Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tano-05)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tano-05)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaApril 28, 2025Updated:April 30, 202528 Comments14 Mins Read7K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 04

    β€œUnamkumbuka Zena?” nilimuuliza, alionekana kutafakari kidogo kisha akaniuliza β€œYule rafiki yako?” 

    β€œNdiyo!” 

    β€œKimetokea nini?” aliniuliza kwa shahuku kubwa sana, sura ya Mama yangu haikua na hatiaΒ  lakini nilijiuliza maswali mengi, nilijiuliza kama kweli hafahamu chochote vipi kuhusu janaΒ  Usiku walipotoka kwenye lile shimo yeye na Baba, wana uhusiano gani na Mwanamke anayeliaΒ  kwenye ile stoo? . Endelea

    SEHEMU YA NNE

    β€œAmefariki Mama” nilisema kwa sauti ya kilio. Mama alishtuka sana kuliko kawaida, alishtukaΒ  kama vile alimfahamu Zena kwa muda mrefu sana, alishika kifua chake hadi nilishtukaΒ 

    β€œMama‼” nilimwita sababu namna alivyoipokea taarifa alikua kama amepandwa na presha.Β  AlinitazamaΒ 

    β€œPole Binti yangu, pokea rambirambi zangu” alisema kwa sauti ya upole sana kisha alisimama.Β  Nilikua namtazama Mama yangu kama vile ilikua ndiyo mara ya kwanza namwona,Β  alivyobadilika ghafla alizidi kunipa mawazo zaidi.Β 

    Simu yangu ilianza kuita tena, pochi yangu ilikua karibu na Mama yangu. Akanipatia Pochi,Β  niliona ni bora niitoe simu niipokee, ilikua ni Namba ngeni. Kilichokua akilini mwangu niliwazaΒ  huwenda napewa ratiba za mazishi ya Zena, taratibu niliipokea na kuiweka sikioni bila kusemaΒ  chochote, niliisikia sauti ya kiume ikiniulizaΒ 

    β€œWewe ni Celin?” moyo wangu ulifanya paaa kama nimewagiwa na maji, nilisimamaΒ  β€œEeh Ni Mimi!” 

    β€œMimi ni Msamalia mwema, nimemsaidia rafiki yako Caren alikua amepata ajali mbaya sanaΒ  jana Usiku. Yupo hapa Hospitalini, namba hii nimeikuta kwenye simu yake ndogo nikaonaΒ  nikueleze kama unaweza kuja hapa Hospitali ya Jiji” Moyo wangu ulianza kunienda mbio,Β  niliyakumbuka maneno ya Yule Bibi wa ajabu kua nitapoteza niwapendao kwa Mpigo.Β 

    Nguvu ziliniisha, nilijikuta nikiidondosha simu sakafuni kisha niliketi kitini kama mzigo. MachoΒ  yangu niliyaelekezea chini, chozi la ajabu lilinitoka. Nilijikuta nina hatia kubwa sana kwaΒ  kumshirikisha Caren kwenye hili jambo. Upepo ulianza taratibu huku ukipeperusha pazia, MamaΒ  yangu alinisogelea kwa utaratibu sana akaniulizaΒ 

    β€œKuna nini Celin?” nilimeza mate, nilikua kama Zezeta. Nilinyanyua macho yangu taratibuΒ  yakiwa yamejawa na uzito wa chozi lililoganda machoni pangu. Nilimtazama Mama yangu kamaΒ  Mtu niliyepooza mwili mzima nikamwambiaΒ 

    β€œCaren‼” Mama alinitikisa kunirudisha kwenye ufahamu wangu lakini juhudi zake hazikufuaΒ  dafu, uono ulinikimbia. Kila kitu nilikiona kipo mbali, hata pumzi zangu zilianza kunisalitiΒ  taratibu, niliona giza huku nikihisi ubaridi mwilini mwangu. Nilipoteza fahamu mikononi mwaΒ  Mama yangu.Β 

    ****Β 

    Nilianza kusikia sauti inayofanana na kengele, sauti ilizagaa kichwa kizima. Ghafla nilishtuka,Β  nilizinduka kutoka Usingizini. Mwili ulikua unauma, nilikua mchovu sana. Niliangaza huku naΒ  kule, niligundua nilikua kwenye chumba cha Hospitali, nilikua kitandani. Macho yanguΒ  yalikutana na macho ya Baba yangu pamoja na Mama yangu.

