Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nne
“Na siku zote Muuwaji hawezi kuishi, ndiyo maana nilikutoaย gerezani ili uje kuitafuta haki iliyoporwa na Faudhia”ย Alikazia Mzee Shomari kisha alimruhusu Diana kuelekea ndaniย ya Benki, mpango wa Mzee Shomari ulikuwa ni Kumuuwa Faudhia,ย kisha kuiba pesa za kimarekani ambazo zilihifadhiwa ndani yaย Benki hiyo katika chemba ya siri, ilikuwa ni zaidi ya Dolaย Bilioni 900 , alimtumia Chogo kama ngao ya kufanya mambo yakeย huku akiweka ubia na rafiki yake wa zamani ambaye alikuwaย akiishi Uholanzi, ndiye aliyemtoa jela na kumfadhili pesa zaย kufanya ugaidi Tanzania, hivyo Mzee Shomari alikuwa ndiyeย Gaidi aliyekuwa akiratibu mipango yote, alikusanya vijana naย kuwapatia silaha nzito, akiwemo Diana na Martin Gimbo maarufuย kama Chogoย
Jinsi alivyowapata Diana na Chogo utakuja kufahamu mbele,ย hebu tosonge..ย
Usiku ulikuwa umeingia, ndani ya Jiji la Arusha, Faudhiaย alikuwa akimlaumu Mohd kwa kosa la Kumuuwa Mama yake naย Martin Gimbo.
SEHEMU YA TANO
“Hakukuwa na sababu ya kuuwa Watu wasio na hatia Mohd, umeuwaย Mwalimu, umeuwa Bibi na Mjukuu wake” Alisema Faudhia kwaย hasira sanaย
“Unanilaumu kwa kutekeleza mipango yangu ya kazi? Unanilaumuย kwa kusafiaha ushahidi wa mwote tulimopita? Faudhia wewe siyoย Mfanyakazi wa kanisa au msikiti, wewe ni askari wa siri waย kitengo cha Usalama wa Taifa! Sisi tunauwa kwa ajili yaย Taifa” Alijitetea Mohdย
“Unauwa kwa ajili ya usalama wa Taifa? Taifa lipi? Kuuwa Watuย wasio na hatia ndio majukumu ya Usalama wa Taifa? Pengineย umeelewa vibaya mafunzo uliyoyapata, siwezi kuendelea kufanyaย kazi na wewe Mohd” Alisema Faudhia kisha alipiga simu kwaย Mzee Shayo akamwambia ambadilishie Mtu wa kufanya naye kaziย
“Kwanini unataka abadilishwe?” Alihoji Mzee Shayo kwa njia yaย simuย
“Sijisikii uhuru wa kuifanya kazi yangu” Alisema Faudhia hukuย akiwa anamtazama Mohd ambaye alikuwa na hasira sana akiwaย ameketi kwenye kiti
“Faudhia Mwanangu..” kabla hata hajamaliza alikatiswa naย Faudhiaย
“Baba nimesema nibadilishie huyu Mtu” Alisema kwa hasira naย sauti ya juu kuonesha msisitizo kuwa alikuwa akimaanishaย alichokisema na hakikuwa utani.ย
“Mpe simu Mohd,” mara moja Mohd alipewa simu na Faudhia,ย kabla hajaongea na Mzee Shayo alimtazma sana kwa hasiraย Faudhia.ย
“Natoa amri ya wewe kurudi Makao Makuu haraka sana” Alisemaย Mzee Shayoย
“Lakini Mkuu..” kabla Mohd hajamaliza kujitetea alikatishwaย na Mzee Shayoย
“Hakuna cha Lakini Mohd, rudi Makao makuu” Alisistiza Mzeeย Shayo, mara moja Mohd alimtupia simu Faudhia kisha alichukuaย koti lake akatoka chumbani hapo lakini kwa bahati mbayaย alikuwa amesahau simu yake ambayo ilikuwa kwenye kochi,ย kitendo cha Mohd kutoka ndani ya chumba hicho, simu yakeย ilianza kuita, Faudhia alinyanyuka na kuangalia aliyekuwaย akipigaย
