Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Goryanah Sehemu Ya Kumi (10)
    Hadithi

    Goryanah Sehemu Ya Kumi (10)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 15, 2024Updated:June 17, 202424 Comments6 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Riwaya ya Goryanah
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia ” Aaah! Mamangu hawezi kuiba pesa nyingi vile! Kwanza hanaga hiyo tabia! Ndio umemtengenezea kesi Mama’ngu! Ni kwakuwa hunipendi Mimi ee? Kwakuwa ni Mama nitaenda kutumikia kifungo… kikubwa aishi tu! Madaam yupo hai halafu leo hii nakamatwa na Police… Nafurahi kusikia anaishi ila naumia kwasababu amesingiziwa.

    Babake Anelisa aliona Kama Gorii” anafanya maigizo aliamuru Police wamkamate.”

    ENDELEA 

    SEHEMU YA KUMI 

     

       “” Hapana hicho sio kigezo Mjukuu wangu akawekwa ndani! Na hawezi kupelekwa kituoni kwa kudhalilishwa njia nzima, nyie tangulieni atapanda kwenye gari yangu! “Jolvin naomba unipakie.”

    ” Aaa.. lakini Bibi.. Mtuhumiwa ni Mtuhumiwa tu! Acha aende!”

    Wakati huo wakiendelea kuvutana, Ma Doreen, na Ma Rich wote waliingilia wakisema wataenda wote. Rich yeye alivunja ukimya kabisa alikimbilia kwenye gari la Police akidai watakuwa wote na Gorii”

    Jolvin alibaki kushangaa, Esau na Joely walimfuata.

    “” Hivi ni kweli kinachoendelea ni sahihi!?”

    “” Mimi sikutegemea Kama Police wangefika hapa! Ilikuwa ni kumuuliza Gorii Kama zile picha ndie Mamake, halafu ndio tuone namna!!”

    Anelisa alifika pale alimshika mkono Jolvin akimhitaji waondoke.

       “” Usijali kwasasa hutawaza tena kuhusu Gorii, hapa tutamuweka ndani akitoka hapo ataenda kuanza maisha na Mamake kijijini kwao!”

    Muda huo Bibi alikuwa tayari kakaa kwenye gari akimsubili Jolvin amwendeshe, lakini kwa Nyuma alikuwa amekaa Gorii katulia huku kajinamia, Jolvin alifanya kumuangalia kwa hasira Kisha alishika usukani kuelekea kituoni.

    Baada ya kufika Wazazi wa Anelisa walitangulia ndani, huku akifatiwa Bibi pamoja na mwanae Mama Rich, siku hiyo kituo kiliwakishwa mwenye pesa,  na mwenye pesa mwenzake kitakachomuonesha mwenzake mshindi ni uharaka wa kudadavua tatizo kwa uelewa zaidi.

    Gorii Baada ya kushuka aliaambiwa asaini jarada la kesi ili waendelee kuifanyia Uchunguzi. Baada ya kumaliza kusaini alienda kujitenga mwenyewe huku akizunguka akikumbuka taswira ya Mamake alivyomuona kwenye picha.

       “” Kumbe Mamangu anaishi vizuri tu, anae mavazi mazuri, nywele yake kaiosha vizuri pia katana, na shingoni anacho kidani kizuri!”

       “” Gorii….!!!”

    Bibi alimuita Baada ya kuona anaongea pekee. 

    Gorii ndio anageuka.

    “” Bibi!! Mama kanifuata!? Kwasasa sitakaa mbali nae!”

    Bibi alitikisa kichwa akiashilia hamna. Muda huo huo Anelisa alifika, alimuijia Gorii ikawa wameongozana lakini Bibi alimkuta hilo jicho huku akiongea kimya kimya.

    “” Kama Mjukuu wangu atakuoa..  labda Mimi Bibi yake niwe kipofu nisione!”

    “” Gorii kwasasa unaweza kurudi Nyumbani! Ila muda wote tutakuita tukuhoji kuhusu familia yako! Huenda hiki ndio chanzo Cha mamako kuiba pesa nyingi!”

    Anelisa aliongea huku akimuacha Gorii kaduwaa asimjibu chochote! Rich alifika pale alimpatia mkono Gorii akimuomba waondoke!

       “” Rich…!! Kwani imekuwaje tena mpaka wameniruhusu niende Nyumbani? Mimi nataka nibaki hapa ili Mama akisikia nimekamatwa lazima atakuja kuniona!”

       “” Gorii!! Bibi anakungoja pamoja na Mama!

    Joely aliamua kuwafuata! Lakini kwa Gorii” hakuwa anataka kwenda Nyumbani aliangalia namna ya kubaki pale, aliinama akachukua jiwe lilokuwa chini Kisha alimlenga Askari mmoja kati ya wale walokuwa wakimhoji.

    Alipiga kelele kwa maumivu, huku akigeuka kumtizama aliyemponda, alikutana na Gorii kasimama wala hajali alimsogelea Yule Askari huku akimtolea maneno makali.

    “” Lazima nitakuua tu!”

    Watu wote walishituka, Kwanini Gorii” aseme hivyo au wanafahamiana? 

    Muda huo huo Police walimrudisha Gorii selo make kamtishia kumuua mtu. 

