Kwa heshima na taadhima nakuandikia barua mwamuzi Ahmed Arajiga,
Natumai barua hii inakukuta wewe na afya njema na ukiwa na ari kubwa zaidi kuelekea mchezo mkubwa wenye hisia kubwa zaidi miongoni mwa mashabiki unaozikutnisha klabu kubwa na kongwe Tanzania. Ningependa kueleza shukrani zangu kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kukuamini na kupewa filimbi ya kuuhezesha mchezo huu.
Kama shabiki wa soka na mwanamichezo kutoka Kijiweni, tunatambua jukumu kubwa ulilonalo katika kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki na uadilifu lakini pia natambua pia kwamba kazi yako ni ngumu na mara nyingine inaweza kuwa changamoto kubwa.
Napenda kukusihi utumie uzoefu wako na hekima katika kusimamia mchezo huu. Tunakutia moyo kufanya maamuzi kwa kufuata sheria za mchezo bila upendeleo au kuweka taswira mbaya yoyote ile kwa wapenzi wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla ambao watakua wanaufuatilia mchezo huu. Tunaamini utaweza kusimamia mchezo kwa haki na kuepuka migogoro au utata wowote.
Sisi kama Kijiweni tunatambua kwamba jukumu lako ni muhimu sana katika kuhakikisha mchezo unamalizika kwa amani na furaha kwa pande zote mbili za mashabiki yaaani mashabiki wa Yanga lakini pia mashabiki wa Simba. Kwa hivyo, tunakuomba ufanye kazi yako kwa umakini na ustadi ili kutuletea matokeo yanayostahili.
Tunakutakia mafanikio katika mchezo wako na tunaamini kuwa utakua mchezo mzuri na wenye kuvutia zaidi kwa upande wako wa maamuzi lakini pia kwa mbinu za makocha pamoja na utekelezaji wa mbinu hizo na wachezaji kwa ujumla wao n ani wazi kuwa tnasubiri kuona mchezo mzuri na wa kuvutia.
Asante kwa kujitoa kwako na kwa huduma yako katika mchezo wa soka.
Kwa heshima kubwa,
Mhariri
SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga



