Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Goryanah Sehemu Ya Sita (06)
    Hadithi

    Goryanah Sehemu Ya Sita (06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 10, 2024Updated:June 12, 202416 Comments6 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Riwaya ya Goryanah
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia ” Wakati wakiwa jikoni wadada wa kazi wote walishadadia Gorii” apeleke kinywaji kwanza kwani wote wanamuogopa Jolvin, muda wote ni kusodoa, wakati mama anaita Goriii ndio alikuwa akimimina Juice kwenye Grass baadae alifika sebuleni na kuweka mezani.

    Endelea
    SEHEMU YA SITA

     

    Baadae aliinua kichwa kumtizama Rich make alimkanyanga mguuni, muda huo alikuwa amewekwa kati na kaka zake.

    Goriii ilibidi amtizame kwanza, Kisha alimaliza kuwatizama na wale wengine Kisha aliongea..

      “” Wajukuu wa Bibi wanamfanana Bibi yao kweli! “” Oooh sorry Sijawasalimia… Shikamoni wajukuu wa Bibi!””

    Jolvin aliishia kumtizama Gorii” huku akimshangaa, lakini Esau na Joely wao waliitikia huku wakimtizama Gorii” alivyomcheshi.

    Muda huo Gorii ndio anagawa juisi kwa Kila mtu alipofikia kwa Jolvin Alibaki kutizama ule mkono ulivyoshika Glass, Kisha alipokea ile Glass akaiweka chini huku akimtizama Gorii”.

       ‘” Your name is…!!!!?”

       “” Gorii” Goryanah!!”

    Rich ilibidi aingilie kati make Kaka anakoendelea sio kuzuri!

    “” Gorii” nenda Basi ukasaidiane na wadada wa kazi mlete chakula!”

    Gorii” alivyoondoka, Jolvin nae alimfuata njia ile ile anakoelekea, kumbe alikuwa akiishia chumbani kwa Bibi.

       “” Wewe Kaka White! Mbona unatembea nyuma yangu!?”

    Jolvin hakujibu zaidi alikata Kona kuingia mlango wa pili ambao ni chumba Cha Bibi.

       ‘” Bibi! Hutaki kumuona mmeo leo!? Ndo umejifungia.

    Chumba kilionekana kuwa kimya, Jolvin ilibidi akae kwanza lakini kwa pembeni aliona Kuna mihogo ya kukaagwa, aliangalia upande wa pili hamna mtu alichukua mhongo mmoja akaula kwa uharaka Kisha alitulia.

     

    Katika pita pita za Gorii” alikuwa akija ndani kumkalibisha Bibi yake chakula, aliingia kimya kimya bila kupiga hodi ndio anamkuta Jolvin akimalizia mhogo wa pili! Ilibidi kwanza acheke huku akichukua sahani ili kuhakikisha Kama bado Kuna mihogo.

    “” Ooh!! Wewe ndie umekataa juisi nilokuletea halafu unakuja kula mihogo ya Bibi, Ngoja nikamwambie Bibi umekula mihogo yake!”

    Gorii” alitoka haraka ili akaseme lakini Jolvin alimuwahi! Kisha alimsogelea Karibu huku akimziba mdomo.

       “” Wewe ni Nani kwanza katika nyumba hii? Umeleta vyakula vya huko nje hata havijachunguzwa! Wataka Bibi yangu ale! Hujui anae magonjwa ya moyo!””

    “” Oooh! Wewe Bibi yako anae magonjwa ya moyo! Vipi kuhusu mama yangu make nahisi anae magonjwa mengi Sana! Mimi najitahidi kumuweka sehemu nzuri Bibi yako! Sijui hata Mamangu huko aliko anaishi katika mazingira gani tu?”

    Wakati wakiendelea kuongea kumbe Bibi alikuwa ametoka kidogo, muda ule anarudi anawakuta wapo kwenye position tofauti kabisa, aliaanza kuwatizama make muda huo kila mtu alikuwa akimtizama mwenzake kulingana na uzito wa maneno aliyoyatoa, Jolvin aliamua kumuachilia baada ya kuhisi Kuna mtu.

