Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Kwanza – 01)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Kwanza – 01)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaApril 23, 2025Updated:April 27, 202538 Comments12 Mins Read8K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Tunaanza simulizi yetu ya Nyumba Juu Ya KABURI kwa namna hii

    Ilikua ni ndoto ya Baba yangu, siku moja akistaafu angenunua nyumba nzuri ya kuishi, wazo hiliย  lilitupatia tabasamu katika nyakati zake za mwisho kazini. Alifundisha shule ya Msingi kwaย  Miaka zaidi ya 20, macho yake yalichoka kwa vumbi la Chaki. Alizeeka haraka kulikoย  ilivyokadiriwa, alibahatika kuowa Mke mzuri mwenye kuipenda familia.ย 

    Baraka nyingine ilikua ni kunizaa Mimi, walinipa jina la Celin, lilikua ni jina la marehemu Bibiย  yangu. Japo mwanzo Mama alikua hataki majina ya kurithi lakini Baba alisistiza hadi jinaย  likakubalika, Mimi ndiye Celin.ย ย 

    Mara zote Baba yangu hujivunia Mimi, nimerithi akili za Baba yangu. Njia yangu ilionekanaย  mapema sana nikiwa na Miaka saba, Baba alipambana kunisomesha kwa Mshahara wake mdogoย  hadi nikafika chuo Kikuu. Nilisafiri kwa ajili ya Masomo ya Chuo Kikuu maarufu Nchini.ย  Nikiwa nakaribia Likizo yangu, siku moja Baba alinipigia simu.ย 

    Ilikua majira ya Usiku, nilikua nimejilaza kitandani nikiutafuta Usingizi, niliposikia simu yanguย  ilikua ikiita. Mara moja niliipokea nikiwa mwenye furaha kubwa sanaย 

    โ€œCelinโ€ Baba aliniita kwa sauti ya furaha, nilihisi ana jambo fulani la kuniambia. Nilitabasamuย  huku nikimtaka Baba aliseme jambo hilo haraka sana.ย ย 

    โ€œMwanangu, Pesa za mafao yangu zimeingizwa jioni ya leo. Nilisubiria muda ambao ungekuaย  umemaliza pirika zako ili nikuelezeโ€ Baba alisema kwa sauti ya Ubaba ambayo ilinifanya nijioneย  Mimi ni Mtu muhimu sana kwake.ย 

    โ€œEnheeโ€ผโ€ย ย 

    โ€œMimi na Mama yako tumekaa tumefikiria sana, tumeona ni bora tuwe karibu na wewe. Siย  unaikumbuka ndoto yangu?โ€ Baba aliniuliza, nisingeliweza kuisahau ndoto yake ya kununuaย  nyumba lakini nilijiuliza wanahitaji kuwa karibu na Mimi kivipi.

    โ€œSiwezi kusahau Baba, lakini mnataka kuwa karibu nami kivipi?โ€ย 

    โ€œTunahamia Mjini, Mjomba wako Mgina ametuambia kuwa atatusaidia kupata nyumba huko.ย  Hatutaki tena kuishi Kijijiniโ€ Nilichokisikia kiliamsha furaha yangu kwa kiasi kikubwa sana,ย  sikuamini. Nilipiga kelele kwa furaha sanaย 

    โ€œBaba unajua siamini kabisa Kama itatimia hivi karibuniโ€milisema kwa shahuku kubwa sana.ย ย 

    โ€œAmini Binti yangu, tayari nyumba imepatikana. Mjomba wako atakupigia simu keshoย  ukaiangalie, kama ni nzuri utatuambia ili tufanye malipo, Mimi na Mama yako tuje mara mojaย  Mjiniโ€ Kiukweli siwezi kuficha, mazungumzo haya yalikua ndio mazungumzo ya furaha zaidiย  kuwahi kunisisimua kiasi cha kupagawa.ย ย 

    Kwa kipindi cha Mwaka Mmoja na miezi kadhaa nilitengeneza marafiki ambao walikua wakiishiย  Mjini, ilinipa uhakika wa kuendelea nao endapo tutapata nyumba ya Kuishi. Siku yangu iliishaย  ikiwa imeniacha na furaha sana.ย 

    Mwanzo wa kila kitu.ย 

    Siku iliyofuata niliamka mapema sana, nilijiandaa huku nikiweka simu yangu kando yangu kilaย  dakika nikiichungulia kama Mjomba Mgina alikua akipiga. Majira ya saa tatu asubuhi alinipigia,ย  niliipokea kwa shahuku kubwa sana, nilisimama kando ya dirisha huku nikiangalia mandhari yaย  nje iliyojaa Miti mirefu na Bustani kadhaa.ย 

