Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    In the name of LOVE – 09

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » In the name of LOVE – 11
    Hadithi

    In the name of LOVE – 11

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoSeptember 29, 2025Updated:September 29, 20251 Comment10 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia sehemu ya Kumi ya In the name of LOVE

    Nilimvuta na kumkumbatia huku nikikisikia kilio chake kwa karibu zaidi.  Nililengwa na Mchozi lakini sikutaka utoke, niliuzuia huku nikimbembeleza 

    “Pole Mpenzi wangu, ukiwa katika Hali ya huzuni unanifanya naumia.”  Nilisema kwa sauti ya utaratibu iliyojaa mapenzi, Zaylisa akajitoa mwilini  Kisha akafuta chozi lake kwa kutumia mikono yake, akanitazama usoni  akaniambia 

    “Samahani sana Jacob”  

    “Hata usijali Mpenzi, nimekuelewa” Endelea

    SEHEMU YA KUMI NA MOJA

    Zilipita siku mbili, hatimaye wiki nzima. Hakuna aliyejua Clara alikua wapi  na kwanini simu yake ilikua haipatikani, kibaya zaidi hata Matilda hakua na  mawasiliano ya Watu wa karibu wa Clara. 

    Tulisubiria Kila siku huwenda Clara angerejea lakini siku zilikua zinaenda  mithiri ya Mshale wa saa. Kila dakika iliyoondoka iliondoka na tumaini,  iliongeza wasiwasi mkubwa. 

    Tabia ya Zaylisa kuondoka na kutopatikana iliendelea, hata nilipoongea nae  alinipa sababu dhaifu ambazo sikuzichuja ila nilimwamini sababu ya  Mapenzi yangu kwake. 

    Siku Moja, alipoondoka asubuhi alisema anaenda kwao. Nilijaribu  kumfuatilia maana alikua hataki Mimi niende kwao kumwona Baba yake  Mgonjwa, japo nilichagua kumwamini lakini Kuna hisia Moja iliniambia  napaswa kumfwatilia hata kama namwamini kiasi gani, kilichonifanya  nipate wazo la kumfwatilia ni kitendo chake Cha kutopatikana kwenye simu  anapoondoka nyumbani. 

    Yeye aliondoka kwa Bajaji, nyuma yake nilimfwatilia kwa kutumia Pikipiki  ya kukodi, nilimwambia dereva aende pole pole nyuma ya Bajaji. Bajaji  ilipofika Mwenge alishuka kisha akaelekea kwenye gari Moja iliyopanda  iliyokua imesimama kando ya Barabara 

    Kisha baada ya dakika kama kumi hivi gari iliondoka na kuelekea barabara  ya Ubungo. Baada ya mwendo kiasi gari ilikunja kushoto kama inaenda  Sinza halafu ikasimama mbele ya Hoteli Moja, halafu Zaylisa alishuka kisha  upande wa pili wa dereva alishuka Mwanaume mmoja aliyevalia ‘Superfly’  nyekundu. 

    Mwanaume huyo hakunipa nafasi ya kumwona sura yake maana muda  wote alisimama akiwa amenipa mgongo, Mwanaume huyo alikua ni mfupi,  ana kitambi pia. 

    Walizungumza hapo kwa dakika Moja Kisha waliongozana wakaelekea  ndani ya Hoteli hiyo, sikujua alikua ni Nani na kwanini walienda hapo  wakati Zaylisa aliniaga anaenda kumwangalia Baba yake.  

    Nilipata shahuku kubwa sana ya kutaka kujua walikua hapo kwa ajili gani,  basi nilimlipa Bodaboda pesa yake halafu taratibu nikaelekea ndani ya 

    Hoteli hiyo, niliangaza huku na kule sikuwaona. Hapakua na dalili ya  kuwaona japo nilikua na uhakika wapo ndani ya Hoteli hiyo 

    Nilikua nimesimama nje eneo la Bustani, palikua kimya sana. Iliniuma  sana kuona Zaylisa alikua anasema uwongo, nusura chozi linidondoke  lakini nilijikaza tu. Niliondoka pale mikono ikiwa nyuma, hasira ilinipanda. 

