Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Viongozi Simba Wanajiroga Wenyewe Na Kujitega Mtego Mbaya
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Viongozi Simba Wanajiroga Wenyewe Na Kujitega Mtego Mbaya

    MhaririBy MhaririApril 29, 2024Updated:April 29, 202419 Comments2 Mins Read894 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Viongozi wa Simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Viongozi wa Simba wanajiroga wenyewe na kujitega kwenye mtego mbaya kwa mashabiki wao kwani ukitazama tu mtiririko wa namna ambavyo kumekua na mabadiliko ya makocha ndani ya klabu hiyo inaonesha kuwa kuna shida mahali ambayo inawafanya mashabiki kutokua na imani na viongozi wao.

    Kama ulikua hufahamu ni kuwa Simba wameendelea kuachana na makocha wao kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo na katika miaka hiyo 3 imekua katika mtiririko huu hapa :

     

    Novemba 2021 – Mei 2022

    Pablo Franco

     

    Juni 2022 – Septemba 2022

    Zoran Mac

     

    Septemba 2022 – Januari 2023

    Juma Mgunda

     

    Januari 2023 – Novemba 2023

    Roberto ‘Robertinho’ Olivieira

     

    Novemba 2023 – Aprili 2024

    Abdelhak Benchikha

     

    Hii inashiria kwamba kuna shida ndani ya uongozi wa Simba na shida kubwa kuna presha ya kutaka kuendelea kupata mafanikio ambayo waliyapata kwa kipindi cha misimu minne mfululizo lakini hadi sasa kumekuwa na kuyumba kwa mafanikio hayo ambayo yanapelekea hata makocha kufukuzwa au makocha kuvunja mkataba na klabu hiyo

    Lakini pia ukitazama ishu ya kuondoka kwa Benchikha si ishu ya mojakwa moja ya matatizo ya kifamilia bali inaonyesha ni makubwa wanayaoyataka Simba lakini hayaendani na uwekezaji waliouweka kwa msimu huu,ikiwemo wachezaji ambao walikuwepo Simba kwa sasa ilikuwa inamuonyesha kocha anawakati mgumu zaidi kufikia kile Simba sc wanachokitaka na ukizingatia hali ya muendelezo wa matokeo yaliyopo licha ya kubeba kombe la Muungano.

    Uongozi wa Simba unapaswa kufahamu kuwa mpira kuna kipindi unaweza ukapitia kwenye wakati mgumu na kwenda nje kabisa ya malengo yao lakini nafasi ipo kwao kujipanga vizuri na kila mmoja atimize majukumu yake bila kuingilia majukumu ya mtu mwingine anaye husika katika usajili wamuache afanye usajili ulio sahihi kwa tafsiri ya kocha ndiye awe na jukumu hilo kwa kushirikiana na skauti aliyekuwepo klabuni hapo .

    Pia watafute kocha mkuu mapema kabla msimu haujaisha ili apate nafasi ya kuchunguza timu na kuanza kusuka timu ambayo italeta ushindani mkubwa zaidi kwenye mashindano yote ikiwemo ile ya kimataifa.

    Maswali ya kujiuliza ni kuwa:

    1.Je wanaohusika kufukuza na kuajiri makocha simba kwenye misimu yote hiyo si ndiyo hao hao viongozi wapo je wao hawana matatizo? Mbona hawawajibiki.

    2.Kama kubadili makocha kuna tija mbona kuleta mataji ya ubingwa hatuyaaoni.?

    SOMA ZAIDI: Waraka Mzito Wa Hamisi Kigwangalla Kuhusu “Kuinunua Simba”

    viongozi wa simba

    19 Comments

    1. Jafari on April 29, 2024 10:47 am

      Viongozi wa club pia na wao wajitazame maana wanaweza wakawa wanalaumu makocha kumbe wao ndio tatizo kubwa linalofanya timu iendelee kuwa katika mtiririko mbaya

      Reply
    2. Tajiri ABAS on April 29, 2024 10:48 am

      Msimu ujao Simba atashuka daraja Kama hawataacha hii Tabia ya kuwafanya makocha kuwa wanakimbia kimbia Hali ndo kwanza inaenda kuwa mbaya zaidi.

