Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane
“Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba kingine ikisema
“Safi” wakimaanisha kuwa vyumba vyao vipo salama hapo ndipo Faudhia aliposhtuka kuwa anapaswa kuwa nje ya chumba haraka sana ili awawahi Wanaume hao, alifanya hivyo upesi sana huku akiwa ameelekeza Bastola yake mbele mahali ambako sauti hizo zilitoka, wale wanaume hawakuisikia sauti ya tatu ya mwenzao ndipo walipotoka nje haraka ila walikuwa wamechelewa, walikutana na mishale ya risasi kutoka kwa Faudhia, Msichana kutoka Mbeya, aliwamaliza kimya kimya bila kusikika popote sababu bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti . ENDELEA
SEHEMU YA NANE
Aliikumbuka vyema ile ramani, ramani ilisema kuwa kwenye kordo hiyo mbele kwenye ukuta ndipo ulipo mlango wa kuelekea ilipo chemba, alipoangalia ukuta huo aliona kulikuwa na picha, aliifuata na kuifunua aliona kuna mlango mdogo wa siri ambao ulifunikwa na picha hiyo kubwa yenye Msaafu, hapo aligundua kuwa mpango huo wa kuiba pesa haukuwa rahisi kiasi hicho.
Ndani ya China Plaza, Mzee Shayo alizidi kuzama ndani kwa kutumia ngazi, jengo lilikuwa refu kiasi chake na haikuwa salama sana kwake kutumia Lifti. Alisogea taratibu tena kwa umakini wa hali ya juu huku akitambuwa fika kuwa uzembe wa aina yoyote utaondoa Maisha yake sababu watu hao ni hatari sana.
Kabla hajafika Floo ya tatu alimuona Mlinzi wa kwanza ndani ya jengo, alikuwa ametulizana akivuta sigara, alisogea kwa umakini sana hadi alipomfikia, alimgusa bega la kulia alipogeuka alimpa ngumi nzito eneo la pua, alimtuliza kwa kumzimisha kisha alisonga mbele.
Alikagua kila mahali, sehemu zingine alikuta familia zilizokuwa zimejificha kwa woga aliwaambia muda wa ukombozi umefika, alihakikisha anamfikia Mzee Shomari kwa mara ya pili baada ya miaka mingi kupita, akiwa ameshafika floo za juu kabisa alisikia sauti ya Mtoto akiwa analia, sauti hiyo ilimkumbusha mbali sana alipokuwa mdogo wakati Nyumba yao ilipokuwa inawaka moto na kuwateketeza Wazazi wake wote wawili, wazo hilo lilimtoa kwenye lengo lililo mbele yake ile anatahamaki alimuona adui mbele yake, alimchapa risasi, kelele za Risasi ziliposikika ziliamsha hali za maadui zake na kujuwa kuwa eneo hilo halikuwa salama.
Yees!! Chogo alimfuata Selina na kumwambia
“Pole sana kwa kila kilichotokea hapa, haikuwa nia yangu kukufanyia vile bali upendo ulioniingia ghafla, natamani kukuona ukitabasamu tena katika Maisha yako japo najuwa itakuwa ngumu sana” Maneno ya Chogo yaliamsha mchozi na kilio kwa Selina, alimwambia Chogo
“Wewe siyo Binadamu, huna utu, hufai hata kusamehewa” Alisema kwa hasira sana
“Selina! Nakupenda sana, nahisi upendo wako kwenye damu yangu, nazisikia punzi zako kwenye masikio yangu, kilio chako ni huzuni kwangu! Unapaswa kupumzika” Alisema Chogo kisha aliachia tabasamu lililomshangaza Selina, Chogo alipiga hatua kadhaa ili kuondoka kisha alimgeukia Selina na Kumwambia tutaonana siku moja, Chogo alifyatua risasi na kumuuwa Selina akiwa juu ya Meza, haraka alikimbilia kwenye chemba ya siri ambayo aliwaambia vijana wake atawakuta huko kisha safari yao kuelekea Upanga ilianza.