    Nilirudi nyumbani, nilihisi bugudha kubwa ndani ya nafsi yangu. Nilijiuliza  mengi yasiyo na Majibu, sikujua yule Mwanaume ni Nani na Wana  uhusiano gani, nilipitiliza Hadi sebleni nikiwa na hasira nikamkuta Matilda  akiwa anaandaa chakula Mezani  

    Aliponiona alihisi kua sipo sawa, alinitazama kwa dakika kadhaa Kisha  aliniuliza 

    “Upo sawa?” nilimtazama kidogo Kisha niliondoka zangu pale sebleni  nikaelekea zangu chumbani.  

    Nilipofika chumbani nilichukua dawa zangu nilizokua nameza ili kutuliza  maumivu ya kinywa nikameza, kichwa kilikua kinaniuma sana. Moyo  Wangu ulivunjika kwa ajili ya Zaylisa, chozi lilinibubujika tu. 

    Nilihisi nahitaji kumjua zaidi Zaylisa, nilihisi hakuwa yule niliyempenda  lakini nilijiuliza alipatwa na Nini kwa Kipindi kifupi au ndoa yake  imembadilisha? Lakini Kila nilipoyakumbuka macho yake yalinianbia kua  alikua akinipenda sana. 

    Niligonga kichwa changu ukutani huku nikitafuta majibu, mara Mlango  uligongwa. Nilifuta chozi langu, nilienda taratibu kuufungua, Matilda  alikua amesimama Mlangoni kama Mlinzi wa zamu, nilipomwona nilihisi  siye niliyemtarajia 

    Sikua na chochote Cha kuzungumza na Matilda, nilivuta mlango ili  niufunge lakini Matilda aliniambia 

    “Nimepokea ujumbe kutoka kwa Dada Clara” angalau hii ilikua taarifa  niliyoisubiria, wazo la kuufunga mlango lilikoma. Nikamtazama Matilda,  nilihitaji kujua ujumbe huo ulisemaje 

    “Unasema umepokea ujumbe kutoka kwa Clara?” 

    “Ndiyo” 

    Hamu na shahuku iliniingia kwa Kasi sana, sikuficha kua nilihitaji kujua  Clara yupo wapi 

    “Amesema yupo wapi?”

    “Hapana, amesema yupo salama wala tusihangaike atarudi akili yake ikiwa  sawa” alisema Matilda, angalau nilishusha pumzi zangu. Nilijua tu kwa kile  kilichotokea kati yake na Zaylisa ndicho kilichomfanya ahitaji kutuliza akili  yake. Sura yangu ilipoa 

    “Basi sawa kama atakutafuta tena uniambie” niliongea kwa sauti ya Upole  tofauti na mwanzo nilivyokua na hasira, niliufungua mlango kwa utaratibu  Kisha nilitembea kidogo na Kuketi kwenye Kitanda. Suala la Clara nililiona  lilikua limeshaeleweka ila sasa kuhusu Zaylisa ilikua kizungumkuti 

    “Kuna Siri gani hapa, yule Mwanaume ni Nani au Ndiyo yule  anayempigiaga simu? Mh, Ndiyo kusema ndiye MZEE WA MIPANGO’?  Sasa kama ni yeye Kuna mpango gani?” nilijiuliza maswali mengi bila  kupata majibu ya maswali yangu. Mwisho nilipata wazo la kwenda  nyumbani kwao Zaylisa 

    Nilitabasamu baada ya kupata wazo hili maana sikua na njia nyingine ya  kujua ni kwanini Zaylisa anapoondoka anakua hapatikani kwenye simu,  lakini pia nilipata Mashaka kua huwenda haendi nyumbani kwa Baba yake  isipokua ni kwa yule Mwanaume mfupi nisiyemtambua. 

