Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03
    Hadithi

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJuly 14, 2025Updated:July 15, 202514 Comments9 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya pili

    Alipiga magoti na kujiinamia huku chozi likimtoka Zahoro, yeye na Baba yake pekee  ndiyo ambao walikua wa kwanza kutambua kua laana ya Kifo cha Masumbuko  iliyotolewa na Bibi Lugumi ilikua imeanza kufanya kazi, lakini ni yeye pekee ndiye aliyegundua kua hakuna anayeweza kuondoka hapo Kijijini kuanzia muda ambao aliiota  Laana ile na kuisikia sauti ya laana ya Bibi Lugumi  

    Akiwa hapo anatokwa na mchozi, mara alivamiwa na walinzi wa Kijiji waliotumwa na  Mzee Kova kumkamata. Dunia yake ilijaa mishangao sana, akawauliza kwa sauti ya  upole huku chozi likimtoka. 

    SEHEMU YA TATU

    “Kwanini mnahangaika na Mimi, sina ubaya. Mmemkamata na Baba yangu pia?” tayari  alikua ameshasimamishwa, hakujibiwa chochote isipokua alisogezwa mbele ya nyumba  ya Mzee Kova kisha mlinzi mmoja akatumwa kuelekea mazishini kumwita Mzee huyo  mwenye mamlaka makubwa kuliko hata viongozi wa Kiserikali wa Kijiji cha Nzena. 

    Alifungwa kamba huku walinzi wakiendelea kumshikilia, Zahoro akawaambia 

    “Kijiji chetu kimelaaniwa, hakuna atakayetoka wala atakayeingia. Tutakufa kama Kuku  kwenye ardhi yetu na hakuna atakayejiokoa” alisema huku mwili ukimsisimka kutokana  na uzito wa Maneno hayo, chozi lilizidi kumbubujika. 

    Wale walinzi walimtazama Tu Zahoro bila kusema chochote kile, sauti ya Mzee Miroshi  ilizidi kusikika pia.  

    Haikuchukua hata nusu saa, msafara wa Wazee wa Kijiji watano ulifika hapo. Mzee Kova  alionekana kua na hamu ya kuzungumza na Zahoro. Alipewa kiti kisha aliketi mbele ya  Zahoro akamtazama kidogo kisha akamwuliza 

    “Ni wewe uliyesema Kijiji hiki kina laana?” alimwuliza kwa sauti ya ukakamavu iliyotoka  taratibu, huku jicho jekundu likiwa linamtazana Zahoro, Wazee wengine wakiwa  wamemzunguka Kijana huyo. 

    “Sio Mimi, bali aliyetoa laana. Tumelaaniwa kwa makosa ya Watu wachache walioamini  wanajua kila kitu. Hakuna atakayeweza kuingia wala kutoka Kijijini kuanzia sasa”  alisema kwa kujiamini sana Zahoro sababu alikua na uhakika na anachokisema. 

    Wazee wote waliangusha vicheko vya dhihaka, ilionekana kua ni jambo lisilowezekana  lakini Zahoro akawaambia 

    “Kifo cha Masumbuko na Bibi yake ni laana kwetu. Tutakufa sote” alisema kwa  kushupaza shingo na sauti yake, akanaswa kibao na Mzee Kova ambaye alionesha  kukerwa na kauli ya Zahoro. Kisha akawaambia Walinzi 

    “Wawili waende haraka Kijiji jirani, mrudi hapa na taarifa njema. Kisha atauawa huyu  Mpuuzi na Baba yake” alisema kisha walinzi wawili walianza safari kwa kutumia  Baiskeli, kutoka hapo kuelekea Kijiji jirani ni mwendo wa nusu saa kwa kutumia  Baiskeli.  

    Mzee Kova na wazee wengine walisubiria huku Zahoro akipigwa na jua lililokua likianza  kua kali, muda ulienda. Macho ya Wazee wote yalikua yakiitazama njia waliyoondoka  nayo wale walinzi. Haikuchukua hata dakika 20 Watu hao walirejea wakitokea njia  nyingine 

    Kila mmoja wao alitoa simulizi ya kutatanisha iliyoamsha hasira ya Mzee Kova, iliamsha  hisia ya tofauti kwa Wazee wengine ambao macho yao waliyapeleka kwa Zahoro  aliyekua akitabasamu licha kufungwa huku akipitia mateso.

    Kisha Mzee Kova akawauliza tena kwa msisitizo huku akiwakazia macho, kwa jinsi  ambavyo alikua akiogopwa isingelikua rahisi wale Walinzi kusema Uwongo. 

