Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 09
Basi nilikata tamaa, chozi lilinibubujika. Nikajikuta nikipandwa na hasira sana, nikasema kwaΒ mara ya mwisho kwa sauti kubwa ya hasira huku chozi likinibubujikaΒ
βFungukaaaβΌ!β ghafla tu nililiona lile shimo la ajabu likifunguka nyuma yangu, palikua panatoaΒ mvuke na joto kwa mbali, rangi nyekundu ilikua imelizunguka shimo lile, nilichungulia ndani yaΒ shimo maana sikuwahi kuingia hivyo nilikua sijui chochote kile hata kunaonekanaje nilikua sijui.Β
Nilitumia muda mrefu nikiliangalia tu, kisha niliisikia sauti nzito ikiuliza kutoka ndani ya shimo. Endelea
SEHEMU YA KUMI
βKwanini umenifungua?β nilishtuka nusura nikimbie, shimo lilikua likiongea. Nilijiuliza nijibuΒ nini, Nani ananiuliza ni shimo au yule jini. Nilimeza funda zito la mate huku vipele vidogoΒ vidogo vya hofu vikianza kunitoka.
βMimiβ¦.mi-mimi naaaβ¦β nilibabaika sana nikiwa napepesa macho yangu, kila nilochofikiriaΒ kukisema niliona kama nitakosea, niliendelea kubabaika. Cha ajabu niliulizwa tena kwa kutajwaΒ kabisa jina languΒ
βKwanini umenifungua Celin?β hapa nilishindwa hata kujizuia nilionesha ni namna gani mimiΒ nilikua mwoga, nilishtuka kiasi kwamba hata mate yaligoma kupita kooni, kifua changu kilijaaΒ upepo huku miguu yangu ikiwa inatetemeka. Nguvu ziliniisha kabisa.Β
Nilihema kuliko kawaida, kisha lile shimo lilijifunga likatoweka baada ya Mimi kukaa kimya.Β Nilishikilia moyo wangu, nilijikuta nikikaa chini taratibu huku nikiendelea kuhema. NilimezaΒ funda kubwa la mate kisha nikajiulizaΒ
βNilipaswa kuingia au kujibu?β Nilikohoa mara moja kisha niliutazama ule ukuta ambaoΒ ulifanya lile pango la ajabu likafunguka. Nilimkumbuka Mama yangu, Baba, Caren na Zena,Β wote walikua wahanga wa hii nyumba ya ajabu yenye kaburi. Niliingiwa na shahuku yaΒ kumaliza tatizo kabisa, basi nikasema tena kwa Ujasiri sanaΒ
βFungukaaaβΌβ Nilisema kwa nguvu hadi vipele vya msisimko vilinitoka.Β
Safari hii sauti yangu moja tu ilifanya lile shimo lifunguke, sikushtuka kama ilivyokua mara yaΒ kwanza. Niligeuka na kulitazama, nilimwomba Mungu maana nilihitaji kushuka chini ndani yaΒ lile kaburi la ajabu ili niipate nafsi ya Sabra.Β
Nilitembea taribu hatua kama tatu hivi kisha nilifika mbele ya shimo, nikachungulia lakiniΒ hakuna nilichoambulia ambacho kingenipa uelekeo sahihi. Sikuitaka ile sauti iniulize ninatakaΒ nini, tayari moyo na akili yangu vilijua nahitaji nini zaidi.Β
Niliingiza mguu mmoja kisha nikaingiza mwingine, ndani yake palikua na harufu kali ya udi.Β Niliuzamisha mwili mzima, ghafla tu nikajikuta ndani ya shimo lenye giza la kutosha, tofauti naΒ mwanzo nilipoona mwanga ndani ya shimo lakini palikua giza kabisa. Hakuna nilichokionaΒ mbele wala nyuma yangu, giza nene lilikua limelifunika shimo lote.Β
Nilisimama huku nikiangaza kama naweza kuona eneo la kutokea lakini haikua hivyo,Β nilijiingiza shimoni bila kujua nawezaje kutoka. Palikua kimya sana, udi uliendelea kunukia,Β nilisimama nisijuwe naelekea wapi. Mara nilisikia sauti ya yule Bibi Kizee, alikua akiimbaΒ nyimbo zake nisizo zielewa.
