Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Goryanah Sehemu Ya Tisa (09)
    Hadithi

    Goryanah Sehemu Ya Tisa (09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 14, 2024Updated:June 15, 202418 Comments8 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Riwaya ya Goryanah
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia ” Jolvin alimwangalia Joely Huku akimpatia ishara ampake dawa make yeye ashaanza kumuonea huruma kwa ile dawa ni Kali sana, ilikuwa ni ” iodine solution”

    Joely alichukua pamba akainoweka kidogo kwenye dawa Kisha alifanya Kama anamfuta, Kelele ya maumivu ya dawa ilisika nyumba nzima ”Β 

    EndeleaΒ 
    SEHEMU YA TISAΒ 

     

    Bibi alikuja anakimbia pamoja na Esau, ile wanafika mlangoni wanakutana na Jolvin akiondoka, kashidwa kuvumilia maumivu anayoyapata Gorii! Ilibidi akae nje kwanza mpaka watakapomaliza kumhudumia.

    Huku kwa Gorii” aliendelea kuugumia maumivu huku akilalamikaΒ 

    “” Ni Moto hii dawa naungua, naunguuua!”

    Kelele za maumivu zikamfanya hata Rich akimbie chumbani, Kama walikuwa wote huenda hata yeye anakidonda, asije pakwa bure maumivu anayoyapata Gorii akayasikia Kwake.

    Baada ya matibabu kukamilika, Jolvin ndio anaingia! Alimkuta Gorii” kalala kwenye sofa ubavu mmoja, ilibidi asogeze kiti kilichokuwa Karibu Kisha alitizama vizuri kile kidonda, muda huo Gorii” alikuwa akisikilizia maumivu kwa mbali huku akijaribu kutafuta usingizi.

    Β Β Β “” Polee Goryanah!”

    Gorii” alisikia vizuri ile sauti kaitwa jina lake kwa kirefu, alimtizama Jolvin Kisha aliongea.

    Β Β Β “” Leo umeniita Kama mama kabisa! Mamangu hupenda kuniita kwa kirefu “” Goryanah”

    “” Basii… Wewe pumnzika kukiwa na shida toa taarifa! Halafu kwasasa unatakiwa uwe na Simu make waweza zidiwa!”

    “” Mimi Simu ya Nini? Wakati Sina hata Ndugu wa kumpigia! Halafu kule kijijini ninae Mamangu anaitwa Ma Muddy nisaidie basi nipate kuwasiliana nao! Sijui hata Muddy anaendeleaje huko!?”

    “” Siku ukipona nitakupeleka ukaione familia yako!”

    “” Ooh! Wao Kaka White… Nitashukuru Sana Kaka White!”

    “” Tulia sasa! Utaumia ukijilazimisha kuamka! Nitakuja baadae kukuona!!”

    Huku Chumbani kwa Esau, walikuwa wamekaa wote na wadogo zake Joely na Rich wakimzungumzia Jolvin.

    Β Β Β “” Mimi naona Jolvin! Ameanza kumjali Sana Gorii” huenda kaanza kumpenda vile!”

    “” Aaah! Ka Joely! Yule ni mdogo kwake, afadhari hata Mimi naendana nae kwa Kila kitu.

    Rich alidakia….

    Esau yeye huwa siyo muongeaji Sana alibaki kucheka tu!Β 

    “” Mi naona aendelee kuwa vile hata hivyo tabia zake za hasira hasira Gorii kamnyosha, Unajua huwa anatabia ya kuzira zira vitu, naona sahii haifanyi.”

    “” Na Da Anelisa Itakuwaje!? ” Make huwa anampenda kweli Jolvin japo Yeye anachukuliwa Kama rafiki tu!”

    Joely alimhoji Esau huenda anajua zaidi kuhusu moyo wa Jolvin.

    “” Anelisa ni rafiki tu! Hata yeye analijua Hilo kwa Jolvin anachukuliwa Kama rafiki!”

    “” Ila Bibi sijui kwanini tu hampendagi Anelisa! Hutaamini humu ndani Gorii” ndie anapedwa kuliko wote! Siku yenyewe ameletwa na Ma Doreen hutaamini Gorii” alikataa kukaa hapa! Bibi akadeshi kuumwa mguu, Gorii akamsaidia hapo hapo Bibi alilazimisha Gorii” abakie!”

