Ilipoishia sehemu ya tisa ya In the name of LOVE
“Kumbe haikua inshu kubwa sana Mpenzi, Presha ilipanda kidogo. Ah! Mama yangu naye akalikuza sana” alisema huku naye akichukua kipande Cha tunda kwa kutumia mkono wake Kisha akaliweka Mdomoni.
“Na vipi kuhusu hiyo simu, una furaha sana”
“Eeh! Mama alikua akinipa mrejesho kuhusu Hali Baba” alisema Zaylisa. Niliguna tu Kisha niliendelea kula matunda.
Siku iliyofuata asubuhi mapema, Zaylisa aliniaga kua anaenda kumjulia Hali Baba yake, tukakumbushana kua ilikua ni siku ya Clara kurudi kutoka Arusha. Endelea
SEHEMU YA KUMI
Zaylisa alipoondoka, niliitafuta tena lile Bahasha yenye jina langu, haikuwepo popote pale, niliitafuta sana lakini halikuwepo, jasho lilikua linanitoka. Nilipoona kua siwezi kuipata nilielekea bafuni kwa ajili ya kuoga, nilipomaliza kuoga Maji ya baridi nilirudi chumbani na kuanza kujifuta Maji, mara nilisikia ‘alam’
“Mh! Itakua Clara huyo” nilijisemea tu, nilimalizia kujifuta Maji. Kisha nilitoka chumbani taratibu nikaelekea sebleni, nilimkuta Matilda akiendelea na usafi, aliponiona alinisalimia
Baada ya salamu Niliketi kochini nikisubiria kuambiwa kua Clara alikua amerudi, kwakua tulikwaruzana alipoondoka sikutaka kuonesha Wazi kua nilikua najali kuhusu yeye maana niliamini hakupenda niendelee kuishi kwake, nilijishughulisha na kuangalia Televisheni.
Matilda aliendelea na kazi zake bila kusema chochote kile, nilizuga kwa muda kidogo. Nilipoona kua Matilda hawezi kusema chochote nilijikoholesha Kisha nikamuuliza
“Dada Yako hajarudi?” niliuliza kwa sauti iliyoonesha kutojali. Matilda alinitazama Kisha akanijibu kwa sauti ya utaratibu
“Ndiyo” nilimtazama
“Hajarudi? Wakati nimesikia Mtu akibisha hodi?”
“Walikosea nyumba, ni mafundi wa Umeme” alisema.
“Aah! Unafikiri najali sana? Hapana wala sijali” nilisema ili kumwonesha Matilda kua nilikua sijali kuhusu Clara lakini ukweli ni kwamba licha ya yote ila yeye alisaidia Maisha yangu.
“Haujali kuhusu nini?” aliniuliza kwa sauti ya utaratibu iliyojaa heshima.
“Ah! Nazungumza mwenyewe” nilizuga Kisha niliondoka pale sebleni nikarudi chumbani. Nilihisi kutamani sana kumwona Clara japo nilikua na hasira naye, sikujua Hali ile ilitokana na Nini.
“Kwanza sijali kuhusu wewe, urudi au usirudi wala hainihusu Mimi” nilijisemea kwa sauti ya kunung’unika. Nilihisi Kuna Upendo Fulani ndani yangu juu ya Clara lakini sikujua ulikua Upendo wa aina gani.
Mara sauti ya Alam ya Getini ililia tena, Ilinishtua. Nikafungua mlango haraka ili nikaangalie ni Nani aliyekua getini, nilipofika sebleni nilimwona Matilda akielekea getini, nilizuga naelekea lilipo friji ili kupata Maji ya kunywa ya Baridi. Sikutaka Matilda agundue kua nilikua na kiu ya kutaka kumwona Clara.
Baada ya dakika mbili alirudi ndani, alinikuta nikiwa nimeketi kitini, mbele yangu kukiwa na meza ndogo niliyoweka glasi. Nilizisikia hatua zake lakini ghafla zilipotea, nilikua nimempa mgongo hivyo ilinibidi nigeuka niangalie kama Kuna Ugeni wowote au yeye alipotelea wapi
Nilipogeuka nilikutana naye macho kwa macho, ilikua kama nimemshtua hivi maana alikua amesimama akiniangalia. Alijishtukia Kisha alizuga kua alikua bize na Mambo yake, sikutaka kumuuliza chochote kile nilikaza sura yangu. Nilielewa kua hapakua na ujio wa Mtu yeyote yule pale ndani
Sikuacha kujiuliza kua Clara atarudi saa ngapi, kingine nilijiuliza hisia ile ya kutaka kumwona Clara ilitokana na Nini, masaa yalienda.