    Mmoja aliketi upande wa kulia na mwingine aliketi upande wa kushoto, wote walionekanaΒ  kunisubiria niamke. Nilipotaka kujitingisha Baba yangu alinizuiaΒ 

    β€œTaratibu Celin” alisema kwa sauti ya kujali sana. Hakuna kilichokua kimbebadilika kichwaniΒ  kwangu. Nilijiuliza kama nilikua nawafahamu vyema wazazi wangu, nilitikisa kichwa kwa mbaliΒ  kua nilikua sijawafahamu vizuri wazazi wangu. Hapo hapo niliikumbuka sababu ya MimiΒ  kuwepo Hospitali, ni simu ile niliyopigiwa kuhusu CarenΒ 

    Nilihema kwa uchovu, halafu nikamtazama Mama maana yeye ndiye aliyekua na Mimi wakatiΒ  napoteza fahamu.Β Β 

    Mama yangu aliyasoma Mawazo yangu akawa wa kwanza kusema.Β 

    β€œCelin‼” aliniita Mama, niliiona sura yake ilivyojaa upole na unyongefu uliopitiliza, alitumaΒ  ujumbe kwa sura yake nikajua fika kua Caren alikua amefariki kutokana na ile ajali, MamaΒ  yangu alinitazama kwa jicho la kunipa pole. Alikua akipepesa macho yake, aligeuza shingo naΒ  kumtazama Baba yangu.Β 

    Baba naye aligeuza shingo yake na kunitazama, alikua na sura ile ile aliyonayo Mama yangu.Β  Sura zao zilikua zimejaa huzuni na huruma. Baba alinishika mkono wangu uliokua una sindanoΒ  iliyotumika kunipatia maji mwilini.Β 

    β€œCelin, pole sana. Umepoteza marafiki wawili ndani ya siku mbili” alisema Baba kwa sauti yaΒ  Upole sana, sura yake ilijaa huruma sana. Hawakuonekana kama wana hatia lakini kwaniniΒ  walikua kwenye lile shimo kule stoo, kuna uhusiano gani kati yao na yule Mwanamke anayelia.Β  Swali hili lilihitaji majibu ya haraka, siyo rahisi wao wakanipatia Majibu.Β Β 

    Chozi lilianza kunidondoka, macho yangu yalianza kuwasha taratibu huku chozi likidondokaΒ  taratibu. Zena na Caren walikua marafiki wazuri kwangu lakini kila kitu kiliharibika baada yaΒ  Wazazi wangu kununua nyumba Mjini.Β Β 

    β€œCelin Binti yangu, najua unavyojisikia. Kupoteza uwapendao kunaumiza sana” alisema MamaΒ  yangu akinitazama kwa sura ile ile. Niliitikia kwa kutumia kichwa changu, sauti haikutokaΒ  kabisa. Nilijihisi ni mwenye hatia, Caren alikufa kwasababu yangu kama ningemzuia asiondokeΒ  Usiku ule basi asingepata ajali iliyopelekea kifo chake. Nililia sana lakini sikuwa na uwezo waΒ  kurudisha wakati nyuma.Β 

    Mchana wa siku hiyo niliruhusiwa kutoka Hospitalini, nilirudishwa nyumbani na Wazazi wangu.Β  Mwili ulikua na uchovu sana, sikuweza kwenda Kumzika Zena maana alizikwa nikiwa Hospitali,Β  hata Sikuwahi kwenda kuuaga mwili wa Caren ambao ulisafirishwa mara moja kuelekea Mji waΒ  Wazazi wake ambako ndiko wanakozikia ndugu zao.Β Β 

    Nilibakia nikiwa mpweke kuliko wakati wowote kwenye Maisha yangu. Mama yanguΒ  alinitazama kwa ukaribu sana kwa siku mbili hadi alipothibitisha kua akili yangu ilianza kutulia.

