Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» MSALA Sehemu Ya Ishirini Na Sita-26
    Hadithi

    MSALA Sehemu Ya Ishirini Na Sita-26

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaSeptember 7, 2024Updated:September 7, 20249 Comments13 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    MSALA
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Muhonzi akafanikiwa kukata kamba alivyofungwa, giza lilikua nene ndani ya ChumbaΒ  alichohifadhiwa, akajaribu kuchungulia dirishani kwa mtindo wa kuruka sababu dirishaΒ  lilikua juu sana lakini hakuambulia kuona chochote kile, akajaribu kuitaΒ 

    β€œKuna nani hapo nahitaji Maji” aliita kwa makusudi huku akifahamu fika kua eneo hilo linaΒ  ulinzi mkali kuhakikisha yeye hachomoki, akaita tena, ndipo aliposikia hatua za kiatu zikijaΒ  upande wake, akarudi haraka kuketi sakafuni alipokua ameketi.Β 

    Mara taa ikiwashwa, kisha akatupiwa maji aliyoyataka. EndeleaΒ 

    SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

    β€œNitakunywaje sasa na umenifunga kamba?” akauliza Muhonzi kwa ujanja huku akiwa tayariΒ  ameshakata ile kamba, yule Mlinzi akamtazama sana MuhonziΒ 

    β€œNi kweli sasa nitakunywaje nina kiu sana Aaaaaahhh” akazidi kusema Muhonzi hukuΒ  akijibaraguza kama Mtu aliyefungwa mikono yake, yule Mlinzi ikamlazimu kufungua sasaΒ  mlango wote kisha akaingia ndani ya chumba hicho, ndicho alichokua anakitaka Muhonzi.Β 

    Akaoneshwa Bunduki, kisha akaambiwaΒ 

    β€œHuwezi kufanya ujanja wowote, nitakupa maji” alisema yule Mlinzi, akaiokota chupa yaΒ  maji kisha akaifungua na kumsogezea Muhonzi ili amyweshe, hakujua kua alikuaΒ  ameshafanya kosa kubwa sana, pale pale Muhonzi akamtandika ngumi nzito ya pua,Β 

    akamfwata kwa haraka na kumvunja shingo. Akaiyokota ile Bunduki kisha akaanza kutafutaΒ  njia ya kutoka ndani ya Godauni.Β 

    Akatembea kwa taratibu kwa mahesabu mazito sana ili asije rudi mikononi mwa Zagamba,Β  akasikia sauti ya TV, akajua fika kua Walinzi wengine walikua huko. Akasogea hadi eneoΒ  hilo na kuwakuta walinzi wakiwa wanakunywa pombe na kuvuta sigara.Β 

    Hakutaka kusema nao, akatafuta kona nzuri akapita ili alifikie lango kuu la kutoka ndani yaΒ  Godauni hiyo iliyojaa giza zito. Taratibu sana Muhonzi akalisukuma lango kisha akatoka njeΒ  ya Godauni, muda ulivyozidi kwenda ndivyo ambavyo wale Walinzi walivyoshtuka baada yaΒ  kuona mwenzao harudi, akatumwa mmoja wao kwenda kuangalia, akamkuta akiwaΒ  ameshakufa. Msako wa kutafutwa kwa Muhonzi ukaaanza ndani ya lile Godauni, walipokujaΒ  kugundua kua alishatoka ndani ya Godauni tayari Muhonzi alikua ameshafika mbali kabisa.Β 

    **Β 

    Baada ya kuchomoka mikononi mwa Watu wa Zagamba, akakimbilia kwenye jumba la siriΒ  ambalo alikua akilitumia kufanyia kazi zake, kichwa chake kikiwa kinawaka moto kwanzaΒ  alihitaji kujisafisha mwili mzima baada ya kukaa godauni kwa siku kadhaa.Β 

    Maji ya Baridi yakakubali kuuufanyia Utakaso wa kutosha mwili wa Muhonzi, akili ilipokaaΒ  sawa akawa tayari kujua ni wapi alipo Elizabeth, bado aliamini kuwa alikua hai. Jambo laΒ  kwanza alilolifanya baada ya kuketi na kuwasha mitambo yake ni kuanza kusaka mara yaΒ  mwisho simu ya Elizabeth ilizimwa wapi.Β 

