Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Saba-07)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Sita-06)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tano-05)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tano-05)
    Hadithi

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tano-05)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 16, 2025Updated:May 16, 20258 Comments7 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya NneΒ 

    “Lengo la kuja huku ni kumpa taarifa Mama lakini hatuweziΒ  kuondoka bila yeye kiridhia, Veronica mpenzi tuvumilie tuΒ  hadi pale hasira zake zitakapoisha”Β 

    “Kwanini Mama ananifanyia hivi mimi, kama hakunizaa yeye?”Β  nilijiuliza baada ya kukumbuka tukio la kubakwa na Anko SangaΒ  ambapo Kwa maelezo ya Mama ilionesha kuwa alikuwa akijua kilaΒ  kitu . EndeleaΒ 

    SEHEMU YA TANO

    “Usiseme hivyo Veronica, Mama amechukia tu kwasababu taarifaΒ  hii siyo njema kwa Mzazi yeyote yule….fikiria ingelikuwa niΒ  wewe ndio Mzazi unamsomesha Mtoto kwa gharama kubwa alafuΒ  anaishia kupata mimba? Inaumiza ndio maana nakwambiaΒ  tusiondoke hadi tupate radhi zake” Yalikuwa ni maneno yaΒ  Jonas yaliyojaa busara na hekimaΒ 

    “Nifanye kuwa Mkeo Jonas”Β 

    “Wewe tayari ni Mke wangu, tusubirie tu baraka za Mama yako”Β  Kutokana na maneno mazuri ya Jonas nilijikuta nikitakaΒ  kumwambia ukweli kuhusu kukeketwa lakini nikaona sio mudaΒ  sahihi.Β 

    Ulipita mwezi mmoja Mama hakuonekana nyumbani na simu yakeΒ  ikawa haipatikani, hofu ilianza kuniingia nikahisi labdaΒ  amepatwa na tatizo. Nilimfuata yule jirani aliyenipa taarifaΒ  kuwa Mama alichukuliwa na gari ndogo ile siku, nilichotakaΒ  kujua ni nani alimchukuaΒ 

    “Jirani samahani, ni mwezi sasa Mama haonekani mpaka naanzaΒ  kuingiwa na wasiwasi”Β 

    Nilimwambia baada ya kinipa nafasi ya kuzungumza nae “Ina maana tokea siku ile hadi leo hajarudi?”Β 

    “Ndio Jirani napata mashaka ni wapi alipo, hivi umemtambuaΒ  aliyekuja kumchukua hapa?” Jirani alionekana kutafakari kablaΒ  ya kunijibu ni wazi alikuwa akimtambuaΒ 

    “Sura yake sio ngeni sana”Β 

    “Anaonekanaje”Β 

    “Mweusi, sijui kuhusu urefu sababu alikuwa ndani ya gari” “Itakuwa Anko Sanga huyo”Β 

    Nilimuonesha picha ya Anko Sanga kupitia simu yangu iliΒ  amtambue kama ni yeye au ni Mtu mwingineΒ 

    “Eeeh! ni huyu hapa, hata hivyo hupaswi kuwa na wasiwasi sanaΒ  kwasababu huyu alikuwa akija hapa mara kwa mara, amesimamiaΒ  ukarabati wa nyumba yenu mpaka ulipoisha”Β 

    “Oooopsss” Nilivuta pumzi na kuzitoaΒ 

    “Ahsante sana jirani”

    Uvumilivu wa kuendelea kumsubiria Mama ulinishindaΒ  nikamueleza Jonas kuwa nimechoka ikiwezekana tuondoke, mimbaΒ  ilifikia miezi minne, hata upande wa Jonas vivyo hivyoΒ  alianza kuchoka licha ya ujasiri wake wa kila siku kusemaΒ  tuendelee kumsubiria.Β 

    Tulikusanya mabegi yetu ili tuondoke, tulipofika mlangoniΒ  tulisikia Mlio wa gari, nilipochungulia nilimuona Mama akiwaΒ  anashuka kwenye gari ya Anko Sanga.Β 