Niliingiwa na hofu lakini niligundua kama vile alikua na pirika zake, kivumbi kilikua ni namnaΒ ya kuyafanya macho yangu yaone angalau nipate pa kuanzia, nilimsikia tena akitafuna hukuΒ akitoa miguno ya kufurahia alichokua anakula, vishindo vya kucheza pia nilivisikia.Β
Sauti yake haikua karibu sana na Mimi, nilichagua kupapasa kwa kutumia mkono wangu waΒ kushoto ambao ndio nilikua nautumia sana, niliendelea kupapasa huku nikipiga hatua fulaniΒ ndogo ndogo za kuvizia. Kadiri nilivyozidi kwenda mbele nilianza kuhisi mwanga kidogo,Β nikapepesa macho yangu halafu nikaendelea mbele taratibu sana.Β Β
Sikutegemea kama kule chini kulikua na nafasi kubwa kiasi kile, niliweza kupiga hatua zaΒ kutosha kuifuata ile sauti ya yule jini, hapakua pa kawaida kabisa maana kadili nilivyosongaΒ nilihisi kuna vitu vinaota kwenye mwili wangu mithiri ya manyoya hivi. Nilisisimka sana, hofuΒ iliendelea kunisumbua lakini sikutaka kukoma nilijiambia kama kufa ni bora nife kulikoΒ kushuhudia Wazazi wangu wakiwa wameharibikiwa.Β
Niliendelea kutembea huku ile hali ya kuota manyoya ikizidi kuendelea hadi nilianza kuhisiΒ nimekua kiumbe cha ajabu sana, ule mwanga ulizidi kujaa machoni pangu kiasi kwamba nilianzaΒ sasa kupata nuru ya kuona mbele. Nilichokua nakiona kilizidi kunitia hofu, palikua na mafuvuΒ mengi chini, panya walikuwa wakiingia kwenye mafuvu na kutoka. Sikutaka hofu iendeleeΒ kunitawala maana nilijua kama hofu itanitawala basi sitaweza kukamilisha kazi ya kuipata nafsiΒ ya Sabra.Β
Pole pole, nilianza sasa kuisikia ile sauti ya Mwanamke anayeimba. Safari hii niliisikia kwaΒ ukaribu zaidi, ilionekana ilitoka eneo ambalo niliisikia sauti ya yule jini, niliendelea kusongaΒ taratibu nikiwa makini sana. Sikutaka hata kujiangalia maana nilijua nikifanya hivyo nitajiogopaΒ kwa jinsi ambavyo mwili wangu ulikua umeota manyoya madogo madogo.Β Β
Nilifika sehemu moja, palikua na mlango ambao ulikua haujafungwa vizuri, upenyo mdogoΒ uliobakia ndio uliokua ukinipa nuru. Ndani palionekana kua na taa kali sana, sauti ya kuimba naΒ sauti ya kutafuna vilikua vinaendelea kusikika. Nilisimama kidogo kabla ya kufanya uamuzi waΒ kuchungulia ndani
Nilimwona Mwanamke mmoja aliyevalia gauni jekundu, alikua amekaa chini akiimba hukuΒ chozi likimtoka. Alikua anatoa chozi la damu machoni mwake, kwa haraka haraka nilitafsri kuaΒ huwenda alikua akimwimbia huyu Jini Bibi Kizee, nilitaka kuona ni nani aliyekua mbele yake.Β Β
Niliuingiza mwili wangu nusu ndani ya kile chumba, nikafanikiwa kumwona yule Bibi kizeeΒ akiwa kwenye umbo la kawaida kabisa kama lile analonitokeaga nalo, alikua akifurahia nyamaΒ aliyoishikilia mkononi lakini pia alikua akicheza cheza ikionesha namna ambavyo ile nyimboΒ ilikua ikimburudisha.Β
Ndipo nilipo yaaminu maneno ya yule Mwanaume kua ndani ya nyumba yetu palikua na kaburiΒ ambalo alizikwa yeye pamoja na Dada yake, haitoshi niliamini kua Dada yake Sabra alikuaΒ akitumikishwa na jini huyo ndiyo maana alikua akiimba huku akiwa analia. Ndani palikua naΒ mwanga mkali kiasi kwamba hata sisimizi angeweza kuonekana kirahisi sana. Kiumbe chochoteΒ ambacho kingeingia ndani ya chumba kingeonekana haraka sana.Β
Sabra alikua akiimba huku akionesha kama vile alihisi mlangoni palikua na Mtu, shingo naΒ macho yake vilikua mlangoni mara kwa mara huku akiendelea kuimba na kumburudisha yuleΒ Bibi kizee.Β Β