    Habari zikaenea kwa muda mfupi hadi zikamfikia Anelisa, ambae muda huo alikuwa bado yupo kituoni na familia yake wakitoa baadhi ya Picha za Mama Gorii” ili atafutwe.

       “” Unaona Mwanangu! Itakuwa kweli huyu Mtoto alivyomkorofi Ni harali Mamake aibe pesa! tabia ya Binti yake ndio imeonekana hapa!

    Baba Anelisa aliongea mbele ya Askari lengo lilikuwa ni kuongea na Binti yake lakini ujumbe ulifika mikononi mwa Askari, Maneno yale yaliwafanya kila mtu atikise kichwa, “Kweli, kwelii”

    Panapo Selo, Goriii alikuwa akihangaika na ile harufu ya pale! Mbaya zaidi ni pale alipoletewa chakula Kuna Askari alikuwa amechomekewa pesa ya kumsulubisha Gorii, alifanya kutumia kazi yake vizuri kutokana na hongo ya pesa.

    Huku Nyumbani familia ilikuwa haina raha kabisa, hasa Bibi ndio alikataa hata kula! Jolvin ilibidi akae na Bibi kumbembeleza lakini Bibi nae alimchunia alijua yeye ndio mwanzilishi wa yote.

       “” Lakini Bibi,” “Mbona unanichukia hivyo!? Utazani mimi ndie nilimshikisha jiwe Gorii amponde Askari!!?”

       “” Adhabu anayopata Gorii” huko yote ni kwaajili yako! Nishakwambia achana na Anelisa bado unajenga nae mazoea! Wazani ungekuwa umenisikiliza huko kupekenyua maneno kuwa Mamake Gorii kapatikana,, hii yote ni mazoea ulojijengea kwa Anelisa. Gorii binti mdogo anapitia mitihani mikubwa katika maisha bado Yule kijana majuzi kamtoa ngeu begani! Sina hata amani huko aliko Kama wanamchukulia ni binti mdogo! Hawanaga huruma wale, nahisi kile kidonda kimekuwa mara tatu yake sahiii!”

     

    Bibi alizidi kuongea, Kuna namna anamjua Mjukuu wake huwa anaogopa Sana kidonda! Ni Kama alimtekenya sehemu.

       “” Kwahiyoo Bibi! Watakuwa wakimjeruhi Tena kwenye kile kidonda nilichokihangaikia kipone!?”

       “” Tena sanaa! Masikini Gorii sijui hata Kama anatembea huko aliko! Akigeuka kila sehemu ni Rungu hadi kukapambazuke! Sizani Kama atakuwa Gorii tenaa! halafu nahisi wanaweza kumfanyia mchezo mbaya…..

    “” Basi Bibi usiseme…  Ngoja nimuwahi kabla hawajamjeruhi kidonda chake!”

    “” Kwasasa ni usiku! Hapa Hadi kesho Asubuhi!”

    Ilibidi waagane pale lakini maneno ya Bibi yalikuwa yamemkaa Jolvin. Asubuhi yake yeye ndie alikuwa wa kwanza kufika kituoni, aliomba aonane na Gorii. Mawazo ya Bibi hayakuwa mbali na fikra zake, alimkuta Gorii” kaegama ukutani huku nguo aliokuwa kavaa imetapakaa damu, alikumbuka maneno ya Bibi tena huenda hata wamemfanyia michezo mibaya!

    Alisogea karibu yake Kisha alimbeba akitoka nae nje.

       “” Vipi Mishoki… Mtuhumiwa wetu Kazidiwa Adhabu nin!?”

    Askari mmoja alihoji kwa Dharau, lakini muda huo huo Mamake Rich aliingia siku hiyo alikuwa amevalia gwanda yupo kikazi zaidi ile walivyomtizama wote waliogopa wakasogea nyuma.

    Gorii” alichukuliwa kupelekwa Hospitalini, alifika akaongezewa Dreep ya maji, Kisha alisafishwa kidonda. Mama Baada ya kuona anaendelea vizuri alimuachia Jolvin amuangalie Kisha alirudi kituoni kuendelea na kesi!

    Gorii ndio anaamka huku akihisi maumivu mwili mzima alitazama Kama Kuna mtu pembeni yake ndio anamuona Jolvin alimuita…

       “” Kaka White!! Upo hapa kunitizama muda wote!?”

    Jolvin aliona aibu hata kumtizama, aliona yeye ndie chanzo Cha yote hayo! Alisimama ili atoke nje lakini Gorii alimuita akaomba chakula.

    Ilibidi arudi Kuna hotpot ilikuwa imeshaandaliwa tayari kwa chakula alipakua kwenye sahani Kisha alimpatia.

     Gorii” alibaki akimtizama tu make hawezi kula kwa kutumia mkono kutokana na maumivu ya kidonda.

       “” Nahitaji msaada wako nipate kula!!”

    Jolvin hakuwa na budi kufanya vile, alianza kumlisha taratibu Kisha alimuuliza.

    “” Mimi ni mwema kwako!?” Usikose Sehemu Ya Kumi Na Moja

    Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

    Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]  

    Goryanah Goryanah Kijiweni Riwaya ya Goryanah
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.