    Tukayarudisha yale mabegi kusudi asijue kama tulikusudiaΒ  kuondoka. wote waliingia ndani na kutukuta tumekaa paleΒ  sebleni. Anko Sanga alitusalimia na kuketi pamoja na sisiΒ  lakini Mama alipita zake na kuingia chumbani kwakeΒ 

    “Hivi Mama yangu amepatwa na nini?” nilimuuliza Anko SangaΒ  maana ndiye aliyekuwa karibu zaidi na MamaΒ 

    “Sijui nikuulize wewe Veronica umemfanya nini Mama yako?”Β 

    “Mimi Anko Sanga? Mama simuelewi naona ameninunia tu,Β  ameondoka bila kusema anaenda wapi!”Β 

    “Mama yako amechukizwa na ulichokifanya unapaswa kumuombaΒ  sana msamaha Veronica, amekupigania sana lakini umemlipaΒ  asichostahili”Β 

    “Anko! makosa hayarekebishwi kwa hasira bali busara zilizoΒ  njema lakini kwa staili hii hapa anajenga au anabomoa?”Β  alidakia JonasΒ 

    “Kijana hata Kama ungelikuwa wewe ndio Mzazi wa Veronica kwaΒ  kilichotokea ungelitumia busara gani? Tunu ya Mama ni kuonaΒ  Mtoto anafikia malengo aliyoyaweka Mzazi sasa kama MtotoΒ  anafikia hatua ya kuharibu Maisha yake, Unafikiria MzaziΒ  atakuwa kwenye wakati gani?”Β 

    “Imeshatokea na tumekiri Makosa, kinachotakiwa Kama MzaziΒ  akubali kuwa Maji yameshamwagika, tuangalie kinachofuataΒ  baada ya hapa….Ujauzito wake unakaribia miezi mitano,Β  tukiendelea hivi atakonda kwa mawazo” Alisema tena Jonas,Β  Dhahiri nilimuona Anko Sanga akimtazama kwa jicho la ubayaΒ  Jonas.Β 

    Alikuwa akimtazama kama Mwanaume wangu au adui aliyekatizaΒ  ndoto zangu? Mbona yeye aliutumia mwili wangu kwa stareheΒ  zake tena akishirikiana na Mama yangu Mzazi? NilijiulizaΒ  nikiendelea kumtazama

    “Chakufanya hapa ni nyie kuongea na Mama Veronica, hakunaΒ  njia nyingine” Alisema kikaksi akafunga mazungumzoΒ 

    “Anko Sanga…kama hatufikii makubaliano hapa nitaondoka,Β  nitakuwa tayari kuishi bila baraka zenu”Β 

    Yalikuwa ndio maamuzi yangu na sikutaka Mtu anipinge, hataΒ  nilipoongea na Mama nilimwambia hivyo hivyo ndipo nilipomuonaΒ  akianza kulegeza hasira zakeΒ 

    “Kwahiyo unataka nifanye nini?” Aliniuliza baada ya kunisikiaΒ  nilikuwa tayari kufanya maamuzi yangu binafsiΒ 

    “Kubali niolewe na Jonas”Β 

    “Unataka awe Mumeo?”Β 

    “Ndio Mama, hata ukisema hapana sitarudi nyuma. Mtoto aliyeΒ  tumboni anatakiwa kulelewa na Baba yake Mzazi” Mama hakuwa naΒ  Jinsi alikubali nifunge ndoa na Jonas, ruhusa ilienda sawa naΒ  mipango ya haraka. Hatimaye tulifunga ndoa Arusha kwenye lileΒ  Kanisa nililokiwa nikisali siku zote.Β 

    Tukarudi Dar tukiwa Mke na Mume Maisha ya ndoa yalianza naΒ  furaha iliyatawala maisha yetu, tukaenda kuishi Mbezi na hukuΒ  ndiko nilikokutana na Mama Sofia, alikuwa jirani yetu sikuΒ  moja alinisaidia nilipokuwa najisikia vibaya ndio ukawaΒ  mwanzo wa kufahamiana kwetu.Β 

