Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 12

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Kwanza-01)
    Hadithi

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Kwanza-01)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 12, 2025Updated:May 23, 202512 Comments9 Mins Read7K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Niliomba niletewe Binti yangu pale Gerezani, Mama SofiaΒ  alimleta Moyo. Nilimkumbatia Mwanangu hadi nikahisi farajaΒ  iliyo pitiliza.Β 

    “Umeongea na Wakili vizuri?” aliniuliza Mama Sofia,Β  nilimtazama na kumwambiaΒ 

    “Ndio”Β 

    “Matumaini yangu utakuwa huru Veronica” Alisema, MudaΒ  ulipoisha Mama Sofia aliondoka na binti yangu aliyeitwa Moyo.Β 

    Nilibakia pale kwenye kiza, Maaskari walinichukua naΒ  kunirudisha kwenye chumba changu! Nilikuwa nikiishi kwenyeΒ  chumba cha peke yangu kutokana na kesi ya mauwaji iliyokuwaΒ  ikinikabili, Moyoni nilijisema kuwaΒ 

    “Sipaswi kuwa huru” niliketi kwenye pembe ya kile chumbaΒ  kilichojaa wadudu wadogo wadogo, chini kulikuwa na majiΒ  yaliyomwagika, niliyamwaga mwenyewe kwasababu sikupenda kula.Β  Kuna wakati niliwahi kumwambia Askari aliyekuwa akinihudumiaΒ  kuwaΒ 

    “Niletee sumu nife, sipendi kuendelea kukaa hapa”Β 

    “Veronica, Bado hii kesi ni mbichi sana. Subiria hukumu yakoΒ  , Kama Mahakama ikikukuta hauna hatia? unataka kufa ili bintiΒ  yako alie kwa uchungu?” aliniulizaΒ 

    “Usiwaze kufa, hakuna anayeijua kesho yako” alisema naΒ  kuondoka zake.Β 

    Sikuona umuhimu wa kuendelea kuwa hai tena nikiwa paleΒ  gerezani kama Mahabusu niliyekuwa nasubiria siku ya hukumu yaΒ  kesi yangu ya Mauwaji

    “Ni kweli umemuuwa Mama yako Mzazi?” yule Wakili alirudi tenaΒ  kuutaka ushahidi ili ajuwe namna ya kunitetea, Wakili huyuΒ  aliajiliwa na Mama Sofia ambaye alikuwa jirani yangu mwema,Β  alipenda kuniona nikishinda ile kesiΒ 

    “Nikikwambia nilimuuwa utaiambia nini Mahakama? UtaidanganyaΒ  kuwa sijauwa?”Β 

    “Ukiniambia ukweli nitajua jinsi ya kukuweka huru Veronica”Β 

    “Uhuru sio kitu ninachokitaka kwasasa, naitaka haki tu”Β  nilisema kisha nilikaa kimya sikutaka kuendelea kuzungumzaΒ  nae hadi Muda ulipoisha nilirudishwa tena kwenye kile chumba.Β 

    Yule Wakili alimpelekea taarifa Mama Sofia, Mama huyu alikuwaΒ  tajiri sana. Alikuwa jirani yangu kule Mbezi Luis nilipokuwaΒ  ninaishiΒ 

    “Ninavyomjuwa Veronica hawezi kumuuwa Mama yake Mzazi Jacob”Β  alisema akimuelekeza yule Wakili..Β 

    “Veronica ni mpole, mcheshi na mtaratibu sana…kusemaΒ  amemuuwa Mama yake hilo haliwezekani kabisa”Β 

    “Unafikiria nitafanya nini na hataki kuzungumza kabisa,Β  amekaa kimya?”Β 

    “Veronica sema ukweli, angalia ulivyodhohofu…Mwanao analiaΒ  na kukuulizia utarudi lini, hivi ni kweli hutaki kuishi tenaΒ  na binti yako Moyo?” Mama Sofia aliongea Baada yaΒ  kunitembelea, ni kweli nilikuwa nimekondeana sana, MwiliΒ  ulidhohofu mno, Afya yangu ilikuwa mbaya!Β 

    Mawazo yalipelekea nidhohofike namna ile, kingine niΒ  mazingira ya pale ambayo hayakuwa rafiki kabisa kwangu!Β 