    “Tumeshindwa kufika kijiji jirani, kila tulivyokanyaga pederi tulijikuta bado tupo Kijiji  Mkuu” Mzee Kova alipepesa macho yake kisha aligeuka kumtazama Zahoro halafu  akarejea kuwatazama Walinzi wale halafu akawaambia 

    “Nendeni mkamfunge Zahoro pamoja na Baba yake chumbani, kisha mniitie Mtimbe  sasa hivi” alisema kwa hasira sana, palikua kimya sana isipokua sauti yake, Mtimbe  ndiye Mganga wa Kijiji cha Nzena, ndiye aliyemuuwa Masumbuko Usiku ule na kufanya  tambiko. 

    Haraka maagizo yake yalitekelezwa ndani ya muda mfupi, Mganga Mtimbe alikua mbele  ya macho yake wakiwa wote wameketi kwenye Baraza lake hapo nyumbani kwake Mzee  Kova.  

    “Bila shaka umeshaipata habari si ndiyo?” alianza Mzee Kova huku mshipa wa kichwa  ukiwa umemtoka. Mtimbe akauliza kwa utiifu sana 

    “Habari ipi hiyo?” 

    “Laana iliyotamkwa na Bibi Lugumi”  

    “Imefanya nini?” 

    “Usiulize kama Mtoto mdogo usiye na maono Mtimbe” akahamaki Mzee Kova kisha  akaweka utuo na kuendelea 

    “Nilitegemea ungekua wa kwanza kuona kisha tukaidhibiti, umezidiwa uwezo na kijana  mdogo wa hapa Kijijini. Ni hivi, hakuna anayeweza kutoka wala kuingia Kijijini, hii  misiba ya mpigo ni kwasababu ya laana hiyo” Maneno ya Mzee Kova yalimnyong’onyeza  Mtimbe, alionekana kulegea mwili mzima huku kijasho kikimtoka 

    “Mkuu ngoja nilifanyie kazi hilo mara moja”  

    “Sema unahitaji nini?”  

    “Ngoja niangalie ukubwa wake kisha tuone tunahitaji nini haraka, wacha nikimbilie  nyumbani kuchukua kila kitu” alisema huku akisimama na kuondoka kwa kukimbia,  aliacha taharuki kubwa sana miongoni mwa Wazee, hadi kufikia muda huo ni wachache  walioigundua laana hiyo hapo Kijijini Nzena. 

    ** 

    Ikulu ya Rais. 

    Rais Besigwe alikua ameketi kitini akitabasamu, mbele yake alikua ameketi waziri wa  Ardhi. Kicheko kilimtoka Rais Besigwe kisha akamtolea sauti Waziri aliyejiinamia 

    “Kijiji kupotea?” 

    “Ndiyo, Mkuu. Kiasi chote cha madini kimebakia kua hadithi ya kusimulia vizazi vyote.  Migodi imepotea na utajiri mwingi wa Nchi, hata ile ardhi tupu iliyobakia yenye pori  dogo hakuna tena madini” alielezea Waziri huku akimtazama Rais kwa macho yake 

    madogo yenye kope fupi. Mikono ya Waziri ilijaa utii mezani, huku Rais akimtazama Waziri kwa jicho lisilo na uhakika wa nini alikua nataka kukisema tena. Sura ya Rais  ilijaa maswali na umakini hasa baada ya Waziri kurudia alichokisema Mwanzo. 

    “Siwezi kuamini, Nahitaji kuelekea huko Mashariki” alisema Rais, mara moja Waziri  aliondoka hapo akiwa anajua kua Rais hakuweza kumwamini. 

    Siku iliyofuata, ndege maalum ya Rais Besigwe iliota mbawa kutoka Mji Mkuu wa Nchi  ya Ganza kuelekea kusini mwa Nchi hiyo, hamu na shahuku yake ilikua kutomasa  alichokisikia. Kila aliyesikia safari ya Rais huyo alijisemea kua Rais alikua Tomaso. Ndani ya ndege aliambatana na Waziri wa Ardhi na Mali kale, pamoja na jopo la Walinzi  

    Hali ya usalama iliimarishwa hadi kufika kwake na kukanyaga Ardhi iliyokua  ikizungumzwa zaidi Duniani. Kwa kutumia magari walianza safari kutoka wilayani  kuelekea Kijiji cha Nzena. Masaa mawili yalitosha kuwafikisha huko 

    Rais alioneshwa mahali hapo kwa kutumia vidole na ramani, kwanza alichuchumaa na  kuchota mchanga kisha akasema 

    “Hakika sikuona kila kitu, leo Mungu ametuonesha na kuturudisha enzi za Mitume”  kisha alisimama na kuagiza mchanga aliouchota upelekwe Ikulu Kama ukumbusho.  Aliporejea Ikulu alihutubia Taifa kwa kutoa taarifa kamili ambayo mwanzo ilidhaniwa  kua ilikua ni uvumi tu. Kisa cha Kijiji cha Nzena kikachukua sura mpya. 

