Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Barua Nzito Kwa Simba Ili Iwe Imara Wawajibike Viongozi
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Barua Nzito Kwa Simba Ili Iwe Imara Wawajibike Viongozi

    MhaririBy MhaririApril 12, 2024Updated:April 13, 202410 Comments2 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Viongozi wa klabu ya Simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Habari Mhariri, 

    Nikiwa na afya njema kabisa na amani ya moyo, Napenda barua hii iwafikie viongozi wa klabu ya Simba maana kinachoendelea ndani ya uongozi matokeo yake ndio haya yanaonekana kwa kipindi cha misimu hii mitatu,

    Ikumbukwe Simba kipindi cha Barbara Gonzalez, tuliiona simba yenye ushindani na yenye mafanikio makubwa kana kwamba kumfunga mtu kama Al Ahly pale kwa Mkapa ikawa ni jambo la kawaida, mpaka hatua ya kuongoza kundi mbele ya bingwa wa kihistoria wa michuano ya mabingwa Afrika na kipekee ndio simba iliopofikia hatua za kutaka kufika mpaka nusu fainali kwa kumpiga Kaizer Chief ilihali mechi iliisha kwa idadi ya magoli isiokua rafiki kwa simba.

    Unadhani kumfukuza Kocha Robertinho ilikuwa suluhisho? mbona amekuja bingwa  wa shirikisho bado mambo ni yale yale?  Hii dhahiri huonyesha udhaifu katika uongozi wa Simba. Katika ukweli pasemwe ukweli kama Yanga wataendelea hivi misimu miwili au mitatu basi ni dhahiri nusu fainali na mpaka fainali wanaingia katika ligi ya mabingwa Afrika maana wamethubutu.

    Yanga ni timu yanye uongozi thabiti kupitia kwa Hersi Saidi na nikiri wazi kuwa anatakiwa kuigwa kwani timu ya soka ni uongozi na sio wachezaji

    Mfano  mzuri klabu ya Simba ilikua na mtu kama Augustine okrah, Jonas Mkude, Baleke Jean pamoja na Phiri Moses, hawa wote walikua wachezaji ambao kabla ya uongozi kupinda pinda wanafanya vizuri, ila sasa baada yake wakaonekana wabovu na kutemwa na ajabu walipo wanakiwasha vibaya mnooo.

    Wekundu wa msimbazi wana watu ambao kama wakienda timu kama Azam au hata Yanga lazima tutashangaa, lakini viongozi wamebaki kaa na kumpangia kocha wale vijana ambao damu bado changa wapo jukwaani,

    Mwisho niseme ikiendelea hivi hivi hata aje Messi au Ronaldo simba haiwezi kua imara kwani timu ni uongozi ndio wachezaji wafuate, 

    Katika Utekelezaji wa majukumu 

    Mohamedi Abdala Mohamedi 

    Mwanafunzi UDSM

    SOMA ZAIDI BARUA NYINGINE HAPA 

     

    simba sc simba sc leo

    10 Comments

    1. Mwita isack on April 12, 2024 1:34 pm

      Mi naona viongozi wajiuzuru wote mana hawajui kuleta maendeleo ya kimpira zaidi ya kujinufaisha wamekalia majungu tu na propaganda

      Reply
    2. Humphrey Starford on April 12, 2024 1:43 pm

      Hakuna viongozi Simba na ndio sababu hata muwekezaji wetu anakata tamaa, viongozi wengi wa Simba wapo kimipigo na wapo kwa maslahi yao binafsi! Tunaomba liangaliwe hili.

      Reply
    3. Ally Mwamlongo on April 12, 2024 3:13 pm

      Ukweli ni kwamba tatizo la Simba halijawahi kuwa kocha hata kidogo bali viongozi. Kwa vikosi vinavyoyoka katika kila mechi ni wazi kuwa kocha ana shinikizo la nani achezee na nani asicheze, sio bure kila kukicha kikosi ni kile kile huku vijana wadogo wanaosajiliwa wanaendelea kukaa bench na wengine jukwaani. Uongozi uwajibike

      Reply
    4. ezekia Chota on April 12, 2024 4:11 pm

      Hap Simba wamtoe matora ndo anaharbu timu mtakuja kunikumbuk

      Reply
    5. Erasto ndulan on April 12, 2024 11:17 pm

      Viongozi waachie ngazi kwakweli inatuumiza sanakuona wachezaji wazuri wanaondika watuletea siasa kwenye Moira wakati mambo yapo hadharani nitoshe kusema viongozi hatuwataki

      Reply
    6. Mzuzu n gwimo on April 13, 2024 8:29 am

      Nakama Simba Kuna sehemu walimkosea mgunda wakamuombe msamaha kama timu aliifundisha akiwa Hana sub natimu ikafanya vizuri harafu hao viongozi wakaona hafai wakaanza kutafuta kocho ambae anasaini Hela ndefu kumbe yake kidogo hii inafikirisha sana ndo maana walimtoa baleke na kumleta Fred wakamtoa phili na kumleta jobe kifupi ipo siku watatukuta pale ofisini tumewasubili tuone wataingiaje ofisini

      Reply
    7. Sabrah Hollylight on April 13, 2024 9:39 am

      N wazi kabisaa viongoz wapo kimaslah Nd màan hata hawaonyesh kushtushwa na MATOKEO màan washaeka Chao mfukon tunaoumia n Sisi…..Viongoz hatuwatak tang mmeingia hamn maendleo yyte nmefanya sio kusajil Wala nn ishort hakun mlichofanya n zerooo sas tumechooka token hapo waje watu weny uchungu wa kuipeleka team mbal na sio siasa

      Reply
    8. Pingback: Itawachukua Muda Mrefu Sana Yanga Kumpata Golikipa Mwingine - Kijiweni

    9. mussa Charles mungwila on April 13, 2024 3:51 pm

      yani wanatuumiza sana mbona kama timu hela inayo alafu wanafanya sajili za bei rahisi mana ukitaka kizurii lazima ugharamikie jaman uongozi wa simba mnatuumiza sana mashabiki

      Reply
    10. Ally Mussa on April 13, 2024 6:43 pm

      Siwezi sema kama kuna upigaji kwa kuwa sina uthibitisho wa ilo ila naweza sema kuna jambo ambalo si jema linaendelea ndani ya uongozi na si kosa lao kuwa nalo ndani ya uongozi nasi kulitoa nje kwani ndiyo uongozi ulivyo si kila jambo litatoka nje, kuna changamoto zingine zinatafutia suluhu ndani kwa ndani na changamoto kwenye jambo lolote ni kawaida sana ila mnaliondoa vipi ilo ndiyo jambo la msingi.

      Kwa upande wangu nawaombea nguvu na busara viongozi wa SIMBA katika utendaji wao wa kazi na kuwa watulivu kwa kutokata tamaa au kusongwa na lawama zinazoendelea.

      Kocha la Mpira,
      Mwl. Ally Mussa
      Ruangwa-Lindi

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.