    Nilijifuta jasho Kisha nilielekea mlangoni nikaufungua na kuondoka, safari  hii nilimuaga Matilda nikamwambia 

    “Natoka mara Moja, kama Zaylisa atarudi utamwambia kua sipo mbali”  nilisema, kwa heshima Matilda aliitikia bila kuuliza chochote japo mdomo  wake ulikua unataka kucheza lakini sikumpa nafasi nilimwacha kama  samaki mwenye Maji mengi Mdomoni.  

    Nilitumia Bodaboda kuelekea Nyumbani kwa Wazazi wake, nilikua  napafahamu ila Wazazi wake walikua hawanifahamu. Nilipofika nje ya  nyumba Yao nilimlipa Bodaboda pesa yake Kisha nilisimama kwa sekunde  kadhaa nikiiangalia nyumba ile, ilikua ni nyumba nzuri sana inayoonesha  wakaazi walikua ni Watu wenye uwezo kifedha. 

    Huo ndio uhalisia, Wazazi wa Zaylisa walikua na uwezo kifedha, nyumba  ilikua imetulia sana. Taratibu nilisogea na kubisha hodi getini, moyoni  nilijiambia kua Liwalo na liwe nahitaji kufahamu mengi yaliyo gizani. 

    Nilisubiria pale kwa dakika Moja huku jua likiwa linanipiga. Mara alikuja  Mdada mmoja mwenye umri sawa na Matilda, alipofika alinikaribisha 

    “Sijui nikusaidie nini Kaka?” aliniuliza, nilitabasamu kidogo Kisha  nikamwambia

    “Nimekuja kumjulia Hali Mzee Paulo” nilisema, Baba yake Zaylisa alikua  akiitwa Mzee Paulo, alikuwa ni Bosi mstaafu wa mfuko wa akiba wa Taifa.  Alikua ni Mzee mwenye hadhi na Maisha mazuri, yule Mdada alionesha  kushangaa kanakwamba jina Hilo lilikua ngeni au hakujua kuhusu kuumwa  kwa Mzee Paulo. 

    “Usijali Mimi ni rafiki wa Binti yake Zaylisa” nilijitambulisha, akazidi  kushangaa Kisha akaniuliza  

    “Umetokea wapi?” aliniuliza huku akinitazama sana 

    “Mimi ninaishi Mbezi, usiwe na wasiwasi nataka kujua Hali yake tu”  nilisema, yule Mdada akacheka kwa mtindo wa kuguna halafu akaniambia 

    “Unanishangaza sana, Mbona simfahamu huyo Mzee?” aliuliza. Sura yake  ilikua ukimaanisha alichokisema na haikua utani.  

    “Humfahamu mwenye nyumba? Ni maajabu haya” nilisema huku  nikicheka, nilikua na uhakika wala sikukosea nyumba. Mara nyuma yangu  lilikuja gari ndogo nyekundu aina ya Alteza, Mwanaume mmoja mwenye  asili ya kiarabu alitokeza kichwa chake akauliza 

    “Kuna nini hapo Sauda?” alikua akimtazama yule Mdada ambaye kwa  hakika alikua ni Msichana wa kazi.  

    “Samahani Bosi, huyu Kaka anamuuliza Mzee Paulo. Mimi simfahamu  lakini anadai anaishi humu” alisema yule Mdada, basi yule Muarabu  akatabasamu tu Kisha akamwambia yule Mdada arudi ndani. 

    Kisha yule Muarabu akashuka kwenye gari akaja karibu yangu. 

    “Wewe ni Mtu wa pili unakuja kuulizia hapa baada ya Miaka minne kupita,  alikuja Mwanamke anaitwa Clara kama sikosei alimuulizia Zaylisa.  Nikamwambia kua Zaylisa haishi hapa, bahati nzuri nilikua na mawasiliano  ya Zay nikampatia. Hata hivyo huyo Mzee alishafariki Miaka minne  iliyopita baada ya kufilisika, nikainunua hii nyumba” alisema kwa kujiamini  sana 

    “Unasemaje?” nilimuuliza kama Mtu aliyechanganyikiwa, yote niliyoyasikia  yalikua yakinichanganya sana.  