       “” Bibi nakusubili Wewe tu! Nataka uniambie ulienda wapi kwanza! Au ushapata mwingine!?”

    Jolvin aliongea huku akivuta kiti akae. Gorii” yeye aliamua kuwapisha!”

    Bibi Alibaki akimtizama Gorii” jinsi anavyoondoka! Mpaka aliingiwa na wasiwasi hata Mjukuu wake alilitambua Hilo.

    “” Bibi! Kwani Gorii” ni mtoto wa Nani!?”

    “” Masikini Gorii” Unajua Sipendi kumuona anakosa furaha Mjukuu wangu! Yaani muda wote huwa anapenda kukaa Karibu na Mimi! Hata Kama akiwa na huzuni hufanyia chumbani Kwake ila akirudi huku ni furaha tu!”

     

    Jolvin aliamua asimhoji kwanza kuhusu Gorii” make hata akili yake ilikuwa mbali!”

     

    Huku kwa Gorii” aliingia jikoni kuandaa Juisi ya Bibi, baada ya kumaliza aliweka kwenye Grass alipeleka chumbani kwa Bibi, alimkuta Jolvin yupo kwenye sitori nzito na Bibi! Aliwaza arudi lakinii aliangalia saa iliyokuwa ukutani! Alijua ni muda wa Dawa.

    “” Kaka White! Nipe nafasi kwanza nimpatie Bibi Dawa!”

    Jolvin ilibidi akae pembeni akiangalia nesi anavyomhudumia mgonjwa!

    Gorii” alimaliza kumpatia dawa Kisha alimsogelea Bibi yake sikioni akamnong’oneza.

       “” Kaka White! Kapita na mihogo yako!”

    Bibi ilibidi amurudishe kwanza Gorii” chini Kisha alimuuliza Jolvin.

       “” Ile tabia yako ya kula mihogo kumbe bado unayo!?”

       “” Mhu mhuu… Mi miimi!!?”

    Goryanah ndio alicheka huku akichukua sahani ilokuwa na mihogo akimuonesha Jolvin.

    “” Ni wewe Ndio! Halafu umenitishia nisiseme kwa Bibi!”

    Bibi ilibididi acheke tu, Kisha alimvuta masikio Jolvin akimuomba aombe msamaha kwa Gorii” kwa kumtishia.

       “” Bibi kabla sijaomba msamaha! Nayeye anitake radhi! Kwanini ananiita Kaka White na si Jolvin!?”

    Gorii” ilibidi acheke kwanza Kisha alijibu.

       “” Mfano Mimi naitwa “Gorii”  “Goryanah” Ila Wewe nimeona waitwa Jolvin huna jina jingine, ukiwa kaka White itapendeza Sana, kwanza wewe msafi, chumbani kwako kumejaa nguo nyeupe! Namimi nimekuita “Kaka White” kwasababu unapenda nguo nyeupe!”

       “” Gorii” chumbani kwangu tenaa!? ” Inamaana umeingia…? “Hivi Wewe ni Nani kwanza katika Nyumba ya Mishoki!?”

    Rich aliamua kuwafuata chumbani baada ya kuwasubili muda mrefu mezani!

       “” Kaka, Bibi.. tunawangoja mezani, chakula kinapoa!

    Maada iliishia hapo! Ilibidi waelekee mezani, lakini Jolvin swala la Gorii” kuingia chumbani Kwake alikuwa akiendelea kulitafakari! Mpaka anamaliza kula.

    Baada ya kumaliza kula ilibidi Maama awaite wanae kwa pamoja alifanya kuwatambulisha vizuri kuhusu Gorii” make walikuwa hawajamuelewa kwa undani! Baada ya utambulisho kila mtu alikuwa kawa mwenyezi hata Gorii” alitambulishwa kuwa wale ndio Kaka zake! Make mama alikuwa anao watoto wa kiume tu na wao ni watatu Rich ndio wa mwisho halafu Esau, Jolvin wamefatana! Na Joely ni mtoto wa ba mkubwa! Wote wapo chuo wanasoma.

