Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 07

    In the name of LOVE – 06

    In the name of LOVE – 05

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » In the name of LOVE – 07
    Hadithi

    In the name of LOVE – 07

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoSeptember 23, 2025Updated:September 23, 20251 Comment7 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia sehemu ya sita ya In the name of LOVE

    Mara mlango uligongwa, Zaylisa aliinuka Kisha alinitazama. Sote tulijiuliza  ni Nani aliyekua anaugonga mlango, Mimi nilinyanyuka na kuelekea  Mlangoni, nilipofungua nilikutana na sura ya Msichana wa kazi, alianza  kunitazama kwa jicho la Upole sana Kisha akaniambia

    “Dada anakuita” niligeuka kumwangalia Zaylisa, hakusema chochote ila  alinitazama kwa jicho la kuniambia kua nitakacho kiamua kitakua sawa  kwake. Nilishusha pumzi kidogo halafu nikamjibu 

    “Sawa, nakuja” sauti ya taratibu iliyojaa uzito ilinitoka. Yule Msichana  aliondoka zake, nilifunga mlango. Nikamwangalia tena Zaylisa, nilishusha  pumzi Kisha nikafungua tena mlango nikatoka kwa ajili ya kwenda  kuonana na Clara.  Endelea

    SEHEMU YA SABA

    Nilimkuta akiwa ameketi kwenye kochi, nilisimama kumtazama. Sikujua  nani ana hatia na Nani Hana hatia, ila nguvu ya Mapenzi iliniambia kua  Clara hakutaka niendelee kuishi hapo.  

    Taratibu nilisogea na Kuketi kando yake, mdomo Wangu ulikua mzito kama  umefungwa na gundi.  

    “Jacob” aliniita Clara. Nilimtazama bila kuitikia Kisha aliendelea kusema 

    “Kesho naenda Arusha, nampeleka Melisa kwa Shangazi yake.”  Nilimtazama kwa Upole, nikamjibu 

    “Sawa” nilitaka kunyanyuka lakini alisema 

    “Samahani kwa kilichotokea, sipendi ukwazike” nilimtazama nikamwambia 

    “Kama unaona ulikosea ni vema ukamwomba msamaha Zaylisa, hivi  Clara…ninalazimisha kuishi hapa?” nilimuuliza, nilimwona akidondosha  chozi 

    “Kama hutaki niishi hapa ninaweza kuondoka muda huu, kumbuka  sikukuomba Nije kuishi hapa isipokua ni wewe ndiye uliyetaka niishi hapa.  Au hutaki Zaylisa awe hapa?” Maswali yangu yalizidi kumfanya adondoshe  chozi zaidi, alifuta chozi lake kwa kutumia mikono yake, pua zake ,zilikua  zimeziba akavuta hewa kubwa Kisha akaniambia 

    “Kwenye hili Giza Kuna Siri Jacob, Siri ambayo siku ukiijua utajutia”  nilishtuka, maneno yake yalikua sawa na Mtu aliyerusha jiwe gizani 

    “Simchukii Zaylisa, wala sitaki uondoke hapa Jacob Ndiyo maana  nimekuomba Msamaha na nipo tayari kumwomba msamaha Mwanamke  wako” alisema, nilimwona ni Mtu aliyebeba mambo mengi kifuani na  hakua tayari kuyazungumza 

    “Siri gani unayoimaanisha?” nilimuuliza, aliishia kunitazama tu huku  mdomo wake ukitetemeka, hakua tayari kusema chochote. 

    “Clara, kama siyo ile ajali ningekua na Mdogo wangu Melisa. Mimi  sikufundishwa kuithamini pesa Bali utu, siku ukinichoka niambie  nitaondoka hapa, sawa? ” nilisema Kisha niliondoka pale taratibu, nyuma  yangu nilisikia kilio Cha chini chini, Nami chozi lilinilenga lakini sikutaka  kugeuka nyuma. 

    Nilipofika chumbani, Zaylisa alinikumbatia kwa hisia sana. Niliamua  kumwamini kwasababu ndiye Mtu niliyemfahamu zaidi, moyo Wangu  ulikua na amani sana nimwonapo Zaylisa mbele ya Macho yangu 

    “Nakupendaa” nilimwambia Zaylisa, Ndiyo….moyo Wangu ulifungwa kwa  ajili yake tu, yeye ndiye niliyempenda na Kumthamini.  

    Mchana, Zaylisa aliniambia kua anataka twende mahali. Nilijiuliza alihitaji  twende wapi, nilimuuliza 

    “Tunaenda wapi Mpenzi wangu?” 