    โ€œCelin, uko tayari?โ€ aliniuliza baada ya salamu, jibu langu lilikua ndiyo.ย ย 

    โ€œNakutumia Namba ya Dalali, bahati mbaya siwezi kufika. Japo nilipendelea niwepo lakiniย  naamini unaweza ukafanikisha ndoto ya Baba yakoโ€ alisema.ย 

    โ€œHakuna shida Mjomba, Tayari mimi ni mwenyeji hapa Mjini. Nina uhakika na hilo, ondoaย  shakaโ€ nilimjibu kwa sauti yangu laini iliyojaa adabu niliyofundishwa na wazazi wangu. Baadaย  ya simu kukatika, mara moja namba ya Dalali iliingia kwenye simu yangu, ilikua ni hatua mojaย  mbele kuelekea kutimiza ndoto ya Muda mrefu ya Baba yangu.ย 

    Nilipozungumza na Dalali, alinielekeza ni wapi tutakutana. Alipendelea tukutane njia panda yaย  kuelekea Benki ya Taifa. Nilichukua Taxi kuelekea huko huku nikiwa na shahuku kubwa sana,ย  kichwani mwangu nilijenga taswira ya aina ya nyumba ambayo nitaoneshwa.ย 

    Tabasamu halikukauka usoni pangu hadi tunafika Njia panda. Nilimlipa dereva pesa yake kishaย  niliteremka na kuangaza huku na kule kabla ya kumpigia, alinipungia mkono akiwa kando yaย  barabara. Nilisogea hapo kisha tulitumia Pikipiki moja, haikua ajabu sababu ni usafiri waย  kawaida sana.

    Alinipeleka mtaa mmoja uliotulia sana, mandhari tu ya mtaa yalinivutia sana. Palikua kimya bilaย  kelele za aina yoyote ile, kisha tulitembea kidogo baada ya kushuka kwenye Pikipiki. Dakikaย  tano baadaye tulisimama nje ya nyumba moja ya ghorofa moja.ย 

    Haikua nyumba niliyoitegemea, japo ilikua nzuri sana kwa nje. Ilikua na Bustani nzuri na hali yaย  hewa ya kuvutia macho na Masikio. Nilisisimka kidogo kisha nikaomba nipelekwe ndani yaย  nyumba hiyo iliyojengwa kwa Mtindo wa ajabu kidogo, ilionekana ni nyumba ambayo yenyeย  mtindo wa nyumba za Ughaibuni. Ilikua na asili ya Uingereza hivi,ilikua rahisi kwanguย  kugundua hilo sababu nilikua nasomea masomo ya Mazingira na usanifu wa Majengo.ย 

    โ€œHii nyumbaaโ€ผโ€ nilitamani kumuuliza dalali, jambo lililonijia kichwani ni asili ya hiyo nyumba.ย  Aliniwahi kama vile alikua kichwani kwangu, alinijibu haraka tena kwa ucheshi wa Kibiasharaย  kama ilivyo kawaida yao.ย 

    โ€œIko tofauti sana na nyumba za Mtaa huu, ni hii pekee imejengwa kizungu zaidi. Usijali, hiiย  nyumba ilijengwa Muda mrefu kidogo lakini bado inavutia sana, ina uimara pia mazingira yakeย  ni kama unavyoyaonaโ€ alikua akiongea huku akiitupa mikono yake kunionesha huku na kule,ย  aliyazungusha macho yake kama Pia hivi, hata hivyo nilitabasamu kisha akaendeleaย  kunizungusha.ย 

    Baada ya kuzunguka maeneo ya nje nilianza kubadilisha mtazamo wangu juu ya nyumba hii,ย  nilianza kuipenda, tukaingia ndani. Tulizunguka kila mahali, nilikubaliana na dalali kua ilikua niย  nyumba nzuri sana ambayo hata Baba yangu angeipenda. Pale pale nilimpigia simu Baba naย  kumweleza kua ni nyumba nzuri ya ghorofa moja. Baba aliniuliza mara mbili mbili kama kweliย  nilikuwa nimeipendaย 

    โ€œBaba ni nzuri sana, ina hewa. Mazingira yake yametulia sana kuliko nilivyofikiria mwanzoโ€ย  nilisema huku nikiwa nimesimama kando ya Dirisha kubwa la juu.ย 