    Sikupata majibu ya maswali yangu hata pale niliporudi tena kule stoo sikuliona lile shimo, sautiΒ  ya Mwanamke anayeimba nayo ilitoweka kabisaΒ 

    **Β 

    Zilipita siku kadhaa, nilianza tena kwenda chuo. Maisha yaliendelea bila Zena na Caren,Β  Wanachuo wenzangu walinipa pole kwa kuondokewa na marafiki wawili niliowapenda.Β 

    Usiku mmoja nikiwa nimelala chumbani kwangu, nilianza kupata njozi ya ajabu sana. NiliotaΒ  nikiwa ninalia halafu pembeni yangu kuna Mtu aliyejifinika shuka gubi gubi akiwa hatikisiki.Β  Nililia sana, chozi lilinitoka huku nikiwa nimejawa na uchungu sana, njozi hii ilikua ikitokeaΒ Β 

    ndani ya chumba kimoja chenye kitanda cha Hospitali, Mtu aliye juu ya Kitanda alikuaΒ  amefunikwa shuka jeupe.Β 

    Nilikua ninalia huku nikisemaΒ 

    β€œUsiniache nitabaki na Nani Mimi, usiende nakuomba rudi” Sijui nilikua namlilia Nani, ghaflaΒ  nilishtuka kutoka Usingizini,niliketi nikiwa nina pumua haraka haraka. Chumba changu kilikuaΒ  giza kidogo, nilisimama baadaye na kuwasha taa. Japo nilipata ndoto ya kutisha lakini UsingiziΒ  ulikua mwingi machoni panguΒ 

    Nilijivuta ili nielekee chini kupata maji ya kunywa, nilijifunga vizuri nguo yangu ya kulalia,Β  wakati nauelekea Mlango nilianza kusikia sauti ya Mwanamke mmoja, ilikua ni sauti ile ile yaΒ  Mwanamke anayeimba lakini safari hii alikua akilia, nilishtuka sana. Nilipigwa na Butwaa hukuΒ  nikisikia vyema kua ilikua ikitokea nje ya Mlango wa chumba changu.Β 

    Hata mate hayakuweza kupita kooni kwa jinsi ambavyo nilikua nimejawa na hofu, nilitamaniΒ  kugumia kuwaita Wazazi wangu lakini sikuweza, butwaa iliyokua imeniingia akilini ilinifanyaΒ  nitulie kimya nikisikiliza ile sauti. Wakati naendelea kuisikiliza ile sauti nilianza kuhisi ilikua niΒ  sauti ya Mtu ninaye mfahamuΒ 

    β€œMamaaa‼” nilipata jibu, ilikua ni sauti ya Mama yangu Mzazi. Alikua akilia kisha alianzaΒ  kuniita jina langu. Hofu ilizidi kuniingia, nilisimama nikiwa ninaangalia sana mlangoni.Β  Nilitamani kumwita Mama na kumuuliza analia nini lakini nilipokumbuka nilichokiona UsikuΒ  ule nikiwa na Caren niliishiwa nguvu kabisa.Β 

    Aliendelea kulia huku akiniita kwa jina langu hali iliyoizidi kunichanganya, mwendo wa dakikaΒ  tano tu kisha sauti ya Kilio iliondoka Mlangoni kwangu, nikawa naisikia ikishuka chini kupitiaΒ  ngazi. Chozi lilinilenga sababu sikujua anayelia kama alikua ni Mama yamgu kweli na kama niΒ  Mama yangu basi ndiye anayeleta Mauzauza.Β 

    Baada ya sekunde kadhaa ile sauti ilitoweka, palikua kimya sana. Sikupata Hata lepe la Usingizi,Β  nilikesha nikiwa macho. Asubuhi mapema niliamka na kujiandaa kisha niliondoka nyumbani bilaΒ  hata kuwaaga wazazi wangu, nilimpigia simu yule Dalali ili nimuulize maswali kadhaa, nilikuaΒ  na uhakika hata yeye alikua anajua ni nyumba ya aina gani aliwauzia Wazazi wangu.

    Wakati natoka niliitazama sana nyumba ya yule Mzee jirani, ilikua tulivu sana. Majani makavuΒ  yalikua yameanguka sana uwani kwake kuashiria kua palikua hapakaliwi na Mtu yeyote yuleΒ 

    Nilimpigia simu kwa namba ngeni, nilikua na uhakika kama angelijuwa ni Mimi asingelinipaΒ  ushirikiano wowote ule. Nilimwambia kua nahitaji chumba cha kupanga, akanitajia mahali alipoΒ  huku akinisistiza kuwa niende hapo akanioneshe chumba kizuri. Kama kawaida yangu nilikuaΒ  napendelea sana treni sababu ya kukwepa usumbufu.Β Β 

