Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Naamini Kuwa Medeama Ndio Msaada Mkubwa Kwa Yanga
    Africa | CAF

    Naamini Kuwa Medeama Ndio Msaada Mkubwa Kwa Yanga

    MhaririBy MhaririFebruary 23, 20242 Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Wachezaji wa Medeama Sc
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Wengi mmejikuta mnaangalia hatma ya Yanga kwa kuangalia tu mechi mbili za Yanga dhidi ya CR Belouizdad na ile ya mwisho dhidi ya Al Ahly. Hakuna ambaye amewaza ni jinsi gani Medeama anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Yanga.

    Ukweli ni kuwa Yanga ni ngumu sana kuvuka kwa kucheza mechi zake pekee maana kama ambavyo tumejadili sana inahitaji amfunge CRB kwa tofauti ya goli 4 jambo ambalo ni gumu sana ingawa kwenye mpira lolote linaweza kutokea. Ikipata ushindi tofauti na huo Yanga inahitaji kupata angalau sare dhidi ya Al Ahly jambo ambalo nalo lina ugumu fulani.

    Njia iliyo rahisi zaidi kwa Yanga ni kwa Yanga kumfunga CRB kwa ushindi wowote ule huku wakiombea Medeama ipate ushindi leo dhidi ya Al Ahly. Medeama ana nafasi kubwa ya kushinda leo kwa sababu Al Ahly bado hawako vizuri na wataendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu kutokana na majeraha. Vilevile changamoto za hitilafu za ndege yao na uchovu wa safari unaweza ukawaathiri kwa kiasi fulani Al Ahly.

    Matokeo ya mechi hizo mbili yakienda kama nilivyosema, kitakachobaki ni katika mechi za mwisho kwa Yanga kuiombea Medeama itoe sare dhidi ya CRB huku yenyewe haihitaji kupata sare wala ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Al Ahly.

    Kwenye mechi walizokutana wenyewe kwa wenyewe ni wazi kabisa kuwa Yanga ina faida mbele ya Medeama kwa hiyo ikitokea wamelingana alama basi Yanga anafuzu.Siioni Al Ahly ikiendelea kuwa na makali hasa nikitazama ile mechi yao dhidi ya CRB, walicheza mpira wa kawaida sana.

    Yanga ana uwezo wa kukomaa kule Misri na akato sare, kikubwa kesho apate ushindi mzuri kama unavyosema, sare Yanga ana uwezo wa kuipata kule Cairo kama akienda kwa nidhamu uwepo wa viungo kama Aucho, Mudathir, Pacome, Maxi ni viungo ila wanajua haswa kukaba pia.

    SOMA ZAIDI: Asec vs Simba Sio Mechi Ya Kawaida , Ni Vita Ngumu Sana

    Al Ahly Medeama sc yanga sc

    2 Comments

    1. Pingback: Ntibazonkiza Ni Funguo Ya Simba Leo Dhidi Ya ASEC - Kijiweni

    2. Pingback: Ningekua Gamondi Ningeanza Hivi Kwa CR Belouizdad - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.