    “Mzee Paulo alishafariki muda sana, Binti yake alishaolewa kitambo na  Mafia mmoja hivi wa hapa Mjini, ulikua wapi Miaka yote hiyo usijue kua  Mzee Paulo alishafariki? Hata Mke wake nasikia ni Mgonjwa sana yupo  Kilimanjaro” swali lake lilikua sawa na kumwaga chumvi baharini, tayari 

    nilikua na maswali chungu mzima yaliyohitaji majibu lakini yeye alinipa  mzigo mwingine mzito. 

    “Mzee Paulo amefariki?” niliuliza huku jasho likinitoka, nilihisi kukaribia  kuujua ukweli Fulani mchungu sana.  

    “Muda sana. Wewe ni Nani yake?”  

    “Aah Usijali, Asante” nilisema Kisha niligeuka niondoke, ile napiga hatua  nilihisi kizungu-zungu nikapepesuka nusura nianguke, yule Muarabu  akataka kunisaidia lakini nilimpa ishara kua nitakua salama tu.  

    Niliondoka taratibu huku nikiwa na maswali mengi. 

    Nilitafuta Sehemu nikakaa ili nijiulize yote hata kama nitakosa majibu ya  maswali yangu. Swali la kwanza nilijiuliza kama Mzee Paulo amefariki, Je  Zaylisa alikua anaenda kumuuguza Baba yake gani? Kama Ndiyo hivyo  maana yake alikua akiniongopea, sasa kama alikua akisema uwongo alikua  akienda kwa yule Mzee Wa Mipango. 

    “Imepita Miaka Minne tangu kifo Cha Mzee Paulo, Miaka mitano baada ya  Kifo Cha Melisa, sasa kwanini sikumbuki chochote kile. Mbona ile ajali  ilitokea siku ya harusi ya Zaylisa na wala hakikua kipindi kirefu nilichokaa  Hospitalini?” nilijiuliza, niliishia kutokwa na Machozi, sikua na Majibu ya  maswali yangu. 

    Nilifuta chozi langu, nikapata wazo la kwenda kule Mgahawani ili  nizungumze tena na yule Meneja wa Mgahawa, niliona ana mengi ya  kunieleza. Nilitumia tena usafiri wa pikipiki kuelekea Mgahawani,  nilipofika nilisimama kidogo huku nikihema 

    “Hapa ndipo mahali pekee palipojaa ukweli kuhusu Mimi” nilijisemea,  Kisha pole pole nilitembea Hadi ofisini kwa Meneja. Mlangoni nilikutana  na kufuri kubwa, nilisimama kidogo nilifikiria nifanyaje mara alipita  Mhudumu mmoja wa kike 

    Aliponiona alikuja Hadi niliposimama Kisha alinisamilia na kuniuliza “Una shida gani?”  

    “Nilihitaji kuonana na Meneja lakini kwa bahati mbaya nimekuta  pamefungwa, ametoka muda mrefu?” nilimuuliza.  

    “Alishaacha kazi mbona tokea juzi, Bosi anatafuta Meneja mpya ndio  maana ofisi imefungwa” alisema Kisha aliondoka zake akionekana ni  mwenye haraka sana, aliniacha na maswali, niliona tumaini Hilo lilikua  hafifu sana. Kama ameacha kazi basi kumpata itakua shida sana

    “Dada Samahani” nilimsimamisha kabla hajafika mbali, Kisha nilimfuata  na kumuuliza 

    “Naweza kupata mawasiliano yake?”  

