โJacob, nataka kuujua Msimamo wako kwangu. Utaniowa lini?โ Aliulizaย Zaylisa, Nilishusha pumzi zangu. Nikageuka huku na kule kama Kuna Mtu alikua anatusikiliza pale Mgahawani. Nilikua nimevalia sare zangu za kaziย ya Uhudumu wa Mgahawa.ย ย
โZaylisa, naomba univumilie Hadi Mama yangu apone. Unajua fikaย anaumwa, Mimi Ndiyo tegemezi. Halafu isitoshe Mpenzi wangu kwasasaย kipato changu kipo chini unafikiria Wazazi wako watanielewa?โย Nilimuuliza, kiukweli nilikua napitia kipindi kigumu Cha kifedhaย
โHadi lini Jacob?โ aliniuliza huku akianza kutokwa na Machozi, machoย yake yalijaa Upendo sana lakini nilihisi Kuna jambo lililokua likimsumbuaย
โMpenzi nivumilie tu, najua unavyojisikia lakini haiwezi kuchukua mudaย mrefu nitakua nimejipataโ Ghafla Zaylisa aliondoka akiwa anakimbia hukuย akionekana kama analia, sikuweza kumsimamisha sababu ulikua ni mudaย wa kazi na sikutaka Mtu yeyote ajuwe kinachoendelea.ย
Nilijaribu kumpigia simu lakini hakupokea, niliumia sana. Sikutaka kuaย chanzo Cha Zaylisa kulia, mara zote alikua akinihimiza kwenda kwaoย kujitambulisha lakini nilijawa na hofu.ย
Familia Yao ilikua na uwezo kifedha, Mimi nilikua masikini ninayeishiย kumlea Mama yangu mgonjwa. Basi nilishusha pumzi Kisha nikaendelea naย kazi huku nikiwa mnyonge sana.ย ย
***ย
Usiku baada ya Muda wa kazi kwisha nilijiandaa kwa ajili ya kuondoka.ย Lakini ghafla alikuja Mdogo Wangu Melisa, alikuja mbio kama Mtuย anayefukuzwa, alishindwa hata kuongea huku akisema.ย
โKaka, Mamaaa!โย
โMama amefanya nini Melisa?โ nilimuuliza huku mapigo ya Moyo Wanguย yakianza kwenda Mbio, hisia mbaya iliniingia. Nilihisi Kuna jambo lisilo laย kawaida lilikua limetokea, hisia mbaya iliendelea kunipanda. Harakaย nikamwambia rafiki yangu Sudi kua naelekea nyumbani.
Tuliondoka mbio pale kuelekea Nyumbani, kutoka kazini kwangu Hadiย nyumbani siyo mbali sana. Tulipofika, nilihisi mwili Wangu ulikuaย unaishiwa nguvu baada ya kumwona Mama akiwa ananingโinia kwenyeย Kamba. Macho yalinitokaย
โMamaaโผโ nilimwita, alikua ameshajinyonga chumbani kwake. Nilifanyaย haraka kufungua nikiamini pengine nitaweza kuokoa uhai wake.ย ย
Basi nikaita Bajaji haraka, tukampeleka Mama Hospitali. Nilimtazamaย Mdogo wangu akiwa analia, iliniuma sana, tumaini la Mama kua hai lilikuaย dogo sana.ย ย
Tuliketi Sehemu ya kumsubiria daktari aliyeingia chumbani, nilimkumbatiaย mdogo wangu Melisa, roho iliniuma sana. Zilipita dakika kumi na tano,ย daktari alitoka Kisha alisimama mbele yetuย
โMnifuateโ alisema yule Daktari, haraka tulimfuata kuelekea kwenyeย chumba kimoja. Alitukaribisha vizuri sana huku akiachia tabasamu kanaย kwamba alikua na habari njema ya kutuambia kuhusu Hali ya Mama yetu.ย
