Habari Mhariri,
Nikiwa na afya njema kabisa na amani ya moyo, Napenda barua hii iwafikie viongozi wa klabu ya Simba maana kinachoendelea ndani ya uongozi matokeo yake ndio haya yanaonekana kwa kipindi cha misimu hii mitatu,
Ikumbukwe Simba kipindi cha Barbara Gonzalez, tuliiona simba yenye ushindani na yenye mafanikio makubwa kana kwamba kumfunga mtu kama Al Ahly pale kwa Mkapa ikawa ni jambo la kawaida, mpaka hatua ya kuongoza kundi mbele ya bingwa wa kihistoria wa michuano ya mabingwa Afrika na kipekee ndio simba iliopofikia hatua za kutaka kufika mpaka nusu fainali kwa kumpiga Kaizer Chief ilihali mechi iliisha kwa idadi ya magoli isiokua rafiki kwa simba.
Unadhani kumfukuza Kocha Robertinho ilikuwa suluhisho? mbona amekuja bingwa wa shirikisho bado mambo ni yale yale? Hii dhahiri huonyesha udhaifu katika uongozi wa Simba. Katika ukweli pasemwe ukweli kama Yanga wataendelea hivi misimu miwili au mitatu basi ni dhahiri nusu fainali na mpaka fainali wanaingia katika ligi ya mabingwa Afrika maana wamethubutu.
Yanga ni timu yanye uongozi thabiti kupitia kwa Hersi Saidi na nikiri wazi kuwa anatakiwa kuigwa kwani timu ya soka ni uongozi na sio wachezaji
Mfano mzuri klabu ya Simba ilikua na mtu kama Augustine okrah, Jonas Mkude, Baleke Jean pamoja na Phiri Moses, hawa wote walikua wachezaji ambao kabla ya uongozi kupinda pinda wanafanya vizuri, ila sasa baada yake wakaonekana wabovu na kutemwa na ajabu walipo wanakiwasha vibaya mnooo.
Wekundu wa msimbazi wana watu ambao kama wakienda timu kama Azam au hata Yanga lazima tutashangaa, lakini viongozi wamebaki kaa na kumpangia kocha wale vijana ambao damu bado changa wapo jukwaani,
Mwisho niseme ikiendelea hivi hivi hata aje Messi au Ronaldo simba haiwezi kua imara kwani timu ni uongozi ndio wachezaji wafuate,
Katika Utekelezaji wa majukumu
Mohamedi Abdala Mohamedi
Mwanafunzi UDSM
SOMA ZAIDI BARUA NYINGINE HAPA