Mara nyingi alikua akipepesa macho yake yaliyokua yakitiririsha chozi, alikua akiniangalia kishaΒ akimwangalia Bibi Kizee, sura yake ilionesha mateso makali aliyokua akiyapitia, alikosa nuruΒ kabisa. Lakini alionesha kunishangaa maana ilikua ndiyo mara ya kwanza Mimi na yeyeΒ tunaonana halafu isitoshe pale chini palikua ni eneo hatari sana kwa Binadamu wa kawaida kamaΒ Mimi.Β
Nilikua na uhakika kabisa kua ndiye ninayepaswa kuondoka naye ili akakutane na Kaka yakeΒ waunganishe nguvu zao kwa ajili ya kumwangamiza Bibi Kizee. Wakati naendelea kufikiria niniΒ cha kufanya nilimsikia Bibi Kizee akisemaΒ
βInatoshaβ alisema kwa sauti kavu iliyojaa amri, kisha naye aliacha kula alichokua anakula.Β Akavuta harufu kwa kutumia pua yake ndefu kama vile alihisi uwepo wa Binadamu.Β
Alianza kuimba yeye kwa kuguna guna huku akitikisa kichwa chake, halafu akaweka mikonoΒ yake mgongoni mwake akaanza mwendo wa kuja mlangoni, Sabra akanipa ishara kwa kutikisaΒ
kichwa chake, papo hapo nikajua napaswa kufanya nini. Nikarudi nyuma haraka haraka halafuΒ nikabana sehemu.Β
Ni hatua chache tu kutoka mlangoni, alipofika nje aligeuka alipotoka kisha akasemaΒ Β
βFungaaaβΌβ Mara moja ule mlango ukafunga kisha akaondoka zake, sikutaka kutingisha hataΒ pumzi zangu, nilizibana vizuri sana hadi pale nilipomsikia akisema Fungukaa akiliamlisha lileΒ shimo nikajua alikua anaondoka.Β
Basi haraka nikafika pale mlangoni, japo palikua na giza la kutosha lakini hisia zanguΒ ziliniongoza vyema hadi nilipofika mlangoni. Mlango ulikua umefungwa, nilipapasa hukuΒ nikiusukuma kuona labda utaweza kufunguka. Nilijaribu mara kadhaa bila mafanikio hatimayeΒ niliona ni bora nimwite kwa jina lakeΒ
βSabraβ nilimwita nikiwa nategemea pengine angesogea mlangoni na kunipa msaada waΒ kuufungua.Β
βWewe ni Nani?β Niliisikia hii sauti ya kike ya Sabra, ilitoka kwa upole sana. Ilijaa mshangaoΒ mkubwa wa kuona Binadamu akiwa ndani ya lile kaburi.Β Β
βMimi ni Celin, Kaka yako amenitumaβ nilimjibu. Pakawa kimya sana, wastani wa dakika mojaΒ hivi nikamsikia tenaΒ
βKaka yangu? Wewe ni Nani hasa na umewezaje kufika huku?β Aliniuliza, nilikua na uhakikaΒ wa jambo moja, alikua amepoteza tumaini, alishaamini kua nafsi yake ingekua utumwani daima.Β Hakutegemea kusikia kua kaka yake bado anamhagaikia.Β
βHaji?β Aliuliza kwa Mshangao zaidi.Β
βNdiyo, ni yeye. Amenituma kukutoa ndani ya kaburi. Kwa pamoja mtaweza kumuangamizaΒ huyu jini ambaye amekua akifanya mauwaji kila uchwao tena kwa Watu wasio na hatia,Β nimepoteza Wazazi wangu kwasababu yakeβ niligongelea msumari wa mwishoΒ
Alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema.
βSijui kama itawezekana, nimedhohofika vya kutosha. Sijioni nikiwa nina nguvuβ alisema, sautiΒ yake ilibadilika kidogo. Aliongea kwa huzuni. Chozi lilikaribia kunitoka, maneno yake yalijaaΒ hatma isiyo na matumaini.Β
βHaijalishi Sabra, ni lazima utoke humu ili ukaungane na Kaka yako kwenye Maisha mengine.Β Hauwezi kua Mtumwa Daimaβ nilijikuta nikianza kumshawishi niondoke naye japo nilikua sijuiΒ uhatari mkubwa uliopo mbele yangu.Β Β
βCelin, upo sehemu iliyojaa hatari kubwa sana. Hiki kiumbe kina nguvu za ajabu sana sijui kamaΒ unaweza ukatoka ukiwa haiβΒ Β