    Tulijenga urafiki na huyu Mama mfanya biashara, alitokeaΒ  kunipenda mno kwa jinsi nilivyokuwa na moyo wa ujasiri naΒ  kujali,Β 

    “Jonas Mkeo ni Mtu wa pekee sana, ana moyo wa dhahabu”Β  Alisema Mama Sofia, nikaona nimueleze kuwa nilikuwaΒ  nimekeketwa na jambo hili lilikuwa siri kwanguΒ 

    “Mume wako anajua?”Β 

    “Hapana nimemficha kwa kitambo sasa”Β 

    “Hupaswi kumficha, atajua tu ni vema ukamueleza” “Nahofia ataniacha Mama Sofia”Β 

    “Usikubali roho ya uwoga ikutawale Veronica, mueleze ajue”Β  Alinishauri hivyo, jinsi ya kumueleza Jonas ilikuwa ngumuΒ  sana.

    Kila alipotaka kusex na mimi nilimwambia nasikia maumivu yaΒ  tumbo, kwakuwa nilikuwa mjamzito ilimfanya anihurumie japoΒ  niliona kama alikuwa anakosa raha.Β 

    Tulikaa miezi mitano bila kufanya mapenzi, mara ya mwishoΒ  ilikuwa wakati tuko Chuo ambapo nilikuwa nahakikisha tumelewaΒ  ndipo tunafanya hata hivyo alinikataza kutumia kilevi baadaΒ  ya kuwa Mjamzito.Β 

    Nilijua tu ipo siku atajua lakini nilijipa muda ili akijuaΒ  niwe nimejitayarisha kwa kila kitu, Nilipoanza KlinikiΒ  daktari aligundua hili jambo na kibaya zaidi alikuwa niΒ  rafiki wa JonasΒ 

    “Shem kumbe umekeketwa?” aliniuliza akiwa ananifanyia vipimoΒ  kadhaa ikiwemo Ultra Sound ili kugundua Mtoto amekaaje naΒ  jinsia yake.Β 

    “Ndio Shem” nilimjibu kwa wasiwasiΒ 

    “Mh!”Β 

    “Mbona unaguna?”Β 

    “Hapana” Nilijua tu atamwambia Jonas lile jambo,Β 

    “Najua umeshtuka sana lakini ndio ukweli huo, Jonas hajuiΒ  hili jambo nakuomba usimueleze nitakaa naye chini nitaongeaΒ  nae” Hakunijibu, aliendelea na vipimoΒ 

    Suala lile lilizidi kunipa mawazo sana na kunifanya nikumbukeΒ  zamani nilipokeketwa, Mama ndiye aliyenilazimisha kufanyiwaΒ  vile akisema ni mila zao na kama nitakataa nitatengwa.Β 

    Mimba ilipofika miezi 6, yule Daktari alinipigia simu naΒ  kunitaka niende tena Hospitali, baada ya kumaliza vipimoΒ  aliniulizaΒ 

    “Umeshaongea na Mumeo?”Β 

    “Hapana sijaongea naye, nitaongea naye siku za hivi karibuni”Β 

    “Ina maana hamkutani kimwili? ilikuwaje asilijuwe hiliΒ  jambo?”Β 

    “Ni stori ndefu sana Dokta”Β 

    “Kuwa makini sana hili jambo halipaswi kuwa siri kabisa,Β  mueleze ukweli” Alinipa tena mtihani wa kuongea na Jonas,

    Nilipanga nizungumze naye niliporudi, kabla hata sijaongeaΒ  naye Mama alinipigia simu na kunitaka niende Arusha, nilianzaΒ  kumkatalia sababu alisema niende mwenyeweΒ 

