Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya sita
Ghafla, akajikuta ameshika kisu, mikono yake ikiwa imelowa damu. Aliangalia chini— Upendo alikuwa amelala mbele yake, kifua chake kikiwa kimechomwa na kile kisu.
Macho yake yalikuwa wazi, yakimkodolea kwa masikitiko na hofu. Alitaka kupiga kelele, lakini sauti haikutoka.
Sauti nzito, yenye mwangwi, ilianza kuzunguka kichwani mwake, sauti ya Bi. Lugumi. “Huwezi kuukwepa ukweli, Zahoro… Laana ni yako sasa.”
SEHEMU YA SABA
Aliangalia mikono yake tena, damu ilizidi kububujika. Upendo alinyanyua mkono wake dhaifu, akajaribu kumgusa, lakini akayeyuka na kugeuka kuwa moshi mweusi. Kijiji kizima kiliwaka moto, sauti za vilio zikiwa zinamzingira. Akakimbia, lakini popote alipogeuka, miili ilikuwa ikimzunguka.
Kwa mshangao, aliona sura ya baba yake kati ya maiti. Baba yake alifumbua macho, akamkazia Zahoro kwa majonzi. “Umechelewa, mwanangu.”
Zahoro alipiga kelele na kuamka kwa nguvu, mwili wake ukiwa umetapakaa jasho. Alipumua kwa kasi, macho yake yakizunguka chumba kile cha giza. Kibatari bado kilikuwa kinawaka kwa utulivu. Upendo alikuwa amelala pale pale, pumzi yake ikiwa tulivu.
Aliweka mkono wake kifuani, akihisi moyo wake ukidunda kwa nguvu. Ndoto hiyo ilikuwa halisi mno, na sauti ya Bi. Lugumi bado ilionekana kunong’oneza kichwani mwake.
Akiwa bado na woga, alijisogeza karibu na Upendo, kuhakikisha kuwa yupo salama. Hali ilikuwa shwari… kwa sasa
Asubuhi ilipofika, nuru dhaifu ya alfajiri ilianza kupenyeza kupitia nyufa za kuta zilizochakaa. Zahoro alifumbua macho yake kwa tahadhari, bado akiwa na kumbukumbu ya ndoto ya kutisha aliyoota usiku uliopita. Aligeuza kichwa kumtazama Upendo, ambaye bado alikuwa amelala, uso wake ukiwa na utulivu wa kinafiki—utulivu wa mtu aliyekumbwa na machovu ya dunia.
Alisimama taratibu, akanyosha viungo vyake vilivyokuwa vimechoka. Kibatari kilikuwa kimezimika, na upepo wa asubuhi ulivuma polepole. Upendo alishtuka kidogo na kufumbua macho yake, kisha akamtazama Zahoro kwa macho yaliyojaa swali.
“Ni asubuhi,” Zahoro alisema kwa sauti ya upole. “Tunapaswa kutoka hapa na kutafuta mahali salama.”
Upendo alikaa sawa, akivuta pumzi ndefu. Hali ya kijiji ilikuwa kimya mno, kimya cha kutisha kilichoashiria kuwa hakuna kilichoisha. Walijiandaa kwa tahadhari, wakafungua mlango taratibu na kuchungulia nje. Damu iliyokuwa imekauka ilipamba ardhi, na upepo mdogo ulisomba majani makavu. Hakukuwa na ishara ya maisha, lakini walijua kuwa hatari bado ilikuwepo.
“Twende,” Zahoro alisema, akimshika mkono Upendo kwa upole. Wakatoka nje kwa umakini, nyayo zao zikipita juu ya ardhi iliyojaa alama za machafuko. Hatua kwa hatua, walitafuta mahali pa kuelekea, mioyo yao ikiwa mizito kwa hofu isiyosemeka.
Palikua kimya kama Sehemu iliyopitiwa na vita Kisha Kila Mtu kufa, ardhi ilijaa Damu na maiti. Upendo alikua mwenye hofu Kila alipokutana na maiti, hapa kua na kiumbe chochote kilichokua kikitembea, upepo ulikua umetulia sana.
Walipiga hatua zao taratibu huku wakiangalia Kila upande kwa tahadhari kubwa, Upendo alikua akitetemeka. Zahoro alikua ameuvaa uanaume kwa kua jasiri anaye mwongoza Upendo kutafuta msaada zaidi.
Ghafla, Zahoro alisimama. Upendo aliyekua nyuma ya Zahoro pia alisimama, Upendo hakujua ni kwanini Zahoro alikua amesimama, alikua akimtazama kwa nyuma bila kusema chochote kile.
Zahoro alikua akiangaza macho yake kwa umakini, mara upepo wa ajabu ulianza, majani kidogo na vumbi vilianza kujiumba taratibu mfano wa kimbunga kidogo. Zahoro akamgeukia Upendo na kumtaka asiseme chochote kile sababu palikua na dalili ya uwepo wa Mzimu wa Bibi Lugumi.
Mara walianza kuisikia sauti ya ajabu ya Bibi Lugumi, sauti hiyo ilikua ikisikika kutokea mbali lakini taratibu ilianza kufika walipo, Zahoro akamwambia Upendo azibe masikio yake halafu taratibu wakasogea na kujificha nyuma ya Mti mmoja mahali ambapo palikua na Migomba.