    ** 

    Kijijini Nzena. 

    Muda ulizidi kwenda, jua lilizidi kutua na kua kali sana kuashiria kua Mchana ulikua  umeshaingia. Mzee Kova na Wazee wengine walikua wakimsubiria Mganga Mtimbe. 

    “Kwanini usitume Mtu kumkagua?” aliuliza Mzee Kisugu. Mzee Kova akamtazama Mzee  Kisugu kisha akamgeukia mlinzi mmoja wa Kijiji akamwambia 

    “Nenda uje na Mtimbe haraka” alisema, kisha haraka Mlinzi mmoja alichukua Baiskeli  na kuelekea nyumbani kwa Mganga Mtimbe. Palikua na umbali kiasi lakini si wa  kuchukua nusu saa haujafika. 

    Mlinzi alipofika aliteremka kutoka juu ya Baiskeli akiitazama nyumba ya Mtimbe  iliyojengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi kavu mpya. Palikua Kimya, haikumtia  hofu, badala yake alisogea mlangoni na kumwita kwa jina lake 

    Aliita kwa dakika mbili za bila kupokelewa, kisha aliilaza basikeli chini, akazunguka  nyuma ya nyumba akiamini huwenda alikua huko. Alipofika nyuma alikutana na habari  mpya ya kuipeleka kwa Mzee kova. Mganga Mtimbe alikua akining’inia kwenye kamba  juu ya Mti mkubwa ulio nyuma ya nyumba yake karibu na choo. 

    Moyo wa Mlinzi ulianza kumwenda mbio akiutazama mwili wa Mtimbe aliyejinyonga  huku Mkononi akiwa ameshikilia kipande kikubwa cha karatasi. 

    Akili na hisia ya Mlinzi vyote vilikubaliana kua asogee hapo kuangalia zaidi, aliangaza  huku na kule, hapakuonekana kua na dalili ya ujio wa Mtu yeyote yule. Basi, mlinzi  alisogea taratibu hadi alipoufikia mwili huo. 

    Macho yake aliyapeleka usoni kwa Mtimbe, povu lilikua likimtoka huku macho yake  yakiwa yamemtoka pia. Aligeuza shingo yake haraka kutazama pembeni huku hali ya  kichefu chefu ikianza kumshika. Mlinzi akahisi hali ya kutaka kutapika, lakini shahuku  yake kubwa ilikua ni kuchukua ile karatasi aliyoishika Mtimbe. 

    Haraka aliivuta kisha alitoka ‘nduki’ kurudi alipokua ameiacha Baiskeli yake. Alipofika  hapo alianza kutapika, alishangaa kuona alikua akitapika damu. Hali ya kumwogofya  ilizidi kuongezeka, alikua akihema sana. 

    Akaona ni bora aangalie kilichoandikwa kwenye karatasi hiyo aliyoichukua kwa Mtimbe,  alikutana na maandishi Yaliyoandikwa kwa wino mwekundu, yakisema 

    “MWISHO UMEFIKA” , alitulia kiasi akiwa amesimama huku akihisi kuna jambo lilikua  likifanyika mwilini mwake. Mlinzi huyo, alihisi eneo la sikio, kisha puani. Alipopeleka  kidole alikutana na damu nyeusi iliyokua ikitoka kwa mabonge mabonge. 

    Hali ya hofu ilianza kumzidia Mlinzi, alihisi hali ya kuchanganikiwa akajikuta akipiga  yowe huku akikimbia kurejea nyumbani kwa Mzee Kova kupeleka taarifa ngumu.  Hakukumbuka kuhusu baiskeli yake, mkononi alishikilia karatasi. Alikimbia sana kiasi  kwamba alihisi kuchoka, kila aliyemwona alimshangaa sana. 

    Alipofika njia panda ya kuelekea nyumbani kwa Mzee Kova alianguka. Mahali hapo  palikua na Watu wawili, Mke na Mume waliokua wamebeba kuni kichwani. Waliona ni  bora wampe msaada, haraka walimkimbilia, walipomfikia walimkuta akiwa amepoa  kabisa. 