    Maneno ya Rich yaliwasitua kwanza ilibidi wabaki wakitazamana, Muda huo huo Jolvin aliingia Kisha alijilaza kitandani kwa Essau, aliongea.

    Β Β Β “” Vipi Kama tutashilikiana kumtafuta Mamake Gorii” akipatikana haraka inabidi aondoke hapa! Make naona Kama kichwa changu kinaniuma kuhusu yeye!”

    Β Β “” Mhuuu aondoke tenaa!! Mimi naona upo KaribuΒ  nae iweje utake aondoke!?”

    Joely alijibu.

    Β Β “” Akakae kwao make anatufanya tubaki tunamtizama yeye! Mpaka tunashidwa kujisomea kwa wakati.”

    Maneno ya Jolvin yaliwachanganya huenda wao walihisi tofauti kuwa anampenda, kumbe kafanya vile ni huruma ya Gorii kuwa mgonjwa.

    Baade walisikia mlango ukibishwa hodi, ni mama yao alirudi Baada ya kutokuwepo wiki moja alipelekwa dolia ya wiki kulinda mipaka, wakati wa kurudi alirudi pamoja na familia ya Ma Doreen.

    Mama aliingia huku akiita Gorii”, Doreen nae pia alikuwa kamumisi kweli Dadake japo wanatofautiana Kama miezi miwili tu, ile wanafungua mlango ndio wanamkuta Gorii” kalala huko jasho jingi likimtoka.

    Rich yeye Baada ya kusikia mama karudi alitoka moja kwa moja kumuona.

    Β Β Β “” Rich nambie! Gorii” kawaje tena!?”

    Rich ilibidi amweleze ilivokuwa ndio Mama akashusha pumnzi huku akimshika kichwani.

    Β Β Β “” Hii familia iliyofanya hivi lazima itatutwe, Kuna siku watamuumiza zaidi.”

    Β Β Β “” Maama! Ka Jolvin tayari kaanza kuifatilia hii familia!”

    Gorii” yeye alikuwa busy na Doreen wakiongea sitori zao, kweli walikumbukana Sana.

    “” Sasa Gorii… Inuka tutembee tembee hata hapo nje upugwe upepo!”

    Waliongozana kwa pamoja Hadi nje huku wakiwaacha kina mama wakiongea kuhusu maendeleo ya Gorii, hata hivyo Gori alikuwa amependeza Sana sio Kama kipindi kile anaingia kwenye nyumba hio. Mama Rich alimwelezea jinsi Bibi anavyomkubali Gorii pamoja na familia yake kwa ujumla.

    Huku nje Doreen pamoja na Gorii” waliendelea kupiga sitori nyingi lakini alimwomba siku moja afike Nyumbani kwao tena! Hata hivyoo wamemumisi.

    “” Sawa Doreen nitafika’ Vipi kuhusu Baba make alinichukia siku ya kwanza tu aliponiona! Maskini Baba sijui nilimkosea nini tu, mpaka nikawa na wasiwasi huenda tuliwahi kukatana ghafra nikamfanyia kitu kibaya, hata siku ile kaniona akataka kulipiza kisasi.”

    “” Achana nae, huwa inatokea tu mtu unaonana nae siku moja lakini damu zinashidwa kuendana, yaani unamchukia Ghafra!”

     

    Muda huo Jolvin alikuwa akipigiwaΒ  Simu na Anelisa, alitoka akizungumza.

    Β Β Β “” Kwamba Yule Mama anaefanya kazi za ndani katoroka na pesa! Kwanini Sasa kafanya hivyoo!? Okay nakuja.”

    Gorii” alimsikia vizuri Jolvin akiongea, Alishangaa ghafra anapata mshituko ilibidi amfuate Jolvin. Jolvin muda huo alikuwa akiingia kwenye gari alimkata jicho Kali lilionesha hataki mazoea.

    Doreen alimfuata Kisha alimshika mkono, wakirudi sehemu walipokuwa wamekaa.

    “” Sijui hata nafanya Nini tu, nimejikuta namhurumia huyo mama alieiba pesa! Huenda hata alikuwa na uhitaji wa hiyo pesa!””

    “” Gorii” usiwe unaingilia vitu visivyo kuhusu! Achana nae, hapa ni mchini Kuna watu huwa wanaomba kazi za ndani kumbe wanayao kichwani!”

