Ilipoishia “Mfukuzano ulikua mkali kwa hatua kadhaa, kisha ghafla yule Mwanaume alisimama,ย aligeuka kisha aliliweka lile Brifkesi chini, akatabasamu na kumwambia Elizabethย
โNajua umekuja kwa ajili ya Nyaraka M21, hiyo hapo lakini unapaswa kunimaliza kwanzaโย alisema kwa kujiamini sana, aliongea kwa sauti iliyojaa Bashasha kama walikua kwenyeย utani, Elizabeth akajua hapo haitokua kazi rahisi kupambana na huyo Mtu, akaangalia saaย yake.. Endeleaย
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
Alibakiza dakika chache za kutoka ndani ya jengo hilo vinginevyo vikosi vitafika hapo naย kunaswa. Akageuka nyuma kuona kama Muhonzi alikua karibu ili kazi ya kupambana naย Mwanaume huyo isiwe ngumu lakini palikua patupu, ilimpasa yeye mwenyewe alichukueย Brifkesi hilo.
Akajiweka sawa ili kuupima uwezo wake kwa Mwanaume huyo asiye mfahamu, wakatiย anamtafakari akaona kwenye shati palikua na namba za utambulisho, akagundua kwa wepesiย kua Mtu huyo alitokea Ikulu kwa Rais Mbelwa. Pengine hiyo ilikua ni silaha ya siri ya Raisย Mbelwa ndani ya Jengo hiloย
Elizabeth akajiandaa kumshambulia kwa kasi ya kicheche ili amalize kazi mapema kulikoย kawaida, lakini kila pigo alilolipeleka kwa Mwanaume huyo lilikumbata na upepo, yoteย aliyoyarusha hayakumfikia aliyakwepa. Kisha alimpa tena tabasamu, Elizabeth akaona hizoย ni dharau za kutosha, akajikunjua na ngumi mbili alizozipangiliaย
Zote zilikwepwa na mwanume huyo ambaye baada ya kukaa sawa alirusha mapigo matatu yaย mguu wa kushoto, mapigo mawili yakatua kwenye bega la Elizabeth, wakati anapepesukaย yule Mwanaume akadandia ukuta na kuachia pigo lingineย
Pigo hilo lilikua maalum kwa ajili ya kukita sehemu ya kifua cha Elizabeth lakini kwa haraka alijivingirisha na kujiokotanisha. Elizabeth akapanga tena pigo, safari hii hakutaka kwendaย kwa pupa sababu alishagundua Mwanaume huyo ana ujuzi mkubwa wa Mapigano.ย
Akawa anatupa mapigo kwa akili kubwa sana, angalau sasa akaweza kumgusa Mwanaumeย huyo kwa ngumi ya kuparaza iliyopita mbavuni hadi akakata kifungo cha Shati la mwanaumeย huyo.ย
Yule Mwanaume akabonyea kidogo kama Mtu mwenye kibiongo halafu akawa anachezeshaย kichwa chake kama nyoka Cobla, mtindo huo ukawa unamchangaya sana Elizabeth akajikutaย akiambulia vichapo vya kufwatana hadi akaanguka chini, hakuweza kumsoma kabisaย Mwanaume huyo ambaye alikua akibadilika sana kwenye mapigano.ย
Damu ikaanza kumtoka mdomoni, akazidi kupandwa na hasira akajikuta akikurupuka kwenye kurusha mapigo, akawa anapigwa kwa kila pigo alilokua anarusha hadi akabamizwaย ukutani kwa nguvu sana, akashindiliwa na pigo zito la shingo, likampeleka chini, kisha yuleย Mwanaume taratibu akamsogelea Elizabeth na kuanza kumkaguaย
โNilikwambia hutoweza kupata M21โ alisema Mwanaume huyo, kisha alisimama naย kunyanyua Mguu wake ili aikanyage sura ya Elizabeth, lakini ghafla alikutana na teke zitoย lililomtupa mita kadhaa, mbele yake alimwona Kijana mwemye umbo kama lake, Kijanaย huyo alikua ni Muhonziย
Kwanza yule Mwanaume hakuamini kama teke hilo zito lilitoka kwa Kijana huyoย Mwembamba ambaye ukimtazama kwa haraka utaona ni namna gani alikua mlegevu, jamboย la kwanza alihitaji kujua kuhusu hali ya Elizabeth Mlacha.ย
โUko sawa?โย ย
โFaili iko kwnye hilo Brifkesiโ akasema Elizabeth akiwa anajivuta aketi vizuri, Brifkesiย lilikua chini, kazi ilikua ni Nani anayeweza kuliokota Brifkesi kwa haraka. Wote wakaiwahiย Brifkesi lakini kuiokota haikua jambo la urahisi, alipozubaa kidogo tu Muhonzi akalambwaย mtama wa nguvu kisha yule Mwanaume akaliokota Brifkesi, alishajua kupambana naย Muhonzi siyo jambo rahisi, alichofikiria hapo ilikia ni kutimka.
