Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Winga Geita Gold FC kutimkia Simba SC
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Winga Geita Gold FC kutimkia Simba SC

    David MohamedBy David MohamedMay 18, 2023No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Klabu ya Simba imeanza harakati za kuimarisha kikosi chake na miongoni mwa nyota wanaotajwa kuwa katika mpango wa kuwanasa ni winga wa Geita Gold, Edmund John na tayari winga huyo mwenye umri wa miaka 20 ameanza mazungumzo na Simba kwa ajili ya kujiunga nayo msimu ujao.

    Nyota huyo wa zamani wa Serengeti Boys, anamudu kucheza nafasi za winga zote mbili kulia na kushoto pia ana uwezo wa kucheza nafasi ya nyuma ya mshambuliaji. Harakati za kumsajili Edmund zimeanza kutokana na mapendekezo ya Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ambaye katika ripoti yake ameutaka uongozi kusajili mawinga wawili wazawa wanaomudu kucheza kila upande.

    “Mazungumzo yanaendelea baina ya Simba na mchezaji na yanakaribioa kufikia pazuri. Tunafahamu ana mkataba na Geita Gold hadi Januari mwakani lakini tunaweza kuzungumza nao na tukafikia mwafaka wala hakuna shida katika hilo. Kocha amependekeza tusajili mawinga wawili wazawa ambao wataleta ushindani kwa wageni na huyu Edmund ni miongoni mwa wachezaji wa nafasi hiyo walioonyesha kiwango kizuri msimu huu,” alisema mmoja wa vigogo wa Simba.

    Licha ya kucheza nafasi ya winga, Edmund ni miongoni mwa wachezaji wa nafasi hiyo walioonyesha uwezo wa kufumania nyavu msimu huu ambapo hadi sasa ameifungia timu yake mabao manne dhidi ya Tanzania Prisons, Dodoma Jiji, Polisi Tanzania na Coastal Union.

    Wakati ikiwa katika mpango wa kumnasa winga huyo, Simba pia iko katika mpango wa kumwongezea mkataba winga wake kiraka Jimmyson Mwanuke ambaye mkataba wake wa miaka mitatu utafikia tamati mwishoni mwa msimu ujao.

    Uwezo mkubwa wa Mwanuke kucheza nafasi tofauti uwanjani pamoja na nidhamu anayoonyesha vinatajwa kama sababu iliyomshawishi Robertinho kufanya maamuzi ya kuendelea kubaki na nyota huyo aliyesajiliwa kutokea Gwambina FC.

    Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema timu yake haijafanya mchakato wa usajili wa Edmund na suala la Mwanuke kama lipo au halipo litatolewa ufafanuzi.

    “Taarifa kuhusu Simba kumhitaji Edmund sisi wenyewe tunaziona tu kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, kuhusu Mwanuke kama kuna chochote klabu itatoa taarifa,” alisema Ally.

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.