama juu— palikuwa na nyoka mkubwa mweusi aliyekuwa akishuka kwa taratibu, kwa mtindo  wa kuvizia. 

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

5 Comments

  1. Somebody essentially lend a hand to make significantly articles Id state That is the very first time I frequented your website page and up to now I surprised with the research you made to make this actual submit amazing Wonderful task

Leave A Reply

Exit mobile version