Ndani ya Chemba hiyo, Faudhia alikuwa akisogea kuelekea Benki kuu wakati huo Chogo na vijana wake walikuwa wakielekea alipo faudhia ambako ndiko iliko njia ya kuchomoka kwenye chemba hiyo yenye giza.
Chogo na vijana wake walikuwa na shahuku ya kuwa Mamilionea, Faudhia alikuwa na shahuku ya kuhitimisha ugaidi huo. Muda huo Mkuu mpya wa Kitengo cha Usalama wa Taifa alikuwa akiwasiliana na Rais, kilichosubiriwa ni amri ya Rais kuhakikisha wanaishambulia benki hiyo mara moja. Punde waliwaona Mateka waliokuwa ndani ya Benki hiyo wakikimbia hovyo kuelekea nje, ilibidi wapeane taarifa kuwa wanapaswa kwanza kuwa watulivu huku wakiwa makini na Mateka hao kuwa huwenda wakawa wamechanganika na Magaidi.
Iliwabidi wawahoji Mateka hao, walisema kile walichokiona lakini kilichowaduwaza Askari ni namna mateka hao walivyosema kuwa Watekaji walikuwa wameshaondoka, iliwalazimu kuingia dani ya benki hiyo kwa utulivu na umakini wa hali ya juu sana, walichunguza kila kona walikuta mwili wa Selina, walimkuta Gavana akiwa hoi sana baada ya kuvuja kwa damu nyingi, Mke wa Gavana alikuwa akilia sana kwa kuhisi Mume wake angelikufa.
Mkuu mpya wa kitengo cha Usalama wa Taifa alimwambia Rais kuwa Huyo Selina ameshauawa, pesa zote zilikuwa zimeshaondoka ndani ya Benki hiyo na haikujulikana magaidi walikuwa wameondoka vipi eneo hilo kwani hata dalili tu kuwa walichimba mahali haikuonekana, iliwapa maswali ya kujibu Askari wa Kitengo na wale wa kawaida, walihangaika kujuwa Magaidi hao waliondoka vipi ndani ya Benki hiyo, kumbe walichofanya Magaidi hao ni kupita juu ya Siling Board na kutokea chumba kingine ambacho kilikuwa cha siri sana ndani ya benki hiyo kisha walichimba huko na kutengeneza njia hivyo ukiingia kwa kawaida tu huwezi kuona japo alama kuwa walichimba wapi, Naam!! Huyo ndiye Mzee Shomari aliyekuwa akiratibu yote hayo na kusuka mipango ya hatari sana.
“Mkuu hakuna mahali ambapo panaonesha hawa jamaa wametoka, pengine wapo humu ndani wamecheza mchezo ili kuvuruga akili zetu” alisema Mkuu mpya wa kitengo akiwa anazungumza na Rais
“Inawezekana vipi Dinonga? Hicho ni kiasi kikubwa sana cha pesa, hakikisha hawaondoki” Alisema Rais kwa sauti iliyoashiria kuwa alikuwa amepagawa.
Msako uliendelea ndani ya Benki kuu huku taarifa za habari zikiendelea kuripoti tukio la kuwa huru kwa mateka waliokuwa ndani ya Benki hiyo.
Mzee Shayo akiwa amejibanza kwenye kona huku tayari akiwa ameshaamsha akili za maadui zake ndani ya jengo la China plaza, alijikuta akiwa anahema juu juu huku akili na moyo wake ukizidi kumwambia kuwa kazi hiyo ni hatari sana. Mlango ambao wale maadui walikuwa wakitokea ndiyo sehemu ambayo Mzee Shomari alikuwemo.