    Jolvin alifika Hadi Nyumbani kwao Anelisa, aliikuta nyumba ipo kwenye simanzi kila mtu anawazua kivyake.

    Β Β Β “” Anelisa nikuone kwanza…!”

    Walitoka nje huku wakizunguka uwani, Anelisa akimwelezea.

    Β Β Β “” Ni mama mpole hivi, ana nywele ndefu huwa anapenda kubana, Mimi nahisi kachukua zile pesa ni kwaaajili ya matibabu, Mwanzoni alivyokuja hapa alikuwa ana afya mbaya! Mwili wake ulikuwa umejaa mapele, Baba alivyomuona vile aliongea na Mama aongee nae vizuri kuhusu huo ugonjwa, Mama Baada ya kuongea nae alikuwa muwazi kweli yeye ni Muathirika wa Ukimwi wa muda mrefu pia huwa anasumbuliwa na kifua! Mama alirudisha majibuΒ  kwa Baba, ilibidi Kama familia ikae muda huo na Kaka alikuwepo wakaona kazi kumfukuza ikabidi wamruhusu aendelee kukaa huku akiendelea kutumia dose, afya yake ilianza kukaa vizuri wote tukawa tumemwamini, hata hivyo alikuwa ni mcheshi Sana muda wote uwepo wake humu ndani ilikuwa ni furaha! Sielewi hata amewaza Nini kachukua pesa chumbani kwa baba akawa ametoroka, tumeamka asubuhi tunakuta kachukua nguo baadhi tu huku nguo zingine kaziacha.

    Β Β Β “” Usijali Anelisa! Atapatikana tu! Huyu atakuwa hayupo mbali, labda unapicha zake nimuonee!”

    Anelisa alichukua Simu yake, Kuna picha nyingi alikuwa akimpiga, muda mwingine wapo wote au na familia kwa ujumla.

    “” Una uhakika ndie huyu? Mbona hafananii? Halafu sura Kama naijua.

    “” Sura…!!?”

    “” Yaaah!! Sijui nimemuona wapi kweli…!?”

    Jolvin alifungua Simu yake, Kuna picha ile siku kaziona chumbani kwa Gorii” alizipiga picha, mpaka kile kipepelushi alichokuwa akisambaza kumtafuta.

    “” Nitakuwa nimemfananisha au macho yangu tu!?”

    Anelisa alidaka ile Simu Kisha alianza kuzipitia zile picha.

    Β Β Β Β Β “” Mbona ni yeye kabisa, unaona hapa alivyobana nywele! Hii sitaili anaipenda kweli! Wewe unamfahamu!?’

    “” Ni Mamake na Yule Binti anaeishi Nyumbani!?”

    “” Kile mnakiita ki Gorii” siku yenyewe ulikisaidia kikiwa na Rich kimejaa tope!?”

    “” Jolvin alimukubalia kwa kichwa.

    Bila kuongea na wazazi wa Anelisa walichukua Gari kuelekea Nyumbani wakapate majibu kutoka kwa Gorii”

    Ile kufika tu Jolvin alikuwa na hasira nyumba nzima alisikika akimuita Gorii” aje sebuleni.. Familia yote nayo ilifika pale wasikilize kipi tena kimejili, muda huo hata Ma Doreen alikuwepo bado.

    Gorii” ndio anatoka chumbani akiwa na Doreen huku akishangaa..

    Β Β Β “” Kaka White… Ndio Wewe unaniita kwa sauti hivyoo! Huoni naumwa!?”

    Β Β Β “” Unaumwa Wewe tapeli mkubwa, yaani mmee……..!”

    Jolvin aliwahi kumustopisha Anelisa, Alichofanya ni kumuonesha picha katika Simu yake.

    Gorii” alichukua Simu huku akipekua picha.

    Β Β Β “” Huyu si Mama? Kaka White mamangu yupo wapi!? Mbona hukuniambia Kama umempata!?”

    Aliendelea kupekua zaidi picha, Baada ya kumaliza kukagua alianza kumuonesha Bibi yake.

    Β Β Β “” Bibi huyu ndio Mama’ngu Mimi ninae mtafuta siku zote! Kumbe yupo hai mama siku zote anaishi!?”

    Kabla hajamaliza kuongea, anashangaa wazazi wa Anelisa wanaingia huku wakiwa na police.