    โ€œKama wewe Celin umeipenda basi nitazungumza na Mjomba wako, kila kitu kitaenda sawa.ย  Hesabia kua hiyo ni nyumba yetu mpyaโ€ alisema Baba.ย 

    โ€œUnanisisimua Baba, ngoja niangalie zaidi Basiโ€ Nilimuaga Baba, Nikiwa na tabasamu teleย  machoni pangu nilianza kuhisi hali fulani ya ajabu. Nilihisi kama nyuma yangu palikua na Mtuย  mkubwa anayekuja taratibu, kivuli chake kilikua kinanisogelea na kwa hakika nilikiona kwa macho yangu kupitia jicho la wizi.ย 

    Nilijawa na hofu sana, niliamua ni bora nigeuke nione ni Nani aliyekua nyuma yangu. Niligeukaย  haraka kwa hofu sana, hapakua na yeyote yule isipokua nilisikia sauti ya Dalali akiniuliza kamaย  nilikua tayari nimemaliza kuongea na simu.ย 

    Nilishusha pumzi zangu, kichwani mwangu na moyoni mwangu nilijiambia ilikua ni hisia mbayaย  ya ghafla. Mara aliingia Dalali, nilijitahidi kujiweka sawa nisimuoneshe wasiwasi wowote ule.ย  Hata hivyo sikua na uhakika na hisia zangu, nilichowaza kilipotelea mawazoni, sikutaka kukipaย  kipaumbele, niliachia tabasamu

    โ€œNimemalizaโ€ nilimjibu, alikua tayari amenisogeleaย 

    โ€œAnasemaje?โ€ aliniulizaย 

    โ€œAtawasiliana na Mjomba Mgina, halafu watarudi kwako kwa ajili ya kukamilisha taratibu zaย  mauzo. Samahani, hii inagharimu pesa ngapi?โ€ nilimuuliza, muda wote tulikua tunazunguka bilaย  hata Mimi kujua nyumba ilikua inauzwa shilingi ngapiย 

    โ€œMwenye Nyumba anataka Milioni 84 tu, ameishusha bei ili aiuze. Kama mtachelewa kidogoย  basi inaweza kuuzwa maana ipo sokoni sanaโ€ alisema Dalali, nilizungusha macho yanguย  kuitathmini upya. Namna ilivyo na kiasi kilichotajwa vilikua mbingu na ardhi. Nyumba nzuriย  kiasi kile, tena ya ghorofa halafu ipo Mjini iuzwe kwa bei rahisi kiasi kile?ย ย 

    โ€œVipi mbona kama unatafakari jambo?โ€ aliniuliza, aligundua tafakari yangu. Sikutaka kufanyaย  mambo yawe magumu, nilimwambiaย 

    โ€œHakuna kitu, hakika ni nyumba nzuri sana. Baba atainunua haraka siyo jambo la kujali, pesa ipoย  mfuko wa shatiโ€ yule Dalali alitabasamu kisha akaniambiaย 

    โ€œHamtojutia kuinunua, nawahakikishiaโ€ alisema kisha tulishuka chini, kisha tulitoka ndani yaย  nyumba. Tulianza safari ya kutoka kabisa nje ya uzio. Tulipofika nje kabisa niliangaza huku naย  kule, nyumba ya Jirani nilimwona Mzee Mmoja aliyevalia Baraghashia, alikua akisoma gazeti.ย ย 

    Alivalia singlendi nyeupe, chini alikua amevalia msuli, nilipomtazama kwa makini niligunduaย  alikua akitutazama kwa macho ya wizi. Nilitamani kujua kwanini alikua akitutazama vile, alikuaย  ameketi kwenye kiti cha kukunja.ย ย 

    Macho ya yule Dalali yalikua kwangu kisha kwa yule Mzee, alionekana ana wasiwasi fulaniย  alioamua kuuficha kwa makusudi, sikujua alikua akificha nini kupitia macho yake. Mara mojaย  yule Mzee alinyanyuka na kuingia ndani, niliporudisha macho yangu kwa dalali alianzaย  kuniambiaย 

    โ€œMazingira ni mazuri sana, mwenye umeona hakuna kelele. Jitahidi sana muichukueโ€ย ย 

    โ€œUsijali, kwanini yule Mzee alikua akitutazama kwa jicho lile?โ€ sikutaka kuliacha jambo lile hiviย  hivi, Dalali akaniangalia kama Mtu aliyekua akitafuta cha kuongea kisha akaniambiaย 