Akaanza kukimbia kuuelekea Mlangoni lakini Muhonzi akafyatua risasi ikamchapaย Mwanaume huyo Mguuni akaanguka chini, Muhonzi akasogea hapo na kuliokota Brifkesi,ย kisha akamtandika risasi nyingine tatu za kumnyongโonyeza. Haraka akarudi kumfwataย Elizabeth, wakaongozana ili waondoke lakini walipofika mlangoni walisikia michakacho,ย wakajua haraka kua kuna askari waliofika hapo.ย
โTunafanya nini?โ akauliza Muhonzi, Elizabeth akautoa mkoba wake mdogo aliouvaaย mgongoni, akatoa baruti, akaziwasha zikaanza kutoa moshi mzito kisha haraka akaufunguaย mlango na kuziachia, zikasababisha moshi mzito. Walinzi wakajikuta hawaoni chochote,ย muda huo Elizabeth na Muhonzi wakautumia kupambana na walinzi wachache kishaย wakazivaa nguo zao na kutoka nje ya jengo la Piza Hunt, huko nje tayari Watu walishaanzaย kujaa baada ya milio ya Risasi kusikika, Muhonzi na Elizabeth walitoka wakiwa wamezibaย sura zao kwa Mask ambazo wale walinzi waliingia nazo.ย
Hakuna aliyewashitukia, wakavuka barabara na kuingia kwenye gari ambayo Elizabethย alifika nayo, wakaishika barabara ya kuelekea njia panda ya Keko, wakatokomea.ย
**ย
Taarifa ya kutoweka kwa Elizabeth na Muhonzi ilizidi kupasua kichwa cha Rais Lucasย Mbelwa, kibaya zaidi tayari mafaili yalikua yameshaibiwa ikiwemo nyaraka M21 ambayoย ilikua na siri za kutosha za Rais Mbelwa. Akaagiza Wasakwe kila koja ya Nchi, tena Msakoย ufanyike kimya kimya ili usije leta taharuki.ย
โHatuna muda wa kuendelea kua hapa Muhonzi, cha Msingi kwasasa ni kukutana naย Mnunuzi tumpatie taarifa kisha tusunde kibunda cha pesa tutafute Nchi tukafurahiโ alisemaย Elizabeth baada ya kufika yalipo Makazi yao ya Siri, maeneo ya Ilala Bungoni.ย
Tabasamu pana likaipamba sura ya Muhonziย
โNina imani tutaishi Maisha ya kifahari sana, kwanini tusiende Moroco my love?โ akaulizaย Muhonziย
โPopote utakapo, nitaambatana na weweโ mara simu ya siri ilianza kuita, hakua mwingine bali Zagamba, alishapewa taarifa na Mke wa Rais Mbelwa kua tayari faili limeibiwa,ย Elizabeth akaipokea simu hiyo.ย
โUko wapi?โ akahoji Zagamba kwa sauti iliyotoka bila salamu.ย
โHapana shaka umesikia kua nyaraka zimepatikana, niambie tunafanyaje makabidhianoโย akauliza Elizabeth, ukimya ukatamaraki kidogo kisha akajibu.ย
โJitahidi ufike Msata, nakutumia Anuani sasa hiviโ akasema Zagamba Halafu simu ikakatika,ย ikamwacha Elizabeth na wasiwasiย
โAnasemaje?โ
โAnahitaji nifike Msata, sijui kwanini, Oooh anuani imeingiaโ akaifungua anuani, akakuta niย Msata tena nyakati za Usiku, kwa kiasi kikubwa ilimpa wasiwasi.ย
