Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Simba Na Yanga Wapo Katika Kesi Kubwa Ya Dunia Sasa
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Simba Na Yanga Wapo Katika Kesi Kubwa Ya Dunia Sasa

    MhaririBy MhaririFebruary 16, 20241 Comment2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Washambuliaji wa Simba na Yanga
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kesi ya washambuliaji kwa sasa ni jambo gumu linaloisumbua dunia ya mpira, zamani ilikuwa rahisi kuwapata wapachikaji wa mabao lakini siku zinavyozidi kusonga imeongeza ugumu zaidi na hata ukiangalia timu zetu Simba na Yanga.

    Chelsea ilikuwa na Didier Drogba, Manchester United na Van magoli huku Liverpool wao walikuwa na Fernando Torres. Hii ilikuwa Dunia ya mpira na tulifurahi  sana wakati ule. Nenda Chelsea ya sasa, Manchester United yenyewe Kisha malizia na Liverpool wanavyohangaika kutafuta washambuliaji.

    Nikirudi kwenye vilabu vyetu vya Simba na Yanga nao hali ni hiyohiyo kwani ukimtazama huyu Freddy Michael namuona akiwataka mashabiki wake waendelee kumsubiri sana, siyo aina ya wale washambuliaji hatari sana kwenye boksi kwani haogopeshi mabeki wala kuwapa uoga.

    Tangu afunge lile goli lake dhidi ya Tabora United, sioni tena ule uwezo wake ni kama ngoma imeanza kuwa ngumu na kutufanya tuendelee kuona washambuliaji ni dunia nyingine kwa sasa, kama utampata inahitajika kumtunza na siyo kumuuza.

    Tuko katika kipindi ambacho klabu zetu zinarudi katika michuano ya mabingwa barani Afrika na wakiwa katika hatua mabyo bila shaka kila mmoja anatamani kuingia hatua ya robo fainali kwanza kwa Simba ambao washaingia mara kadhaa pamoja na klabu ya Yanga ambayo wanapambania kuingia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika histori ya timu yao.

    Wanachokipitia Simba unaweza kusema ndicho ambacho wanapitia Yanga kwani wamekua na changamoto msimu huu ya kupata mshambuliaji hatari wa kufunga magoli kama ambavyo alikua akifanya mshambuliaji wao Mayele, kwa kiasi kikubwa msimu huu magoli mengi ya Yanga yamefungwa na viungo wao hii ni kuonesha kuwa wana wakati mgumu katika upande huu wa ushambuliaji.

    Nadhani ni wakati sasa wa klabu za Simba na Yanga kufikiria upya kuhusu bajeti zao haswa katika kutafuta washambuliaji wa timu zao kwani ndio mojawapo ya silaha kubwa kwa ajili ya kufanikiwa katika mechi za kimataifa za ngazi ya klabu.

    SOMA ZAIDI: Ratiba Kamili Ya Mwezi Wa Pili Ligi Ya Mabingwa Afrika

     

    Simba yanga

    1 Comment

    1. Pingback: Hii Ndio Ligi Yetu? Tubadilike Kama Tunataka Mafanikio Kimataifa - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.