βHaijalishi Sabra,nikifa kwenye mapambano itakua haki yangu kuliko kuishi kwa furahaΒ iliyokandamizwa na upweke na mateso. Natafuta haki ya kifo cha Mama yangu pamoja na hakiΒ ya Baba yanguβ nilisema kwa Ujasiri, kiukweli nilikua nimefika mwisho wa hofu yangu.Β Β
βSawa, fungua unitoeβ alisema, nilikumbuka namna yule Bibi Kizee alivyoufunga huu mlangoΒ kwa kusema tu Funga. Nikakumbuka namna hata lile shimo la ajabu linavyofunguka kwaΒ kuliamrisha, basi nikajiweka sawa ili nisemeΒ
βFungukaaaβΌβ Nilisema kwa ujasiri na Mamlaka makubwa sana, mara mlango ulifunguka.Β Ndani palikua pana nuru ya ajabu inayowaka na kufanya pawe na Mwanga mkali. PalijaaΒ mafuvu ya vichwa vya Watu, macho yangu yalikutana na macho ya Sabra. Alichokua amekisemaΒ ndicho nilichokiona kwenye sura yake, alikua amechoka na kukata tamaa.Β
βTwende Sabraβ nilisema kisha nilimpa mkono, aliutazama sana Mkono wangu kwa sekundeΒ chache za kuhesabu. Hakunipatia mkono wake, sikujali nilichotaka ni kuondoka naye. BasiΒ tuliongozana akiwa anatembea kwa kuchoka choka hivi.Β
Hakutaka nimguse kabisa, hata alipoonekana kua amechoka anaelekea kuanguka, tulisogeaΒ taratibu na alikua akizijua njia za mule ndani ya lile kaburi kubwa la ajabu, akawa ananiambiaΒ kila kitu kinachohusiana na njia za mule kwa kila hatua ambayo tuliipiga.Β
Alikua anajua kila kitu hata lilipo lile shimo la kutokea ndani ya lile kaburi, kuna namnaΒ nilijiuliza maswali mengi inawezekanaje Mtu anayejua pa kutokea na asitoroke siku zote hizo?Β
Nilipotezea suala hili, nikaweka nguvu zaidi kuhakikisha tunaondoka tukiwa salama kabisa.Β AkaniambiaΒ
βNatamani sana kumwona Kaka yangu, ni muda mrefu nimeishi nikiwa mpwekeβ alisemaΒ maneno yaliyonigusa moja kwa moja.Β
Nilitabasamu kidogo maana aliongea maneno yaliyojaa tumaini na kiu ndani yake, binafsiΒ sikujua tunawezaje kutoka maana ndani ya kaburi ni udongo, hakuna simenti hivyo hata mahaliΒ pa kutokea sikupajua.Β
Akapaza sauti akasemaΒ
βFungukaaβΌβ Haikuchukua hata sekunde nyingi, shimo likajitengeneza. Mwanga wa chumba chaΒ stoo ukaonekana. Nikageuka kumtazama, nilikua na swali la kumuuliza lakini niliona ni boraΒ tukitoka nimuulize. Tukafanikiwa kutoka salama ndani ya lile shimo, tukawa tumefika stoo.Β Kumtoa Sabra ndani ya lile Kaburi ilikua rahisi kuliko hata kaka yake alivyoniambia kituΒ ambacho kilinipa maswali mengi yasiyo na majibu.Β Β
Mara lile shimo likatoweka. Alikua anahema sana kama Mtu aliyechoka, alikua amedhohofuΒ mno hadi nilimwonea huruma ila nilimuulizaΒ
βKwanini haukutoka siku zote hizo ikiwa unajua kila kitu?βΒ Β
Nilikua na kiu sana ya kutaka kujua, alinitazama akanijibu harakaΒ
βKila jambo na wakati wake Celinβ lilikua ni jibu fupi jepesi ambalo halikua chakula kizuri chaΒ fikra zangu. Akanitazama kisha akaniulizaΒ
βUmevaa nini mkononi?β Swali lake lilinishtua kidogo na kuanza kunipa hofu maana kule chiniΒ alikataa kabisa kumgusa. Nilijiuliza kwanini alikataa ikiwa yeye ni nafsi salama kama ya KakaΒ yake ambaye ndiye aliyenipatia ile shanga.Β
Nilimeza funda la mate, nikatabasamu kidogo nikampa jibu bila kusema UwongoΒ
βHuu ni ulinzi amenipatia Kaka yako, ni kinga dhidi ya yule jiniβ nilimjibu, nilimwonaΒ akitafakari jambo halafu mdomo wake ukawa mzito kama vile alitaka kusema jambo alafuΒ akaghaili.
