Ilipoishia sehemu ya sita ya In the name of LOVE
Mara mlango uligongwa, Zaylisa aliinuka Kisha alinitazama. Sote tulijiuliza ni Nani aliyekua anaugonga mlango, Mimi nilinyanyuka na kuelekea Mlangoni, nilipofungua nilikutana na sura ya Msichana wa kazi, alianza kunitazama kwa jicho la Upole sana Kisha akaniambia
“Dada anakuita” niligeuka kumwangalia Zaylisa, hakusema chochote ila alinitazama kwa jicho la kuniambia kua nitakacho kiamua kitakua sawa kwake. Nilishusha pumzi kidogo halafu nikamjibu
“Sawa, nakuja” sauti ya taratibu iliyojaa uzito ilinitoka. Yule Msichana aliondoka zake, nilifunga mlango. Nikamwangalia tena Zaylisa, nilishusha pumzi Kisha nikafungua tena mlango nikatoka kwa ajili ya kwenda kuonana na Clara. Endelea
SEHEMU YA SABA
Nilimkuta akiwa ameketi kwenye kochi, nilisimama kumtazama. Sikujua nani ana hatia na Nani Hana hatia, ila nguvu ya Mapenzi iliniambia kua Clara hakutaka niendelee kuishi hapo.
Taratibu nilisogea na Kuketi kando yake, mdomo Wangu ulikua mzito kama umefungwa na gundi.
“Jacob” aliniita Clara. Nilimtazama bila kuitikia Kisha aliendelea kusema
“Kesho naenda Arusha, nampeleka Melisa kwa Shangazi yake.” Nilimtazama kwa Upole, nikamjibu
“Sawa” nilitaka kunyanyuka lakini alisema
“Samahani kwa kilichotokea, sipendi ukwazike” nilimtazama nikamwambia
“Kama unaona ulikosea ni vema ukamwomba msamaha Zaylisa, hivi Clara…ninalazimisha kuishi hapa?” nilimuuliza, nilimwona akidondosha chozi
“Kama hutaki niishi hapa ninaweza kuondoka muda huu, kumbuka sikukuomba Nije kuishi hapa isipokua ni wewe ndiye uliyetaka niishi hapa. Au hutaki Zaylisa awe hapa?” Maswali yangu yalizidi kumfanya adondoshe chozi zaidi, alifuta chozi lake kwa kutumia mikono yake, pua zake ,zilikua zimeziba akavuta hewa kubwa Kisha akaniambia
“Kwenye hili Giza Kuna Siri Jacob, Siri ambayo siku ukiijua utajutia” nilishtuka, maneno yake yalikua sawa na Mtu aliyerusha jiwe gizani
“Simchukii Zaylisa, wala sitaki uondoke hapa Jacob Ndiyo maana nimekuomba Msamaha na nipo tayari kumwomba msamaha Mwanamke wako” alisema, nilimwona ni Mtu aliyebeba mambo mengi kifuani na hakua tayari kuyazungumza
“Siri gani unayoimaanisha?” nilimuuliza, aliishia kunitazama tu huku mdomo wake ukitetemeka, hakua tayari kusema chochote.
“Clara, kama siyo ile ajali ningekua na Mdogo wangu Melisa. Mimi sikufundishwa kuithamini pesa Bali utu, siku ukinichoka niambie nitaondoka hapa, sawa? ” nilisema Kisha niliondoka pale taratibu, nyuma yangu nilisikia kilio Cha chini chini, Nami chozi lilinilenga lakini sikutaka kugeuka nyuma.
Nilipofika chumbani, Zaylisa alinikumbatia kwa hisia sana. Niliamua kumwamini kwasababu ndiye Mtu niliyemfahamu zaidi, moyo Wangu ulikua na amani sana nimwonapo Zaylisa mbele ya Macho yangu
“Nakupendaa” nilimwambia Zaylisa, Ndiyo….moyo Wangu ulifungwa kwa ajili yake tu, yeye ndiye niliyempenda na Kumthamini.
Mchana, Zaylisa aliniambia kua anataka twende mahali. Nilijiuliza alihitaji twende wapi, nilimuuliza
“Tunaenda wapi Mpenzi wangu?”
