Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Barua Kwako Mwamuzi Arajiga Kuelekea Yanga vs Simba
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Barua Kwako Mwamuzi Arajiga Kuelekea Yanga vs Simba

    MhaririBy MhaririApril 19, 2024Updated:April 20, 202424 Comments2 Mins Read9K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Barua kwa Arajiga
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kwa heshima na taadhima nakuandikia barua mwamuzi Ahmed Arajiga,

    Natumai barua hii inakukuta wewe na afya njema na ukiwa na ari kubwa zaidi kuelekea mchezo mkubwa wenye hisia kubwa zaidi miongoni mwa mashabiki unaozikutnisha klabu kubwa na kongwe Tanzania. Ningependa kueleza shukrani zangu kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kukuamini na kupewa filimbi ya kuuhezesha mchezo huu.

    Kama shabiki wa soka na mwanamichezo kutoka Kijiweni, tunatambua jukumu kubwa ulilonalo katika kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki na uadilifu lakini pia natambua pia kwamba kazi yako ni ngumu na mara nyingine inaweza kuwa changamoto kubwa.

    Napenda kukusihi utumie uzoefu wako na hekima katika kusimamia mchezo huu. Tunakutia moyo kufanya maamuzi kwa kufuata sheria za mchezo bila upendeleo au kuweka taswira mbaya yoyote ile kwa wapenzi wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla ambao watakua wanaufuatilia mchezo huu. Tunaamini utaweza kusimamia mchezo kwa haki na kuepuka migogoro au utata wowote.

    Sisi kama Kijiweni tunatambua kwamba jukumu lako ni muhimu sana katika kuhakikisha mchezo unamalizika kwa amani na furaha kwa pande zote mbili za mashabiki yaaani mashabiki wa Yanga lakini pia mashabiki wa Simba. Kwa hivyo, tunakuomba ufanye kazi yako kwa umakini na ustadi ili kutuletea matokeo yanayostahili.

    Tunakutakia mafanikio katika mchezo wako na tunaamini kuwa utakua mchezo mzuri na wenye kuvutia zaidi kwa upande wako wa maamuzi lakini pia kwa mbinu za makocha pamoja na utekelezaji wa mbinu hizo na wachezaji kwa ujumla wao n ani wazi kuwa tnasubiri kuona mchezo mzuri na wa kuvutia.

    Asante kwa kujitoa kwako na kwa huduma yako katika mchezo wa soka.

    Kwa heshima kubwa,

    Mhariri

    SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga

     

    live simba vs yanga mwamuzi arajiga simba leo YANGA LEO

    24 Comments

    1. Masalu jr on April 19, 2024 1:00 pm

      Mwamba na nusu ana uwezo wa kuihandle dabi kwa uzuri kabisaa

      Reply
    2. Taisoni Chijoja on April 19, 2024 1:09 pm

      Kikubwa anatakiwa ajiamini na maamuzi anayo chukua ila asifuate mkumbo wa kele za mashabiki ataiharibu daby

      Reply
    3. Fadhael mboi on April 19, 2024 1:10 pm

      Tunakuamini katika kazi yako, tuaminishe zaidi ya tunachoamini

      Reply
    4. Adelick on April 19, 2024 1:23 pm

      Avoid self feelings to handle the game

      Reply
    5. Tajiri ABAS on April 19, 2024 1:29 pm

      Nimuombe mwamzi asiwe Kama yule aliyeamua mechi ya yanga na mamelod aamuwe mchezo kwa haki na azingatie Sheria zote 17 bila upendeleo.

      Reply
    6. P boy on April 19, 2024 1:32 pm

      Akapambane tu this is life

      Reply
    7. Franaely Issangya on April 19, 2024 1:34 pm

      Tunamwombea aweze kutafsiri vizuri sheria 17 pasipo kuibeba timu yeyote katika mchezo wa kesho.

      Reply
    8. John mussa on April 19, 2024 1:35 pm

      Tuna amini arajiga ata handle mchezo vizuri sana

      Reply
    9. Kevin Mbeikya on April 19, 2024 1:35 pm

      Pressure ni kubwa sana kuanzia kwa viongozi hadi wachezaji.
      Mwamuzi anabid kuhandle game vzr kulingana na ujuzi wake sio mapenzi binafsi.

      Reply
    10. Mr unknown on April 19, 2024 1:37 pm

      Mwamuzi akapambane ya ela yote asionee wala kuzulumu haki iwe sawa ili aepuke maneno ya watu kwa kaz yake

      Reply
    11. John mussa on April 19, 2024 1:38 pm

      Tuna amini arajiga ata handle mchezo vizuri

      Reply
    12. Timoth komba on April 19, 2024 1:43 pm

      apunguze kujiamin kila jambo linahitaj nidhamu sababu yeye ni binadamu kwahiyo inahitaj maamuz magumu

      Reply
    13. Kessie_kestain on April 19, 2024 1:49 pm

      Kwa yanga hii kesho ata refa awe mangungu ushindi lazima
      @daima mbele 💛💚

      Reply
    14. [email protected] on April 19, 2024 2:11 pm

      🤛🤛🤛🤛🤛🤛🤛🤛 all the best

      Reply
    15. beatusi ulalo on April 19, 2024 2:31 pm

      mimi nafikiri huyu refa yupo vinzuri kwani. kwanza ni mzoefu wa kuchezesha mechi kubwa hakika yangu ni mcheki mpira wa viwango vya juu kasimamie sheria na kanuni za mpira na mungu akutangurie

      Reply
    16. Georgendoma71 on April 19, 2024 4:33 pm

      Apambane Tu mechi za Simba na yanga uwavinavitu vingi sana

      Reply
    17. Rance on April 19, 2024 5:32 pm

      Akazingatie sheria vizuri wala pessure ya wachezaji isi mtoe kweny mchezo mana izi game za derby wachezaj wanakua na pressure mpaka wanamtoa mwamuzi mchezoni

      Reply
    18. Lenkai junior on April 19, 2024 6:36 pm

      refa bora mwenye bej ya Fifa huna baya ukifa huozi na ukioza hunuki ila usifanye vise-versa kuwa ukweli ni hayo tu

      Reply
    19. Michael on April 19, 2024 7:23 pm

      Yeye ni refa mzuri sana
      Lakini kama ilivyo kwa waamuzi wetu hapa tz! Mahaba kwa timu zao hufanya wakose aibu na kuvuruga ladha ya mechi, ajitahidi tu kuwa thabiti…….. Hana baya arajiga

      Reply
    20. Chard on April 19, 2024 7:25 pm

      Yeye ni refa mzuri sana
      Lakini kama ilivyo kwa waamuzi wetu hapa tz! Mahaba kwa timu zao hufanya wakose aibu na kuvuruga ladha ya mechi, ajitahidi tu kuwa thabiti…….. Hana baya Arajiga

      ILA IKIWEZEKANA AIBEBE TU SIMBA NISIWE MNAFIKI😂😂😂😂

      Reply
    21. Kanuth on April 19, 2024 8:08 pm

      Tunamkubali kazi kwake sasa

      Reply
    22. plan B on April 19, 2024 9:47 pm

      uyo anajua

      Reply
    23. Pingback: Tabiri Sasa Matokeo Ya Dabi Ya Kariakoo Hapa Kijiweni - Kijiweni

    24. Kingboyone on April 20, 2024 11:35 am

      Ushindi upo kwa Mnyama

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.