      TAJIRI ABAAAS.

      Reply
    3. Maege himself on April 29, 2024 10:52 am

      Shida sio makocha , shida inaanza kwa viongozi wetu ila nngependa kutoa ushaur kwamb team iwee inamilikiwa na rais na sio kam ilvyo kila mtu aweke hisa zake, achaguliwe mwenye kiti afu aje kutupiga , uhalisia ni kwamb kweny mpira na kupanda na kushuka ila sisi tunashushwa na viongozi wetu wenyew…..

      Reply
    4. Victoris on April 29, 2024 10:55 am

      Tunangoja msimu Uishe ,alafu waone nguvu ya mashabiki ,tusipoenda kuwatoa wenyewe huko maofisini…🤯🤯🤯#simbanguvumoja

      Reply
    5. [email protected] on April 29, 2024 10:56 am

      Kosa la Simba haijui muda sahihi WA kuachana na mchezaji katika wakati sahihi regardless umuhimu wake ukoje… Mfano juzikati Yanga imeachana na Jesus moloko, kabla waliachana na djuma shabani , yaniq bangala, Feisal Salim ambao wote Bado ukiwaangalia ni kama Wana umuhimu kwenye club,, 🤬🤬🤬🤬. Naomba kuwasilisha ✍🏿

      Reply
    6. Barcowinya on April 29, 2024 10:57 am

      Huu ni mfumo wa ulaji nazani Kwa viongoz wa Simba ndio maana timu haifanyi vizur. Hii timu mwekezaji angekabiziwa timu tu

      Reply
    7. milles1410 on April 29, 2024 11:21 am

      Daaah sema mashabiki wa Simba huwa wanafurahisha yani wanachekesha sana, leo Mchezaj X ata perform vibaya au tim nzima itapata matokeo mabaya…then after game mashabiki watalalamika sana watausema uongozi ufukuze wchezaji ila utashangaa next game wakishinda ata goli moja wanasahau yote utaskia ohh dhambi za Mchezaj X nipewe mimi Mara Fundi wa magoli cha ajabu wakifungwa tena lawama kama mwanzo
      😀😀😀

      Reply
    8. Muddy Nakua on April 29, 2024 11:24 am

      Viongozi wapnguzwe na timu bora abaki nayo mgunda awe kocha mkuu basii.
      Na wachezaji wazee wote wapunguzwe
      Akianzwa na saido

      Reply
    9. Muddy Nakua on April 29, 2024 11:26 am

      Na uongozi wa simba wtolewe wote
      Na wachezaji wazeee wote watoke

      Reply
    10. Met Millz on April 29, 2024 11:27 am

      Wakuu c nmechukua muungano kelele za nini 😅

      Reply
    11. Emma tz on April 29, 2024 11:33 am

      Asilimia kubwa ya timu zetu hizi kubwa azisajiri zinaokoteza wachezaji yanga kwa misimu hii mitatu kaokota supa ila simba kajiokotea magarasa yote ila utafika msimu simba simba kuokota supa naye ataludi kwenye fomu

      Reply
    12. Daniel cupa official on April 29, 2024 11:36 am

      Imebaki kuachana na mashabiki pia🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣.