“Jiandae Mpenzi, utaona” Alisema, basi niliingia bafuni nikaoga vizuri halafu nikajiandaa haraka. Kisha nilipomaliza nilikua tayari kwenda aliposema yeye. Sikujua ni wapi
Tulipotoka chumbani tulikutana na Clara. Alikua akitutazama akiwa amesimama kwenye korido, sura yake ilikua imejawa na huzuni iliyo gizani, macho yake yalinitazama sana. Zaylisa akanishika mkono
“Twende” hakutaka kuzungumza na Clara, nyuso zao zilijaa nyufa isiyoelezeka, sura ya Clara ilikua Ina huzuni isiyo mithirika lakini sura ya Zaylisa ilikua imejawa na hasira na jeuri, nilielewa ni kwanini Kila mmoja alikua na sura yake
Tulimpa mgongo Clara asijuwe tunaelekea wapi. Midomo yake ilitamani kusema kitu lakini aliishia kututazama Hadi tulipo ishiria. Zaylisa alikua tayari ameshaita gari ya kukodi kupitia mtandao, tuliingia ndani ya gari
nikiwa na maswali mengi kichwani, sikujua tulikua tunaenda wapi na kufanya nini.
Safari ilianza taratibu kutoka kwenye jumba la kifahari la Clara, tulielekea Mjini. Alinitembeza Sehemu mbali mbali, mwisho akanipeleka kwenye Mgahawa mmoja ulio katikati ya Jiji
Aliagiza chakula, sikujua alipata wapi pesa za kufanya yote Yale. Nilikua nimejawa na Mshangao tu lakini sikiliza chochote.
“Unajua Leo umenishangaza Zaylisa, sikutegemea ujue” nilisema nilitabasamu, naye aliachia tabasamu
“Sikupenda kilichotokea pale kwa Clara, nilihitaji utulivu zaidi ili kuweka akili yangu sawa Jacob…..unajua Clara ana dharau sana” alisema Zaylisa, nilimwambia
“Usijali, hata hivyo amejutia. Nakuamini sana Zay, kwani ilikuwaje mkaingia kwenye Hali ile ya Kupigana?” alinitazama Kisha akaonesha kutokupenda sana kuongelea suala lile
“Ahh‼ unajua Jacob, Mimi sipendi Mtu anayemdharau Mtu ninayempenda. Yule alileta kejeli na dharau, nilichofanya ni kukulinda. Wewe unasema tu eti amejutia, hawezi yule ni kiburi sana….. Mpenzi…” akanishika mkononi huku akiongea kwa huzuni
“Hata iweje siwezi kuachana na wewe, nakupenda sana Jacob. Nimekupa Nusu ya Maisha yangu….Nisamehe kwa kitendo changu Cha kuolewa, Wazazi walinishinikiza” alisema Zaylisa, Kila alichosema nilikiona kilikua sawa
Chozi lilimdondoka, nilijihisi huzuni ndani yangu.
“Usijali Mpenzi kua na amani, kwakua upo hapa na Mimi basi hakuna kitakacho tuweka mbali tena” nilisema pole pole, nikaangalia kama Kuna Watu waliokua wakitutazama lakini niliona Kila Mtu alikua bize na mambo Yao.
“Naomba niende bafuni Mpenzi”
“Sawa Mpenzi” Zaylisa aliniaga Kisha aliondoka huku akikitumia kitambaa kufuta chozi lake. Nilimtazama Hadi alipozama, kiukweli nilikua najisikia vibaya sana. Nilitamani ningekua na pesa ili nitafute mahali pa kuishi na Zaylisa, sikupenda kuendelea kuishi nyumbani kwa Clara
Nilijiinamia, nikiwa hapo niliguswa begani. Nilipoinua macho nilikutana na Mtu nisiyemfahamu lakini uso wake ulionesha kunifurahia na kuniheshimu sana. Hakunipa hata muda wa kumtafakari, akasema
“Sikutemegea Kama ungepona kwenye ile ajali Bosi” nilishtuka, aliniita Bosi.
“Umeniita Bosi?”