    “Sina hakika sababu inasemekana ameondoka Nchini, familia yake ipo  Malawi. Sijui kama unaweza ukampata” alisema Kisha aliondoka,  nilisimama huku nikijiuliza mengi yaliyopita kichwani kwangu. Mshumaa  nilioutegemea ulikua umezimika ghafla, niliishiwa nguvu  

    Nikapata wazo jipya la kuelekea kule alikokua anaishi Sudi. Nilihitaji  kuelewa kuhusu Miaka mitano iliyopita maana nilihisi huwenda jambo Hilo  lilikua kweli japo sikua na kumbukumbu ya Miaka hiyo. Hadi kufikia hapo  nilihisi uwepo wa Siri fulani nisiyoifahamu 

    Niliondoka pale Mgahawani nikaanza safari fupi ya kuelekea Nyumbani  kwa Sudi, nilikatiza mitaa Hadi kufika huko. Jua lilikua Kali sana lakini  halikuzuia dhamira yangu ya kufika alipokua anaishi Sudi. 

    Nilipofika niligonga geti kama kawaida ili nifunguliwe, bahati nzuri alikuja  yule Mdada aliyenifungulia siku ile. Alinisalimia kwa Bashasha maana  alinikumbuka, nami nilionesha Upendo kwake 

    “Karibu tena Kaka” alisema akiwa anatabasamu.  

    “Asante sana Dada yangu, nimerudi tena” nilisema, akanitazama Kisha  akaguna na kuniambia 

    “Kuna jipya gani tena?” 

    “Aaah! Unajua Kuna mengi sana yanaumiza kichwa changu Dada yangu,  nimetafuta sana Majibu ya maswali yangu nimeona hapa ndipo mahali  pekee ninapoweza kupata majibu.” Nilisema. 

    “Sasa kaka yangu kama nilivyokwambia, Mimi ni mgeni hapa sijui mengi  kukuhusu. Hata hivyo Leo Baba mwenye nyumba yupo” Mwili ulisisimka  baada ya kusikia kua Baba mwenye nyumba yupo, angalau yeye angenipa  mwanga zaidi.  

    “Yupo wapi?”  

    “Ingia tu” Niliingia Hadi Uwani, nilimwona Baba mwenye nyumba akiwa  anatoka kwenye kile chumba ambacho Sudi alikua akiishi. Nilikua  nikimfahamu juu juu tu, basi haraka nilisogea kabla hata hajakifunga kile  chumba, nikamsalimia kwa heshima sana 

    “Marahaba” aliitikia akiniangalia kwa jicho la kutonikumbuka.

    “Ni Mimi Jacob Baba” nilisema. 

    “Jacob?” 

    “Ndiyo, rafiki yake Sudi” 

    “Ahaaa‼ Sasa wewe Kijana ulipotelea wapi, tulifanya jitihada za kukutafuta  lakini hatukukupata, ilikuaje ukamtelekeza Mdogo wako hapa?” alisema  yule Baba mwenye Nyumba, Kisha akamwambia yule Mdada atupatie viti tukae, ilionekana alikua na mengi ya kuniambia 

    Moyo Wangu na akili yangu vilikua tayari kusikia chochote kile hata kama  kitaniumiza kiasi gani lakini Ndiyo ukweli pekee niliouhitaji kuusikia ili  nifahamu mengi yaliyokua yakinitatiza.  

    Nilikua kimya huku moyo Wangu ukinidunda, viti vilipoletwa tuliketi  kando ya kile chumba Kisha yule Mzee alishusha pumzi zake akaniuliza 

    “Ulikua wapi Kijana?” 

    Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya KUMI NA MBILI

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love 

    hadithi za mapenzi mapenzi riwaya riwaya mpya stori za mapezni

    1 Comment

    1. Salma Ibrahim on September 29, 2025 7:10 pm

      🔥 aiseee hongera mtunzi

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 29, 2025

    In the name of LOVE – 11

    Ilipoishia sehemu ya Kumi ya In the name of LOVE Nilimvuta na kumkumbatia huku nikikisikia…

    In the name of LOVE – 10

    In the name of LOVE – 09

    In the name of LOVE – 08

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.