    β€œPicha ya Ndege” ndiyo sehemu pekee ambayo simu ya Elizabeth ilizimwa kwa mara yaΒ  mwisho, aina ya simu aliyoitumia ilionekana lakini uzuri simu hiyo bado ilikua Hewani,Β  Usiku ulikua mwingi, akajipumzisha kwanza Kitandani ili akiamka aendelee na upekuziΒ  wake kwa njia ya Mtandao, masuala hayo ndiyo yaliyokoleza ukaribu wake na ElizabethΒ  Mlacha.Β 

    **Β 

    Saa 3 Asubuhi, TanzaniaΒ 

    Muuwaji wa kuaminika alikua akipata chai ya asubuhi sehemu fulani ya Tanzania, safariΒ  yake ya Usiku mzima ilikomea kwenye moja ya Hoteli, alipumzika hapo ili afanye safari yaΒ  kuelekea eneo nyeti la Black Site.Β 

    Baada ya kumaliza, aliingia kwenye gari kisha akaendelea na safari yake ya Masaa matatuΒ  baada ya Chai, sasa aliushika Msitu mmoja, akaisweka gari eneo fulani, akachukua begi lakeΒ  na kupandisha kilima kimoja. Alionekana ni Mtu anayejua anachokifanya, kazi aliyopewa naΒ  Waziri Mkuu ni kuhakikisha anamchukua Elizabeth kutoka Mikononi mwa Walinzi wa BalckΒ  Site.Β 

    Begi alilolibeba lilikua na silaha moja ya masafa marefu pamoja na Darubini, aliketi juu yaΒ  kilele cha kilima hicho, huku macho yake akiyaelekeza eneo la umbali wa Kilomita Nane,Β  hapo ndipo ilipo Black Site.

    Akatoa Ramani ya jengo la Black Site, ramani hiyo ilichukuliwa Ikulu baada ya Waziri MkuuΒ  kuikamata Ikulu, muuwaji akatabasamu. Kisha akalala usawa mzuri na kuiweka Bunduki yaΒ  Masafa marefu vizuri, akachukua Darubini na kuanza kulikagua jengo hilo kwa uzuri.Β 

    Akajifunika kofia nyeusi, kisha akairejesha Darubini ndani ya Begi, akaanza kuitumiaΒ  Darubini iliyo kwenye Bunduki yake, macho na hisia zake akayaelekeza ilipo Black Site,Β  eneo alilolala alikua akilitazama jengo hilo lenye vioo kwa uzuri sana.Β 

    Aliona na kuhesabu idadi ya Walinzi walio ndani ya Jengo ambao ni Makomandoo waΒ  kuaminika aliokua akiwatumia Rais Lucas Mbelwa, alihitaji kuwamaliza kwanza. Ndani yaΒ  jengo palikua na zaidi ya Makomandoo hamsini. Wote aliwapigia mahesabu, kisha akaikunjaΒ  Bunduki yake na kuizamisha ndani ya Begi, akarudi chini ya Kilima na kuanza kutembeaΒ  kwa kutumia barabara ya vumbi iliyokua ikielekea Black Site.Β 

    Muuwaji huyo, alipokaribia aligundua kwa haraka uwepo wa ulinzi maalum wa NyayaΒ  nyembamba za Umeme ambazo ndizo zilizokua zikilinda eneo hilo, alishajiandaa sababu siriΒ  za ulinzi wa ndani na nje ya Jengo alikua amezipata.Β 

    Akachomoa kifaa kidogo chenye mfanano na Simu, kisha akauzima umeme huo ndani yaΒ  sekunde ishiri akawa amezivuka nyaya hizo. Taratibu akakimbia na kujificha nyuma ya ukutaΒ  wa jengo la Black Site, kuhusu idadi ya walinzi wa ndani ya Jengo hakua na wasiwasi naoΒ  sababu alishawapigia mahesabu makali sana.Β 

    Akasimama hapo kwa mahesabu mazito, kisha akachungulia, jengo hilo lililokua na viooΒ  vingi ambavyo vingefanya urahisi wa Muuwaji kujulikana kua amefika, akapiga hatua zaΒ  haraka na kuuwahi ukuta wa pili, akajificha kisha akatoa kamba kutoka ndani ya Begi lake,Β  akairusha kamba kuelekea juu, iliponasa akawa na zoezi moja tu la kuifuata paa ya jengoΒ  hilo.Β 

