Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya tanoย
Waziri akajitupa kitini huku akifumba macho yake, hakujua atamweleza vipi Rais waย Ganza, utajiri uliopotea kwenye Kijiji cha Nzena ni utajiri mwingi sana wa Madini.ย
Mara mlango wa gari ulifunguliwa haraka sana, Waziri na Mshauri walishtuka. Mtuย mmoja kutoka kwenye timu yake alikuja ghafla na kumwambia kua kuna Mtu kutokaย Kijiji cha Nzena amepiga simu. Macho yalimtoka Waziri wa Maliasili, ingewezekanajeย kua simu itoke kuzimu? Alikua kama Mtu aliyezinduliwa kutoka usingizi wa Pono,ย akatupa swali moja ngangariย
โUnasemaje?โย ย
SEHEMU YA SITA
โNdio Mkuu, tumepokea simu sasa hivi kutoka Kijiji cha Nzenaโย ย
โHa! Ha! Hebu acha ndoto za Asubuhi, mmefikia wapi kwenye utafiti?โ Aliuliza Waziriย akihisi huwenda Mtu huyo alikua akiingiza utani. Lakini alipoitazama sura ya huyo Mtuย aligundua msisitizo, akasikika tena akikazia
โSio utani Mkuu, ni simu ya Mkazi wa Nzenaโ alisema, Waziri aliona jambo hilo lilikuaย siyo la mzaha, akajisogeza kidogo karibu na huyo Mtu akamwulizaย
โInawezekanaje?โย
โMkuu hakuna anayejua, sababu simu nyingi zilipigwa kwa kufuata anuani, hakunaย simu iliyoita isipokua simu moja. Kisha simu hiyo ikapigaโย ย
โHebu nieleze, alisema nini?โย
โTulichokisikia ni kelele za kuomba msaada, anasema hakuna anayeweza kutoka walaย kuingia ndani ya Kijiji. Inaonesha kipo lakini ni ngumu kwa akili ya kawaidaโ alisema,ย Waziri akamtazama mshauri wake na wote wakajikuta wakiyakubali maneno ya yuleย Mganga kua Kijiji hicho kwasasa kinapokea laana ya kifo na Mauwaji ya Kutisha.ย
Akashusha pumzi zake kisha akaongozana na mtoa taarifa hadi eneo ambalo Linaย mtambo wa kupiga na kupokea simu. Taarifa ile ikathibitishwa na wataalam wengine,ย japo wengi wao hawakuwa na imani sana lakini iliwalazimu kukubali, simu hiyoย haikuonesha eneo ilipopigwa.ย
Wakajaribu kupiga tena lakini simu hiyo haikupatikana.ย
โShitโผ hakikisha mnampata huyo Mtu na atoe taarifa ya Kijiji kipo wapi na niniย kinaendelea.โ Alisema kwa msisitizo Waziri wa Maliasili kisha alirejea ndani ya gari.ย
**ย
Ndani ya Kijiji Cha Nzena.ย
Zahoro alikua amerudisha fahamu, alikua amejiegemeza ukutani akiwa amekaa. Alikuaย kwenye maumivu makali ya kichwa, mkononi alikua ameshikilia simu yake ndogoย akijaribu kupiga huku na kule.ย ย
Chozi lilikua likimbubujika, mwili wa Baba yake Mzee Miroshi ulikua ukituama nzi.ย Mara simu yake aliyokua akiipiga iliita na kupokelewa haraka sana, akababahikaย kuongea. Akasikia sauti ikimuulizaย
โUpo Nzena?โย ย
โNdiyo, tunakufaaa. Mtusaidieโ alisema huku akiwa analia, upande wa pili ukamwambiaย
โUsilie, hebu tueleze nini kinaendelea. Mko wapi, Unaongea na Waziri wa Maliasiliย Majula Majulaโ ulisema Upande wa pili, simu ilipokelewa na kitengo cha Waziri walioย nje ya Kijiji wakiendelea kutafuta namna Kijiji hicho kilivyopotea.ย
โTupo Kijijini Nzena lakini hatuwezi kutoka. Watu wanakufa kwasababu ya Laanaโย alisema, hapo hapo simu hiyo ilikatika. Aipojaribu Kupiga, simu haikuita.ย
Alilia sana Zahoro, hakujua ni namna gani anaweza kuondoka Kijijini hapo, macho yakeย yalikua yakishuhudia moshi Mkali uliokua ukifuka Kijijini hapo. Kelele ziliendeleaย kupaa za kuomba msaada, lakini kichwani pake Zahoro alijua fika kua kuisikiliza sautiย ya Bibi Lugumi ndiyo sababu ya vifo vya Watu.