    โ€œPenye kheri hapakosi husda, naye ni Dalali pia. Hawezi kufurahia pesa ya Udalali ikiingia kwaย  mwingine, anaihangaikia sana nyumba hii kuiuzaโ€ alinipa jibu ambalo lilinifungua kidogo naย  kunipa mwanga kiasi fulani nikatoka gizani, niliondoa wasiwasi wangu. Basi,tuliachana hapoย  nikachukua Bajaji kurudi Chuoni nikiwa tayari nina uhakika kua kila kitu kipo sawa.ย 

    Kila kitu kilienda sawa, Baba aliinunua ile nyumba kwa bei rahisi sana, alipofika Mjiniย  alishangaa sana kukutana na nyumba nzuri ya ghorofa moja tena iko Mjini. Tulihamia ndani yaย  Nyumba yetu mpya, Maisha mapya yalianza.

    Maisha mapya Mjini yalianza kwa furaha sana, kuwaona Wazazi wangu wakiwa kando yanguย  ilinipa faraja na nguvu ya kuzidi kusoma kwa Bidii. Baba yangu aliishi kama Mstaafuย  aliyetimiza malengo yake, aliandaa tafrija fupi kusherehekea Miaka yake ya kazi. Tuliwaalikaย  ndugu jamaa na marafiki walioko Mjini, tuliandaa chakula, nyama choma na vinywaji vyaย  kutosha.ย 

    Marafiki zangu Ziada na Caren walifika nyumbani kwetu, waliisifia sana nyumba yetu.ย  Tulifurahi kwa pamoja eneo la Bustani mahali ambapo Tafrija hiyo ilikua ikifanyika. Tafrijaย  ilifanyika Usiku kama saa mbili hivi, ilimlazimu Baba kupanga muda huu ili kutupatia fursa sisiย  Wanafunzi tuwepo baada ya muda wa chuo kwisha.ย 

    Vinywaji vilikua vya kutosha, anayejisikia kunywa soda aligida, anayejisikia kunywa maji kamaย  Mimi naye aligida, wanaopenda bia waligida pia. Muziki wa taratibu ulikua ukituburudisha hukuย  stori za hapa na pale zilikua zikiendelea.ย 

    Nikiwa nazungumza na marafiki zangu nilimwona tena yule Mzee wa nyumba jirani, alikuaย  amevalia shati lenye vyumba vidogo vidogo vya rangi nyeusi na nyekundu, alivalia mawani yaย  macho, alikua amesimama getini. Sikumbuki kama nilimwalika hapo, istoshe hakuna aliyekuaย  amemzoea. Nilishtuka kidogo, nikawatazama Ziada na Caren kisha nikawaambiaย 

    โ€œSamahani, nakujaโ€ nilisema huku nikiweka mezani glasi yangu ya soda, lakini ziada akanishikaย  mkono, alikua ametumia kilevi kidogoย 

    โ€œCelin, nahitaji kutumia chooโ€ aliniambia, nilipeleka macho kwa yule Mzee kuona kama alikuaย  pale pale getini, ndiyoโ€ผ alikua amesimama bado akiniangalia bila kutingisha shingo yake,ย  nikayarudisha macho kwa Ziada.ย 

    โ€œPandisha juu, mkono wa Kuliaโ€ nilisema, nilimtaka aende mwenyewe ili Mimi nikazungumzeย  na yule Mzee.ย 

    โ€œTwende nitamsindikiza, usijali Celinโ€ alisema Caren, niliachia tabasamu la kukubali waende iliย  nikaongee na yule Mzee, hisia yangu ya ndani ya moyo wangu iliniambia jambo moja kuhusuย  yule Mzee.ย 

    โ€œKuna jambo huyu Mzee analijuaโ€ nilijisemea, niliwasindikiza kwa macho Caren na Ziadaย  wakielekea ndani kwa ajili ya kutumia choo, nilipohakikisha kua walikua wameshaingia ndani,ย  niliangaza huku na kule kama kuna Mtu yeyote aliyekua akimtazama yule Mzee, niligundua kilaย  Mtu alikua bize na maongezi ya hapa na pale.ย ย 

    Nilishusha pumzi zangu kisha taratibu niligeuka na kuelekeza macho yangu getini, nilistaajabuย  kutomwoma tena yule Mzeeย 

    โ€œAtakua ameenda wapi?โ€ nilijiuliza, niliangaza huku na kule lakini niliambua patupu, harakaย  nikaelekea getini mahali ambapo palikua na umbali wa hatua zaidi ya ishirini kutoka eneo laย  Bustani ambako Palikua na tafrija.