    Mume alimtazama Mke wake kwa Mshangao, wote walitazamana huku wakigeuza  macho yao na kumtazama mlinzi aliyekua amelala kifudi fudi akiwa ameificha sura yake. 

    “Tumsaidie?” aliuliza Mume, Mke alimtazama Mume wake kisha akatikisa kichwa  kuashiria kua wamsaidie. Taratibu, Mume alimgeuza Mlinzi. Aliona namna ambavyo  damu ilikua imetapakaa usoni, wote kwa pamoja waliiona karatasi ambayo yule Mlinzi  alikua ameishikilia 

    Mara moja yule Mume aliichukua ile karatasi na kuanza kuisoma, akakutana na neno  lile lile “ MWISHO UMEFIKA’’ 

    Baada ya kuisoma ile karatasi alijikuta akitafakari bila kusema chochote kisha  akamtazama Mke wake ambaye aliingiwa na wasiwasi kutokana na ukimya wa Mume  wake. 

    “Mbona upo kimya, umekutana na nini?” aliuliza yule Mke huku uso wake ukiwa  umejawa na Mshangao Mkubwa sana. Mume wake akampatia ile karatasi Mke wake bila  kusema chochote kile huku akimtazama yule Mlinzi aliyelala chini akiwa hapumui. 

    Mke alipoisoma ile karatasi aligeuza macho kumtazama Mume wake kisha kwa  mshangao akamwambia 

    “Mume wangu unatokwa na Damu puani” alisema akiwa anarudi nyuma taratibu,  Mume wake akapeleka kidole puani. Alikua akitetemeka akikiangalia kidole chake  kilichotapakaa damu. Kisha alimtazama Mke wake, aliiyona damu pia puani kwa Mke 

    wake. Akamnyooshea kidole kumwambia kua anatokwa na damu, naye Mke alipopeleka  kidole puani aliiyona damu mbichi. 

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Hapa Hapa Kijiweni

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    riwaya mpya riwaya za bure riwaya za kuvutia soma riwaya bure

    14 Comments

    1. VERONICA on July 14, 2025 3:00 pm

      Duh! Mpaka nimeogopa

      Reply
    2. LUCCAH ☺️ on July 14, 2025 3:05 pm

      Yaan Ukis0ma karatasi t umekwish😅💔🙌

      Reply
    3. Tomson on July 14, 2025 3:07 pm

      Aiseee mzigo ni wa moto ila fupi jmn

      Reply
    4. Dory on July 14, 2025 3:09 pm

      Mh mbona inafanana copyright n mobie ya kizungu inaitwa witch revenge kila kitu we umebdlish kdg san il hayo damu karts na vingn ving vinafanana na hyo movie

      Reply
    5. Moussa Camara on July 14, 2025 4:18 pm

      This is so funny…. The end is coming 😁😁

      Reply
    6. Jeremy443 on July 14, 2025 8:13 pm

      Drive sales and watch your affiliate earnings soar! https://shorturl.fm/ruwJK

      Reply
    7. Jesse4418 on July 14, 2025 8:40 pm

      Join our affiliate community and start earning instantly! https://shorturl.fm/DR071

      Reply
    8. Claire4015 on July 14, 2025 9:56 pm

      Partner with us and enjoy recurring commission payouts! https://shorturl.fm/2WDAH

      Reply
    9. Jenny887 on July 15, 2025 3:07 pm

      Promote our products—get paid for every sale you generate! https://shorturl.fm/221q4

      Reply
    10. Makayla4211 on July 15, 2025 4:12 pm

      Promote our products—get paid for every sale you generate! https://shorturl.fm/221q4

      Reply
    11. Wade3849 on July 16, 2025 4:40 am

      Tap into unlimited earnings—sign up for our affiliate program! https://shorturl.fm/jFw9m

      Reply
    12. Stella4510 on July 16, 2025 7:45 am

      Share our products and watch your earnings grow—join our affiliate program! https://shorturl.fm/0wkCq

      Reply
    13. ✒ Reminder: TRANSFER 1,430506 BTC. Continue >> https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=7e2e84890911207e0cf465ec1e25601f& ✒ on July 16, 2025 8:51 am

      9jzmxm

      Reply
    14. Luca886 on July 16, 2025 6:00 pm

      Your audience, your profits—become an affiliate today! https://shorturl.fm/U7xCc

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 15, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya tatu Mke alipoisoma ile karatasi aligeuza macho kumtazama Mume…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.