โNyie ni Nani yake?โ aliuliza. Tulitazamana Mimi na Melisa, tulihisi amaniย ndani yetu.ย ย
โWatoto wakeโ nilijibu Kisha nilimwulizaย
โHali yake ipoje Dokta, ni mzima?โ Daktari akabadilisha uso wake,ย akaondoa tumaini mioyoni mwetu, sura yake ikaonesha kua Kuna asilimia sifuri ya Uhai wa Mama yetu.ย ย
โPoleni, amefarikiโ alisema.ย ย
โMamaa!โ aligumia Melisa, pale pale alipoteza fahamu. Tulianzaย kuhangaika na Hali ya Melisa, akakimbizwa wodini haraka. Chozi lilikuaย likinibubujika bila kukoma, hapakua na Mtu kando yangu wa kuhisiย maumivu yangu, Niliketi peke yangu nikiweweseka, sikujua nilishike lipi niliache lipiย
Moyo Wangu uligawanyika, upande mmoja alikuwepo kwa Meliza naย Upande mwingine alikuwepo kwa Marehemu Mama yangu. Dunia ilikuaย nzito, ilishuka kichwani kwanguย
Chozi lilikua likinibubujika, siku yangu iliharibika dakika za jioni kabisa.ย ย
Nilijiinamia, nilikosa tumaini. Ghafla nilihisi kuguswa begani, nilishtuka.ย Niliinua kichwa changu ili nimtazame aliyenishika
Macho yangu yalikutana na sura ya Mwanamke mmoja, sikukumbuka kamaย niliwahi kumwona popote katika Maisha yangu, sikumfahamu lakini suraย yake ilionesha kunitambua na kuguswa na ninayoyapitia. Nilifuta choziย langu Kisha nilijiweka tayari kumsikilizaย
โPole..โ sauti yake ya kwanza ilinifanya nizidi kudondosha chozi, alikua niย Mtu wa kwanza kunitia moyo. Niliitikia kwa kichwa, mdomo Wangu ulikuaย mzito, ulikua ukitetemeka tu.ย
โNaitwa Clara, sijui kama unanikumbukaโ nilitikisa kichwa changuย kuashiria kua nilikua simkumbukiย ย
โUsijali, kimetokea nini? Ulitoka mgahawani mbio, niliguswa sana. Hataย hivyo Mimi ni mteja uliyenihudumia kwenye meza namba 6โ Niliitikia kwaย kichwa huku chozi likinibubujika, sikuweza kusema chochote zaidi ya kulia.ย Akaniweka kifuani pake, alionesha kunijali sana. Nililia Hadi nililalaย kifuani kwake, akaja kunishtua saa Sita Usikuย
Melisa alikua amesharejesha fahamu, daktari alitupatia utaratibu wa jinsiย ya kuuchukua mwili wa Mama. Gharama zote za Hospitali akazilipa Claraย
โAsante sana Claraโ nilimshukuru, sijui ningetoa wapi pesa za matibabu yaย Melisa pamoja na gharama za kutoa Mwili wa Mama.ย
โUsijali, tutakua pamoja Hadi mwisho Jacob. Mungu alipanga iwe hiviโย alisema. Tukaurudisha mwili wa Mama nyumbani, tulipofika tulikutaย ndugu wengine wakiwa wamefika hapo, Mjomba Masawe alikuaย amesimama Mlangoni Kisha akaniuliza swaliย
โHukuona umuhimu wa kutupigia simu Hadi tumetaarifiwa na Majirani?โย alikua amekasirika, mara zote yeye ni mkorofi sana.ย
โAnko, ningewezaje? Nilikua nimechanganikiwa sana. Samahaniโ nilisema,ย Clara aliniangalia kwa jicho lenye maswali mengi sana. Basi akatupishaย tukaingiza maiti ndani, taratibu na mipango ya mazishi ikaanzaย