    Kisha taratibu akatembea juu ya paa la jengo huku akiwa anapiga mahesabu yake vizuri,Β  alikua na ramani nzima ya jengo hilo la Black Site, ilikua rahisi kwake kujua ni wapi atawekaΒ  kambi hapo juu ya paa ya Jengo, akafika mahali ambapo palikua na pambo kubwa la saa,Β  eneo hilo lilikua karibu na mlango Mkuu wa Kuingia ndani ya Jengo hilo, kando ya jengoΒ  ndimo walimokua wakikaa makomandoo.Β 

    Kwake hao ndiyo kikwazo kikubwa kufanikisha kazi ya Kumchukua Elizabeth, akaiwekaΒ  vizuri kofia yake kisha akalala kwa ustadi mzuri huku akilitazama jengo ambaloΒ  Makomandoo walikua wakipatikana.Β 

    Akaishusha Bunduki yake ya Masafa marefu kutoka ndani ya Begi lake kisha, akaitega vizuriΒ  kuelekea kwenye jengo, kichwani alikua na ramani yote. Kitu pekee alichohitaji kukifanyaΒ  hapo ni kuufunga mlango wa Umeme ambao ndio uliokua ukitumika na Makomandoo hao,Β  mwendo wa dakika ishirini awe tayari ameshamchukua Mateka wake kwani kupambana naΒ  Makomandoo hao haikua kazi rahisi kwake.Β 

    Akafunga kiwambo cha kuzuia sauti, kisha akalenga kitasa cha Umeme ambachoΒ  kingemfanya atenganishe kati ya Makomandoo na Walinzi wa kawaida wa Black Site,Β  umbali wa jengo hilo ni zaidi ya Mita sabini.

    Dakika moja na nusu ilimtosha kujihakikishia kua risasi atakayoiachia hapo itaenda kukataΒ  mawasiliano ya jengo la Makomandoo na jengo la Black Site. Akavuta hewa nyingi kishaΒ  akaiachia taratibu na kukaza mikono yake kisha kidole kikafanya kazi ya kusukuma risasiΒ Β 

    Haraka Alam ikalia kuashilia kua palikua na hitilafu mlangoni, hii ni baada ya Muuwaji huyuΒ  kukita risasi mlangoni. Haraka walinzi wa Black site pamoja na Makomandoo walio ndani yaΒ  jengo lililopigwa risasi wakawa kwenye taharuki nzito, akasubiria kwa sekunde kadhaa iliΒ  Mlango wa Black Site ufunguliwe, alipousikua umefunguliwa akajirusha mithiri ya NyaniΒ  mzeeΒ 

    Akatua chini kama Buibui, haraka akaachia pigo takatifu la Risasi za mahesabu naΒ  kusambaratisha walinzi watatu waliokua eneo la Mlango kisha akaingia ndani ya Jengo hilo.Β 

    Elizabeth aliposikia Alam ikilia kuashiria kuna tatizo alishaanza kuhisi ujio wa Mtu mbayaΒ  ndani ya Jengo la Black Site, japo alikua amechoka sana lakini akaweza kumwambia MlinziΒ  kua amfungue kwani eneo hilo siyo salama kabisaΒ 

    β€œUsipofanya hivyo Utakufa” akakazia Elizabeth huku akijitingisha kwa nguvu chacheΒ  alizobakiwa nazo, yule Mlinzi hakutaka kumwelewa Elizabeth hadi pale aliposikia risasiΒ  ikisikika karibu na Mlango wa chumba cha Mateso ambacho Elizabeth alikua amehifadhiwa.Β 

    β€œNifungue tafadhali” alisema Elizabeth, lakini akili ya yule Mlinzi ikajikuta imezubaaΒ  kidogo, ghafla akapigwa risasi ya Kichwa, kisha Mlango ukafunguliwa, akaingia Muuwaji,Β  akamtazama Elizabeth kisha akatoa tabasamu la kufanikisha kazi yake.Β 