βTwende anaweza kutukuta hapaβ akasema kisha nikaongoza mbele maana mimi ndiyeΒ ninayejua nini cha kufanya. Nilikua tayari nimempata Sabra ila sikujua ni namna gani nitawezaΒ kumpata Kaka yake ili waunganishe nguvu zao na kupambana na kile kiumbe.Β Β
Tulitoka ndani hadi nje kabisa ya nyumba, palikua kimya lakini hali ya kusisimka mwili ilikuaΒ ikinianza. Hisia hii iliniambia kua lile jini lilikua karibu na Mimi, nilihisi kuchanganikiwa maanaΒ tayari nilikua nimefanikiwa kumtoa Sabra mle kaburini hivyo kama atatukuta basi ataniuwa.Β Β
Barabara ilikua tupu, sikujua nifanye nini lakini kwa haraka haraka nilifikiria niondoke na Sabra kutoka pale kwenda mbali kidogo mahali ambapo yule Kaka yake angeliweza kututokeaΒ nikamkabidhi mdogo wake.Β
Tulitembea taratibu tukiiacha nyumba yetu nyuma, sikutaka tuelekee upande ule wa nyumbaΒ jirani ya yule Mzee, tulisonga mbele kwa hatua nyingi za kutosha, hadi tulipofika mbali kiasiΒ chake. Tulisimama, palikua kimya hakuna mazungumzo, niliangaza huku na kule kuonaΒ huwenda angetokea lakini alikua kimyaΒ
βYupo wapi Haji?β Aliniuliza, sikua na jibu la moja kwa moja la kumpa maana Haji sikujuaΒ nawezaje kumwita akatokea maana alikua kama Mzimu fulani hivi wa ajabu ambao ungewezaΒ kutokea popote pale. Mahali tulipokua tumesimama palikua na miti mikubwa miwili, mmojaΒ ulikua upande wa pili na mwingine ni upande tuliokua tumesimama Mimi na Sabra.Β
Tulisimama kwa dakika kama tano hivi nikiwa sielewi nafanya nini, kwakua Haji ni nafsi basiΒ atakua ametuona lakini kwanini hatokei kumchukua Dada yake? Nilijiuliza swali hili nikiwa sinaΒ jibu la moja kwa moja. Niliangaza huku na kule bila mafanikio, nikakata tamaa bila kujuaΒ nitaenda wapi na Sabra.Β
Alikua akiniuliza mara kwa mara mahali alipo Kaka yake, hata pale nilipompa mgongoΒ nilipogeuka alikua akinitazama sana lakini alikua hataki nimguse kabisa kitu ambacho kilikuaΒ kinanishangaza kila dakika. Mara nilianza kuhisi kama vile nilikua napigwa na vitu mgongoniΒ mwangu, sikutaka kugeuka moja kwa moja. Hapo mwili ulikua unazidi kusisimka sana.
Akili yangu iliwaza mara moja kua pengine yule Bibi Kizee alikua ndiye anayenipiga na vituΒ mithiri ya vidude vidogo vidogo ambavyo haviumizi lakini baadaye akili yangu ikanambiaΒ huwenda nilipaswa kugeuka taratibu ili nijuwe ni Nani aliyekua akinishtua kwa nyuma naΒ kwanini alifanya kua siri.Β
Niligeuza shingo kitaalam sana sidhani hata kama Sabra aliweza kungβamua, nilifanya kamaΒ nageuka hivi. Ndipo nilipomwona Haji Kaka yake Sabra, akanipa ishara ya kunitaka nikaeΒ kimya.Β
Sikujua ni kwanini alitaka nikae kimya, nikawa nazugazuga kama naangalia huku na kuleΒ kumtafuta Kaka yake Sabra, nikawa naendelea na ule mchezo, nageuka kwa siri siri. BaadayeΒ akawa ananiambia kwa ishara akimaanisha kua niliyekua nimesimama naye alikua siyo DadaΒ yake Sabra. Jicho lilinitoka, msisimko ulizidi kuongezeka, mwili ulikosa nguvu ghaflaΒ nikatamani nipate mahali nikae.Β
Sasa nikawa naunganisha mambo kadhaa na moja wapo ni kitendo cha kukataa nisimguse, hapoΒ nikapata picha halisi sasa kua niliyetoka naye kaburini kwa kufikiria ni Sabra alikua ni yule BibiΒ Kizee aliyejivika sura ya Sabra. Nilimeza funza zito la mate huku macho yakiwa yamenitoka,Β japo nilijawa na hofu lakini sikutaka kumpa mwanya wa kugundua kua nimemshtukia.Β
βHuyo Haji anakuja saa ngapi jamani, siwezi kusubiria kumwona maana niliamini siweziΒ kumwona tenaβ alisema Bibi kizee mwenye sura ya sabra, nilimtazama nikaachia katabasamuΒ nikamwambiaΒ
βAtakuja muda sio mrefu, mimi sijui namna ya kumwitaβΒ
βOoohβΌβΒ Β
Bado alikua akinikwepa, alikua hataki nimguse hata kwa bahati mbaya, alikua anapiga hatua zaΒ kunikwepa. Nilishajua hawezi kunidhuru kwasababu ya ule ushanga niliopewa na Haji. SikujuaΒ nini Haji angefanya maana Bi Kizee alikua makini kunitazama kila hatua ninayoipiga, nilielewaΒ lengo lake lilikua ni kupiga ndege wawili kwa jiwe moja.
