Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Wachezaji Hawakuutaka Ushindi Licha Ya Zambia Kuwa Pungufu
    Africa | CAF

    Wachezaji Hawakuutaka Ushindi Licha Ya Zambia Kuwa Pungufu

    MhaririBy MhaririJanuary 21, 2024No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mchezaji wa Tanzania Ibrahim Bacca aliyecheza dhidi ya Zambia
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Katika mchezo ambao Zambia walikuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 45 alafu wanapataje sare katika mchezo huu? Hapa nadhani Tanzania mechi wameitupa wenyewe kwani timu ilikuwa inakaa nyuma kitu ambacho ni kibaya hasa ukizingatia Zambia walikuwa na mchezaji hatari Patson Daka. Matumaini ya kwenda hatua 16 bora yamekuwa hafifu kwa sababu hata hao DR Congo wanaipigia hesabu Tanzania katika mchezo wa mwisho.

    Bao la dakika ya 88 la Zambia limefuta matumaini ya Tanzania kuandikisha ushindi wa kwanza katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (Afcon).Tanzania iliandikisha goli la kwanza katika dakika ya 11 kupitia winga wake wa kimataifa Simon Msuva akiunganisha pasi maridhawa kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta.

    Zambia ilipata pigo kwa kutolewa kwa kadi nyekundu kwa nahodha wao Rodrick Kabwe katika dakika ya 44 ambapo ilipelekea Tanzania kuutawala mchezo na kukosa nafasi kadhaa za wazi kuongeza goli la pili wakati Zambia ikicheza mchezo wa kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

    Mashambulizi hayo ya kushtukiza yalizaa matunda katika dakika ya 88 ambapo mshambuliaji wa klabu ya Leicester City ya England Patson Daka alipofunga bao la kusawazisha kwa kichwa kikali akiunganisha krosi ya Clatous Chota Chama anayechezea klabu ya Simba ya Tanzania.

    Hii ni sare ya pili kwa Tanzania katika michuano ya AFCON. Sare ya kwanza waliipata kwa Ivory Coast katika michuano ya mwaka 1980 ambapo magoli yalikuwa 1-1. Katika michuano ya mwaka 2019 Tanzania ilipoteza michezo yote mitatu.

    Kwa matokeo hayo sasa Tanzania inaendelea kushikilia mkia wa kundi Fwakiwa na alama moja huku Zambia na DRC wakiwa na alama mbili kila mmoja na kinara wa kundi ni Morocco wenye alama nne. Morocco na DRC walitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa awali wa kundi hilo.

    Tanzania sasa itaminyana na DRC siku ya Jumatano katika mchezo wa mwisho wa makundi, Morocco na Zambia pia wataminyana siku hiyo. Mpaka sasa hakuna timu yoyote katika kundi hilo ambayo imekata tiketi ya kucheza katika hatua ifuatayo.

    SOMA ZAIDI: Unajua Kwanini Taifa Stars Watapata Alama Kwa Zambia?

    zambia vs Tanzania afcon 2023
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.