    Hakutaka kupoteza muda akamzimisha kwa kumchoma sindano ya Usingizi, akamfungua naΒ  kumweka begani, maiti za Walinzi zilikua za kutosha sakafuni, akatoka hadi nje ya Jengo laΒ  Black Site wakati huo Makomandoo wakiwa wanahangaika namna ya kufungua ule MlangoΒ  wa Umeme ambao kwa kawaida hufunguka baada ya dakika ishirini endapo utapata Hitilafu.Β 

    Akauvuka uzio wa Umeme kisha akaanza kuzikata Kilomita kuelekea lilipo gari lake aanzeΒ  safari ya kurejea Ikulu, mara zote alikua akiitazama saa yake kwa maana zikitimia dakikaΒ  ishirini wale Makomandoo watatoka ndani ya jengo na kuanza kumsaka kila kona. AkaianzaΒ  riadha baada ya kugundua kua alikua amebakisha dakika tatu kumalizika kwa ule mudaΒ  aliokua ameupangilia kulifanya tukio la kuvamia Black Site.Β 

    Ndani ya jengo tayari makomandoo walishajiandaa kutoka huku wakisubiria muda muafakaΒ  ambao Mlango huo wa umeme utakapokua umefunguka, Muuwaji alikua akikimbia naΒ  Elizabeth aliyepoteza fahamu, akapandisha kilima kidogo lakini kwa Bahati mbaya akaterezaΒ  na kujikuta akimtupa Elizabeth ambaye akavingirika na kutumbukia kwenye korongo, kwaΒ  Bahati nzuri akanasa kwenye Mti.Β 

    β€œShit!!” akasema Muuwaji, akaanza harakati za kutaka kumtoa Elizabeth, lakini kelele zaΒ  Makomandoo zikasikika, akatazama saa yake na kuona tayari muda ulikuwa umekwisha naΒ  tayari Makomandoo walikua wakija kwa kasi mahali ambapo Muuwaji alikua amesimama.Β 

    Kwanza akatafuta mahali na kujificha ili Makomandoo wasiweze kumwona, akaangalia risasiΒ  zilizopo kwenye Bastola yake, kisha haraka akaenda mbali na eneo lile, akauzunguka mlimaΒ  mmoja na kwenda kujificha huko kisha haraka akaitoa Bunduki yake kutoka ndani ya Begi.

    Akaielekeza eneo ambalo Elizabeth alikua ametumbukia, alikua akihema kutokana naΒ  kukimbia kwa muda mrefu, Makomandoo wakalipita lile eneo kisha walipofika mbeleΒ  walitawanyika ili kumsaka kwa uzuri adui yao baada ya kugundua adui yao hakuitumiaΒ  Barabara ya vumbi bali alizama Msituni.Β 

    Muuwaji akautumia Mwanya huo kuuzunguka Mlima mdogo na kisha kutokea nyuma yaΒ  Makomandoo kisha akapiganisha akili namna ambavyo anaweza kumchukua ElizabethΒ  kutoka juu ya Mti ulio korongoni, mara akasikia mlio wa gari ukija kutokea Upande wa kuliaΒ  ambapo ndiyo palikua na njia ya kutoka Black Site, haraka akajitupa Korongoni na kutuaΒ  kwenye ule Mti ambao Elizabeth alinasia kisha kwa haraka akamsomba na kushuka nayeΒ  chini ambako palikua Na Msitu wa kutosha.Β 

    Akajipigiza bega kwenye jiwe, kila mmoja akatua upande wake lakini hakuna HataΒ  Komandoo mmoja aliyeshtuka kua Adui yao alikua Korongoni, wenge zito likamzongaΒ  Muuwaji akiwa anajitafuta, akayaruhusu macho yake kutulia, akamwona Elizabeth akiwaΒ  mita kadhaa kutoka alipo yeye.Β 

    β€œAgggghhh” akagugumia kwa maumivu makali huku akinyoosha bega lake, lililo jaa damu,Β  kisha akajisomba na kumsogelea Elizabeth. Akasimama na kuvuta hewa ya kujituliza vyemaΒ  halafu akaangaza juuΒ 

    Jua lilikua likiwaka, ndege wa Msituni walikua wakipiga kelele za hapa na pale, PurukushaniΒ  eneo la juu zilikua za kutosha kisha akajishika kiuno chake na kujinyoosha vyema, hakuishiaΒ  hapo akachana tisheti lake na kujifunga eneo la Bega, kisha akiwa amebakiwa na vest nyeusiΒ  akajitwika Elizabeth, akaanza kuisaka njia ndani ya Msitu wenye giza.Β 

