Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Hapa Ndipo Ambapo Walikosea Simba Na Kufungwa
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Hapa Ndipo Ambapo Walikosea Simba Na Kufungwa

    Living ShayoBy Living ShayoApril 20, 2024Updated:April 21, 202413 Comments3 Mins Read8K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Yanga vs Simba sc
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Namna timu zote mbili yaani Yanga pamoja na Simba zilivyoingia uwanjani na kucheza ni jambo ambalo wengi walitarajia na imetokea hivyo na tofauti ya mchezo wao wa mwisho kukutana na hii ni ndogo sana, Yanga SC alimuachia Simba SC kumiliki mpira kwa dakika 20 za mwanzo na dakika zilizobaki alizichukua na kumiliki mchezo kwa kasi kubwa.
    Kasi Ya kushambulia kwa timu zote ilikuwa juu kwa dakika za mwanzo na timu zote mbili zilitengeneza nafasi za magoli, Simba SC wakitengeneza nafasi nzuri za kufunga na zote zilikuwa kwa Sadio Kanoute ila walishindwa kutumia, ubora wa Yanga SC ulikuwa kwenye matumizi ya nafasi chache za kufunga walizopata na wamezitumia vizuri.
    Tatizo lilikuwa wapi kwa timu zote mbili ? Simba SC waliacha mianya au nafasi sana hususa kwenye eneo lao la kati na mikimbio mingi waliyoamua kuanzisha Yanga SC kuelekea mbele ilikuwa ikipitia katikati. Yanga SC kwao ilikuwa rahisi kuzuia mashambulizi ya Simba SC kwani walikuwa haraka sana kureact kukava mianya yao.
    Kipindi cha pili kilibadilika sana na Simba SC, walikubali kuwa chini kidogo na kuhepusha kupishana sana na Yanga SC wakiwa kwenye 4-2-2-2 na Yanga SC waliamua kuwa chini kuufanya mchezo uwe taratibu na hiyo ilisababishwa na ubora waliyonao na matokeo walishakuwa nayo kwa muda mrefu hata hivyo wakati ambao waliamua kuondoka taratibu na kushambulia walikuwa sahihi ila kuna wakati maamuzi hayakuwa sahihi.
    Kuna wakati Simba SC ilikuwa inashindwa kueleweka wafanye “press” au wazibe mianya kwanini ? Kubwa ni walikuwa wanapanda sana na wakati mwingine walikuwa wachezaji wawili hadi watatu kwenye mpira jambo lililofanya mpira ukiamishwa basi mianya kuonekana.
    Magoli yote mawili waliyofungwa Simba SC yalikuwa na makosa ya wachezaji wao, goli la kwanza kosa lilikuwa kwa Hussein Kazi kushindwa kufanya maamuzi ya haraka na kupelekea presha “press” kuongezeka kutoka kwa Aziz Ki na kupelekea kufanya kosa, goli la pili uharaka wa Joseph Guede na pasi ya Khalid Aucho ilikuwa bora ila kwa kosa alilofanya Mohamed Hussein ni lazima upate adhabu na adhabu hiyo ni kufungwa goli, kwa upande wa Simba SC umakini mdogo wa mabeki wa Yanga SC ndiyo uliyowapa adhabu ya kuruhusu goli wachezaji 3 dhidi ya Mmoja na bado waliruhusu goli Mchezaji pekee aliyeonyesha kutaka kufanya maamuzi haraka ni Ibrahim Bacca pekee.
    Sadio Kanoute nafasi mbili za kufunga goli ila anashindwa kufunga jambo linalompa nafasi mpinzani wako kukuadhibu kwa nafasi chache alizopata. Kibu Denis kasi nguvu na kujituma kwake hakuna shida ila eneo lake la mwisho bado linahitaji maboresho zaidi, Stephane Aziz Ki amekuwa na msimu bora sana namna anamiliki na kuondoka na mpira zaidi amekuwa hatari sana kwenye kupiga pasi mara nyingi pasi zake alizopiga zilikuwa zinafika na hatari sana, Clatous Chama kuna kitu ameongeza kwenye uchezaji wake amekuwa akishuka chini kuchukua mipira na kukaba pia amekuwa ndiyo msingi mkubwa wa kuanzisha mashambulizi kwa Simba SC msimu huu hususa kwenye raundi hii ya pili.
    Mchezo wa leo ulikuwa wa kimbinu zaidi kwa pande zote mbili Simba SC na Yanga SC na ulifanya kuwa wa tofauti na matarajio ya wengi.

    SOMA ZAIDI: Tabiri Sasa Matokeo Ya Dabi Ya Kariakoo Hapa Kijiweni

    magoli yote yanga vs simba pacome yanga ynga vs simba
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.