โSikia Muhonzi, hatuwezi kwenda wote huko, utabaki hapa na nitakupa taarifa ya kila hatuaย nitakayoipiga, kama kuna baya basi lisitupate wote, naamini hii itakua kazi ya mwishoโย alisema Elizabeth kisha akayatupa macho yake kwemye Brifkesi.ย
โUnafikiria nini?โ akauliza Muhonzi akiwa naye analikodolea macho Brifkesi lililo juu yaย meza ndogoย
โNi lazima tulifungue kwanza, hatuwezi kuifanya Biashara tusiyoielewaโ akasema Eizabethย kisha akafungua droo na kuchukua vifaa kwa ajili ya kufungua Brifkesi hilo lililofungwa kwaย namba Maalum, ikawachukua dakika ishirini kulifungua bila kulivunja, ndani yakeย mlihifadhiwa Flashi moja mpya, ndicho kitu pekee kilichotunzwa humo.ย
โNafikiri hii ndiyo yenye kutunza, basi tuiangalie kwanzaโ akasema Elizabeth, akampatiaย Flashi Muhonzi. Baada ya kuiweka kwenye kompyuta yao walianza kuziona taarifa zaย kutisha ambazo zilitunzwa ndani ya flashi.ย ย
Giza lilipoingia Elizabeth alianza safari ya kuelekea Msata kwa ajili ya kufanyaย Makabidhiano na Zagamba, ndipo Mkasa mzito ulipomkuta huko hadi akakutana naย Benjamin Kingai.ย
**ย
Muhonzi alipomaliza kukumbuka namna walivyoiba Nyaraka M21, akakumbuka kua alikuaย na kazi ya kuhakikisha anatoroka ndani ya Godauni hiyo vinginevyo anaweza akauawa hapoย na Zagamba mwenye hasira. Akajisogeza hadi mlangoni, palikua na eneo la ukuta lenyeย ncha, akaanza kufanya jitihada za kukata ile kamba kwa nyuma, aliendelea na zoezi hilo kwaย zaidi ya dakika kumi na tano bila mafanikio hadi akakata tamaa ya kutoroka hapo.ย
Upande wa Pili, ndami ya Msitu wa Magoroto. Jua la utosi lilikua likiipiga ardhi hiyo pamojaย na kila kilichomo ndani yake, Malikia Zandawe alikua amesimama juu ya mlima mdogo ulioย pembezoni mwa Msitu huo, macho yake yalikua yakiangalia uzuri wa Bonde la Maji lililokuaย likitiririsha Maji kutoka juu ya Kilima hicho.ย
Hali ya hewa ilikua nzuri na ya kuvutia sana iliyompa utulivu wa kutosha, mara ndege wake anayemtumia kwa ajili ya Ulinzi alifika hapo, ndege huyo aliyempa jina la Gola alituaย akitokea safari ya Mbali kuitafuta Black Site ambako mateso makali yalikua yakifanyika.ย
Haraka Zandawe alipiga goti ili azungumze na ndege huyo kwa Lugha ya ndege ambayoย alikua akiielewa vizuri, akapewa taarifa ya wapi ilipo Black Site, Basi uso wa Zandaweย ukatawaliwa na tabasamu la maana, akampa busu ndege huyo kisha akamruhusu aondoke,ย yeye akakimbilia yalipo Makazi yake.ย
Akamkuta Benjamin akiwa anacheza na Sokwe Mkubwa ambaye ni rafiki wa Zandawe,ย alifika akiwa anahema huku tabasamu likizidi kuongozekaย
โKuna nini, mbona uso umechanua kiasi hicho?โ aliuliza Benjamin huku akiacha kucheza naย sokwe, akili yote akaihamishia kwa Zandawe.