“Ndiyo, Mungu ni mwema sana. Ninafurahi kukuona ukiwa mzima” alisema Kisha alinitazama kwa furaha sana, yeye alikua Ni Mwanaume mrefu kiasi, Maji ya kunde
“Unanifahamu?” nilimuuliza, aliondoa utulivu na tabasamu akaketi kwenye kiti alichokua ameketi Zaylisa.
“Bosi ni Mimi Kitime, umepatwa na Nini usinifahamu?” alijieleza kwangu, kiukweli sikumtambua na wala sikukumbuka hiyo heshima ilitokana na Nini.
“Mbona sikufahamu ndugu yangu, utakua umenifananisha” nilimwambia huku nikigeuza shingo kuangalia kama Zaylisa alikua akirejea ili nimuulize.
“Hapana siwezi kukufananisha Bosi Jacob, ni wewe.” Alisema, nilishtuka zaidi alipotaja jina langu, alionekana kunifahamu lakini bahati mbaya sikua na kumbukumbu hata Moja kuhusu yeye.
“Umelifahamu vipi jina langu ndugu yangu, Mimi sijawahi kua Bosi. Sikufahamu, tafadhali sana ondoka hapa” nilisema, yule Mtu aliyejitambulisha kama Kitime aliniangalia kwa Mshangao kama vile alikua ameona mzimu.
“Kuna kitu hakipo sawa kwako Bosi” alisema Kisha aliondoka zake pale, aliniacha nikishusha pumzi nzito sana Hadi kichwa kilianza kunigonga. Mara Zaylisa alitokea, akanikuta nikiwa na mawazo lukuki, alipoketi aliniuliza
“Unawaza nini baby, Bado unamfikiria Clara?” nilimeza funda la mate, nikimtazama Zaylisa.
“Kuna kitu kinanichanganya Zay, Kuna Mtu amekuja hapa anaonesha kunifahamu halafu ametaja jina langu pia ameniita Bosi. Nahisi Kama Kuna Maisha siyakumbuki” nilisema, Zaylisa akaniuliza
“Ni Mtu gani huyo Jacob”
“Amejitambulisha kama Kitime, anaonekana kunijua lakini simfahamu” nilisema huku kichwa kikiwa kinapata moto haswa
“Aaaah Baby, huwenda tu una wenge. Tule tuondoke” Zaylisa alisema huku akionekana kutojali kuhusu nilichomwambia, pengine alifikiria baada ya ajali akili yangu haijakaa sawa, nilijisikia vibaya japo sikutaka kumwonesha Moja kwa moja. Nililiacha lile jambo lipite japo liliniumiza kichwa sana
Tulipomaliza kula, Zay alilipia bili Kisha aliita gari ya kukodi tukarudi nyumbani. Tuliikuta nyumba ikiwa kimya kama vile hapakua panaishi Watu, tuliingia chumbani kwetu tukajipumzisha, kwakua tulikua tumeshakula hivyo hatukutoka tena Hadi kesho yake.
Asubuhi mapema sana, Clara aliugonga mlango wa chumba changu, nilipofungua nilikutana na yeye akiwa amemshika mkono Melisa, kando
palikua na Begi kubwa la nguo, nikakumbuka kua aliniambia atampeleka Melisa Arusha kwa Shangazi yake
“Habari ya Asubuhi Jacob” alisalimia.
“Niko salama”
“Nampeleka Mtoto Arusha, kesho nitarudi. Ubaki salama” alisema Kisha aligeuka na kuondoka hapo huku Melisa akigeuka geuka mara kwa mara kuniangalia, sikujua ni kwanini alikua akiniangalia sana lakini hisia zilinianbia nilikua na uhusiano wa Maisha yaliyopita na Mtoto yule.
Nilirudi chumbani, nilianza kujihisi huzuni kiasi. Nilimtazama Zaylisa aliyekua amelala, nilijiinamia huku kichwa kikiwaka moto kwa mawazo lukuki, nilitamani kujua kitu ambacho nilihisi kilikua muhimu kukijua lakini sikujua nitafanya nini. Nilishusha tu pumzi zangu, Usingizi ulikua umeshaisha
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya SABA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love
1 Comment
y7iuua