    “Nenda Veronica” Jonas alisemaΒ 

    “Naendaje bila wewe Mume wangu?”Β 

    “Kitakachojiri huko utaniambia”Β 

    Moyo wangu ulisita sana kelekea Arusha tena bila Jonas, MamaΒ  yangu nilianza kutomuelewa kwa kauli zake tata kilaΒ  alipozungumza na mimi.Β 

    Sikuwa na budi bali kuondoka na kwenda Arusha kuitikia witoΒ  wa Mama. Mimba ilifika miezi 7 kasoro, Mama alitaka nikaeΒ  Arusha hadi nitakapo JifunguaΒ 

    “Mama hilo halitawezekana, nitajifungua vipi bila JonasΒ  kuwepo?”Β 

    “Veronica usiwe mbishi, unatakiwa kujifungua kwa mila naΒ  tamaduni za kabila letu” Alisema Mama kwa msistizo,Β  nikakumbuka maneno ya daktari kuwa nilikuwa nina ujauzito waΒ  Mtoto wa Kike, hofu ya mtoto wangu kufanyiwa kamaΒ  nilivyofanyiwa ilinijia nikamwambia MamaΒ 

    “Mtoto wangu hawezi kufanyiwa kama mlivyonifanyia mimi” “Unamaanisha nini?”Β 

    “Hawezi kukeketwa kama mnavyotaka”Β 

    “Nani amekwambia tunataka kumkeketa Mtoto wako? na kama niΒ  wakike ni lazima afanyiwe hivyo Veronica”Β 

    “Sitakubali Mama, nitapingana na wewe hadi naingia kuburini”Β 

    “Anhaa! Huyo Jonas anakupa kiburi sana, tutaona” Alisema MamaΒ  kisha alicheka na kujifanya ameongea utani ila kwa akiliΒ  zangu na jinsi nilivyomtafsiri niligundua kuwa alimaanishaΒ  alichokisema.Β 

    Nilijawa na hofu kila nilipomfikiria Mwanangu, Yule jiraniΒ  alinifuata na kunipongeza kutokana na ujauzito wanguΒ 

    “Ahsante Jirani, ndio ukubwa huu”Β 

    “Lakini Veronica unatakiwa kuwa makini sana na Mama yako!”

    “Kwanini?”Β 

    “Mama yako ana sifa mbaya hapa mtaani, inasemekana yeye naΒ  Kaka yake wanashiriki ushirikina”Β 

    “Unamaanisha Mama yangu ni Mchawi?”Β 

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β 

    riwaya mpya riwaya za kusisimua riwaya za kusoma mtandaoni

    8 Comments

    1. Lus twaxie on May 16, 2025 3:48 pm

      Huyu veronica nae kama hana akili….anapekekeshwa sna an mamake

      Reply
      • Maestro05 on May 16, 2025 4:48 pm

        Hii kaliiπŸ”₯πŸ”₯ kesho zitoke mbili Admin.😜

        Reply
        • Gervase on May 16, 2025 9:37 pm

          Aah hiki kipande ni. Shidaa,, admin tunaomba utuwahishie mwendelezo kwa wakati πŸ™

          Reply
    2. Adam on May 16, 2025 9:38 pm

      Kesho Fanya Utoa Double Mr Admin

      Reply
    3. Gervase on May 16, 2025 9:39 pm

      Aah hiki kipande ni. Shidaa,, admin tunaomba utuwahishie mwendelezo kwa wakati πŸ™

      Reply
    4. Imma on May 16, 2025 10:10 pm

      Unachelewa Kutuma mwendelezo

      Reply
    5. Cathbert on May 17, 2025 5:22 pm

      Mzuri

      Reply
    6. πŸ”’ Notification; TRANSACTION 1.727294 BTC. Receive > https://yandex.com/poll/7HqNsFACc4dya6qN3zJ4f5?hs=3e7b2bc4f52f0a08fd37b64428d57f32& πŸ”’ on May 19, 2025 12:13 pm

      mu34jk

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi May 19, 2025

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Saba-07)

    Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Saba Ile simu ilikuwa ndogo tu yaani ya…

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Sita-06)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tano-05)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Nne-04)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.