Hapakua na Clara wala hapakua na ujio wa yeyote yule, hata simu ya Zaylisa ilikua haipatikani. Ilinifanya nijiulize maswali mengi ambayo hayakua na Majibu. Nilikua Mtu wa kuingia na kutoka chumbani, mara nikae sebleni, mara niende kukaa eneo la Bustani ilimradi tu nisikie geti likigongwa
Hadi Giza linaingia palikua kimya sana, Giza lilinikuta nikiwa nimeketi kwenye Bembea ndani ya Bustani nzuri ya mauwa. Taratibu niliondoka nikarudi ndani, nilimkuta Matilda akiwa ameshikilia kisikilizio Cha simu ya Mezani, aliponiona wala hakushtuka
Nilimwona ni Mtu mnyonge aliyejawa na huzuni, Ilinishtua kidogo. Nikataka kufahamu sababu ya mabadiliko yake, nilisogea taratibu Hadi
alipokua amesimama, alikua akiniangalia Hadi namfikia, macho yake yalipoteza uchangamfu kabisa
“Wewe” nilimwita, namna alivyokua akinitazama ni kama Mtu aliyezama sana mawazoni, jicho lake kwangu halikubanduka. Aliweka kisikilizio Sehemu yake Kisha akanitazama kwa jicho lile lile la huzuni
“Si naongea na wewe, mbona umekua mnyonge hivyo?” nilimuuliza wakati huo tayari na Mimi nilikua nimeingiwa na wasiwasi japo kidogo.
“Dada hapatikani kwenye simu yake, mara ya mwisho niliongea naye Mchana kua anaondoka na ndege ya Mchana kutoka Arusha, angefika huku mapema sana” alisema, kidogo nilisisimka. Nikameza funda zito la mate huku nikitafakari, nikamuuliza
“Hakukwambia kua atapitia popote?” nilimuuliza kwa sauti ya utaratibu iliyojaa umakini sana huku macho yangu yakishindwa kuvumilia wasiwasi nilionao
Matilda akanitazama kwa sura ile ile ya huzuni Kisha chozi kidogo lilimtoka, halikua chozi la kawaida, lilikua chozi la Upendo na kujali. Akajifuta kwa kutumia mkono wake wa kulia Kisha nikaisikia sauti yake ya kuvuta hewa
“Hapana, alisema anakuja Moja kwa moja lakini pia alisema akifika ataongea na wewe kuhusu jambo muhimu” alisema Matilda, alizidi kunifanya nisisimke kwa wasiwasi
“Mimi?” nilihoji huku kidole kikiwa kinaonesha kifua changu, nilitaka uhakika wa alichokisema Matilda.
“Ndiyo” alisema Matilda akiwa anamaliza kufuta chozi, alinitazama kwa jicho lililojaa Siri fulani nisiyoifahamu. Nilimeza funda zito la mate
“Alisema ni jambo gani Hilo?” niliuliza huku nikisikia mapigo ya Moyo Wangu yakienda mbio, nilipepesa macho yangu haraka haraka. Kichwani nilikua na jambo Moja ambalo niliamini lilikua muhimu nalo ni kufukuzwa nyumbani kwa Clara kutokana na kilichotokea kati ya Zaylisa na Clara.
Nilikuna nywele zangu katika Hali ya kuchanganyikiwa huku nikisubiria jibu la Matilda
“Hakuniambia, lakini…..” nilikua makini, Matilda alitaka kusema jambo Fulani ambalo nilihisi lilikua likimfanya anitazame kwa jicho kavu
Moyo Wangu ulikua ukijisemea na kuhimiza kua Matilda aseme haraka ili nijuwe kama alitaka kunifukuza au laa. Alipoanza kunyanyua midomo yake
mara Mlango uligongwa, haukuwa mlango wa geti Bali ulikua ni mlango wa kuingilia sebleni, nilimtazama Matilda
Hisia zangu ziliniambia alikua Clara au Zaylisa, nilitegemea ujio wao. Mtu asiyeifahamu nyumba asingeliweza kuingia getini Kisha kuja kugonga mlango wa kuingilia Sebleni.