    Haikua rahisi kwake kujua alikua akielekea upande upi kwasababu alikua ameshapotezaΒ  mwelekeo sahihi, akajikuta akisambaa Msituni kwa muda mrefu hadi pale Helkopta za BlackΒ  site zilipoanza Msako kila kona ya Msitu.Β 

    **Β 

    Kelele za popo na sokwe zilianza kusikika ndani ya Msitu wa Magoroto, hatua kubwa zaΒ  vishindo zilimfanya Benjamin Kingai aliye ndani ya pango atoke, kwanza alikutana naΒ  Zandawe akiwa amevaa nguo za ngozi za wanyama. Pili alikua ameongozana na kundiΒ  kubwa la Popo waliozingira eneo la juu ili kumpa kinvuli.Β 

    Tatu, alikua ameshikilia Mkuki aliouchomeka chini, vyote hivi vikamfanya BenjaminΒ  ashangae, lakini tabasamu la kuchanua lilikua likiongezeka kwenye sura ya Malkia Zandawe.Β  Taratibu Benjamin alisogea karibu na Zandawe na kumuuliza kwa utaratibuΒ 

    β€œKuna nini?” alihoji kwa sauti ya chini ili adokezwe lakini Malkia Zandawe akajibu kwaΒ  sauti.Β 

    β€œLeo ni siku ya Ukombozi Benjamin, siku ambayo unaenda kurudisha kila ulichokipoteza”  alisema kisha alikaa kimya, akamfanya Benjamin atupe swali jingineΒ 

    β€œUnamaanisha nini kusema kila nilichokipoteza?” akauliza Benjamin Kingai, kisha akamezaΒ  funda zito la mate huku kivuli cha wale popo ambao ndiyo jeshi la kuaminika la MalkiaΒ 

    Zandawe likiwa linamsaidia pia Benjamin kuikimbia mionzi ya jua ambayo ilianza kuaΒ  Mikali.Β 

    β€œUmepoteza familia, umepoteza haki ya kuishi ndani ya Nchi yako, pia Mtoto na MpenziΒ  wako.” Benjamin akatoa tabasamu lenye Maswali mengiΒ 

    β€œUnamaanisha……” kabla hajamaliza kusema alikuja ndege mpelelezi wa Zandawe kishaΒ  akatua chini na kusema kwa Lugha ya ndege kisha Zandawe akamjibu BenjaminΒ 

    β€œEneo uliloteswa imevamiwa” alisema Kama vile Mtu aliyejua haswa anachosema, taarifaΒ  zote alipewa na ndege wake mpelelezi, hii ilimshtua sana Benjamin akajawa na taharukiΒ 

    β€œVipi kuhusu Mtoto na….” 

    β€œMpenzi wako” akadakika Zandawe kisha akasemaΒ 

    β€œInatupasa kwenda sasa hivi huko kujua kinagaubaga, huo uvamizi hatuna hakika unafanywaΒ  kwa lengo gani, lakini yupo Msichana aliyetoroshwa huko” alisema Malikia Zandawe kishaΒ  alisubiria jibu la Benjamin, kabla hajajibu chochote Benjamin akamtazama yule ndege kishaΒ  akainama na kumwambia ndege huyoΒ 

    β€œAhsante” aliposimama akamuuliza Malikia ZandaweΒ 

    β€œTunafikaje huko?” 

    Malikia Zandawe akatabasamu kisha akamjibu kwa kumwambia nifuate, aliposema alikuaΒ  tayari amegeuka na kuanza kutembea huku wale Popo wakimfuata kwa juu, akamsogeza hadiΒ  eneo la wazi ambalo lilikua halina Miti kabisa ila lilizungukwa na Msitu mkubwa waΒ  Magoroto.Β 

    Katikati ya eneo hilo palikua na kitu kilichofunikwa Majani mengi makavu, Malkia ZandaweΒ  akasogea hadi hapo kisha akaanza kuondoa yale Majani yaliyokuaa yamerundikana,Β  Benjamin alipata Mshangao mkubwa baada ya kuona Helkopta ikiwa ndiyo iliyokuaΒ  imefunikwa hapo.Β 