    Baada ya kufika eneo ambalo tulikubaliana tukutane, yeye sikumkuta hapo. Niliangaza huku naΒ  kule lakini sikufanikiwa kumwona, niliketi mahali nikimsubiria huku nikijaribu kumpigia simuΒ  lakini simu yake ilikua haipokelewi kwa zaidi ya dakika tano, mwanzo niliona ni jambo laΒ  kawaida lakini baadaye nilipata hisia ya tofauti.Β 

    Nusu saa nzima simu yake ilikua haipokelewi kisha baadaye ilizimwa kabisa. Mahali alipokuaΒ  amenielekeza palikua ni Kijiwe cha kahawa, hapo ndipo anapopatikana kwani hata mara yaΒ  kwanza nilikutana naye hapo. Nilikata shauri la kuendelea kumsubiria hapo, nilinyanyuka naΒ  kuuvaa mkoba wangu ili niondokeΒ 

    Mara akaja Mwanaume mmoja aliyekua akiendesha Pikipiki kwa kasi sana, japo alikua hajiΒ  upande wangu lakini mwendo wake Ulinifanya niwe macho kumtazama. Aliegeshe PikipikiΒ  kando kidogo ya kundi la Wanaume walioizunguka meza ya kahawa kisha akaketi hukuΒ  akisikitika kama Mtu aliyepoteza Umakini wake.Β 

    Nilinogewa na kuwatazama. Nilisimama nikiwa sikwepeshi macho yangu huku masikio yanguΒ  yakiwa kama antena, walianza kumuuliza kwanini alikua katika ile hali ya kuchanganikiwa,Β  akawa anajisonya-sonya tu huku akishikilia kichwa chake, walianza kumzingatia hata kwa waleΒ  walioanza kuhisi ulikua ni utani walianza kuweka Umakini huku wakizidi kumuulizaΒ 

    β€œSheby jamani‼” alianza kusema huku akihema sana.Β 

    β€œSheby amefanya nini?” aliuliza mmoja wao akiwa anamtikisa bega, walionekana kumjua huyoΒ  Sheby na pengine alikua ni Mtu wao wa karibu.Β 

    β€œSheby eeeee haaaaa‼” alitoa sauti kubwa iliyoambatana na kilioΒ 

    β€œSheby amefanya nini?” aliuliza mwingine, shahuku ikazidi kuwa kubwa, siyo kwao tu hataΒ  kwangu. Taratibu nilianza kupiga hatua ndogo za kuhebu ili nisikie neno.Β 

    β€œAmekufaaβ€Ό ajali jamani aaaah Maisha hayaaaβ€Ό!” yule Mwanaume alizidi kuendelea kulia,Β  Watu walisikitika sana kusikia taarifa za kifo cha huyo Mtu, papo hapo akili yangu ikakaa sawaβ€Ό Yes, Dalali niliyewasiliana naye anaitwa Sheby. Nilihisi mwili kama unatengana na roho yanguΒ  Jamani, nilikua na tumaini la kupata majibu ya maswali yangu kwa huyo Sheby halafu ghaflaΒ  nasikia taarifa ya kifo chake.Β 

    Niliishiwa nguvu, nikasogea na kuketi juu ya gogo moja. Ndiyo maana simu zangu zilikuaΒ  hazipokelewi, nilipata mfadhahiko mkubwa sana. Chozi lilikua likinimwagika, nilijuwa kua kunaΒ 

    jambo lisilo la kawaida linaloondoa uhai wa Watu wasio na hatia, moyo wangu ulivunjikaΒ  vipande vipande hata ile nguvu niliyokuja nayo ilipungua kabisa.Β 

    Nilitazama juu huku chozi likizidi kunibubujika kutoka machoni kuteremka hadi mashavuniΒ  kisha kwenye gauni langu, nilihisi Dunia ikizunguka. Nilikosa majibu ya maswali yangu yote,Β  Uchungu ulipanda kutoka kifuani niliuhusi ukija hadi puani na kunipa maumivu makali sana.Β  Hali ya mafua ya ghafla ilianza pale pale nikiwa bado kichwa changu kimeelekea juu.Β 

    Imani ya moyo wangu iliniambia kua Mungu alikua angani akinitazama kila hatua lakiniΒ  hakutaka kunisaidia, nilisema ndani ya Moyo wangu.Β 