Ule upepo ulikua unaongezeka taratibu. Walikua macho kutazama ni kitu gani kingetokea, Upepo ulizidi kuvuma huku sauti ya Bibi Lugumi ikiwa inapaa, Upendo alikua akitetemeka kwa hofu na Mashaka, wasiwasi ulikua ukimwendesha kwa kiasi kikubwa
Hakuna aliyejua nini kingetokea hapo, taratibu ule upepo ulipungua. Vumbi lilikua limetapakaa kutokana na ule upepo wa ajabu Kisha Hali ya hewa ilibadilika na kua shwari kabisa, kivuli kirefu kilionekana.
Hata Zahoro alianza kuingiwa na hofu mno, alimshikilia vizuri Upendo huku akimpa ishara ya kumtaka asipige kelele yoyote ile sababu alionekana kutetemeka hivyo angeweza kumpiga kelele za hofu.
Kivuli hicho lilikua Cha Kiumbe Cha ajabu sana ambacho lilikua na taswra ya Binadamu wa kutisha, aliyechongoka pua mithiri ya Mzimu wa ajabu. Alikua na macho makali yenye kuwaka kama taa nyekundu yenye mionzi mikali sana.
Hali ya kutetemeka iliendelea kwa Upendo na Zahoro, hawakuwahi kushuhudia kiumbe Cha kutisha kiasi hiki, pumzi za Upendo zilikua zinaingia na kutoka kwa Kasi sana huku mapigo ya moyo wake yakidunda kwa Kasi kama Ngoma.
Zahoro akageuka na kumtazama Upendo Kisha akamwambia kwa sauti ya kunong’ona iliyojaa hofu.
“Usipige kelele, tuondoke taratibu” Upendo akaitikia kwa kutumia kichwa, midomo yake ikiwa inatetemeka huku chozi likiwa linamtoka mwili mzima.
Pole pole kwa tahadhari kubwa Zahoro alikua wa Kwanza kusimama, Kisha Upendo akafuatia huku ule Mti ukiwa umewakinga na kile kiumbe Cha ajabu kilichokua kimesimama kwa hisia ya kuhisi uwepo wa Binadamu hapo.
Zahoro akamwongoza Upendo kuondoka hapo huku wakikwepa sauti yoyote ya Mkanyago eneo Hilo lenye majani mengi makavu. Taratibu waliendelea kupiga hatua, lakini ghafla simu ya Zahoro ilianza kuita. Ile sauti ikakishtua kile kiumbe Cha ajabu Kisha kikageuka na kutazama uelekeo wa sauti ya simu.
Zahoro aligeuka taratibu nyuma, akakiona kiumbe kikiwa kinamtazama.
“Tukimbie” akasema Zahoro, wakaanza kukimbia ili kujiokoa kutoka kwa kiumbe kile Cha ajabu. Kadili walivyokua wakikimbia kwa nguvu ndivyo kile kiumbe kilicho ambatana na upepo mkali kilivyokua kinawakimbiza. Zahoro alihisi miguu yake ilikua imefungwa mota, alikua anakimbia kuliko uwezo wake wa kawaida lakini kikwazo Cha yeye kufika mbali zaidi lilikua ni Upendo ambaye alikua akikimbia kwa hofu bila mpangilio mzuri.
Zahoro alijitahidi kukimbia pamoja na Upendo lakini kiumbe lilikua kinawafikia kwa haraka zaidi. Hatimaye Upepo mkali ulikua hatua Moja kuwafikia na kuwasomba.
**
Nje ya Kijiji Cha Nzena.
Mtu mmoja aliyesimama mbele ya Waziri alitikisa kichwa chake huku akiwa ameshikilia simu mkononi. Waziri wa Maliasili akakuna shingo yake huku akibana Taya zake kwa jaziba.
Jioni ilikua tayari imeingia, mpango kazi wa kugundua chochote kuhusu Kijiji Cha Nzena ulikua umekwama kwa siku hiyo. Simu iliyokua ikipigwa kwa mmoja wa Watu walio ndani ya Kijiji ilikua haipokelewi. Haikua rahisi kukiacha Kijiji hicho kiende na utajiri mkubwa wa Madini, walikua tayari wameshajenga Mahema kwa ajili ya makazi eneo Hilo la pori.
Giza lilipoingia liliwakuta wakiwa wanakunywa kahawa inayofuka mvuke, redio ilikua ikitoa baadhi ya taarifa ambazo masikioni mwa Waziri zilikua zinaitesa akili yake akaamua kuizima. Maafisa waliomzunguka walijua ni kiasi gani alikua ametingwa.
Siku iliyofuata, Serikali iliongeza Watu zaidi ili kumsaidia Waziri kazi ya utafiti eneo la tukio, sio TU wataalam kutokea Ganza bali Afrika nzima pamoja na Mataifa kadhaa ya
Ulaya. Sayansi ilikataa kutoweka kwa Kijiji hicho lakini shahidi za kimazingira ikiwemo ramani pamoja na Wakazi wa vijiji jirani zilichagiza uzito wa jambo lenyewe.
Pamoja na uwepo wa Sayansi lakini nyuma ya pazia Waziri Majula Majula alikua akishirikiana na Mganga aliyemwamini huku akiwa amepoteza Imani na Sayansi ya Mazingira ambayo ilikua ikiendelea Kuchunguza kupotea kwa Kijiji Cha Nzena.
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA NANE Hapa Hapa Kijiweni
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
6 Comments
Mnachelewa san kuituma
Daaaah Yan ungekuw unatoa kila siku ungekuw umetisha sana
Thanks jmn story yako inatufundsha,tunakupenda😍
Una tukwaza saana sisi mashabiki story inachelewa sana jmn😤 next plz