Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE
“Basi hakuna shida Zaylisa, mnaweza kuishi wote ikiwa jambo lako la talaka litakamilika” maneno ya Clara yalinipa tabasamu kubwa, basi Tuliachana na Zaylisa ambaye aliaga kua anarudi kwake.
Mimi na Clara tuliondoka Kisha tulimpitia Mtoto wake ambaye ni Melisa, Kisha tulielekea nyumbani kwa Clara. Kila kitu kilikua kipya kwangu, niliyaona mazingira yakiwa mageni kabisa, sikukumbuka kuhusu Mtoto Melisa kua ni Mwanangu wa Damu kabisa na Clara ni Mke halali wa ndoa. Endelea
SEHEMU YA TANO
Tulipofika, nililishangaa jumba Zuri sana la kifahari. Tulifunguliwa geti na kuingia ndani, mahali ambapo niliishi kwa Miaka mitano sikupakumbuka tena. Msichana wa kazi alitupokea na kunipa sura ya Ugeni kama alikua akiniona kwa mara ya kwanza
“Hapa ndio nyumbani kwangu Jacob, jisikie huru kabisa” alinikaribisha
“Asante sana Clara, nitajisikia hivyo taratibu” Mara zote Melisa alikua akinitazama sana kama Alikua akitaka kuniambia kua Mimi ni Baba yake lakini aliishia kuwa mnyonge tu, Kuna kitu Cha ajabu ambacho nilikishangaa sana. Mara zote nimwonapo Melisa nilihisi Upendo mwingi sana juu yake.
Nilioneshwa chumba changu Cha kulala, baada ya kuingia chumbani basi Mtu pekee niliyemfikiria alikua ni Melisa mdogo wangu lakini niliamini pengo lake lingezibwa na Zaylisa.
Ndani ya chumba hicho palikua na picha ya Melisa akiwa na Mama yake, hapakua na kumbukumbu nyingine. Niliketi pembeni ya Kitanda, Kila nilichokigusa kilinianbia kua ilikua ni mara ya kwanza naingia hapo lakini nafsi yangu ilianza kupata wasiwasi kua kama niliwahi kua hapo, iliponijia hisia hii nilianza kuhisi maumivu makali ya kichwa.
Nilihisi kama naishiwa nguvu nikajikuta nikijiinamia, mara Mlango uligongwa. Sauti ya Clara ilipenya Ngoma za masikio yangu, nilijikuta nikimkaribisha huku nikiwa ninajisikia vibaya.
Alipoingia ndani, alinikuta nimejiinamia. Akajaribu kunikagua nikamwambia anipe dawa zangu. Haraka alipekua Begi na kutoa dawa, akanipa nikameza Kisha akaketi huku akifuatilia Hali yangu
“Jacob, unajisikiaje?” aliniuliza, niligeuka kumtazama.
“Nilihisi kama Kuna kitu kilikua kinakuja kichwani kwangu lakini kiligoma, sijui ni kitu gani Clara” alinitazama kabla ya kunijibu.
“Bado Hali Yako haijatengemaa Jacob, unahitaji muda zaidi wa kupumzika. Basi, ngoja nikuletee chakula” alisema akanyanyuka, nikamshika mkono. Namna nilivyomshika nilihisi Kuna uhusiano Fulani kati yetu, lakini ni uhusiano gani usiojitokeza, sikuweza kuelewa. Ghafla nilimwacha
“Nahitaji kupumzika kwanza Clara, nitakula nikiamka”
“Basi sawa. Pumzika Jacob, nitakuona baadaye” alisema Kisha alifungua mlango na kuondoka, aliniachia maswali mazito sana. Akili yangu iliniambia kua sikuwahi kua na rafiki kama yeye lakini nafsi iliniambia palikua na uhusiano uliojificha, sikutaka kuumiza akili yangu.
Nilipanda kitandani pole pole, punde Usingizi ulianza kuninyemelea nikajikuta nikilala.
**
Siku iliyofuata, niliamshwa na sauti ya kugongwa kwa mlango. Nilijiinua pole pole bila kusema chochote, nilitembea kwa kupepesuka kidogo kutokana na usingizi Hadi mlangoni. Nilipofungua nilikutana na Clara
“Habari ya Asubuhi Jacob” alinisalimia, namna alivyokua akinijali ilinishangaza sana.
“Nzuri sijui wewe na Melisa wako”
“ Sote ni wazima Jacob. Nimekuandalia chai, jitahidi ukapate kifuangua kinywa”
“Sawa” Niliitikia, lakini nilikumbuka kuhusu Zaylisa
“Hakupiga simu?”
“Nani?”
“Zaylisa”
“Bado, Jacob kwasasa angalia zaidi afya Yako. Zaylisa atakuja usiwe na wasiwasi sawa?” alisema huku akitabasamu kama vile alikua akiongea na Mtoto mdogo.
