Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Simba Wanatakiwa Kufanya Haya, Ili Kurejea Kwenye Ubora
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Simba Wanatakiwa Kufanya Haya, Ili Kurejea Kwenye Ubora

    MhaririBy MhaririApril 22, 2024Updated:April 22, 202413 Comments2 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    SIMBA
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kama kawaida yangu Mhariri nimepitapita pita katika mitandao ya kijamii na kukutana na chapisho ambalo ameandika mchambuzi wa soka kutoka hapa nchini Tanzania anayefahamika kama Presenter Noah kuhusu klabu ya Simba.

    Katika chapisho lake ambalo nimeona niwashirikishe wadau wa Kijiweni na kupata maoni yao ni kuhusiana na mabadiliko ndni ya klabu ya Simba na kichwa cha chapisho lake ameandika SIMBA WANATAKIWA KUFANYA HAYA, ILI KUREJEA KWENYE USHINDANI WA UBORA nisiandike sana na mimi lakini tusome kile ambacho amekiandika kisha acha maoni yako hapo chini

    1. Badili viongozi- Wanaweza wakawa wamefanya mengi makubwa ila muda umefika wapishe sura mpya, zenye Maono mapya na vision mpya, kiongozi anayeleta mchezaji wa Timu nyingine kama maonesho ili kupooza mashabiki na kuamini kama kutengeneza whatsapp channel ni mafanikio kwa karne hii ni mambo ya aibu
    2. Watu wakae kwenye nafasi zao ofisini kutokana na majukumu yake kitaaluma(positions based on their merits)- Hakuna mambo ya kujuana au fulani katoka na timu mbali, na ndiomaana unaona kuna mashabiki wa Mnyama wanafanya kazi Yanga na wanafanya kwa ufasaha, so mtu bora apewe nafasi na afanye kazi
    3. Vunja Kikosi- wachezaji wanaotakiwa kubaki na wanapaswa kua kwenye first eleven ya Simba hawafiki sita, kikosi kifumuliwe na waje wachezaji wa maana kama ambavyo hua tunaambiwa thamani ya kikosi Ila wachezaji masalu wote watolewe na tuwashukuru kwa utendaji wao wakati wakiwa Simba
    4. Benchikha apewe Muda- sidhani kama panahitaji maelezo hapa, kocha ni bora na analijua soka la Africa, sasa chukueni report yake mpeni mahitaji yake achape kazi.
    5. Simba inatakiwa kua moja, slogan yetu ni Nguvu moja ila kwa sasa kila mtu anaimba wimbo wake, Simba hakuna kabisa unity na hii ni sababu ya uwepo wa watu wengi wenye ego na kutopenda sikiliza ushauri au kukosolewa, hii inafanya idara nyingi kuzorota na kutokua na ufanisi

    Mwisho Tajiri Mo tunajua unaumia ila mashabiki wanaumia zaidi,  tunaomba muwahurumie, uzuri kwenye moja ya interview zako ulisema Unawajua viongozi wanaoikwamisha Simba na ipo siku utawataja,  sasa tunaomba usiwataje ila WATOKE ndani ya klabu. Ijengwe Simba mpya kuanzia kwenye uongozi mpaka kikosi.

    Nawasilisha

    Wewe maoni yako ni yapi? Tuambie kwenye comments hapa chini sasa

    SOMA ZAIDI: Yanga Inabebwa Na Uimara Wa Eneo Hili Mbele Ya Simba

    simba sc wachezaji simba sc yanga sc

    13 Comments

    1. Tajiri ABAS on April 22, 2024 1:05 pm

      Ili kurejea katika ubora inahitajika afumue kikosi chote na akisuke upya hapo atarudi kwenye ubora tofauti na hapo,? Yuko hatarini kushuka daraja kabisaaaaa

      By tajiri ABAS

      Reply
    2. Abdulrahim on April 22, 2024 1:12 pm

      Kwenye uongozi hapo upo Sahihi asilimia zote ni muda Sasa wa kupata watu wapya na kubadilisha ufanisi kwenye kuendesha klabu wakati mwingine mambo ya kujuana yanatukwamisha Wanasimba

      Reply
    3. Malingila@ on April 22, 2024 1:29 pm

      Toa viongozi wote Tyr again Mangungu boy Kajula hawa wote tupa kule hawana msaada kwa simba kwa sasa

      Reply
    4. Mr ngozi chilumba on April 22, 2024 1:35 pm

      Mazao yakisua sua ng’olea mbali yapandwe mengine,,

      Reply
    5. Dè Harson on April 22, 2024 1:39 pm

      Inabidi tupate uongoz mpya wenye views za kuifikisha Simba mbele. Pia wachezaj wanabidi wajitume Kwa mechi zilizobaki Ili walau tuambulie nafasi ya pili kabla Panga halijapita mwisho wa msimu.

      Reply
    6. Kara Cocuk on April 22, 2024 1:48 pm

      Magugu,Try again na Kijola waondoke…hatuwezi Kaa na watu wa hovyo kiasi hiki kwa sasa

      Reply
    7. Hamisi on April 22, 2024 2:11 pm

      Mambo yasiwe mengi….
      Kikubwa ni kitendo waache brabraaaaaa….

      Reply
    8. Tajiri ABAS on April 22, 2024 2:21 pm

      Msimu umeshawaacha wajipamge upya wasikate tamaa Hali wakijua ni suala la mda tu

      Tajiri Abaaas

      Reply
    9. Sarya Flavian on April 22, 2024 2:24 pm

      Benchikha siyo kocha mbaya lakn kila kocha anahitaj uongoz bora na Scouting ya maana ili kupata wachezaj aoneshe ubora wake haya mambo yafanyiwe kazi kuelekea next Season tunaitaka Simba tuliyozoea kuiona na siyo ya sasa hv

      Reply
      • GODLISTEN MOSES on April 22, 2024 2:36 pm

        Labda mbadilishe timu iitwe simba wa yuda ila ivi ivi never 🤐🤐

        Reply
    10. Lukman Ali on April 22, 2024 2:26 pm

      Mimi nichoona na ninachopenda kuongea saahz si muda wa kubezana na wala kulaumiana yalipita ndio yashapita japo hatuwezi kuyafuta kwa muda huu kilichobaki sasa ni kumuachia kocha Benchikha timu apange kikosi atuletee wachezaji wa viwango kwa ajili ya msimo ujao sasa hapo tutamjua mchawi wetu

      Reply
    11. May tallent on April 22, 2024 2:33 pm

      Wakubaki ni
      1.ayoub
      2.Israel
      3.chama
      4.kibu
      5.(chasambi,duchu,barua ni hazing)
      6.benchi zima la ufundi

      Reply
    12. Mr ngozi chilumba on April 22, 2024 2:37 pm

      Wachezaj Wakigen wakubaki ni Chama, ayoub, Malone baaaas hao wengine wapewe kiinua mgongo wajikatae na viongoz wao

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.