    “Mahakama itatenda haki kwangu Mama Sofia, Mungu ndiyeΒ  anayejua kilichojificha” nilisema kwasababu sikupenda kabisaΒ  kuzungumzia jambo lile lililotikisa vichwa vya Watu wengiΒ  sana.Β 

    “Kwanini hutaki kusema kama kweli umeuwa au haujauwaΒ  Veronica?” Alihoji lakini sikumpa majibu kila alipokuja yeyeΒ  au Wakili wa ile kesi.Β 

    Tukio hili lilitokea Mwaka 2009, lilizua gumzo kubwa, hakunaΒ  aliyeamini kama kweli Nimemuuwa Mama yangu. Ni kweli nilikuwaΒ  nimemuuwa Mama yangu Mzazi na chanzo cha tukio hili alikuwaΒ  ni Mume wangu aliyitwa Jonas.

    Baada ya siku 21 nilirudishwa tena Mahakamani ili kusikilizaΒ  kesi yangu iliyojaza waandishi wa habari, kurasa zote zaΒ  Magazeti zilipambwa kwa picha yangu na maelezo juu ya tukioΒ  langu la Mauwaji.Β 

    Hakimu alinitazama kabla ya kuanza ile kesi, jicho lakeΒ  lilijaa huruma ambayo niliweza kuiona pindi nilipogongana naeΒ  macho, nilimuona akitoa kitambaa chake na kufuta choziΒ  lililokuwa likimbubujika. Mahakama ilizizima kusikilizaΒ  atasema nini, niliweza kuzisikia pumzi zangu nilipokuwaΒ  nikihema ilitokana na ukimya uliotawala pale Mahakamani.Β 

    Nilipotazama pembeni nilimuona Mwanangu Moyo, aliniangalia naΒ  kutabasamu na kunifanya na Mimi nitabasamu.Β 

    Kila Mtu alikuwa kimya, wengine wakinitazama Mimi na wengineΒ  wakiwa wanamtazama Hakimu aliyekuwa amejiinamia kwa zaidi yaΒ  dakika 10, sikujua alikuwa akifikiria nini.Β 

    “Veronica!” aliniita yule Hakimu mwenye umri mkubwa, alivuaΒ  miwani yake na kunitazama tenaΒ 

    “Abee!”Β 

    “Uko tayari kusema ukweli?” aliniuliza, nilikaa kimya kwaΒ  dakika moja kisha nilimpa jibuΒ 

    “Ndio”Β 

    “Ilikuwaje ukamuuwa Mama yako Mzazi?” alihoji tena,Β  nilimtazama Mama Sofia ambaye alinipa ishara niwe jasiriΒ  niseme.Β 

    Alitamani kusikia nikikanusha kuwa sijamuuwa Mama yangu, WatuΒ  wote wakawa bize kunitazama, waandishi wa Habari walitegaΒ  karamu zao kwenye karatasi ili wapate cha kuandika kwenyeΒ  Magazeti yao.Β 

    Nilianza kwa kigugumizi, pale pale chozi lilianzaΒ  kunibubujika, midomo yangu ilikuwa ikitetemekaΒ 

    “Nisamehe Mwanangu Moyo” nilisema huku nikiwa ninalia,Β  niliendeleaΒ 

    “Ni kweli nimemuuwa Mama yangu Mzazi” kauli hii iliwashtuaΒ  wengi, Hakimu alionekana kuvunjika moyo kabisa aliinamishaΒ  kichwa chake chini huku akijifuta Machozi.

    Nilianza kueleza kilichotokea, Naitwa Veronica Moyo, najuaΒ  wengi mmeshtushwa kusikia nimemuuwa Mama yangu, baada yaΒ  kueleza haya naomba Mahakama inihukumu kifo.Β 

    MIAKA MINGI KABLA YA TUKIOΒ 

    Nilipofika chuoni kusomea masuala ya Utalii nilikutana naΒ  Mwanaume aliyeitwa Jonas, nilitokea Kumpenda nae piaΒ  alinipenda sana lakini hofu yangu ilikuwa kwenye maumbileΒ  yangu, nilihofia kumwambia Jonas kuwa nimekeketwa na huoΒ  ukawa udhaifu wangu katika Maisha yangu.Β 