“Clara, baada ya Mdogo wangu Melisa anafuatia Zaylisa. Sijawahi kumpenda Mwanamke mwingine zaidi yake, uwepo wake ni tiba kwangu” nilisema kwa utulivu sana, nilikua usoni kwa Clara, alionekana kukosa Raha kama Mtu anayekaribia kulia muda wowote
“Kwanini nimtajapo Zaylisa wewe unakua hauna amani Clara? Nakupa mzigo mzito Mimi kuishi hapa?”
“Hapana Jacob, nimeona ni jinsi gani uliamua kupenda kwa moyo wako wote. Hakika Zaylisa hawezi kukusahau kamwe” Nilitabasamu, maneno yake yalikua kama kisu kwenye mfupa. Yaliingia Hadi ndani kabisa ya moyo Wangu na kunipa Raha sana
“Clara, ninapopenda nazama mazima. Najua kupenda sana Ndiyo maana nilipomchagua Zaylisa sikuwahi kujutia” nilisema, hakuonekana kua na Raha kabisa
“Basi twende tukapate kifuangua kinywa Jacob” alisema, Taratibu Hadi tulipofika Mezani, Melisa alikua hapo akinitazama sana kama kawaida yake. Nami nilimwachia tabasamu
“Baba” aliita Melisa, niligeuka kuangalia nyuma yangu pengine kulikua na Mwanaume mwingine, niligundua hapakua na mwingine. Macho ya Melisa yalikua yakinitazama Mimi tu huku akiwa analengwa na Mchozi
Sikutegemea kama angeniita Baba, kwangu alikua Mtoto mgeni, lakini kwake nilikua muhimu lakini kwenye kumbukumbu nilizozisahau, nilimtazama Clara ili kupata taswira ya alichokisema. Niliona alikua akionekana ni mwenye huzuni ya ndani kama Mtu anayevuja damu ndani kwa ndani.
Sikujua Baba yake Melisa alikua wapi, hatukuwahi kuzungumzia Hilo Mimi na Clara. Nilihisi labda Melisa alikua amemkumbuka Baba yake, basi nilitabasamu tu Kisha nikamwambia
“Unasemaje Binti yangu?” nilihisi kama ninaongea na Mtu ninaye fahamu vizuri lakini nisiyemkumbuka. Melisa alimwangalia Mama yake. Kisha alinyanyuka na kuondoka pale akaelekea chumbani, Clara akaniambia
“Samahani ngoja niongee na Melisa” Kisha naye aliondoka hapo, Kuna namna nilianza kujihisi. Ni kama Nina mzigo Fulani ndani yangu. Mzigo ambao ulikua ukinielemea Kila nilivyomwona Melisa.
“Au kwasababu ana jina la Marehemu mdogo wangu?” nilijiuliza. Kabla hata sijazama sana kifikra, mara Mlango uligongwa. Dada wa kazi hakua karibu, niliona ni Bora nielekee mlangoni.
Taratibu sana nilisogea, nilipofungua mlango nilimwona Zaylisa. Alikua amesimama akinitazama kwa tabasamu sana, niliishiwa hata neno la kumwambia. Nilimkumbatia kwa hisia kubwa sana, moyo Wangu uliniambia kua nilikua namkosa ndani yangu
Tukiwa hapo, nyuma yangu alikuja Clara. Alisimama akitutazama, nilipoacha kumkumbatia Zaylisa niligeuka, niliuwona Mshangao mkubwa ambao Clara alikua nao, nilipomtazama Zaylisa niliona sura ya tofauti.
Alikua akimtazama huku kama alikua akimtumia Clara ujumbe wa hisia ambao sikuweza kuelewa kabisa.
Macho ya Clara yaliingiwa na huzuni, kidogo chozi lilikua likimlenga lakini Zaylisa alikua na sura kavu.
“Clara” alisema Zaylisa, alionesha pia sura ya Huzuni, akamfuata Clara alipokua amesimama Kisha akamwambia
“Samahani, najali kuhusu Hali ya Jacob. Nitakua hapa kwa ajili yake” Clara akamtazama sana Zaylisa
“Hatukukubaliana hili si Ndiyo? Sasa unafanya nini?” alisema kwa sauti ya chini lakini niliweza kusikia, Kisha Zaylisa akageuka na kunitazama.
“Babe! Nitakua hapa kwa ajili Yako” nilitabasamu lakini nilikua na maswali mengi kichwani, Zaylisa ni Mke wa Mtu angewezaje kukaa na Mimi?
“Lakini wewe si?…” kabla hata sijamaliza kuongea alinikatisha akasema
“Ndiyo, lakini sasa siyo Mke wa Mtu tena. Talaka hii hapa” alisema akaonesha bahasha aliyokua ameishikilia mkononi, Mimi na Clara tulitazamana kwa Mshangao. Japo nilikua nahitaji sana kua na Zaylisa lakini alichosema kilinishtua kidogo.