    “Jiandae Mpenzi, utaona” Alisema, basi niliingia bafuni nikaoga vizuri  halafu nikajiandaa haraka. Kisha nilipomaliza nilikua tayari kwenda  aliposema yeye. Sikujua ni wapi 

    Tulipotoka chumbani tulikutana na Clara. Alikua akitutazama akiwa  amesimama kwenye korido, sura yake ilikua imejawa na huzuni iliyo gizani,  macho yake yalinitazama sana. Zaylisa akanishika mkono 

    “Twende” hakutaka kuzungumza na Clara, nyuso zao zilijaa nyufa  isiyoelezeka, sura ya Clara ilikua Ina huzuni isiyo mithirika lakini sura ya  Zaylisa ilikua imejawa na hasira na jeuri, nilielewa ni kwanini Kila mmoja  alikua na sura yake 

    Tulimpa mgongo Clara asijuwe tunaelekea wapi. Midomo yake ilitamani  kusema kitu lakini aliishia kututazama Hadi tulipo ishiria. Zaylisa alikua  tayari ameshaita gari ya kukodi kupitia mtandao, tuliingia ndani ya gari  

    nikiwa na maswali mengi kichwani, sikujua tulikua tunaenda wapi na  kufanya nini. 

    Safari ilianza taratibu kutoka kwenye jumba la kifahari la Clara, tulielekea  Mjini. Alinitembeza Sehemu mbali mbali, mwisho akanipeleka kwenye  Mgahawa mmoja ulio katikati ya Jiji 

    Aliagiza chakula, sikujua alipata wapi pesa za kufanya yote Yale. Nilikua  nimejawa na Mshangao tu lakini sikiliza chochote.  

    “Unajua Leo umenishangaza Zaylisa, sikutegemea ujue” nilisema  nilitabasamu, naye aliachia tabasamu

    “Sikupenda kilichotokea pale kwa Clara, nilihitaji utulivu zaidi ili kuweka  akili yangu sawa Jacob…..unajua Clara ana dharau sana” alisema Zaylisa,  nilimwambia 

    “Usijali, hata hivyo amejutia. Nakuamini sana Zay, kwani ilikuwaje  mkaingia kwenye Hali ile ya Kupigana?” alinitazama Kisha akaonesha  kutokupenda sana kuongelea suala lile 

    “Ahh‼ unajua Jacob, Mimi sipendi Mtu anayemdharau Mtu ninayempenda.  Yule alileta kejeli na dharau, nilichofanya ni kukulinda. Wewe unasema tu eti amejutia, hawezi yule ni kiburi sana….. Mpenzi…” akanishika mkononi  huku akiongea kwa huzuni 

    “Hata iweje siwezi kuachana na wewe, nakupenda sana Jacob. Nimekupa  Nusu ya Maisha yangu….Nisamehe kwa kitendo changu Cha kuolewa,  Wazazi walinishinikiza” alisema Zaylisa, Kila alichosema nilikiona kilikua  sawa 

    Chozi lilimdondoka, nilijihisi huzuni ndani yangu.  

    “Usijali Mpenzi kua na amani, kwakua upo hapa na Mimi basi hakuna  kitakacho tuweka mbali tena” nilisema pole pole, nikaangalia kama Kuna  Watu waliokua wakitutazama lakini niliona Kila Mtu alikua bize na mambo  Yao. 

    “Naomba niende bafuni Mpenzi”  

    “Sawa Mpenzi” Zaylisa aliniaga Kisha aliondoka huku akikitumia kitambaa  kufuta chozi lake. Nilimtazama Hadi alipozama, kiukweli nilikua najisikia  vibaya sana. Nilitamani ningekua na pesa ili nitafute mahali pa kuishi na  Zaylisa, sikupenda kuendelea kuishi nyumbani kwa Clara 

    Nilijiinamia, nikiwa hapo niliguswa begani. Nilipoinua macho nilikutana na  Mtu nisiyemfahamu lakini uso wake ulionesha kunifurahia na kuniheshimu  sana. Hakunipa hata muda wa kumtafakari, akasema 

    “Sikutemegea Kama ungepona kwenye ile ajali Bosi” nilishtuka, aliniita  Bosi. 

    “Umeniita Bosi?” 

    “Ndiyo, Mungu ni mwema sana. Ninafurahi kukuona ukiwa mzima”  alisema Kisha alinitazama kwa furaha sana, yeye alikua Ni Mwanaume  mrefu kiasi, Maji ya kunde  

    “Unanifahamu?” nilimuuliza, aliondoa utulivu na tabasamu akaketi kwenye  kiti alichokua ameketi Zaylisa.