Bado Haji alikua akinipa ishara za siri nigeuke, pengine alikua na mpango fulani ila sasa BibiΒ Kizee alikua hanipi huo muda, alikua makini zaidi na Mimi. Nilijaribu kugeuza jicho la kuibaΒ lakini sikufanikiwa kumfikia Haji, ikabidi nimwambie Bibi KizeeΒ
βNinahisi Mkojo, nahitaji kujisaidiaβ nilimwambia nikiwa nina mtazama, nilihitaji nafasiΒ muhimu zaidi kupata wazo la Haji maana aliyekua mbele yangu alikua siyo Sabra bali ni Jini.Β
βHaina shida, Mimi nitasimama hapa kumsubiria Haji. Usikawieβ alinijibu, nilihisi nilikuaΒ nimeukaribia ushindi. Nyuma yangu palikua na pori dogo lenye mti mkubwa ambao Haji alikuaΒ amejificha, nikajifanya kuangaza huku na kule kisha nikakimbilia pori dogo ambalo ningekutanaΒ na Haji.Β
Lakini wakati natoka nililiona tabasamu la Bi Kizee, nikajua sasa huwenda amejua kua nilikuaΒ nimemshtukia. Nilipofika nyuma ya ule Mti nilimkuta Haji, upepo ulikua ukivuma kiasi kwambaΒ maua yalikua yakituangukia. Haji aliniambia haraka harakaΒ
βYule Bibi amejua kua umejua, anaweza akaucheza mchezo lakini hawezi kushinda. Chukua hiiΒ kamba, hakikisha unamfunga popote kwenye mwili wakeβ alinipa kamba ndogo nyekundu kamaΒ zile wanazovaa wahindi mkononi.Β
Akanipa ishara ya kuondoka, kweli niliondoka pale na kurudi barabarani. Nilipofika nilikutaΒ peupe. Yule Bibi Kizee hakuwepo pale barabarani, niliangaza huku na kule pengine ningemwona.Β
Macho yangu yalikua kodo kila mahali, nilihesabu idadi ya gari zinazopita bila mafanikio.Β Hatimaye nilipogeuza shingo yangu nilimwona akija akitokea upande wa pili wa barabara.Β Maswali hayakuniisha sababu nilikua sina uhakika kama alikua amegundua jambo au laa. IlaΒ moyo wangu ulinieleza mengi juu yake, nilihisi aligundua jambo kama alivyonieleza Haji.Β Nilipaswa kua muigizaji nguli japo yeye ana nguvu za kutambua mambo kwa haraka kutokanaΒ na uwezo wake wa Kijini.Β
Alipofika nilipo, nilimtazama usoni pake. Alikua na haya fulani iliyoficha jambo. βBado hujaonana naye?βΒ
βNani?βΒ
βUlisema Haji!βΒ
βAaah ndiyo, samahani hiki kichwa kinafikiria sana.β Nilisema huku nikifikiria zaidi namna yaΒ kumfunga kamba yule jini, niliishikilia ile kamba kwa nguvu mkononi nikiwa nimeificha vizuri.Β
βMimi nafikiria turudi kule ndani, pengine anaweza kuja kule. Kumsubiria hapa ni kamaΒ tunapoteza mudaβ alisema, machale yalinicheza kua alikua na lengo la kuniingiza mtegoni.Β
βAaahβΌ Alisema hawezi kuingia mle sababu anamwogopa yule Jini, Mimi naona angalau tuketiΒ chini ya ule Mti kwa kitambo fulani. Huwenda anaweza kujaβ naye aligeuka kuutazama mti huo,Β ulikua Mti mkubwa uliomea vizuri kijani cha kutosha na matawi makubwa yaliyopeba majaniΒ mapana. Alinitazama kisha akajibuΒ
βHakuna shida, kama tunaweza kufanya hivyo. β Nilisubiria atangulie mbele ili nimfunge ileΒ kamba haraka, kweli aliongoza mbele nami nikawa nyuma ya mgongo wake. Alikua mwingi waΒ mazungumzo yasiyo isha, ndani yake alionesha alikua akimtaka sana Haji sababu nilishampa siriΒ pasipo kujua kua yeye ni jini, ile siri ya nafsi mbili kuungana na kummaliza yeye.Β
Alikua akiutupa sana mkono wake wa kulia, alikua akitembea kwa kujiachia achia kama siyoΒ yule aliyedhohofika. Macho yangu yalikuwa hayatulii, mapigo ya moyo yalinienda mbio. KilaΒ hatua niliyoipiga ilikua ikitoa sauti ya kunikumbusha wajibu wangu wa kumfunga ile kambaΒ lakini nilijawa na hofu sana.Β
Hadi tunafika chini ya Mti sikuweza kumfunga. Tulipokaa chini akaniulizaΒ
βUmekunja ngumi muda wote huumii?β Aliniuliza huku akiutazama mkono wangu wa kuliaΒ ambao niliishikilia ile kamba, nilitabasamu kuondoa ngoma juani. Nilikua nawaza mamboΒ mawiliΒ
Pale Mtini ni mahali nilipomwacha Haji, vipi kama atamwona? Swali la pili nilijiuliza nitamjibuΒ nini?Β
βAaahβΌ Nimezoea siwezi kuumia, wala usihofuβ Nilipomjibu hakusema chochote, alipelekaΒ macho yake barabarani. Kumfunga ile kamba ilikua kazi ngumu sana, aliketi hatua moja kutokaΒ kwangu pia alikua akigutuka mara kwa mara na kunitazama kama Mtu aliyejiandaa zaidi, hiiΒ ilinipa hofu sana.