Sote tulijawa na kiu ya kutaka kujua alikua ni Nani, mlango uliendelea kugongwa ndipo nilipoanza kuhisi pengine alikua Mtu mgeni, isingeliwezekana kwa Zaylisa au Clara kugonga mlango muda wote huo maana ilikua inaelekea dakika Moja.
Matilda alielekea mlangoni huku nikimsindikiza kwa macho ya utayari wa kumwona mgongaji, pumzi zangu zilikua kama za kuhesabu huku nikiweka umakini zaidi mlangoni, sikuruhusu jicho langu hata Moja kufumba
Matilda alipotekenya kitasa niliyasikia mapigo ya Moyo Wangu yakiongezeka, mara nilipatwa na Hali ya Ubaridi sana niliposikia sauti ya Mwanaume akiuliza.
“Hapa ni nyumbani kwa Clara?” Matilda aligeuka kunitazama Mimi, Kila mmoja alikua na wasiwasi maana kutopatikana kwa Clara Kisha ujio wa Mwanaume tusiyemfahamu kulifanya wasiwasi uongezeke. Nilitembea taratibu Hadi mlangoni, nikamwona Mwanaume mmoja mwenye ndevu nyingi nyeusi, mnene kidogo, mfupi kiasi na mwenye macho yaliyoingia ndani, alikua amevalia tisheti nyeusi na Suruali ya kaki.
Nilimtazama juu Hadi chini, alikua mgeni machoni pangu hata machoni pa Matilda maana hata sura ya Matilda ilionesha Wazi kua alikua akimwona kwa mara ya kwanza.
Alikua na sauti nzito ya Kiume.
“Ndiyo” niliitikia kwa sauti ya taratibu iliyojaa wasiwasi na kiu ya kutaka kujua ni kwanini alikua akiulizia.
Alinitazama kwa sekunde kadhaa, ghafla tulisikia geti likifunguliwa ilibidi sote tuangalie getini, aliingia Zaylisa akiwa anayumba kama Mtu aliyelewa, sote tulihamisha umakini kutoka kwa yule Mwanaume kuelekea kwa Zaylisa.
Nilikua wa kwanza kumkimbilia na kumdaka asianguke, huku kichwa changu kikizunguka maswali mengi sana yasiyo na Majibu. Niligeuka kumtazama Matilda aliyekua tayari ameshafika tuliposimama, naye alinitazama kwa jicho lenye maswali mengi sana
Kisha sote kwa pamoja Mimi na Matilda tuligeuka kumtazama yule Mwanaume pale tulipomwacha, tulishangaa hakuwepo, Zaylisa alikua amezima mikononi mwangu.
Matilda akaangaza huku na kule Kisha akaniambia
“Hayupo”
Hatukujua alienda wapi, alipotea kama Mzimu? Yeye ni Nani na alikuja kufanya nini pale, hatukua na Majibu ya maswali yetu. Zilikua dakika chache za kustaajabisha, dakika zilizozaa maswali zaidi ya majibu.
Tulisaidiana kumpeleka Zaylisa ndani, Matilda alibeba mkoba pamoja na viatu vya Zaylisa. Tulimpeleka Hadi chumbani, alikua hajitambui kabisa yaani alilewa kwa kiwango kisicho Cha Kawaida.
Matilda aliondoka pale chumbani, nilimfuata Kisha nilimsimamisha kwenye korido, alisimama akiangalia mbele bila kugeuka. Taratibu nilimfuata nikasimama nyuma yake, ukimya wenye maswali mengi ulinizonga
“Ahsante Matilda” nilisema, aliondoka zake bila kunijibu chochote kile. Nilihema kidogo, Kisha nilirudi chumbani, nilimpunguza nguo Zaylisa Kisha nilimlaza vizuri, alikua hajitambui kabisa
Kisha nilitembea taratibu na Kuketi kitini, nilimtazama tena Zaylisa Kisha nilijiuliza ni kwanini amelewa, lini alianza kutumia kilevi? Maana katika mahusiano yetu sikupata kabisa kumwona akitumia pombe
Nilipogeuza shingo yangu kuelekea Upande mwingine ilinijia ile taswira ya yule Mtu nisiyemfahamu, yule Mwanaume aliyekuja muda mfupi kabla ya Zaylisa kuingia. Nilijiuliza alihitaji kusema nini, kwanini aliuliza kama hapa ni nyumbani kwa Clara?