Akanyanyuka na kufikiria aingilie wapi ili aanze kuwaeleza Watu kua wazibe masikioย yao ili wawe hai.ย ย
Taratibu Zahoro aliondoka nyumbani kwa Mzee Kova huku akimwacha Baba yake akiwaย amesha fariki. Chozi lilikua likimbubujika, alitembea akiwa ameziba masikio kwaย kutumia mikono yake. Maiti zilikua zimetapakaa Kila mahali alipokua akipita.ย
Miguu yake isiyo na kiatu ilikua ikifanya safari isiyo na uhakika, uharibifu mkubwaย ilikua umetokea Kijijini, mifugo ilikua imekufa kama jinsi ambavyo Watu walikuwaย wamekufa. Kila mwili ulikua umetapakaa Damuย
Alipata kichefu chefu na kujihisi kama Mtu anayetaka kutapika, akajikuta akitapikaย huku akipepesuka kama mlevi Hadi eneo la Migomba, akapiga magoti na kuendeleaย kutapika huku akihisi nguvu ilikua imemwisha.ย
Alipoinua kichwa chake ili anyanyuke alimwona Msichana mmoja wa miaka 17,ย Msichana huyo alikua ametapakaa masizi usoni, alikua akimtazama Zahoro kwa hofuย sana huku akiwa anarudi nyuma taratibu akihitaji kukimbia. Zahoro akagundua harakaย kua Msichana huyo alikua akiogopa.ย
Zahoro akamwambia yule Msichana kwa sauti ya utaratibu.ย
โUsikimbie, Mimi siyo Mtu mbaya tafadhaliโ alisema huku akiwa amenyooshea mkonoย mmoja na mwingine akiwa ameshikilia eneo la kifua ili kumwaminisha zaidi Msichanaย huyo mrefu, aliyesuka mabutu lakini akiwa amevalia gauni lenye maua ya bluu.ย Msichana huyo alisimama baada ya kusikia maneno ya Zahoro, macho yake Msichanaย huyo hayakuonekana kama alikua akimfahamu Zahoro.ย
โMimi ni Muhanga kama wewe, Naitwa Zahoroโ hatimaye akajitambulisha Zahoro hukuย akinyanyuka na kusimama. Macho Yao yalikua yakitazama kimkakati sana, Badoย Msichana alihitaji uhakika zaidi kua Zahoro hakua Mtu mbaya.ย
โUnaweza kuzungumza?โ aliuliza Zahoro maana Msichana huyo aliyekauka mdomoย wake hakuufungua mdomo huo. Akaitikia kwa kutumia kichwa chake kua anawezaย kuzungumza.ย
โSura Yako ni ngeni, huonekani kama mkaazi wa Nzenaโ alisema Zahoro, yule Msichanaย hatimaye akafungua mdomo wake huku chozi likimbubujika, midomo ilikua ikitetemekaย
โNdiyo, Mimi nimetokea Mjini. Nilikuja kwa Shangazi yangu, sijui nipo wapi kwasasaย maana ni mgeni. Nimepotezana na Shangazi yanguโ Chozi lilikua likimbubujika, suraย yake ilionesha maumivu ya kihisia ambayo Binti huyo alikua nayo.ย ย
โUsijali, Bado upo Kijijini. Unasikia hebu sogeaโ alisema Zahoro huku akianza kusikiaย sauti ya Bibi Lugumi, sauti ambayo inauwa. Akamwambia yule Msichana kwa harakaย
โKamwe usiisikilize hiyo sauti, ziba masikio yako!โ Zahoro alipaza sauti kwa nguvu.ย Msichana huyo, akiwa amechanganyikiwa, akatizama huku na kule, macho yake yakiwaย na hofu iliyojaa machozi. Alilia kwa kwikwi, mwili wake ukitetemeka kwa hofuย isiyoelezeka.