Hakuna aliyenishirikisha kwa lolote, walikaa vikao vyao vya Siri naย kupanga taratibu zote. Sikujali sana sababu hata Mama alipokua haiย walikua ni Watu wenye Hila zao, hawakutaka sisi tuishi kwenye nyumbaย Yao ya Urithi, walipigania kuiuza ila Mama ndiye aliyekua kizuizi chao.ย
Siku iliyofuata, mazishi ya Mama yalifanyika. Baadaye kikao Cha familiaย kiliketiย
Walikubaliana kwa Kauli Moja kua Mimi na Melisa tuondoke, wanauzaย nyumba Yao. Hatukua na mahali pa kwenda. Nilimtia moyo Melisa,ย
tulikusanya Kila kilicho chetu, hatukujua tungeenda wapi, hatukujuaย tungeishi vipi lakini tulijipa moyo kua Kila kitu kitakua sawaย
Tulienda kwa Sudi maana ndiye Mtu pekee ambaye ningeweza kwendaย kwake na kutarajia msaada, ni rafiki pekee niliye naye. Sudi alitupokeaย vizuri tu lakini palikua na kikwazo kimoja, tutawezaje kukaa wote watatuย chumba kimoja, Melisa ni Mwanamke angalau Angekua Mwanaumeย
โKaka, tusaidie kwa siku kadhaa wakati Mimi nahangaika nijue nampelekaย wapi Melisaโ nilimwambia Sudi, akamtazama Melisa Kisha akakubali.ย ย
Tulianza Maisha mapya nyumbani kwa Sudi, siku iliyofuata nilimtafutaย Zaylisa maana tokea ile siku hatukuwasiliana tena. Simu ya Zaylisa ilikuaย haipatikani, ilianza kunipa Mashaka. Hapakuwahi kutokea siku Zaylisaย asipatikane kwa simu, nilijiuliza huwenda alikua amepata tatizo maanaย sikumwona hata kwenye Mazishi ya Mama.ย
Tuliondoka na Sudi kuelekea kazini, nilifanya kazi Hadi mida ya Mchana.ย Baadaye niliitwa na Bosi, nilitegemea kusikia akinipa pole lakini Hali ilikuaย ya tofauti kabisa, alinieleza kua hawezi kuendelea na Mimi kwambaย amepata Mtu mwingine.ย ย
โBosi, kwanini ni ghafla?โย ย
โJacob, siku zote Shilingi Ina pande mbili. Huu ni upande mwingine ambaoย ulikua hauutazamiโ alisema, nilihema. Sikutegemea kabisa kamaย ningeikosa kazi bila sababu ya Msingi tena ndani ya Siku chache tu zaย Matatizo ya kufiwa na Mama yangu.ย
Miguu yangu ilikufa ganzi, mwili mzima ulikua ukiweweseka lakini manenoย ya Bosi yalikua kama msumali wa mwisho uliogongwa moyoni mwangu,ย kilichoniumza zaidi ni Maisha tunayoishiย
โAsante Bosi..โ Nilisema, Kisha niligeuka na kuondoka zangu, sikuaminiย kama nilikua nikiziacha Kuta nilizozizoea, Watu niliowazoea hata kelele naย usumbufu wa wateja ambao nilishauzoea.ย ย
Sudi alipoiona sura yangu alijua nilikua nimezongwa na mawazo, nilipotezaย Nuru. Niliona nimepoteza thamani juu ya uso wa Dunia, nilihisi uzito waย Mzigo mwingine mzito nilioubebaย
โJacobโฆMbona una huzuni?โ aliniuliza Sudi, nilishusha pumzi hukuย nikizuia chozi lisinitoke mbele yake. Nikajikaza Kiume lakini moyo Wanguย ulijenga ufa.
