Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Kibu Kuna Muda Ni Lazima Kukubali Kufanya Maamuzi Magumu
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Kibu Kuna Muda Ni Lazima Kukubali Kufanya Maamuzi Magumu

    Oscar EvodiusBy Oscar EvodiusMay 3, 2024Updated:May 3, 202419 Comments2 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Kibu Denis wa SIMBA
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kibu Denis Prosper ndio ajenda iliyopo mezani kwa sasa na Tanzania nzima ipo mezani kujadili mada hii! Kwanza sipo hapa kuzungumza kuhusu Takwimu za Mchezaji wala kuchagua upande wowote kuhusu hili bali nasimama hapa kwenye uhalisia

    Sidhani kila mmoja kama anajiuliza maswali haya ninayojiuliza Mimi!  Moja, Je ni kweli Thamani inayotajwa inafaa kusimama kwa Mchezaji husika? Je, hiyo pesa ambayo anahitaji ni sahihi Simba kuitoa kwa sasa? Tatu, Simba hawawezi kupata mchezaji mzuri kwa pesa hiyo? Nne, Kwanini Simba matukio ya hivi yananirudia sana? Simba wanahitaji kutoka wapi na kwenda wapi?

    Baada ya kumaliza kujibu maswali hayo nadhani umeanza kupata picha taratibu, binafsi sina upande wowote ila ukweli ni kwamba nyakati kama hizi Menejimenti nyingi za wachezaji ndio sehemu zao na wanajua namna ya kucheza nazo ukikaa vibaya utashindwa kwenda njia sahihi kwa wakati huo kutokana na msukumo uliopo nje

    Kinachofanywa ni mchezaji kupandishwa Thamani kwa Mchezaji ambapo mara nyingi Timu Pinzani, Waandishi wa habari na Vyombo vya habari na vingine hutumiwa kwa kiasi kikubwa sana kusukuma Thamani ya kitu husika kwa wakati huo hivyo usipokuwa makini utaacha njia yako na utatembea kwenye njia yao bila kujua

    Labda nitoe vitu vichache tu ambavyo vinafanya Thamani ya mchezaji kuwa kubwa ambapo vichache ni Umri wa mchezaji husika, kiwango chake kwa wakati huo na Thamani ya mkataba wake kwa sasa! Chukua hivyo vitu vichache kisha vitumie kwenye mada iliyopo mezani kuhusu Kibu Denis ndani ya Simba SC halafu chukua hapo juu vile vitu ambavyo nisema vinatumiwa kupandisha Thamani ya mchezaji

    Last! Kama unahitaji kupiga hatua kubwa kutoka ulipo basi kuna muda ni lazima kukubali kufanya maamuzi magumu ambayo yataendana na mipango yako kwa wakati husika, THAMANI DHIDI YA MABADILIKO 🇹🇿

    Let’s Go!!.

    SOMA ZAIDI: Simba SC Na Roho Ngumu Kwa Mtibwa Sugar Ligi Kuu

    kibu denis mkataba wa kibu simba

    19 Comments

    1. Ochu master on May 3, 2024 11:56 am

      Tatizo ni kuwa hajafanya makubwa Simba… Hata akiondoka barida tuu 😂😂😂

      Reply
      • Abdul on May 3, 2024 12:07 pm

        Aende tu

        Reply
    2. milles1410 on May 3, 2024 11:58 am

      Madhara ya kuruhusu watu wa nje ya kazi kukushauri, iko hivi Kibu Denis ni mchezaji wa kawaida sana ila anajazwa kiburi na wachambuzi na mashabiki ndo maana anajiona anastahili malipo zaidi ya hapo alipo lakini uhalisia wakubaliane abakie Simba ili afanye Improvements lakin kuhama Tim sio best option
      Milles^

      Reply
      • Weldo Edmond on May 3, 2024 12:26 pm

        Of course yes 👌 nakubaliana na wewe

        Reply
      • Jomokeys77 on May 3, 2024 5:06 pm

        Sasa kama ni kawaida, kwanini Simba wanamlazimisha kusaini. Wamwache aende kama ni wa kawaida 😂

        Reply
    3. Makoye Malonja on May 3, 2024 11:59 am

      Nafikiri wanasimba hawanabudi kumuacha Kib D akatafute changamoto zingine maana hiyo ni kazi yake Zaid lazima angalie kuliko na manufaa Zaid maana anaandaa kesho yake but awe mwangalifu Kwa uchaguzi atakao ufanya