โZiba masikio, usiisikie!โ Zahoro alipaza tena sauti, lakini bado msichana huyoย alizunguka kama mtu aliyekosa mwelekeo, kama aliyekuwa tayari ametekwa na sauti yaย Bi. Lugumi. Hatua chache tu zilimfanya kuwa karibu na Zahoro, aliposimama karibuย naye, bila kufikiria, Zahoro alimshika kwa nguvu na kumpiga kibao usoni. Msichanaย huyo alishtuka, macho yake yakikosa mwelekeo wa awali. Wenge liliondoka taratibu.ย
โZiba masikio yako!โ Zahoro alirudia kwa msisitizo. Msichana huyo alifanya kamaย alivyosema. Sauti ya Bi. Lugumi ikapita, ikiambatana na kimbunga cha majani makavuย na vumbi lililopeperuka juu ya ardhi. Zahoro alisubiri kwa tahadhari hadi upepo huoย ulipopotea, akapumua kwa nguvu na kuondoa mikono masikioni mwake. Kisha,ย akamshika msichana yule na kuondoa mikono yake pia.ย
โHaya yote unayoyaona hapa kijijini ni matokeo ya laana ya miaka mingi,โ Zahoroย alisema kwa sauti nzito, macho yake yakikagua mazingira yaliyojaa maiti na damuย iliyomwagika ovyo.ย
Msichana huyo alishindwa kusema neno, mwili wake ukiwa dhaifu kwa hofu. Gizaย lilianza kuingia, hewa ikawa nzito na baridi ikaanza kupenya. Zahoro alimshika mkonoย na kumwongoza hadi kwenye nyumba ya karibu. Ndani, waliwasha kibatari kidogo naย kujikunyata kila mmoja pembezoni mwake kama makinda ya ndege yaliyoachwa naย mama yao.ย
Kimya kilitawala. Wadudu wa usiku pekee ndio waliotoa sauti ya chinichini. Zahoroย alipumua kwa kina, akamtazama msichana huyo kwa mara ya kwanza kwa makini.ย โUnaitwa nani?โ aliuliza, sauti yake ikiwa na mshikamano wa uchovu na tahadhari.ย
Msichana alinyanyua macho yake taratibu. Kivuli cha huzuni kilikuwa kimetanda usoniย pake. Alijua maisha yake yameingia katika giza lisilojulikana. Mtu pekee aliyekuwa nayeย kwa sasa ni Zahoro.ย
โUpendo,โ alijibu kwa sauti ndogo, akipepesa macho yake. Tabasamu dhaifu, lisilo naย maana, liliganda usoni mwake kwa sekunde chache kabla halijazimika kabisa.ย
Baridi ilikuwa kali. Zahoro alitazama kibatari, mwali wake ukitingishika kwa upepoย mdogo uliopenya kupitia nyufa za ukuta. โMaisha yetu kwa sasa ni mfano wa hikiย kibatari,โ alisema kwa sauti ya mawazo. โKosa dogo, mwanga unazimika, nasiย tunapotea.โ
Alitulia kwa muda, kisha akaendelea kwa sauti iliyokuwa na maumivu mazito. โKwenyeย dunia hii ya ghafla, nimempoteza mtu aliyenipambania maisha yangu yote. Baba yanguย amekufa mbele ya macho yangu.โ Machozi mepesi yakamtoka lakini alijifuta haraka.ย
Moyo wa Upendo uliingiwa na baridi ya huzuni. Alimwonea huruma Zahoro kwa namnaย isiyoelezeka.ย
โSijui hatma ya maisha yetu hapa, Upendo,โ Zahoro alisema, sauti yake ikiwa nzito naย polepole. โHakuna anayeweza kuingia wala kutoka kijijini.โย
Upendo aliinamisha kichwa chake, akavuta pumzi kwa tabu. โKama hatuwezi kutokaย hapa, basi kwa nini tunapambana kuishi?โ aliuliza kwa sauti ya kutapatapa, akimtazamaย Zahoro kwa macho yenye ukungu wa machozi yaliyokuwa karibu kudondoka.ย
โKwasababu hatuwezi kufa kama kuku,โ Zahoro alijibu kwa msisitizo. โTunapokea laanaย isiyo yetu. Hatuhusiki kwenye dhambi hii.โย
Kimya kikarejea. Upendo akajiegemeza kwenye kona ya chumba, mwili wake ukawaย dhaifu. Hatimaye, alifumba macho yake na kuanza kukoroma polepole kwa uchovu.ย