    Palikua kimya sana, niliangaza huku na kule, swali pekee lililozunguka kichwani kwanguย  nilijiuliza ni kwanini alikuja nyumbani kwetu, alialikwa na Nani, kwanini alikua akinitazamaย  sana? Nani angenipa majibu ya maswali haya isipokua yule Mzee lakini yuko wapi, si getiniย  wala karibu na eneo nililopo. Macho yangu yakaingiwa na shahuku ya kutazama nje.ย 

    Niligeuza shingo kuwaangalia wazazi wangu, walikua bize na wageni. Niliona ni bora nimtafuteย  zaidi yule Mzee wa nyumba jirani. Hata nilipofungua geti hakuwepo, palikua kimya sana.ย ย 

    โ€œAu atakua ameelekea nyumbani kwake?โ€ nilijiuliza, bado kiu ya kutaka kumuuliza iliendeleaย  kunishika, moyo wangu uligawanyika vipande viwili, kimoja kikiniambia niende nyumbani kwaย  yule Mzee haraka, kingine kiliniambia nitazungumza naye kesho. Kila nilichohitaji kukifanyaย  nilijiona mzito sana, kwenda ndani au kuendelea na safari.ย 

    Kipande kimoja kiliishinda hii vita nzito ya dakika moja ya kusimama nje ya geti nikipigwa naย  Baridi. Nilipata ujasiri wa ajabu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee, ilikua ni nyumba ya jirani,ย  wastani wa hatua chache sana. Mbwa walikua wakibweka sana nyumba moja inayotazamana naย  nyumba yetu lakini sikuogopa.ย 

    Mwili ulinisisimka kwa kiasi fulani lakini sikujali sana, kila nilivyozidi kupiga hatua ndivyoย  mwili ulivyozidi kusisimka na kunipa hali ya hofu, mtaa ulikua kimya isipokua sauti ya Mbwaย  na Upepo fulani wa hapa na Pale, nilisimama na kuangalia nyuma. Hakuna Mtu, mbele hakunaย  Mtu, mi Mimi na fikra zangu, mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio.ย 

    Niliweka pumzi sawa ili nizidi kusonga mbele, mara nilisikia sauti ya Caren.ย 

    โ€œCelin, unaenda wapi?โ€ sauti ilinishtua, sikutegemea kuisikia. Bado nilikua nimetazama mbele,ย  nikakata shauri nikageuka. Caren alikua ameshanisogelea, mkononi alikua ameshikilia chupa yaย  Bia.ย 

    โ€œWhat is wrong? ( Kuna tatizo?)โ€ Aliuliza kwa udadisi wa hali ya juu, japo alikua amelewa kiasiย  lakini alionekana kuwa na wasiwasi, haraka niliachia tabasamu la kujibalaguza na kufanyaย  dimpozi zangu zionekane.ย 

    โ€œAahโ€ผ hapana, nilikuaโ€ฆyessโ€ผ hakuna kitu, tunaweza kurudi ndaniโ€ niliamua kusema uwongo,ย  sikutaka kumweleza yeyote yule juu ya wasiwasi wangu na hatua ninazozipiga. Bado mbwaย  alikua akibweka sana, tulipiga hatua za taratibu kurejea nyumbani huku nikiwa nina hisia kuaย  kuna Mtu nyuma yetu alikua akitutazama.ย 

    Caren alisimama baada ya kuniona simjibu alichokua akinisemesha, nilianza kuhema kwa kasi,ย  hofu ilikua imenitawala vya kutosha.ย 

    โ€œKuna nini Celin?โ€ aliniuliza, nilimjibu Caren kwa sauti ya chini iliyojaa hofu na mtetemo waย  Uwoga uliopitiliza.ย 

    โ€œKuna Mtu nyuma yetuโ€ Nilitamani kulia kwa jinsi woga ulivyokua umenishika, Caren aligeukaย  nyuma kisha akarejesha macho kwangu. Akaangua kicheko na kuanza kuongea kama mlevi .