Mzee Shayo alifumba macho yake na kuibusu Bastola aliyoishika mkononi, zaidi ya Wanaume sita walikuwa wakisogea mahali ambapo Mzee Shayo alikuwa amejificha tena wlaikuwa makini sana baada ya kutambuwa kuwa Mtu huyo alikuwa hatari sana kwao.
Mzee Shayo aliutumia ufundi wake kwa kusoma milio ya hatua ya maadui hao kisha akatambuwa namna walivyokuwa wamejipanga, alihesabu 1,2,3,4,5,6 kisha alijitoa mafichoni kama chui mwenye hasira
Alifanya kama vila anakatisha kwenye korido kutoka ukuta mmoja hadi mwingine huku akiwa amefumba macho yake, hisia pekee ndizo zilizokuwa zikimuongoza, alifyetua risasi sita ambazo aliamini zilikuwa ndiyo misumali ya kuwamaliza Maadui hao, sauti za kuanguka zilisikika, Ndiyo!! Mzee Shayo alifanikiwa kuwamaliza maadui hao sita kwa kutumia hisia zake kali za Kijeshi. Alipofika ukuta mwingine alijipa muda wa kuendelea kusikiliza tena lakini hakukuwa na sauti ya hatua hata moja iliyokuwa ikisikika.
Aliweka vizuri bastola yake kisha alichomoka kwa makini sana, alisogea taratibu akiwa anaegemea ukuta huku Bastola yake ikielekeza kwenye ule mlango ambao wale maadui walikuwa wametokea, alipiga hatua 10 za Kijasusi hadi alipofika, mlango ulikuwa wazi na hakukuonekana kuwa na dalili za kuwa na Mtu kwenye chumba hicho, aliona chupa za vinywaji na Michoro baadhi ya tukio walilokuwa wakilifanya
Aliona ni bora azidi kupandisha juu ambako kulikuwa na hiyo Helkopta ili kama Mzee Shomari anatoroka aweze kumnasa.
Tuachane na Mzee Shayo, sasa turudi ndani ya Chemba ya kusafirishia pesa, Chogo na Watu wake walizidi kuchanja mbunga bila kujuwa kuwa Faudhia alikuwa akienda upande wao, walipofika katikati ya safari yao Chogo aliwaambia vijana wake watulie, alihisi ujio mbele yao, ni kweli Faudhia alikuwa mbele yao, naye alihisi ujio wa Watu. Mkononi alikuwa na Bastola huku Bastola nyingine akiwa ameiweka kiunoni, alijiweka sawa huku Chogo na Watu wake wakijiweka sawa ili kukabiliana na hatari iliyo mbele yao, eneo ambalo liliwatenganisha Faudhia na Timu ya Chogo ni sehemu yenye kona, Faudhia alizima tochi yake ili kuwe giza, upande wa pili Chogo naye aliwaambia vijana wake wazime tochi zao. Walivalia miwani ambazo ziliwasaidia kuona kwenye giza, walikuwa wamejipanga huku kila mmoja akiwa na Begi moja lenye pesa
Chogo alituma Watu wawili wasogee mbele zaidi kuangalia kulikuwa na nini, Faudhia alishashtuka aliweka sawa Bastola yake ili awashambulie, walipojitokeza japo kulikuwa na giza
Faudhia aliweza kucheza na hisia kama alivyofanya Mzee Shomari na ndiyo yalikuwa mafunzo ya kupambana na adui pale ambapo unahisi kwa macho ya kawaida huwezi kufanya hivyo, alisikiliza hatua za Wanaume hao wawili akajuwa namna walivyo kaa, wanaume hao walikuwa na AK47 mikononi mwao hivyo Faudhia alipaswa kuwa makini zaidi, alifumba macho na kuinyanyua bastola yake hadi usawa ambao aliona unafaa.