    Kila nilipo kumbuka juu ya kile kitendo cha kukeketwaΒ  nilijisikia vibaya sana lakini kwa kipindi chote hichoΒ  nilikuwa bado sijawahi kukutana na Mwanaume na kufanya naeΒ  mapenzi.Β 

    Jonas ni binadamu mwenye hisia kama Wanaume wengineΒ  alionekana kuanza kukata tamaa kila nilipompa visingizio kuwaΒ  nipo kwenye siku zangu, naogopa Mimba au tutafanya tukimalizaΒ  chuo.Β 

    Nilimsikia rafiki yangu aliyeitwa Konzo akisema kuwa naendaΒ  kumpoteza Jonas siku za usoni kwani hawezi kukaa bila kusexΒ  na mimiΒ 

    “Ooh! amekwambia hivyo?”Β 

    “Ndio, anataka kujua ni kwanini humpi tendo…Mwaka wa piliΒ  sasa”Β 

    “Sikia Konzo, naogopa Jonas atanikimbia akishakula tundaΒ  langu”Β 

    “Hofu yako haina msingi, haishawishi kabisa Veronica au weweΒ  ni msichana bado?” Aliniuliza, sikuwahi kumwambia kuwa mimiΒ  ni Bikra nikaona ni vema nimwambieΒ 

    “Ndio, mimi ni Bikra na sijawahi kushiriki tendo na Mwanaume” “Unasema kweli? Jonas anajua?”Β 

    “Hajui konzo na sitaki ajue kwasasa, acha iwe siri bainaΒ  yetu” Nilimueleza hivyo, kitendo cha kukeketwa kilinifanyaΒ  nikose kujiamini kwasababu niliwahi kusoma majarida kadhaaΒ  yanayozungumzia suala hilo kwa Wanaume, wengi wakisemaΒ  Wanaume hawapendi Wanawake waliokeketwa kwa madai kuwa sioΒ  Watamu.

    “Sawa nitaitunza Veronica na sitamwambia Mtu hapa Chuoni”Β  Alisema na kunifurahisha Konzo, siri ya kukeketwa ikabakiaΒ  kwenye nafsi yangu!Β 

    Nilipomwambia Mama yangu Mzazi aliniambia kuwa nikionaΒ  Mwanaume anasema hapendi Mwanamke aliyekeketwa basi MwanaumeΒ  huyo hajui nini maana ya Mapenzi wala radha ya tendo haijuiΒ  vizuriΒ 

    “Mama! mbona wataalam wanathibitisha kuwa kukeketwaΒ  kunamfanya Mwanamke akose radha halisi?”Β 

    “Mtaalam gani huyo anayeshindana na mababu wa Kabila letu?Β  Sayansi inakupoteza Mwanangu” Maneno ya Mama yaliniweka njiaΒ  panda kwa kipindi kirefu hasa baada ya kuvunja ungoΒ 

    Niliishi na Mawazo ya aina mbili, Sikujua nimfuate nani katiΒ  ya Mama yangu au Wataalam walioandika majarida yale. NikasemaΒ  ipo siku nitaujua ukweli ingawa sikutaka kumpoteza Jonas,Β  Mwanaume mzuri wa sura, alitokea kwenye maisha bora sana,Β  Mcheshi na mkarimu. Alinisaidia Mambo mengi sana tukiwaΒ  chuoni.Β 

    Alinipa robo ya pesa alizotumiwa na Wazazi wake wakati MamaΒ  yangu Mzazi akinihimiza kuishi kulingana na mazingira, hakuwaΒ  na uwezo wa kunisomeshaΒ 

    “Veronica Mwanangu! Nenda kasome huko lakini tambua kuwaΒ  Maisha ni magumu mno, nitakachopata nitakituma kwako naΒ  nikikosa ishi kulingana na mazingira” alisema Mama nikiwaΒ  ninaenda kujiunga na Chuo Jijini Dar kutokea Arusha.Β 

    “Sawa Mama! nitatimiza malengo yangu na ya kwako, nitaishiΒ  kama ulivyoniagiza” Jinsi alivyonilea ilikuwa ni rahisi sanaΒ  kukubaliana na hali zozote za kimaisha, Baba yanguΒ  alitutelekeza nikiwa mdogo, Kwa mujibu wa Mama alisema kuwaΒ  Baba alikimbia madeni yaliyokuwa yakimuandama.Β 