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Piliย 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

    riwaya mpya Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni Riwaya ya Fungate Riwaya ya Goryanah riwaya za bure

    38 Comments

    1. Lus twaxie on April 23, 2025 8:08 pm

      Wa kwanza miee admin

      Reply
      • Mofire on April 23, 2025 9:06 pm

        Kuna mtu nyuma yetu…itakuwa wew admini

        Reply
        • cathy on April 23, 2025 9:54 pm

          Nzury sana sehem ya pili jmn๐Ÿ˜…

          Reply
          • Wasokye Ramazani on April 24, 2025 9:28 am

            Yes, hii noma sana. Nitakufa nayo mwanzo mwisho !!

            Reply
          • Neema gervas on April 24, 2025 4:04 pm

            Nzuri mno

            Reply
        • Me_salmah on April 25, 2025 6:49 am

          ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚haaa

          Reply
      • Phina on April 23, 2025 9:35 pm

        Nzuri

        Reply
    2. Silva on April 23, 2025 9:06 pm

      Riwaya ni ya ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
      • Neema gervas on April 24, 2025 3:41 pm

        Nzuri mno

        Reply
    3. Dark phoenix on April 23, 2025 9:10 pm

      Very good story

      Reply
    4. Nyaiboitz on April 23, 2025 9:11 pm

      Noma sana

      Reply
      • Alhaji Kising'a on April 25, 2025 12:15 am

        ๐Ÿค

        Reply
    5. Classic loverz on April 23, 2025 9:29 pm

      Kaliii

      Reply
      • Phina on April 23, 2025 9:36 pm

        Hatar

        Reply
      • Wasokye Ramazani on April 24, 2025 9:30 am

        Ina sisimua adm ๐Ÿ™

        Reply
    6. KingzJeelay on April 23, 2025 9:31 pm

      Uhuuuuuuuuu….โค๏ธโ€๐Ÿ”ฅโค๏ธโ€๐Ÿ”ฅโค๏ธโ€๐Ÿ”ฅโค๏ธโ€๐Ÿ”ฅโค๏ธโ€๐Ÿ”ฅ
      Add more

      Reply
      • Joely on April 24, 2025 4:34 pm

        Ni balaa

        Reply
    7. KingzJeelay on April 23, 2025 9:32 pm

      Mambo ni ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    8. Phina on April 23, 2025 9:35 pm

      Nzuri

      Reply
    9. Jasmine3343 on April 23, 2025 9:47 pm

      Very good https://shorturl.at/2breu

      Reply
    10. Mgote on April 23, 2025 9:50 pm

      ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅโœŠ

      Reply
    11. Young sir on April 23, 2025 10:10 pm

      Nazipenda simulizi kama hizi

      Reply
    12. Henry598 on April 23, 2025 10:34 pm

      Very good https://shorturl.at/2breu

      Reply
      • Sharyf shabani Jumanne on April 24, 2025 6:45 am

        Nice story

        Reply
        • Wasokye Ramazani on April 24, 2025 9:31 am

          Ina sisimua adm, simulizi kama hizi hua nazipenda kinomanoma

          Reply
      • Layman Donsue on April 24, 2025 7:32 am

        Nzuri kabisa.. kama unapenda simulizi tukutane kwenye hii page huku.. https://whatsapp.com/channel/0029VaiF6i065yD2Hm0hdH0F

        Reply
    13. Slavius nguvumali on April 23, 2025 11:59 pm

      Ya motooo

      Reply
    14. Boniventure raphael on April 24, 2025 7:12 am

      Daah nzur sana asee

      Reply
    15. Beryl3190 on April 24, 2025 11:34 am

      Awesome https://shorturl.at/2breu

      Reply
    16. Nailaty on April 24, 2025 2:33 pm

      Iko fireee

      Reply
    17. Fau the boss on April 24, 2025 4:49 pm

      Nice

      Reply
    18. Hamisi halidi on April 24, 2025 8:34 pm

      ๐Ÿ’ฅ๐Ÿ’ฅ

      Reply
    19. Maya3718 on April 27, 2025 4:30 am

      Awesome https://t.ly/tndaA

      Reply
    20. Anthony1874 on April 29, 2025 10:22 pm

      Good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    21. Justin Peter on April 30, 2025 11:01 pm

      Imenyooka โ™ฅ๏ธ

      Reply
    22. Walter1047 on April 30, 2025 11:41 pm

      Awesome https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    23. Cathbert on May 1, 2025 10:04 am

      Mzuri

      Reply
    24. ๐Ÿ–‹ ๐ŸŽ‰ Limited Promo: 0.4 BTC gift available. Get now >> https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=465becb0f053293ebbfdbdd92b35c690& ๐Ÿ–‹ on September 9, 2025 9:20 pm

      g1dq3h

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE โ€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.