โNimejua ni wapi ilipoโย
โIlipo nini?โย
Basi Zandawe akamsogelea Benjamin na kumwambiaย
โSehemu uliyoteswaโย
โSehemu niliyoteswa?โ akahoji Benjamin kwa Mshangao mkubwa sana, alichokisikia alihisiย kama yupo Usingizini, ndipo akakumbuka kua Zandawe alimtuma ndege kuchunguza ilipoย Black Site. Akanyanyuka alipokua ameketi akamsogelea Zandaweย
โUna hakika?โย
โNilikwambia, Gola ni mpelelezi wangu nimtumainiye, yeye ndiye anayenipa taarifaย nisizozijua, nzuri na Mbaya, hata siku ulipoanguka kutoka juu ya Helkopta ni yeye ndiyeย aliyenipa taarifaโ alisema Zandawe, uso wa Mshangao ukamjaa Benjamin Kingai.ย
โKwahiyo imejulikana ilipo, sasa…โ Benjamin mwenye wenge zito akakatishwa na kauli yaย Malkia Zandaweย
โTulia kwanza Benjamin, naamini kama Mtoto wako na Mpenzi wako wapo hai basiย utawapata tuโ kisha aligeuka pembeni, japo alisema hivyo lakini alijisikia kuumia ndani yaย nafsi yake, kisha akageuka akiwa mwenye kutabasamuย
โTutaenda huko kwa ajili ya kuikomboa familia yakoโ alisema Malkia Zandawe kishaย aliondoka hapo ndani ya Pango, yule Sokwe akamfwata kwa nyuma Zandawe. Woteย walimwacha Benjamin akiwa ana furaha ya ajabu sana.ย
**ย
Mateso makali yalikua ndiyo sehemu ya Maisha ya Elizabeth Mlacha, kila kona ya mwiliย wake ilitawaliwa na maumivu makali, alikua amefungwa mnyororo mikononi akiwaย ananingโinia huku damu iliyoambatana na udenda ikiwa inaendelea kumvuja. Hata nguoย aliyokua ameivaa ilikua imetapakaa damuย
โIko wapi M21?โ aliuliza Bi. Sandra, masaa kadhaa yalipita Elizabeth akiwa anaendeleaย kuteswa bila kusema chochote.ย
โIf you want to Kill Me, just Go ahead, but youโll find nothing ( Kama unataka kuniuwaย niuwe lakini hutoambulia chochote)โ alisema Elizabeth kwa sauti chovu iliyojaa maumivuย makali sana, Bi. Sandra alimtazama Elizabeth, moyoni akajisemeaย
โSijapata kumwona Mwanadamu Mbishi na Mgumu kama huyuโ aliutupa mkono wakeย uliojaa damu kwa hasira sana kisha akarudi kuketi kitini akitafakari ni namna gani afanye iliย apate taarifa nyeti. Haraka akanyanyuka kutoka kitini kwa hasira akamfwata tena Elizabeth,ย akamwambia
โUkiendelea kuwa jeuri utamfuata Rais alipoโ alisema kisha akaondoka ndani ya chumbaย hicho, haraka Elizabeth akatambua fika kua Rais alikua ameshauawa na kilichokua kinaendaย kufanyika ni Uasi mkubwa wa kuitawala Nchi.ย
Elizabeth akiwa ananingโinia akaukumbuka Usiku wa Heka Heka.
Nini kitaendelea?ย
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA


10 Comments
Leo nami mnisome wa kwanza jmn
WA kwanza kusomaaaa mieeee
Duuuh msala unazidi kuwa msala๐ฅ, haswa kwa wenye msala,,๐ can’t wait for the next episode ๐๐
Tukumbuke kidogo๐
Unajua naisoma mara mbili mbili lakini naona Bado napaswa kuirudia kongore sana Kwa ndugu Mwandishi hakika ni utunzi maridhawa
Adimi utapata chodaaa
Admin unaatarii nitakupa dada๐๐
๐ฅ
Kaa.move vile najiona natazama๐๐
Jaman simulizi nzuri ningepata kuanza simulizi mwanzo ningefurahi sana naipataje admin