    Pale pale kabla hata hajamaliza kushangaa akaletwa Mtu mmoja aliyefungwa mdomo wake kwa kitambaa, aliletwa na Sokwe Mkubwa ambaye ni rafiki wa Malkia Zandawe, Mtu huyoΒ  alikua na mavazi ya Urubani, alionekana wazi kua ndiye aliyekua rubani wa Helkopta hiyo.Β 

    β€œNitakuacha Huru ukinifikisha nitakapo” alisema Malkia Zandawe kisha akamtoa kitambaaΒ  eneo la Mdomo.Β Β 

    β€œSiyo Mtu mbaya, ila mmenifanya nimekua Mbaya kwasababu hamtaki kuuheshimu naΒ  kufuata Misingi na mila za Msitu huu” alisema Malikia ZandaweΒ 

    β€œNaomba tafadhali, mateso niliyopata yametosha kua funzo kwangu, naomba niendeΒ  nitawaeleze ukweli kuhusu huu Msitu, naamani hakuna mwingine atakayetia mguu kwenyeΒ  huu Msitu.” Alisema yule rubani huku chozi likimbubujika, Malkia Zandawe akainama naΒ  kumwambia

    β€œNimeshakwambia kua sina ubaya na wewe, hamkutaka kusikiliza onyo langu, ukawe chanzoΒ  cha wengine kuupa heshima huu Msitu” Alisema kisha aliposimama akamwambiaΒ 

    β€œNaamini hili litakua funzo kubwa kwenu, sikutaka kukuuwa kwa maana nilikua na UwezoΒ  wa kukufanyia ubaya kama niliowafanyia wengine walioingia ndani ya Msitu bila kufuataΒ  utaratibu. Kuna viumbe vinaishi humu, vinahitaji utulivu n amani kama ambavyo nyinyi kilaΒ  siku mnapigania” alisema Malikia Zandawe, kidogo akaanza kulengwa na Mchozi.Β 

    Benjamin akamsogelea Malkia Zandawe na kumtuliza kwa kumshika bega, hata yule rubaniΒ  wa Helkopta ya Kijeshi aliona wazi kua Binti huyo alikua akizungumza kwa hisia kali iliyomuumiza. Malkia Zandawe akafuta chozi lake kisha akamwambia ndege wake mweupeΒ  aongoze njia, akamtaka na Benjamin aingie ndani ya Helkopta hiyo pamoja na sokwe wakeΒ  ampendaye.Β 

    Kitendo cha ndege kuruka kiliwafanya na Popo kuzama Msituni zaidi kwa kukimbia kwaΒ  spidi kali kisha Benjamin, rubani, Malkia Zandawe na Sokwe wakaingia ndani ya HelkoptaΒ  hiyo tayari kuelekea ndani ya Black Site kuikomboa familia ya Benjamin Kingai. DakikaΒ  tano baadaye Helkopta ikawa angani ikimfuata ndege mkubwa mpelelezi aitwaye Gola.Β 

    Nini kitaendelea?Β 

    Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

    MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

    Msala Msala Kijiweni Riwaya Ya Msala

    9 Comments

    1. Cesilia Nkunga on September 7, 2024 6:21 pm

      Hatareee, mambo ni πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

      Reply
    2. Given Gihsy on September 7, 2024 6:26 pm

      nice sasa kwel ubaya ubwela , ila prime ministerπŸ™ŒπŸ™Œ

      Reply
    3. Katie on September 7, 2024 6:28 pm

      Wooow mambo yanzd kuwa mamboπŸ”₯πŸ”₯

      Reply
    4. Rumbyambya Jr on September 7, 2024 6:36 pm

      Tuwekee na sehemu inayofata ya 27 leo saa 3 😁

      Reply
    5. Ganai on September 7, 2024 7:00 pm

      Konki

      Reply
    6. Bplm1664 on September 7, 2024 7:04 pm

      🐐🐐

      Reply
    7. Deo on September 7, 2024 7:09 pm

      πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

      Reply
    8. Yuliakimario on September 7, 2024 7:43 pm

      Admin kazi nzuri πŸ‘πŸ‘

      Reply
    9. Clever David on September 8, 2024 8:30 am

      πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.