Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Robertinho: Ipo Siku Nitampiga Mtu Goli 10
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Robertinho: Ipo Siku Nitampiga Mtu Goli 10

    David MohamedBy David MohamedJune 9, 2023No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kocha Mkuu wa Simba SC Robert Oliveira ‘Robertinho’ ametamba kwamba endapo Simba itafanya usajili ambao amezungumza na mabosi wake Kuna uwezekano mkubwa wekundu hao wakampiga mtu hata 10 -0 msimu ujao.

    Kauli hiyo ya Robertinho inakuja kufuatia juzi kuichapa Polisi Tanzania kwa mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, matokeo yaliyoishusha rasmi maafande hao kwenda Ligi ya Championship kwa msimu ujao.

    Katika mchezo huo uliopigwa Azam Complex, Chamazi, kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza alifunga mabao matano pekee yake, huku jingine likiwekwa kimiani na Israel Mwenda na kumfanya nyota huyo wa Burundi kuifikia rekodi ya Nsa Job na Edibily Lunyamila walioiweka 1998 na 2009 walipofunga mabao matano kwenye mchezo mmoja dhidi ya Kagera Stars na Villa Squard.

    Robertinho alisema hashangazwi na matokeo hayo kwa timu yake na kwamba falsafa wanayoitumia ni rahisi kutengeneza mabao mengi endapo watakutana na timu isiyojua kucheza kwa nidhamu.
    Robertinho alisema endapo kikosi chake kitapata mastaa wakubwa zaidi mithili ya Said Ntibazonkiza ‘Saido’aliyefunga mara tano katika ushindi huo wa juzi Simba itakuja kumfunga mtu mabao 10 msimu ujao.

    Robertinho

    “Wala sio kitu cha kunishtua ni vile bado tuna wachezaji ambao wanakosa utulivu lakini falsafa yetu inaturuhusu kushinda zaidi ya mabao haya ambayo tumeyapata kwa Polisi,” alisema Robertinho

    “Mara ya kwanza tulishinda mabao Saba dhidi ya Horoya watu waliona kama tumebahatisha, Horoya hawakuwa timu mbovu lakini ubora wa soka letu uliwaadhibu, Saido ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa alitulia akatumia nafasi nyingi.

    Alisema msimu ujao anawasubiri mastaa wapya ambao endapo watawapata wachezaji wanaowataka basi Simba itacheza mpira mkubwa zaidi ya huu unaocheza sasa.

    “Kila ukitembea barabarani unakutana na shabiki wa Simba anakuomba kutengeneza timu bora kwa msimu ujao, hii ni klabu kubwa inastahili matokeo bora na mataji mengi.”

    Tufatilie zaidi hapa kwa habari za michezo.

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.