    Pale chuoni kwetu wengi walinifahamu, na msemo ulikuwaΒ  ukitamba sana ni ‘Tazama Pisi kali ya Arusha ile’ ulikuwa niΒ  msemo uliopendwa, nilikuwa mzuri, macho makubwa yakukonyeza,Β  shepu ilikuwa ya kawaida tu lakini ilitosha kunifanyaΒ  nikamilike sana, Mapedeshee waliokuja kutafuta WanawakeΒ  wazuri pale chuoni hawakuacha kunisumbua kila wakatiΒ  waliwatuma rafiki zangu akiwemo KonzoΒ 

    “Una bahati sana Veronica, mabosi wanakuulizia wewe tu”Β  alisema rafiki yangu Konzo, alinichekesha mno

    “Sasa Bahati au usumbufu? ni kheri wewe unaishi upendavyoΒ  kuliko mie ”Β 

    “Ningekuwa ndio wewe! ningeshapata gari maana Mabosi wakoΒ  tayari kukupatia upendacho” Nilitamani sana Maisha mazuriΒ  lakini ile siri ya kukeketwa niliogopa itasambaa pale chuoniΒ  ndio maana nilihakikisha namkataa kila aliyenitongoza.Β 

    “Huyu Mwanamke anaringa sana hapa chuoni sijui anajikuta naniΒ  yaani” Ni miongoni mwa kauli nilizowahi kuzisikia kutoka kwaΒ  Baadhi ya Wanaume walionikataa, niliona ni bora wasemeΒ  naringa kuliko ile siri ifahamike kwenye hadhara.Β 

    Jonas alifanya kila mtego ili nifanye nae tendo lakiniΒ  nilikuwa makini kuhakikisha namaliza kwanza chuo ili hataΒ  kama akijua mbele ya safari sitapata aibu kama ambayoΒ  nitaipata nikiwa bado chuoni, alinitoa Out kila mara.Β 

    Konzo aliniletea majarida mbalimbali ili nijifunze jinsiΒ  Mwanamke anavyotolewa usichana akiamini naogopa kufanyaΒ  hivyo, aliniletea hadi video za ngono ili nishawishike! Ndio,Β  zilinihamasisha sana na hofu yangu ikawa pale paleΒ 

    “Nimefanya jitihada zote Veronica, kinachokukwamisha niΒ  usichana wako huo, unakosa madili ya pesa”Β 

    “Imeshakuwa Bwana Konzo, acha iwe hivyo hivyo wakati ukifikaΒ  nitapata hayo madili”Β 

    “Tatizo lako wewe ni mbishi sana Veronica, jaribu usiseme tuΒ  wakati…unaogopa utafikiria unataka kutolewa uhai?”Β 

    “Ha! ha! ha!”Β 

    Nilimzoea Konzo, siku moja Mwalimu Kasase aliniita ofisiniΒ  kwake, alikuwa ni miongoni mwa Watu waliokuwa wakinitongozaΒ  pale chuoni, nilipofika aliulizia kuhusu jibu lakeΒ  nilimwambia aendelee kusubiria, alinielewa.Β 

    Basi Maisha ya Chuo yalikuwa matamu na ya kukera kwa wakatiΒ  mmoja, kuna wakati nilisikia raha sana lakini wakati mwingineΒ  nilikereka, likizo ilipofika nilirudi Arusha nikiwa msichanaΒ  bado yaani Bikira. Pale nyumbani nilimkuta Mjomba yaani KakaΒ  yake Mama aliyeitwa Sanga.Β 

    “Eeh! Veronica umekuwa Mkubwa hivi?” aliponiona aliniuliza,Β  niliishia kucheka tu maana ukubwa wa Mtu unaonekana kupitiaΒ  kwa wengine, mimi nilijiona nipo vile vileΒ 

    “Huyu Mtoto kafanana sana na Baba yake”

    “Sana, hasa anavyotembea kama anarudi vile”Β 

    “Ha!ha!ha!” Mama aliingiza utani wake kwa kilugha cha kwetu,Β  tukawa tunacheka lakini Mjomba akionekana kama kunishangaaΒ  sana hadi nikawa naona aibuΒ 

