Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Ahmed Ally Uko Sahihi Ila Wakati Uliotoa Kauli Yako Sio Sahihi
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Ahmed Ally Uko Sahihi Ila Wakati Uliotoa Kauli Yako Sio Sahihi

    MhaririBy MhaririFebruary 26, 20241 Comment2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Kauli za Ahmed ally
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Tarehe 23 ya mwezi wa 7 mwaka 2018 majira ya saa 2 za aubuhi yaani mapema kabisa mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji Mo kupitia mtandao wa X ambao kipindi hiko ulikua ukifahamika kama Twitter aliweza kuchapisha ujumbe wake ambao kwa namna moja au nyingine ulichukuliwa kitofauti na mashabiki wa soka wa Tanzania kumbuka ni miaka  sasa imepita tangu andiko hilo.

    Aliandika “Tunahitaji Yanga imara ambayo inaweza kushindana na Simba.Tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu bora ya Taifa Stars.Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulie na waungane upya” baada ya miaka hiyo ni wazi tunawaona Yanga wakifuzu hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Afrika.

    Naweza kusema kauli aliyoitoa Meneja Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba ni sahihi kabisa lakini ameshindwa kujua ni wakati gani wa kuitoa kauli hiyo kama ulikua hujui tu nimnukuu kile ambacho ametoa na anasema kufuzu kwa Yanga katika hatua ya robo fainali anaepaswa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba Mohammed Dewji na wa pili Club ya Simba.

    “Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika, wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua”

    “Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri, kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi, huu ndio ukweli ambao utadumu milele”

    Kila mmoja atakua na lake na kuzungumza vile ambavyo anajiskia lakini alichosema Ahmed ni sawa kabisa kwani kupitia kauli ya Mo Dewji miaka 6 baadae tumekuja kuiona yanga ambayo imekua bora sana na ikiwa na wachezaji ambao ni hatari lakini kubwa zaidi ni kuondoka katika kipindi kigumu ambacho walikua wakikipitia na kupata mfadhili ambaye ameipeleka mbali klabu hiyo.

    SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Wa Simba Kwenda Kwa Yanga

    ahmed ally mo dewji Simba

    1 Comment

    1. Pingback: Yanga Sc Kutinga Robo Fainali Imekuwa Nongwa? - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 15, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya tatu Mke alipoisoma ile karatasi aligeuza macho kumtazama Mume…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.