โMoshi mweusi Sudi, nimepoteza tena Mimiโ nilisema, ule Ujasiri ulianzaย kuondoka niliangusha kilio mbele ya Sudi, chozi likinitiririka.ย ย
โUna maanisha nini?โย
โSina kazi tena, nimefukuzwa. Sijui nimeambukizwa mkosi gani Sudi, sijuiย wengine wamemfanyia nini Mungu ambacho Mimi sifanyiโย
โShii! Bro, nenda nyumbani, tutaongea zaidi hukoโ alisema Sudi,ย niliondoka kazini taratibu. Macho yangu yalikua yakiyatazama mazingiraย ya Mgahawa kwa mara ya mwisho, nilitembea kama Mtu aliyepoteza Kilaย kitu.ย ย
Nilipofika nyumbani kwa Sudi, nilimkuta Melisa akiwa ameketi kwenyeย kochi dogo, aliponiona aligundua haraka sana kua siko sawa, alinifuata naย kunikumbatia. Sikusita kulia tena mbele yake, nilikosa ule Ujasiri waย Kiume mbele yakeย
Tuliketi nikamsimulia kilichotokea, niliona jinsi hata moyo wakeย ulivyosononekaย
โUlifanikiwa kumpata Wifi kwenye simu?โ aliniuliza baada ya kumalizaย kumsimulia kuhusu kazi. Kiukweli Hadi muda huo simu ya Zaylisa ilikuaย haipatikani, sikujua kama alipatwa na tatizo au aliamua kuzima simu yake,ย kwa jinsi nilivyokua namfahamu isingelikua rahisi akae siku zote hizo bilaย kuwasiliana na Mimi.ย
โMelisa, Usijali. Naenda kwao sasa hivi nikazijue mbivu na Mbichi. Usijaliย Mdogo wangu, Kila kitu kitakua sawa. Nitampata pia nitapata kazi nzuriย itakayobadilisha Maisha yetuโ nilisema, angalau nilifamfanya atabasamuย kidogo, nikamfuta chozi lakeย
โVipi ulikula?โย
โNdiyo Kaka, nimebakiza kwa ajili Yakoโย ย
โUsijali, nikirudi nitakula sawa?โย
โSawa, unaenda sasa hivi eeeh?โย
โNdiyo, angalau nikimwona nitajisikia ahueni. Ubaki salamaโ nilisemaย Kisha niliondoka.ย ย
**ย
Nilipofika nyumbani kwao Zaylisa ilikua ni mishale ya jua la utosi lililokuaย likikimbia haraka, jasho lilikua likinitoka maana nilitembea kwa umbaliย
mrefu. Nilishtuka kuona palikua na magari mengi, pia Watu walikua wengi.ย Ilinifanya nijiulize maswali mengi yasiyo na Majibuย
โKuna nini? Itakua amepatwa na Tatizo gani, au labda amefiwa na Wazaziย wake, auโฆ?โ kabla hata sijamaliza kutafakari nilimwona Mtu mmoja akijaย upande Wangu akitokea nyumbani kwao Zaylisa. Niliona ni Boraย nimuulize, nilimsimamisha Kisha nilimsalimia kwa sauti ya kiungwanaย sana, baadaye nikamuulizaย
โSamahani Kaka, pale Kuna nini mbona naona Kuna Watu wengi?โย akanitazama Kisha naye akageuka kuangalia tena kama vile hakutokeaย huko, Kisha akaniulizaย
โWewe ni ngeni hapa mtaani?โ nikajichekesha chekesha kidogo Kishaย nikamjibuย
โNdiyo, nilikua napita tu.โย
โKuna harusiโย
โHarusi?โย
โNdiyo, vipi umeshtuka Mzee?โย
โNani anaolewa?โย
โMtoto wa Mwenye nyumba anaolewa, anaitwa Zaylisaโ alisema Kishaย aliondoka zake, hakujua alikua ameupasua moyo Wangu kiasi gani, hakujuaย alikua ameuunguza moyo Wangu kwa kiasi gani. Chozi la pole pole lilianzaย kunitoka, nilihisi kuishiwa nguvu.
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya PILI
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xxย
8 Comments
https://shorturl.fm/AdLg6
https://shorturl.fm/uQzHP
Naqubali
๐ฅ๐ฅ๐
https://shorturl.fm/ZSSyX
wtmpejopseftlhugezzqkjgiyifqzi
8iqutt
z4zfch