    Asubuhi kulipopambazuka Kama kawaida Goryanah aliamka asubuhi kufanya kazi za ndani akishilikiana na wadada! Baada ya kumaliza waliweka chai mezani huku kila mtu ni kujisevia.

    Majira ya mchana Gorii” alikaa bustanini akipunga upepo! Mwisho kabisa aliamua kujilaza kwenye nyasi, usingizi nao ukawa umemchukua! Ile anakuja kuamka anamkuta Rich kakaa pembeni yake huku akiwa na note book ya Gorii” muda mwingi alizoea kumchora mamake huku akiandika maneno mengi, mama nimekumisi, mama hivi uwapi? Lini nitakuona?”

    Gorii” ndio anaamka huku nywele zake zimejaa majani alianza kujitengeneza huku akitumia kioo Cha Simu ya Rich. Rich ilibidi amsaidie kumtolea.

    “” Nishakwambia umefikia muda wa kuwa na mchumba ili awe anakutolea Kama hivi na sio Mimi kakako!?”

    “” Wewe nae! Kunitolea tu Hadi niwe mchumba wako! Sa mbona unanitolea Sasa na si mchumba wangu!?”

     

    “” Kuna siku nitakuoa! Kama utakosa mtu wa kukuoa!”

    Goryanah ilibidi amsine mguuni kwanza Kisha walianza kurushiana majani wakikimbizana, lakini kwa bahati mbaya wakati Gorii” anarusha yalimuangukia Jolvin kichwani na mengine usoni. 

    Jolvin ilibidi asimame kwanza make alikuwa haoni, alinyanyua mkono wake kwanza ili afute kwa bahati mbaya tenaa Simu yake ilianguka chini, Rich baada ya kuona vile ilibidi akimbie huku msala ukibakia kwa Gorii’‘

    Nini Kitaendelea Usikose Sehemu Ya Saba 

    Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

    Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]  

    Goryanah Goryanah Kijiweni Riwaya ya Goryanah

    16 Comments

    1. mamu on June 10, 2024 7:46 pm

      Stori imenoga

      Reply
    2. Bplm1664 on June 10, 2024 7:47 pm

      Poor Goryiiiiiiiiiiiiii

      Reply
    3. Stephen on June 10, 2024 8:54 pm

      Hapa ndo penyewe Sasa 🔥🔥🔥

      Reply
    4. Stephen on June 10, 2024 8:55 pm

      Hapa Sasa ndo penyewe 🔥🔥🔥

      Reply
    5. Bintimanoti on June 10, 2024 9:03 pm

      Sa itakuaje kwa goryanah wetuuu ….next pls

      Reply
    6. Mabadiliko on June 10, 2024 9:11 pm

      Utam kunoga Sana ❤️❤️❤️❤️❤️

      Reply
    7. Mosos on June 10, 2024 9:17 pm

      🔥🔥🔥

      Reply
    8. MOSSES on June 10, 2024 9:18 pm

      🔥🔥🔥

      Reply
    9. Joji on June 10, 2024 10:49 pm

      Shida ni hizo ..kunae,panae,hamnae.. ndugu mwandishi,Kiswahili basi kidogo tuzingatie 🙏😁
      ULUMBI kila mahali

      Reply
    10. Noryn on June 10, 2024 11:21 pm

      Hapo sasaaa

      Reply
    11. Halinga on June 10, 2024 11:52 pm

      Kazi ipo Goriiii kaya timba

      Reply
    12. Teddy on June 11, 2024 9:52 am

      Hii story inazidi kunoga

      Reply
    13. Hance on June 12, 2024 8:52 am

      Imengoa ila kaka white inaonekana ndo atakuja kumpenda gor

      Reply
    14. Makoye Malonja on June 12, 2024 9:01 am

      Admin hatuelewi riwaya ya Goryanah ndo imeishia sehemu ya 6?

      Reply
    15. Benjamin Makonda on June 12, 2024 2:06 pm

      Kaka unajua sana yyn inafurahisha mnoo🤓

      Reply
    16. Abdallah on June 12, 2024 7:21 pm

      Chai inaelekea kuiva tuandae vikombe

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.