    Wote walitoa macho hawakuamini, Sikuzote unaambiwa familia yenye uwezo huwa wanafanya kile wanachokitaka na sio kinachotakwa.

    Β Β Β “” Police tenaaa…..!!?”

    Kila mtu aliduwaa asiamini hata Jolvin hakujua itakuwa vile, ilibidi amgeukie Anelisa.

    “” Wewe ndio umefanya hivyoo!?”

    Anelisa alitabasamu Kwanza Kisha alimsogelea Gorii” amjibu kipi kinaendelea..

    Β Β Β Β Β “” Mamako wewe ni mwizi! Kaiba million tano Nyumbani! Haijulikani kakimbilia wapi!? Nahisi tukikukamata Wewe mamako atajisalimisha kwahiyo sahii upo chini ya ulinzi.”

    “” A aah! Mamangu hawezi kuiba pesa nyingi vile! Kwanza hanaga hiyo tabia! Ndio umemtengenezea kesi Mama’ngu! Ni kwakuwa hunipendi Mimi ee? Kwakuwa ni Mama nitaenda kutumikia kifungo… kikubwa aishi tu! Madaam yupo hai halafu leo hii nakamatwa na Police… Nafurahi kusikia anaishi ila naumia kwasababu amesingiziwa.

    Babake Anelisa aliona Kama Gorii” anafanya maigizo aliamuru Police wamkamate. Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KumiΒ Β 

    Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment YakoΒ 

    Ulipitwa naΒ SIMULIZI NYINGINE?Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoΒ kijiweni.co.tzΒ unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiΒ [email protected]Β Β 

    Goryanah Goryanah Kijiweni Riwaya ya Goryanah

    18 Comments

    1. mwanamani on June 14, 2024 4:25 pm

      ongeza nyingine jmani

      Reply
    2. Teddy on June 14, 2024 4:53 pm

      Maskini GoriiπŸ˜”

      Reply
    3. Stephen on June 14, 2024 4:54 pm

      Hii. Baab kubwaaaa πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

      Reply
      • Bintii kimmy on June 14, 2024 10:54 pm

        πŸ₯²πŸ₯²πŸ˜­πŸ˜­goriiii

        Reply
    4. Jack bujo jr on June 14, 2024 5:03 pm

      Tatizo kaka unatucheleweshea story mpaka tunajikuta bando lina kata jitahidi bana ujue sio wote ni watu wa mpira au Mambo ya siasa twende kwa usawa kaka acha upendeleo wa sehemu moja

      Reply
    5. Avilly on June 14, 2024 5:25 pm

      Ipost sehem ya kumi Leo jamni mbona unatuweka roho juu jamn

      Reply
    6. Bplm1664 on June 14, 2024 5:37 pm

      Kutokaaaa alooooo
      Ni ya motoooo sanaaaa hii

      Reply
    7. YOHANA on June 14, 2024 6:30 pm

      Nasubir nyingine apaa hiyoo ya Jana bado ya Leo 🀣 ,imeanza Kua fire kwerii πŸ™ŒπŸ™Œ

      Reply
    8. Farnoush on June 14, 2024 7:30 pm

      Oooh Goryanah jamaniii duuuh

      Reply
      • Ibrahim Mohammed on June 15, 2024 1:21 pm

        Habar yo moo

        Reply
    9. Candy on June 14, 2024 7:38 pm

      Post ya leo bas jana hujapost

      Reply
    10. Amayrah on June 14, 2024 8:08 pm

      Jamaniiii gory 😭😭😭

      Reply
    11. Kibasa on June 14, 2024 9:22 pm

      Mbana story Haina muda maslumu

      Reply
    12. Jimmy Gebhard on June 15, 2024 12:32 am

      ni speed ya chui….

      Reply
    13. Shuwena on June 15, 2024 10:28 pm

      Safi sana

      Reply
    14. Mabadiliko on June 16, 2024 12:32 am

      Waatu tunakopa bando na kumaliza kazi zote mapema kisa hadithi ila tunakula ni mambo za mipira mmmmmmmmh hpn bhna sio wote twapeda mipila πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ™„

      Reply
    15. Tinner Rober on June 16, 2024 3:34 pm

      ❀❀❀❀

      Reply
    16. Veronica William on June 17, 2024 1:44 pm

      Jamaniii gorii pole sana 😭😭😭

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.