Zahoro alimtazama kwa muda mrefu. Alipohakikisha amelala, alichukua kibatari naย kuingia chumba kingine kutafuta nguo ya kumfunika. Bahati nzuri, alipata nguo nzitoย na akarudi kumfunika Upendo. Kisha, akajiegemeza kwenye kona yake, akifanya uamuziย wa kukesha usiku huo. Kama sauti ya Bi. Lugumi ingerudi tena, alitaka kuhakikishaย kuwa angeweza kumwamsha na kumlinda Upendo kwa gharama yoyote.ย
**ย
Uchovu ulimwelemea bila kujua, macho yake yakafumba taratibu, na usingizi mzitoย ukamchukua. Ndoto ikaanza kumvaa kwa kasi, dunia ya giza na maangamizi ikajitokezaย akilini mwake.ย
Alijiona akitembea katikati ya kijiji, lakini hakikuwa kile alichokijua. Kila nyumbaย ilikuwa imejaa damu, miili ya watu waliokatwa vipande ikiningโinia kwenye kuta, machoย yao yakiwa wazi bila uhai. Kilio cha maumivu kilisikika mbali, lakini hakukuwa naย aliyebaki kuweza kusaidia.ย
Ghafla, akajikuta ameshika kisu, mikono yake ikiwa imelowa damu. Aliangalia chiniโ Upendo alikuwa amelala mbele yake, kifua chake kikiwa kimechomwa na kile kisu.ย
Macho yake yalikuwa wazi, yakimkodolea kwa masikitiko na hofu. Alitaka kupiga kelele,ย lakini sauti haikutoka.ย
Sauti nzito, yenye mwangwi, ilianza kuzunguka kichwani mwake, sauti ya Bi. Lugumi.ย โHuwezi kuukwepa ukweli, Zahoroโฆ Laana ni yako sasa.โย
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Hapa Hapa Kijiweni
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย


68 Comments
Get started instantlyโearn on every referral you make! https://shorturl.fm/pD7kQ
Hatร ri sana na huu ndo kwanza moto unaanza
Story tamu sawa ila tatizo hi;I: you’re now admin) sijapenda kabisa๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Share your link and rake in rewardsโjoin our affiliate team! https://shorturl.fm/mIe1t
Refer friends, collect commissionsโsign up now! https://shorturl.fm/IDd4J
https://shorturl.fm/1eb7S
https://shorturl.fm/8ojWc
https://shorturl.fm/175m4
Dah nilijua zahoro anaweza Kuwa star kweny hii story ๐ค
https://shorturl.fm/jLDrL
https://shorturl.fm/6Ij8t
https://shorturl.fm/A98lB
https://shorturl.fm/n18PQ
https://shorturl.fm/xSeM2
https://shorturl.fm/93kS6
https://shorturl.fm/f3Cmu
https://shorturl.fm/iJN1W
https://shorturl.fm/bMEcC
https://shorturl.fm/7NlED
https://shorturl.fm/W8CvZ
https://shorturl.fm/hDSXc
https://shorturl.fm/vWTdw
https://shorturl.fm/ibdka
https://shorturl.fm/ik4H3
https://shorturl.fm/jUT9U
https://shorturl.fm/neNtG
https://shorturl.fm/WQg12
https://shorturl.fm/KrXO4
https://shorturl.fm/fgfoU
https://shorturl.fm/Z81ij
https://shorturl.fm/Qahjh
https://shorturl.fm/yAaQ4
https://shorturl.fm/wvzhn
https://shorturl.fm/wx4aU
https://shorturl.fm/DE9JS
https://shorturl.fm/FmnuU
https://shorturl.fm/I215V
https://shorturl.fm/E6d08
https://shorturl.fm/3kA1P
https://shorturl.fm/K9X2X
https://shorturl.fm/W3QuC
https://shorturl.fm/zGBJd
https://shorturl.fm/zKYrZ
https://shorturl.fm/4mfaI
https://shorturl.fm/LkJH0
https://shorturl.fm/G5NXC
https://shorturl.fm/mfI4Q
https://shorturl.fm/cVnDJ
https://shorturl.fm/LYvtl
https://shorturl.fm/ykvxP
https://shorturl.fm/PXxEe
https://shorturl.fm/Rqhg6
https://shorturl.fm/iCPac
https://shorturl.fm/52KYG
https://shorturl.fm/Kh4O0
https://shorturl.fm/5GA4W
https://shorturl.fm/ogrlX
https://shorturl.fm/OnHOf
https://shorturl.fm/SvbUb
https://shorturl.fm/miH1n
https://shorturl.fm/XQBKW
https://shorturl.fm/n3xiu
https://shorturl.fm/PuRS7
https://shorturl.fm/bVTYO
https://shorturl.fm/6aiLr
https://shorturl.fm/vdw2l
https://shorturl.fm/0QXXL
https://shorturl.fm/SOeVT