    β€œEeh Mungu, nitapoteza wangapi? Hii ni ndoto, niamshe basi nikutane na wapendwa wangu”  niliumia sana ndani ya moyo wangu, Mungu aliniachia mizigo yote niibebe mwenyewe katikaΒ  wakati mgumu ambao kila niliyemshilisha alikufa kifo cha ghafla. Nilipoteza Watu watatu,Β  mmoja ni dalali niliyeamini alikua akiyajua mazingira ya nyumba yetu na wengine ni marafikiΒ  zangu wawili niliowapenda kama nilivyozipenda mboni za macho yangu.Β 

    Ghafla nilisikia sauti kando yangu, nilishtuka. Ilikua ni sauti ya kiume iliyoanza kwa utaratibuΒ  sana kisha kuniachia tabasamu la mwongeaji.Β 

    β€œPole, haijalishi unapitia nini kwenye Maisha yako. Mungu atashinda na wewe” niligeuka harakaΒ  kumtazama aliyeongea, alikua upande wangu wa kulia, ni Mwanaume mwenye ndevu nyingi,Β  mtanashati aliyenizidi Umri lakini alikua rika langu.Β 

    Nilisogea pembeni haraka kwa hofu maana sikutaka kumwamini Mtu yeyote yule.Β 

    β€œUsiogope Celin‼” Mungu wangu, alinifahamu kwa jina. Hii siyo tu ilinishtua pia iliniacha naΒ  Butwaa la ajabu sana, nikamkumbuka yule Bibi wa Ajabu ambaye alinisemesha kwenye treni naΒ  kuanzia hapo kila kitu kiliharibika.Β 

    β€œTafadhali kaa mbali na Mimi, hunijui sikujui. Jina langu siyo Celin” nilisimama kisha nilipazaΒ  sauti yangu, kila mmoja aliye jirani na sisi alitutazama kwa Mshangao na maswali mengi. YuleΒ  Mwanaume wala hakujali, aliendelea kutabasamu na kunidhihirishia kua alikua Mtu wa ajabuΒ  kama yule Bibi.Β 

    Niliondoka hapo haraka huku akiniita kwa jina langu akidai napaswa kumsikiliza, sikutaka hataΒ  kugeuka nyuma, niliyaziba masikio yangu ili hata kumbukumbu ya Sauti yake isibakie masikioniΒ  mwangu.Β 

    Nilipofika barabarani nilisimamisha Taxi ya njano kisha haraka nikaingia na kuketi siti ya nyumaΒ  kisha nikamuamuru dereva aondoe gari anipeleke chuoni, hapo chozi lilikua likinibubujika. BadoΒ  sauti yake ilikua inasikika masikioni mwangu. Maneno ya yule Mwanaume yalikua yakijirudia.Β 

    β€œEndesha haraka” nilisema kwa sauti ya juu ili dereva aongeze mwendo, nilikua nimegubikwa naΒ  woga wa ajabu, hofu na Mashaka vilikua vimenitawala kwa kiasi kikubwa sana. Nililia kamaΒ 

    Mtoto mdogo, sikujua nilikosea kuichagua ile nyumba au kuna mahali familia yangu ilifanyaΒ  kosa na sasa tunaadhibiwa.Β Β 

    Dereva aliongeza mwendo kama ambavyo nilikua nimemwambia. Nilikua nimejiinamia nikiwaΒ  nimeziba masikio yangu, taratibu ile sauti ilianza kupotea masikioni mwangu. Zilipita dakikaΒ  kadhaa ambazo zilitosha kwa dereva kukaribia chuoni. Nilijihisi nafuu sana, kisha nilitoaΒ  kitambaa na kujifuta chozi kisha nilifuta pua zangu.Β 

    Niliponyanyua Sura yangu nitazame nje nijuwe kama tulikua tunakaribia chuoni au laa,Β  nilipigwa na Butwaa nyingine. Nje ya gari palikua na Msitu mkubwa sana, halafu gari lilikuaΒ  likitembea kwa mwendo wa kawaida.Β Β 

    Nilipaza sauti yangu β€œ Wewe dereva umenileta wapi huku?” nilisema huku nikijaribu kufunguaΒ  mlango lakini ulikua umefungwa. Hofu niliyoiacha ilianza kunivaa upya halafu nikaisikia sautiΒ  ile ile ya yule Mwanaume niliyemkimbia akisemaΒ 