      Reply
    13. LO-KI MASTER on April 29, 2024 12:30 pm

      Basically, Simba ni timu nzuri lakini Ina minimum mibovu hapa karibuni shida ya kwanza ni uongozi wa simba unashindwa kufanya maamuzi kwa usahihi mfano kwenye ishu ya scouting. Cha pili ni kwamba simba nzima imeshindwa kuelewa namna kiwanda cha mpira kinavoendeshwa..Profesional football ni lazima UMPE KOCHA MUDA WAKUTOSHA ASUKE TIMU KUTOKANA NA FALSAFA ZAKE NA ANUNUE WACHEZAJI ANAO WATAKA YEYE SIO MASHABIKI WANAVOTAKA. MFANO MZURI JURGEN KLOPP ALIVOTUA LIVERPOOL ILIMCHUKUA MIAKA MI4 KUTWAA KOMBE LAKE LA KWANZA.
      NI MUDA WA SIMBA KUBADILI MFUMO MZIMA WA KUENDESHA TIMU

      Reply
    14. LO-KI MASTER on April 29, 2024 12:33 pm

      Kipengele ambacho Simba imezingua ni kwenye ishu ya CEO na scouting..Babra Gonzalez alikuwa anajitahidi sana kuongoza club vizur ila saiz sijui inakuwaje pale Msimbazii…Linganisha scouting ya Simba na Yanga…Yanga yuko Miles nyingi away from Simba…

      Reply
    15. LO-KI MASTER on April 29, 2024 12:36 pm

      Hivi fikiria MASHABIKI WA SIMBA NDO WAKO SERIOUS KULIKO WACHEZAJ NA UONGOZ MZIMA..MATOKEO YATATOKA WAPI.🤣 KUNA MDA TUWE WAKWELI SIO KWA UBAYAA…

      Reply
    16. Valence on April 29, 2024 12:53 pm

      Mlivyokuwa na hasira wanathimba utadhani siyo nyie mliochukua kombe la muungano! Hongereni watani,,, fukuza wote hadi akili iwakae sawa,,,,,, YANGA BINGWA!

      Reply
    17. Pingback: KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kwanza) KOTI JEUSI - 01 - Kijiweni

    18. Rown on April 29, 2024 9:17 pm

      Viongozi wa simba tunaomba mjiuzuru kwa kurinda heshima yenu na kwa faida ya tumu kiujumla, nyinyi sio viongozi wa mpila, Sawa tunajua hakuna timu isiyopitia wakati mgumu lakini kwa timu kubwa kama SIMBA haitakiwi kusota na matokeo mabovu kwa zaidi ya misimu miwili hadi mitatu na sasa ni wazi kabisa kuwa tutaenderea hivi kwa msimu wa nne, HII NI BARUA YA WAZI KWENU VIONGOZI kama kweri ni wapenzi wa simba basi mnatakiwa kuchukua maamuzi magumu na kuwapa wengine dhamana ya kuiongoza SIMBA. Benchika ni kocha mwenye CV kubwa  sana kama dirisha dogo mngempatia wachezaji aliowataka  huwenda leo hii asingeondoka na kuvumilia dirisha kubwa aboreshe tena timu, wachezaji waliopo saizi sio kwamba ni wabovu au hawana viwango la hasha ila simba kwa sasa inahitaji wachezaji wenye status kubwa zaizi ya hawa wa sasa, lawama ata sio kwa  wachezaji wala kwa kocha lawama ni  kwenu viongozi mlioshindwa kwenda na wakati na kujua football ya sasa inataka nini. Mfano, hauwezi kumuacha mchezaji kama Baleke na Phili nakumleta Jobe na Fredi ambao hata haiitaji kuwa na taaluma ya ukocha unaona kabisa wapo chini ya uwezo wa Baleke na Phiri na bado mmekuwa mkibolonga kwa wachezaji wengi tuh. Tafadharini sana tunawapenda na tunashukuru kwa kile mlichotupatia saizi wapeni nafasi wengine tena😢🙏 KUJIUZURU SIO ZAMBI NI KUJITUNZIA HESHIMA KAMA ALIVYOFANYA KOCHA BONCHIKA.

      Reply
    19. Pingback: Mashujaa vs Yanga Tutegemee Mchezo Wa Aina Gani? - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.