Niliipokea bahasha, nikaifungua pole pole. Ndani yake mlikua na karatasi tatu zenye maandishi ya kuchapwa. Palindikwa ‘TALAKA’
Moyo ulinienda mbio, palikua na Saini zao kua walikua wameachana. Sikujua nifanye nini kati ya kufurahi au kuendelea kuuliza, hata hivyo ningeuliza nini tena wakati tayari Kila kitu kipo kwa maandishi, lakini uso wa Clara ulijawa na Mshangao na huzuni iliyochanganika na hasira.
Nilihisi furaha Iliyo changanika na hisia ya maumivu, sikua na kumbukumbu ya kumpenda Mwanamke mwingine isipokua yeye. Nilijikuta nikimkumbatia kwa nguvu Zaylisa mbele ya Clara
Clara hakutaka kututazama, aligeuka pembeni akiwa analia Kisha alifungua mlango akaingia chumbani kwake.
“Kwanini Clara anaonekana ana huzuni kukuona wewe?” nilimuuliza Zaylisa, alinitazama akitabasamu kidogo huku akionesha vishimo kwenye
mashavu yake. Akanishika mabegani kwa mahaba mazito sana, akaniambia huku akinitazama usoni kama vile ilikua ni mara ya kwanza tunaonana
“Jacob, siwezi kujua labda hakutaka niwe hapa” alisema, nilishusha pumzi kidogo. Clara ni Mtu wa muhimu sana aliyenisaidia nilipopata ajali hivyo kubadilika kwake kulinipa maswali mengi yasiyo na Majibu.
“Najisikia huzuni sana, siiyoni Nuru machoni pake. Nahisi Kuna kitu hakipo sawa kwake”
“Hata hivyo karibu, nitaongea naye…” nilisema Kisha nilikamata Begi lake, akanishika mkono akaniambia
“Jacob, usimuulize chochote kile. Mimi nitaongea naye, sawa?” niliyatazama macho ya Zaylisa, yalikua ni macho Yale Yale yaliyojawa na Upendo ule ule, sikua na shaka naye. Nilitabasamu kidogo
“Sawa babe” nilikokota Begi, nikamshika mkono Zaylisa Kisha nikaelekea naye chumbani kwangu.
Tulipofika chumbani ni kama tuliamsha mashetani ya mapenzi, japo Bado nilikua sijapona vizuri lakini sikutaka Usiku unipite, nilikula tunda lililokua limekaribia kuchukuliwa na mwingine. Lakini Kila sekunde nilihisi palikua na Mtu mlangoni, ile amani ilianza kuondoka
“Vipi?” aliniuliza Zaylisa akiwa anajilaza kando baada ya kuona kama akili yangu haipo.
“Hakuna” nilitabasamu ili kumwondoa hofu lakini haikumsaidia akaniuliza “Unahisi afya Yako inabadilika?”
“Hapana, unajua baada ya ajali Kuna vitu vipo kichwani ila sijui ni nini, Wacha nipate Maji ya kunywa kidogo” nilisema Kisha nilivalia pensi, nikamwacha Zaylisa Kitandani, nikafungua mlango nikaelekea sebleni.
Nilishangaa kuona taa ilikua Bado inawaka na hapakua na dalili ya uwepo wa Mtu, basi nikaona nipate Maji kwanza Kisha nizime. Nilipofika kwenye friji nilihisi Hali isiyo ya kawaida, kama vile palikua na kumbukumbu Fulani ya Mimi kufika hapo kabla lakini sikutaka kuipa nguvu sana kumbukumbu hiyo, nilihisi ni wenge tu.
Upepo ulivuma kidogo ukapeperusha pazia, nikamwona Clara akiwa amesimama varandani kwa nje, alikua kama analia hivi. Niliacha zoezi la kuchukua Maji, nilimtazama kwa makini sana akiwa anaangalia pembeni bila kujua nilikua nikimtazama.
Upepo ulikua ukisukuma nywele zake, nilipata shahuku ya kutaka kuongea naye. Nilielekea mlangoni nikafungua mlango taratibu, sauti ya mlango ilimfanya ashtuke na kugeuka. Aliniona nikiwa nimesimama mlangoni nikimtazama, alikua akidondosha chozi bila kuficha.
Tulitazamana bila kusemeshana kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari nini maana ya chozi lake, mbona Kila niwapo karibu naye hua nahisi Hali isiyo ya kawaida. Nilisogea taratibu nikimtazama, macho yetu yalikua thabiti yasiyo kwepana
Hadi namfikia hakuna aliyeongea na mwenzake, nilijikuta nikimweka vizuri nywele zake.
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya TANO
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love