    “Bosi ni Mimi Kitime, umepatwa na Nini usinifahamu?” alijieleza kwangu,  kiukweli sikumtambua na wala sikukumbuka hiyo heshima ilitokana na  Nini. 

    “Mbona sikufahamu ndugu yangu, utakua umenifananisha” nilimwambia  huku nikigeuza shingo kuangalia kama Zaylisa alikua akirejea ili nimuulize. 

    “Hapana siwezi kukufananisha Bosi Jacob, ni wewe.” Alisema, nilishtuka  zaidi alipotaja jina langu, alionekana kunifahamu lakini bahati mbaya sikua  na kumbukumbu hata Moja kuhusu yeye.  

    “Umelifahamu vipi jina langu ndugu yangu, Mimi sijawahi kua Bosi.  Sikufahamu, tafadhali sana ondoka hapa” nilisema, yule Mtu  aliyejitambulisha kama Kitime aliniangalia kwa Mshangao kama vile alikua  ameona mzimu. 

    “Kuna kitu hakipo sawa kwako Bosi” alisema Kisha aliondoka zake pale,  aliniacha nikishusha pumzi nzito sana Hadi kichwa kilianza kunigonga.  Mara Zaylisa alitokea, akanikuta nikiwa na mawazo lukuki, alipoketi  aliniuliza 

    “Unawaza nini baby, Bado unamfikiria Clara?” nilimeza funda la mate,  nikimtazama Zaylisa. 

    “Kuna kitu kinanichanganya Zay, Kuna Mtu amekuja hapa anaonesha  kunifahamu halafu ametaja jina langu pia ameniita Bosi. Nahisi Kama  Kuna Maisha siyakumbuki” nilisema, Zaylisa akaniuliza 

    “Ni Mtu gani huyo Jacob” 

    “Amejitambulisha kama Kitime, anaonekana kunijua lakini simfahamu”  nilisema huku kichwa kikiwa kinapata moto haswa 

    “Aaaah Baby, huwenda tu una wenge. Tule tuondoke” Zaylisa alisema huku  akionekana kutojali kuhusu nilichomwambia, pengine alifikiria baada ya  ajali akili yangu haijakaa sawa, nilijisikia vibaya japo sikutaka  kumwonesha Moja kwa moja. Nililiacha lile jambo lipite japo liliniumiza  kichwa sana 

    Tulipomaliza kula, Zay alilipia bili Kisha aliita gari ya kukodi tukarudi  nyumbani. Tuliikuta nyumba ikiwa kimya kama vile hapakua panaishi  Watu, tuliingia chumbani kwetu tukajipumzisha, kwakua tulikua  tumeshakula hivyo hatukutoka tena Hadi kesho yake. 

    Asubuhi mapema sana, Clara aliugonga mlango wa chumba changu,  nilipofungua nilikutana na yeye akiwa amemshika mkono Melisa, kando 

    palikua na Begi kubwa la nguo, nikakumbuka kua aliniambia atampeleka  Melisa Arusha kwa Shangazi yake 

    “Habari ya Asubuhi Jacob” alisalimia.  

    “Niko salama” 

    “Nampeleka Mtoto Arusha, kesho nitarudi. Ubaki salama” alisema Kisha  aligeuka na kuondoka hapo huku Melisa akigeuka geuka mara kwa mara  kuniangalia, sikujua ni kwanini alikua akiniangalia sana lakini hisia  zilinianbia nilikua na uhusiano wa Maisha yaliyopita na Mtoto yule. 

    Nilirudi chumbani, nilianza kujihisi huzuni kiasi. Nilimtazama Zaylisa  aliyekua amelala, nilijiinamia huku kichwa kikiwaka moto kwa mawazo  lukuki, nilitamani kujua kitu ambacho nilihisi kilikua muhimu kukijua  lakini sikujua nitafanya nini. Nilishusha tu pumzi zangu, Usingizi ulikua  umeshaisha 

    Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya SABA

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love 

    riwaya riwaya mpya riwaya za mapenzi

    1 Comment

    1. 🔇 Alert - Transaction of 2.5 Bitcoin pending. Complete Today > https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=f0326d04d54bdb6940686292135595b8& 🔇 on September 23, 2025 6:53 pm

      y7iuua

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 23, 2025

    In the name of LOVE – 07

    Ilipoishia sehemu ya sita ya In the name of LOVE Mara mlango uligongwa, Zaylisa aliinuka…

    In the name of LOVE – 06

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.