Kichwa changu kilikua kizito kikiwa na maswali mengi, yaliyotokea siku iliyopita yaliendelea kuniwinda huku nikiamini kua palikua na Maisha yangu yaliyorukwa, sikua na kumbukumbu za Maisha Fulani. Nilijikuta tu chozi likinitiririka bila kujizuia.
Sikuweza kupata hata lepe la Usingizi, nilielekea sebleni. Palikua kimya sana, nilielekea ilipo simu ya Mezani, nilinyanyua na kuipiga namba ya Clara, Bado ilikua haipatikani. Nilizidi kuchoka sana, nikaketi kochini nikiendelea kufikiria. Nilijikuta nikipitiwa na Usingizi wa ajabu, Usingizi ulionichukua bila magutu Hadi kulipo pambazuka
Niliposhtuka asubuhi, nilipiga mihayo ya Uchovu huku nikijinyoosha kidogo. Akiili yangu ilivyotulia ilimkumbuka Zaylisa, haraka nilielekea Chumbani.
Zaylisa hakuwepo kitandani, moyo ulinidunda sana nikawa nimekodoa macho kitandani nilipomwacha ule Usiku, nilijiuliza alikua ameenda wapi? Mara nilisikia Maji yakimwagika mafuni, nikashusha pumzi zangu baada ya kugundua Zaylisa alikua bafuni.
Niliketi kitandani nikiwa nimejiinamia, nilihitaji zaidi kuongea na Zaylisa ili aniambie kwanini alirudi akiwa amelewa.
Alipotoka bafuni alinikuta nikiwa nimekaa kitandani, alikua akijifuta Maji mwilini mwake akiwa amevalia taulo tu. Alisogea Hadi karibu yangu
“Umeamkaje my love” alinisalimia kwa sauti nzuri huku akitoa tabasamu.
“Salama japo sio salama sana” nilijibu kama Mtu aliyesusa, basi akaacha kujifuta Maji akasogea karibu yangu zaidi
“Kuna nini?” aliuliza akiwa ananitazama kwa umakini usoni kwangu.
“Jana ulirudi ukiwa umelewa, sikuwahi kukuona ukiwa umelewa hata siku Moja tangu nimekufahamu” nilisema, alipepesa macho yake kama aliingiwa na mdudu Kisha alinionesha uso wake wa huzuni kidogo akasema
“Jana nilipoenda kwa Baba, nilikutana na Mjomba wangu. Alinisemea maneno mabaya sana kua simjali Baba yangu” alisema Kisha alikatishwa na chozi, halafu akaendelea
“Kiukweli niliumia sana. Sikuweza kuzuia hisia zangu niligombana naye, nilipotoka nilikua na hasira nikajikuta nikipata wazo la kunywa” alisema, alikua akidondosha chozi lake. Baada ya Mama yangu na Melisa huyu ndiye Mwanamke ninaye mwamini sana, sikupata hata huo muda wa kuchuja maneno yake
Nilimvuta na kumkumbatia huku nikikisikia kilio chake kwa karibu zaidi. Nililengwa na Mchozi lakini sikutaka utoke, niliuzuia huku nikimbembeleza
“Pole Mpenzi wangu, ukiwa katika Hali ya huzuni unanifanya naumia.” Nilisema kwa sauti ya utaratibu iliyojaa mapenzi, Zaylisa akajitoa mwilini Kisha akafuta chozi lake kwa kutumia mikono yake, akanitazama usoni akaniambia
“Samahani sana Jacob”
“Hata usijali Mpenzi, nimekuelewa”
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya KUMI NA MOJA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love
3 Comments
Usituche kila siku kurudia hadithi hiyohiyo kama bando ni bureee.
https://shorturl.fm/PXhLS
Unazingua hadithi kali ila unazingua unachelewa kuleta muendelezo kaka