    β€œHaijalishi unapitia nini, kumbuka maneno yangu. Utashinda” Masikini, yule dereva alikua niΒ  yule Mwanaume niliyemkimbia, aliwezaje kuingia ndani ya gari sijui, nitamkimbia vipi sijui naΒ  kwanini anajua kila kitu kuhusu Mimi pia sijui.Β 

    Nilikua ninatetemeka sana. Kisha lile gari likachepuka kutoka barabara kuu na kuingia barabaraΒ  ya vumbi iliyo kimya sana, hapakua na yeyote.Β 

    β€œWewe ni Nani?” nilimuuliza nikiwa ninalia, nilijua haiwezekani tena kumkimbia. Kwa namnaΒ  alivyo siyo rahisi pia kupambana naye. Alisimamisha gari kisha aligeuka na kunitazama, suraΒ  yake ilionesha alikua na jambo kubwa analohitaji kuniambia.Β 

    Alinionesha sura ambayo haikua na hatia, wala hakuonesha kama alikua na nia ya kunifanyiaΒ  jambo baya, kisha kwa sauti ya taratibu aliniambiaΒ 

    β€œUsiniogope Celin, nahitaji Msaada wako. Nitakusaidia pi, tusaidiane” kauli hii ilianza kunipaΒ  tumaini la kuishi tena, kama alihitaji msaada wangu asingeliweza kunidhuru lakini haraka harakaΒ  akiwa ananiangalia nilijiuliza alihitaji Msaada gani kutoka kwangu wakati yeye anaonekana kuaΒ  ni Mtu wa ajabu ajabu kama yule Bibi.Β Β 

    Nilibabaika kumjibu, sauti ilitoka kwa wasiwasi tena isiyo na nguvu. β€œNikusaidie nini? TafadhaliΒ  usidhuru Maisha yangu” nilisema huku nikiwa ninalia, niliweka mikono yangu kifuani kwanguΒ  kwa isharaka ya kumwomba ahurumie Maisha yangu, alikuwa akinitazama nusu bega hukuΒ  mwili wake wote ukitazama mbele.Β 

    β€œNingekua na nia ya kuyadhuru Maisha yako ningefanya hivyo muda mrefu, nina ombi moja tuΒ  kwako Celin” Maneno ya yule yalianza kunipa tumaini zaidi na zaidi kua pengine nitapata nafasiΒ  nyingine ya kuishi, alionesha wazi kua alikua akinifwatilia kwa muda mrefu sana.Β Β 

    β€œNitakusaidia nini Mimi Kaka yangu?” nilimuuliza, angalau swali hili lilitoka huku nikiwaΒ  nimetuliza kilio changu.

    Alikunja midomo yake, ishara hii iliniambia ndani yangu kua alihitaji kuzungumza jambo zitoΒ  sana, alitafakari huku akinitazama akiendelea kukunja midomo yake. Halafu akaniambia β€œNatakaΒ  umtoe Dada yangu ndani ya nyumba yenu”  

    β€œDada yako?” 

    β€œNdiyo!” 

    β€œKivipi, ni yupi mbona sisi tunaishi watatu, Mimi na Wazazi wangu?” nilimuuliza huku moyoΒ  wangu ukiamini kua nilikua karibu kugundua siri fulani ya nyumba yetu. Alishusha pumzi zakeΒ  kisha akaniambiaΒ 

    β€œTeremka kwenye gari, nitakueleza zaidi. Najua una maswali mengi sana” alisema kishaΒ  alifungua mlango wa gari kisha aliteremka na kusimama mbele ya gari akiegemea β€˜Boneti’Β 

    Nilikua ninamtazama kwa makini nikiwa bado nina jishauri kama nitaweza kumwamini MtuΒ  nisiyemjua, lakini niliuvaa ujasiri wa ghafla kisha niliufungua mlango kirahisi sana, mlangoΒ  uliokua Mgumu hapo awali, safari hii ulifunguka nilipoutekenya.Β 

    Sekunde kadhaa nilikua nikiivuta hewa ya jua kali lililokua likiwaka nje, niliyatazama mazingiraΒ  tuliyopo. Niliona miti mingi iliyofungana, tulikua msituni japo kwa mbali nilisikia sauti yaΒ  magari yakitembea kwa kasi. Upepo wa taratibu ulikua ukiendelea na kufanya eneo hilo kua naΒ  hali mbili tofauti. Jua kali lakini pia upepo uliopoza joto kaliΒ 