Hakuruhusu nimsogelee sababu hakutaka kugusana nami akihofia kupata madhara sababu ya uleΒ Ushanga wa ulinzi niliopewa na Haji. Kimya kilitawala, hisia ilizidi kuniambia kua atanigeukaΒ endapo nitaonesha dalili zote kua nimegundua siri yake.Β
Kuna nyakati alinitazama kama vile alikua anataka kuniambia amegundua kila kitu lakiniΒ nilimkatisha kwa kuzungumza, sauti za magari zilikua zikisikika kwa kuvuma.Β Β
βUna hakika Haji atakuja?β Akaniuliza, alijawa na shahuku sana sababu aliona muda ulikuaΒ ukienda.Β Β
βNaamini hilo litafanyika, cha msingi ni kuendelea kusubiriaβΒ Β
βTutasubiria hadi saa ngapi Celin?βΒ
βSijui lakini hakuna kitakacho haribika, cha muhimu ni kwamba nimekutoa kwenye mateso yaΒ yule jini mshenziβ nilisema kwa kujikaza ili angalau kumwaminisha kua hakuna kilichojulikanaΒ kuhusu yeye. Alitoa tabasamu tu wala hakusema neno lingineΒ
Muda ulivyozidi kwenda nilianza kuingiwa na hofu sana, maana alinionesha dalili kuaΒ angenidhuru. Kuna muda akawa anazungusha sana macho yake kisha akasimama nikamuulizaΒ
βKuna nini?β Nilimuuliza nikiwa nimesimama pia, alinitazama tu kisha aliketi bila kusemaΒ chochote kile. Aliufanya moyo wangu udunde sana, hofu ilizidi kuongezeka. Mwili ulikuaΒ ukisisimka sana.Β
Alikua kama mbwa, alikua akinusa harufu sana. Akapiga hatua kama mbili hivi, akawaΒ amesimama mbele yangu akiwa amenipa mgongo. Harufu ya kifo ilianza kukita pua zangu,Β damu yangu ilizunguka haraka, mapigo ya moyo yalizidi kuongezeka.Β
Silaha pekee niliyonayo ilikua ni ile kamba nyekundu niliyopewa na Haji, sikujua baada yaΒ kumfunga kingetokea nini lakini nilipaswa kuamini kua ilikua ni silaha muhimu sana, nilionaΒ wazi kua alikua akihangaika kunusa jambo, nikaukunjua mkono wangu. Kiganjani nilikua na ileΒ kamba, safari hii nilijiambiaΒ
βLiwalo na liwe, ni kheri nife kuliko kuuishi UwogaβΒ
Nilivuta pumzi zangu katika hali ya kujiandaa, nilijiapiza kisha nilifanya uamuzi wa kumfuataΒ kwa kasi kisha nikaushika mkono wake, kitendo cha kumshika alibadilika na kua KiumbeΒ chenye sura mbaya iliyoungua. Macho yalimtoka kisha alipiga ukunga kama tembo anayemtafuta Mtoto wake. Sikujali sababu hakuna nisichokiona kutoka kwake, nilimfunga ileΒ kamba halafu nikasogea pembeniΒ
Akabadilika kabisa kutoka kwenye sura ya Sabra hadi kua Bibi Kizee mwenye sura mbaya sana.Β Kitendo cha kumwacha kilimfanya aache kupiga ukunga, aliuinua mkono wake kisha akaiangalieΒ ile kamba halafu akaniambiaΒ
βHii vita haitakuja kufika mwisho Celin, kama unafikiria utashinda basi ndiyo kwanza vita hiiΒ imeanzaβ alikua akisema huku akinifuata, nilikua ninarudi nyuma nyuma lakini kadili alivyokuaΒ akinifuata niliona alikua akibadilika viungo vyake na kua sanamu kavu la kufinyangwa.Β
Akawa ameganda akiwa anapiga hatua kuja nilipo kisha akaniambiaΒ
βSiku nikiwa huru Dunia yako itapiga yowe Celin, hakuna Mtu atakusaidiaβ kisha alipomalizaΒ aliganda kila kiungo chake na kua sanamu. Nilichoka kwa hofu nikajikuta nikianguka na kukaaΒ chini. Chozi lilikua likitoka, sanamu lake lilikua hapo mbele yanguΒ
Mara alikuja Haji, alinitazama huku chozi likiwa linambubujika. Akaniambia βNi muda wa kumkomboa Sabra, twende kwenuβΒ Β
βVipi kuhusu hilo sanamu?βΒ