      Reply
    4. Peter Ignas on May 3, 2024 12:11 pm

      Kama anaenda aende tu, wakajazane yanga, mana tumechoka kila matukio Simba hayaishi

      Reply
    5. Imma MK on May 3, 2024 12:20 pm

      Naongea ukweli mchungu Kibu ni mchezaji mzuri hatukatai ila anatakiwa ajue kama kamaliza mkataba wake ndani ya Simba njia bora kwake na kwa Simba ni aongeze tu mkataba ila kuhusu swala la kuachana na Simba na kutegemea apate Team bora kuliko Simba ndani ya nchi na nje ya Nchi hilo ni swala zito sana lina fikirisha sana sana atapata Team zenye uwezo wa kawaida tu sio zile Big Profile…✍️

      Reply
    6. Peter Ignas on May 3, 2024 12:21 pm

      Kama anaenda aende tu, wakajazane yanga, mana tumechoka kila tukiamka matukio Simba hayaishi,

      Na hapo bado mana utasikia chama nae kaliamsha huko mara kidogo utaskia inonga nae, hujakaa vizuri utasikia chemalone mara ngoma

      Kwa style hii tutauana kwa stress

      Reply
    7. [email protected] on May 3, 2024 12:23 pm

      Huu ndio wakati sahihi WA Simba kuachana na kibu Denis de Ili zije damu mpya zenye uchu na mafanikio kuliko kuendelea na Hawa wachezaji ambao hâta umri wao umeenda

      Reply
    8. Gwaks on May 3, 2024 12:35 pm

      Ifike mahali watu wajue mpira ni kazi,
      Mfano; Ukiambiwa huku tutakupa 15 million/month, na ulipo unalipwa 8 na mkataba unaisha na unawaambia wakupandishie hawataki, Je utabaki hapo? Kwa upande wangu mimi siwezi kubaki! Sasa ya nini maneno kumsema Kibu, ww baki na mapenz yako ya ushabiki, mchezaji yupo kazini na ni lazima aangalie kwenye maslahi yake binafsi kwanza kwasababu yeye tayar ni pro kwa Tz

      Reply
    9. Ki aziz on May 3, 2024 1:25 pm

      Aje yanga ale matunda ya nchi

      Reply
    10. Ki aziz on May 3, 2024 1:28 pm

      Aje yanga ale mema ya nchi

      Reply
    11. Tajiri ABAS on May 3, 2024 1:37 pm

      Aje kwa wananchi huku kumenogaaa,huko msimbazi anapoteza uwezo wake na kipaji chake,

      Tajiri Abaaas- MWANZA.

      Reply
    12. Peter Airtel on May 3, 2024 2:40 pm

      Kafanya mengi aondoke tu

      Reply
    13. Calvin's HD on May 3, 2024 2:49 pm

      Kwa thamani iliyopo mezani ni thamani tofauti na thamani ya mchezaji mwenyewe, Maana yake nini mchezaji thamani yake kwanza huanza pale anapokua na mchango positively Kwa timu. Kibu ana mchango ila Siwa thamani hii, Kwa nafasi yake alitakiwa kuwa na mchango zaidi ya tunaouona Kwa Sasa hivyo wake Maza Moja wafanye Negotiation

      Reply
    14. Young ramson on May 3, 2024 7:59 pm

      Kwa kibu bado mapema Sana kufanya maamzi ya kuihama Simba. kwa Sasa atulie huku akiimarisha ubora wake kwan Kila mchezaj mzaw anahitaj kua Kama SAMATA hivo inahjitaj kuvumilia ili kuyafikia malengo. Isitoshe kibu anahitaj kuimarisha uwezo wake ili akitoka simba aende kilabu kubwa Zaid ambayo itampa mafanikio aliyo kuwa anahitaj. Huwez kutoka Simba ukaenda YANGA Wala AZAM, unakua unajirudisha nyuma mwenyew. KIBU TULIA MAFANIKIO YAKO YAPO HAPO ULIP ILA UKTOKA KABLA NDO TUMEKUSAHAU HIVO.✍️✍️🤝🤝

      Reply
    15. Pingback: Pamba Jiji FC Ni Mkombozi Wa Soka Na Maisha Mwanza? - Kijiweni

    16. Gasto on May 8, 2024 12:21 pm

      Mwanetu kibu akitaka kusepa asepe tu hakuna halicho fanya kikubwa akiwa pale unyamani

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.