    Taratibu nilitembea kuelekea mbele ya gari kumsikiliza yule Mwanaume, alikua mnene kiasi naΒ  pia alikua na ndevu nyingi mfupi wa wastani, alikua ananukia manukato makali sana. NilitembeaΒ  taratibu huku nikijikwaa jiwe dogo lililonipa mwendo zaidi hadi nilisogea kabisa karibu yake,Β  akanipa pole huku akigeuka na kunitazama nikitembea taratibu hadi nilipofika mbele yake.Β 

    β€œUsiwe na wasiwasi Celin, usiogope sababu nusura ya Maisha yenu yapo mikononi mwako” niliyafinya macho yangu kwa mshangao mkubwa sana, moyo ulilipuka ghafla na kuanza kwendaΒ  mbioΒ 

    β€œUnamaanisha nini?” nilimuuliza nikiwa na mhemko wa alichoniambia, tayari nilikuaΒ  nimepoteza marafiki zangu wawili.Β Β 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA

    COMMENTS ZIWE NYINGI SASAΒ 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

     

     

    riwaya mpya riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni riwaya za kuvutia soma riwaya bure

    28 Comments

    1. David ben on April 28, 2025 10:22 pm

      Nzuri dah

      Reply
    2. Monica on April 28, 2025 10:57 pm

      Mwendelezo jamn story nzuri sana

      Reply
    3. Kelly1366 on April 29, 2025 5:27 am

      Very good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    4. Brama05 on April 29, 2025 11:55 am

      Hii ya Moto mbn sehemu ya 6 itoke leoleo tu

      Reply
    5. Rio on April 29, 2025 12:18 pm

      Sehemu ya sita bhc dah

      Reply
    6. Rio on April 29, 2025 12:19 pm

      Sehemu ya sita πŸ™

      Reply
    7. Marvin4520 on April 29, 2025 12:49 pm

      Good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    8. Piana on April 29, 2025 12:55 pm

      Next plz

      Reply
    9. Lusitaah on April 29, 2025 1:50 pm

      Admin nkuonba leo leo toa sehemu ya sita

      Reply
      • Rodgers on May 1, 2025 10:32 am

        Wow nimeipenda

        Reply
    10. Mercy on April 29, 2025 2:08 pm

      Noma sanaaaa

      Reply
      • Sospiter Paulo on April 29, 2025 7:38 pm

        Good

        Reply
    11. G shirima on April 29, 2025 2:15 pm

      Watunzi mnatumia akili nyingi sana adi nimecheka mwenyewe adi kujikwaa kwenye kijiwe kidogo

      Reply
    12. Igor3112 on April 29, 2025 2:25 pm

      Good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
      • Sospiter Paulo on April 29, 2025 7:38 pm

        Very nice .give us next episode

        Reply
    13. Aura on April 29, 2025 2:43 pm

      Leoleo tuendelee admin bas

      Reply
    14. Melstusi lungika on April 29, 2025 3:57 pm

      Next please

      Reply
    15. Astery Komba on April 29, 2025 4:13 pm

      harakisha ya 6

      Reply
    16. Calvin paul on April 29, 2025 4:24 pm

      Ni fireeee

      Reply
    17. Hamisi halidi on April 29, 2025 4:52 pm

      Duh kwel πŸ’₯πŸ’₯

      Reply
      • Neema on April 29, 2025 6:19 pm

        Inauma sana ila celin ni jasiri sana

        Reply
    18. Yamungu.E.Dawson on April 29, 2025 10:54 pm

      Duuuh!!….mpaka nimeogopa kuisoma usiku,,,,,inatisha saaana.
      But all in all, well done.

      Reply
    19. KingzJeelay on April 30, 2025 7:40 am

      Mifano tenaaaaπŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ’ͺ🏽πŸ’ͺ🏽πŸ’ͺ🏽

      Reply
    20. Hector2592 on April 30, 2025 10:28 am

      Good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    21. Mtu baki on April 30, 2025 2:29 pm

      Admin tunasubr ya sita

      Reply
    22. JACKSON JACKSON on April 30, 2025 3:31 pm

      Ooh woow, stori nzurii sana asee,, nimeipenda sana

      Reply
    23. Said on May 1, 2025 6:56 am

      πŸ‘

      Reply
    24. Cathbert on May 2, 2025 3:37 pm

      Mwisho wa matatiz unakalibia

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.