Aliona namba imeandikwa Boss, alifikiria afanye kitu ganiย aipokee au aiache iendelee kuita hadi ikate, aliichukua naย kuchungulia dirishani, alimuona Mohd akilielekea gari lakeย kwa ajili ya kuondoka, aliona ni bora aipokee simu hiyoย sababu alimtilia sana Mashaka kuwa huenda akawa sio Mtu mzuriย kutokana na mauwaji ya Watu wasio na hatia ambayo alikuwaย akiyafanya.ย
“Mohd! Muuwe Faudhia sasa hivi kisha urudi hapa” Ilisikikaย sauti ambayo Faudhia aliitambua, ilikuwa ni sauti ya kizee yaย Mzee Shomari, mara moja aligundua kuwa Mohd alikuwa ni askariย aliyekuwa akifanya kazi na magaidi, akatambuwa kuwaย kilichobakia kwake ni kifo pekee. Alipochungulia tenaย alimuona Mohd akiwa anapiga hatua kurudi ndani baada yaย kugundua kuwa amesahau simu yake, Faudhia alimtazama vizuriย Mohd akiwa bado amesimama pale pale, Mohd alikifikia kitasaย cha mlango bila kujuwa kuwa Faudhia alikuwa amemshtukia kuwaย ni Mamluki anayekisaliti kitengo cha Usalama wa Taifa.ย
Alipofungua mlango alimkuta Faudhia akiwa amesimama, Unajuwaย Mohd alikuwa ni askari wa kitengo cha Usalama wa Taifa hivyoย alipoingia tu aligundua kuwa kuna jambo ambalo halikuwa sawa,ย alimtazama sana Faudhia akiwa ameganda pale mlangoni,ย walikutanisha macho yao ya Kijasusi huku kila mmoja akiwaย anamsoma mwenzake.
Mara simu ya Mohd iliita tena na mpigaji alikuwa ni yule yuleย Mzee Shomari, aliisikilizia kidogo kisha aliifuata simuย lakini kabla hajapokea Faudhia alimnyooshea Mohd Bastolaย
“Tulia hivyo hivyo Msaliti wewe, kumbe wewe ni mamlukiย unayefanya kazi na Mzee Shomari? Nilikuwa nakutilia mashakaย sana Mohd” Alisema Faudhia, Mohd alikuwa amesimama huku simuย ikiendelea kuita mkononi mwakeย
“Isogeze hiyo simu kwangu” Alisema tena Faudhia hukuย akihakikisha kuwa Mohd hachomoki wala hafanyi ujanja wa ainaย yoyote ile. Mohd alimtazama Faudhia kisha alimsoma jinsiย alivyokuwa amesimama ila Faudhia alishtuka mapema kuwa Mohdย anamsoma kisha akamwambia.ย
“Ujanja wowote utakaoufanya Mohd napasua kichwa chako”ย Alisema Faudhia, Mohd aliinama kidogo kisha aliiburuza simuย ikafika kwenye miguu ya Faudhiaย
“Umeanza kutumika upande huo kwa muda gani?” Aliuliza Faudhiaย huku akizuga ili ainame aichukue simuย
“Faudhia! Usifikiri kamwe naweza nikasema chochote au hiiย siri ikafika makao makuu, katu kitengo hakita ifahamu hiiย siri” Alisema Mohd kwa kujiamini kisha alishusha mikono yakeย akamwambia Faudhiaย
“Si ulikuwa unataka kunitwanga risasi? Fanya hivyo kablaย sijakuwahi” Alisema maneno yaliyojaa ulaghai Mkubwa, ilikuwaย ngumu kwa Faudhia kumuuwa Mohd, alichotaka ni kufikishaย taarifa kwenye kitengo cha Usalama wa Taifa.ย
Mohd alianza kumsogelea Faudhia taratbu huku akizidi kuongeaย maneno ambayo yalimchanganya Faudhiaย
“Wewe ndiyo sababu ya Mama yako kufa, hukustahili kubaki haiย kwa uchafu ambao ulikuwa ukimfanyia Mama yako, laiti kamaย taarifa hizi zitavuja ndani ya kitengo basi hautokuwa na sifaย ya kuwa Undercover!! Mtu ambaye amemsaliti Mama yake kwa Babaย yake anaweza vipi kutunza siri za Nchi hii” Alisema Mohd hukuย akizidi kusogea, Maneno ya Mohd yalimtia uchungu sanaย Faudhia, ni kama alitoneshwa kidonda kilichoanza kukaukaย