    “Msindikize Mjomba wako Kanisani” Alisema Mama baada ya sikuΒ  mbili za kuwa ArushaΒ 

    “Ina maana Anko Sanga hakujui kanisani Mama? siku zote hizoΒ  alizokaa”Β 

    “Mpeleke bwana!! Hakuwa na Mtu wa kumsindikiza huko, ukirudiΒ  utayarishe chakula cha Usiku”Β 

    Basi, tuliingia kwenye gari lake tukaanza safari ya kuelekeaΒ  kanisani kwetu, palikuwa na umbali kiasi, mwendo wa KilomitaΒ  15 hadi kufika huko, palikuwa karibu na nje ya Mji wa ArushaΒ  kulikuwa na hilo kanisa la Mzungu ambalo tangia nikiwa mdogoΒ  nilikuwa nikisali hapo hadi nakuwa mkubwa.Β 

    “Kumbe ni mbali hivi?” aliniuliza tukiwa tumebakishaΒ  takribani Kilomita 4, Kwa mbali mlima kilimanjaro ulikuwaΒ  ukionekana kwa uzuri sana, tulipishana na magari ya WataliiΒ  waliokuwa wakielekea hukoΒ 

    “Umeshawahi kwenda kufanya utalii?” aliniuliza tena,Β  nilitabasamu tu kwani sikuwahi hata kuusogelea ule mlima japoΒ  nilizaliwa Arusha.Β 

    “Hapana Anko sijawahi kufanya utalii, ule mlima nauona kwaΒ  mbali tuu” Mjomba alicheka sana akaniuliza kama ningependaΒ  twende huko mlimaniΒ 

    “Ndio napenda”Β 

    “Nitaongea na Mama yako” alisema kisha tuliendelea na safariΒ  ya kuelekea Kanisani, tulipofika nilimuacha akanipatia pesaΒ  kama Elfu 50 hivi kisha akaniambia nisimwambie Mama MaanaΒ  ataichukuaΒ 

    “Sitamwambia Anko”Β 

    “Haya natumaini mapishi yako yatakuwa Bul bul leo Veronica”Β 

    “Ha!ha!ha!” nilikuwa napenda sana kucheka nilikuwa siweziΒ  kununa yaani, nilifurahi kisha nilipanda daladala na kurejeaΒ  Nyumbani.

    Β Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA PILIΒ 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β 

    riwaya mpya riwaya za kusoma mtandaoni

    12 Comments

    1. Aura on May 12, 2025 8:20 pm

      Woow inakujakuja vikee 🧐

      Reply
    2. Given Gihsy on May 13, 2025 12:39 am

      dadeq anko ankol 🫠🀣🀣

      Reply
    3. Lilian on May 13, 2025 10:51 am

      Ni nzuri sana

      Reply
      • Shammy on May 14, 2025 6:34 pm

        Woooh

        Reply
    4. Tunu on May 13, 2025 1:01 pm

      Ankolllll

      Reply
    5. Bartazary haule on May 13, 2025 2:15 pm

      nzuri

      Reply
    6. G shirima on May 13, 2025 3:23 pm

      Ankol tena

      Reply
    7. Shedrack Mkwawa on May 13, 2025 5:23 pm

      Ni story nzuri inapendeza

      Reply
    8. Cathbert on May 14, 2025 12:29 pm

      Mzuri

      Reply
    9. Saeed on May 14, 2025 2:52 pm

      Anko atuachie vero wetu bwanaπŸ˜†πŸ˜†

      Reply
    10. Saeed on May 14, 2025 2:55 pm

      Ankoo atuachie vero wetu bwanaπŸ˜†πŸ˜†

      Reply
    11. πŸ–² + 1.827105 BTC.GET - https://yandex.com/poll/enter/4Joc2mvUbapjsUMcMcKM3z?hs=a17f470df2d0ae2ddbf5202c812023dc& πŸ–² on June 21, 2025 2:00 am

      ryoq5t

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi October 1, 2025

    In the name of LOVE – 12

    Ilipoishia sehemu ya Kumi na moja ya In the name of LOVE Moyo Wangu na…

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    In the name of LOVE – 09

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.