βUtalivunja kisha utatenganisha udongo wake, udongo mwingine uchome moto kisha mwingineΒ utupe Baharini, hawezi kamwe kurudi Dunianiβ alisema Haji, sikutaka kumwambia alichokisemaΒ Bibi KizeeΒ
Basi, kwa uwezo wake wa kimiujiza tulitoweka pale pamoja na lile sanamu. Tukajikuta ndani yaΒ nyumba yetu. Kila kitu kilibadilika kuanzia hewa na hata mimea ilionekana kua na nuruΒ kuashiria ukombozi. Tulipofika kwenye korido tuliiacha sanamu kisha tuliingia stoo pamoja,Β kitendo cha kuingia tu shimo lilijitengeneza kisha lilituulizaΒ
βMnataka niwafayie nini?β Tulitazamana halafu Haji akasema
βTunamtaka Sabra kutoka kwakoβ pakawa kimya kisha ikaja harufu kali ya marashi, Sabra akatoka ndani ya lile shimo, alipomwona Kaka yake alimfuata na kumkumbatia kwa nguvu.Β Ilinifanya nitabasamuΒ
βCelin, asante kwa msaada na ujasiri ulionao. Nimempata Sabr, tunakutakia Maisha MemaΒ rafikiβ alisema Haji kisha walitoweka sikujua hata walielekea wapi, lile shimo liliniulizaΒ
βUnataka nifanye nini tena?β Nikalitazama kisha nikasemaΒ
βFunga na usifunguke Daima Milele, usiwe njia ya kufika chiniβ baada ya kusema lile shimoΒ lilitoweka kabisa, nikatoka stoo kisha nikaenda kwenye korido, nikalichukua sanamu kishaΒ nikaenda nalo njeΒ
Nikalivunja vunja, nikatemganisha udongo kisha nikauchoma moto. Mwingine nikaenda kuutupaΒ Baharini, nikawa nimemaliza kazi nzito ya kuliangamiza lile jini, nikaenda Gerezani kumuelezaΒ Baba yangu. Alifurahi kisha akaniambiaΒ
βMama yako atakua amepumzika salama, hata Mimi sina wasiwasi na adhabu yangu sasa. NendaΒ ukatimize ndoto zako za kua Msanifu Celinβ alisema Baba, tokea siku hii nilianza Maisha mapyaΒ ndani ya nyumba yetu, palijaa tumaini, amani ya kutosha. Sikusikia mauzauza wala Mazonge yaΒ aina yoyote ile, kilichobakia ni kutimiza ndoto ya kua Msanifu.Β
Nataka kuwashuri mnaonunua Nyumba au viwanja kua makini sana sababu nyumba zingine zinaΒ maagano mabaya ya kichawi, viwanja vingine ni makaburi ya zamani. Nyumba nyingi zipo juu yaΒ Makaburi.Β
MWISHOΒ
MNATAKA SIMULIZI IJAYO IWE YA NAMNA GANI? MAPENZI AU UJASUSI? COMMENTS ZIWE NYINGI SASA NIIACHIE MAPEMA MAANA KAKA MKUBWA AMEREJEA NA SIMULIZI ZA KUTOSHA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
29 Comments
Mapenzi
Kabisa
Nzuri ila inatisha nmejifunza na nimependa asanteh adimin
Tuletee story nyingn adimin
Ujasui
Asantee β€οΈππ
Dah inafunzaa snaa sna hiii Dram aiseh Pongeziii Adminii ππ.. story ijayo iwe ya KIJASUSI
Ujasusi
Aisee funzo kubwa nmepata katk hii story,,honger sana Kaka Mkubwaa
Now
Tuletee ya Mapenzi
Admin ajengewe sanam manzese anajua sana
Ujasusi kama hile ya msala
Iwe ya mapenzi
Kabisa admin azingatie
nzurii sanaa duh inatisha lakini inamafundishooo mazuri
Iwe ya mapenzi
Iwe ya kijasus jinsi gan unaweza kutoka katika hali Fulani ya maisha na kuingia kwenye matumaini mfano kutoka kwenye umaskin kwenda utajiri asante admin
Iweya majini
Mapenzi
Iwe ya mapenzi kaka mkubwa
Ya mapenzi tuliosalitiwa tupate mbinu mpyaππ
Mapenzi
IT’S TIME FOR UJASUSI KAKA MKUBWAAAππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½
IT’S TIME FOR UJASUSI KAKA MKUBWAAAππ½ππ½
Emu tuanze na UJASUSI kwnz..halaf. ndo yafate mapenzi pliz ππ½ππ½
Daaah ni nooooumaaaaa
Ujasusi
Ujasusi
Dah noma sana admin we noma sana kwakweli imetoa funzo kubwa. UJASUSIβοΈ
Shukran mtunzi, nimejifunza mengiπ€π