“Acha Mohd! Achaaaaa” Alisema Faudhia kisha aliweka kidoleย sehemu ya kufyatulia risasi ili ammalize Mohd, haraka Mohdย alimuwahi Fadhia na kuushika mkono ambao ulikuwa na Bastola,ย Faudhia alipofyatua risasi zote zilipiga juu ya dali. Mohdย alimkunja Faudhia na kumpa mateke matatu ya Mbavu kabla yaย Faudhia kujikunjua
Bastola ilikuwa chini, aliponyanyuka Faudhia alijikuta akiwaย mikono mitupuย
“Nilikwambia hii siri haiwezi kufika kitengo cha Uslama waย Taifa, kwakuwa nimepigiwa simu nirudi Makao makuu basi weweย utaonekana umeuawa kwa kuvamiwa hapa Hotelini.” Alisema Mohdย huku akiwa anakunja Shati lake, alikuwa ni mwanaume mwenyeย mazoezi na roho ya kikatili sana.ย
“Mradi wa kukutengeneza wewe uje kuwa Askari wa kitengoย unafia hapa rasmi” Alisema Mohd kisha alimfuata Faudhiaย ambaye alikuwa amejiandaa kukabiliana naye, alirusha ngumiย mfululizo ambazo zote Faudhia alizikwepa lakini alifanyaย ujanja wakati anamaliza kurusha ngumi ya mwisho alikunjuaย Mguu wa kulia na kumpiga teke la tumbo Faudhia, alijikutaย akianguka chini kisha alijinyanyua na kupanga pambano upya.ย
Wote walikuwa na mafunzo ya Kijeshi hivyo kila mmoja alijuwaย namna ya kupambana, Faudhia alijibu mapigo kwa kumpa matekeย mawili yaliyofika hadi kwenye kifua cha Mohd, alisogezwaย pembeni karibu na mlango ambapo kochi lipo, aliangalia chiniย kulikuwa na Bastola, pembeni kulikuwa na simu yake yenye siriย nzito, aliona ni bora afanye ujanja.ย
Aliokota mto wa kochi kisha alimtupia Faudhia usomi kishaย aliinama ili aichukue bastola lakini Faudhia alikuwa shapu,ย kabla hajaokota Bastola alipigwa teke la Mgongo kisha Faudhiaย akaipiga teke ile simu na Bastola vikaingia uvunguni mwaย Kochi, alimlazimisha Mohd apambane kwanza.ย
Mohd aliinuka na kunvaa Faudhia, aliambulia kutupwa chiniย kutokana na namna Faudhia alivyo Shapu. Kabla hajakaa sawaย alipokea ngumi la shingo ambalo lilimsogeza kwenye kochi,ย kabla hajatulia tena Faudhia alimpelekea Mohd teke ambaloย Mohd alilidaka kisha alitumia nguvu kubwa alimsukuma Faudhiaย ambaye aliangukia kwenye mezaย
“Assssh” aligumia Faudhia kutokana na maumivu ya kujigongaย kwenye meza, Mohd hakutaka kusubiri alimrushia ngumiย mfululizo, ngumi ambazo zilimpekeka Fuadhia ukutani, bahatiย mbaya ngumi nyingi zilimpata na kumfanya aumie usoniย
Mohd alimpiga Faudhia mateke mfululizo eneo la mbavu hukuย akimwambiaย
“Unakufa leo” Alisema huku akiwa anamuangalia Faudhia akiwaย anaanguka chini.
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA SITA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
13 Comments
Mbona fupi sana jamani
Imeishia patamuu
mbna fupi hvo mzee
Bado mda huko adm, rusha sehemu ya sita. Hii tamu sana kabisa.
Good ๐๐
Admn Ahsante Kwa Story Nzuri Saanaa Hii
Fupi inakera
Fupi innboa sana jmn ….kama utaki acha tu kutuma
Admin hapa umezingua….
Stori ni fupi mnooooo ๐ฏ๐ฏ๐ฏ
Admini hauna vitabu tununue tu
8qqlk0
3z4675
urf8ny