Aliendelea kusikiliza hatua zao kisha alifyatua risasi mbili kwa kutumia Bastola yake ambayo ilifungwa kiwambo, risasi hizo zilifika kwenye paji la uso la kila mmoja, japo sauti ya risasi haikutoka lakini sauti ya kuanguka kwao iliwashtua Akina Chogo ambao haraka walianza kurusha risasi mbele, Faudhia alijificha mahali huku ule mwanga wa zile risasi ukimfanya aone watu aliowauwa kuwa walikuwa wamevalia miwani za kuona wakati wa giza, baadaye risasi hizo zilikoma.
Hakuna risasi iliyomfikia Faudhia kwenye mwili wake kwasababu alikaa kwenye kona, alipoona ukimya umetawala alipiga mahesabu ya kuichukua miwani, alitoa bastola zake mbili kisha aliziweka sawa, alijichomoa na kuanza kurusha risasi kwa lengo la kuwazuga huku haraka akichomoka na kufika zilipo zile maiti mbili, alisogea kwa mmoja na kumvua ile miwani ila bahati mbaya alipigwa risasi ya Bega, alijibu mapigo huku akiokota AK47 kisha alirudi kujificha, alikuwa na maumivu makali ya bega.
Alichana kilemba kisha alijifunga kwenye bega kwa usaidizi wa meno yake, alivalia miwani akawa anaona kama kwenye mwanga vile, kisha aliiweka sawa AK47 kwa ajili ya majibizano ambayo yalianza kuwashtua polisi walio ndani ya Benki huku wakijiuliza risasi hizo zilikuwa zikitokea wapi, Chogo na timu yake walijipanga vizuri, walikuwa kama Watu 11 waliobakia
Faudhia alianza kutoka pale huku akisogea kwa tahadhari kubwa, alikuwa na ujuzi wa kulenga hivyo ilikuwa kazi rahisi sana kwake kukabiliana na Wanaume hao, alipochungulia aliona miguu yao ikisogea, alilenga miguu ya Watu wawili akafyatua risasi, walipoanguka aliwamaliza moja kwa moja na kufanya idadi yao kupungua, Alizidi kuwamaliza kwa kuwavizia hadi alipofanikiwa kuwabakiza maadui wanne tu, chogo akawaambia
“Turudi ndani ya Benki” Alisema kisha waliokota mabegi machache huku mengine yakiwa chini, waliona hawataweza kukabiliana na Hatari hiyo huku wakishindwa kujuwa kuwa Mtu huyo alikuwa peke yake au kilikuwa kikundi cha Watu.
“Benki itakuwa imeshavamiwa na askari” Alisema mmoja wa vijana wake
“Sasa tufanye nini, tusogee tukafe?, turudi ndani ya Benki” Alisistiza Chogo, wakiwa wanarudi, Faudhia aliwatungua wawili kati yao na kuwabakisha wawili ambao ni Chogo na mwenzake mmoja, chini huko hakukuwa na mtandao labda angewasiliana na Mzee Shomari na kumuomba msaada hata hivyo Mzee Shomari mwenyewe alikuwa akijivuta na mguu wake mbovu kuifuata ilipo Helkopta ili aweze kukimbia baada ya kuona Mambo hayapo sawa.
Mzee Shayo alikuwa nyuma yake akiwa anakuja kwa kasi kuhakikisha Mzee Shomari hachomoki, ilikuwa ni wahi nikuwahi, kama siyo Mguu mbovu wa Mzee Shomari basi angelikuwa ameshaifikia Helkopta, alifanikiwa kuufungua mlango wa mwisho kisha Mtu mmoja alishuka kutoka kwenye Helkopta ili ampe msaada Mzee Shomari, ghafla jamaa huyo alipigwa risasi ya kichwa na Mzee Shayo ambaye alikuwa ameshafika eneo la Mlango, kuona hivyo Mzee Shomari aligeuka akamwambia Mzee Shayo
“Ni bora uniache niondoke vinginevyo nitabonyeza hii rimoti kwa ajili ya kutegua mabomu yote yaliyopo kwenye makambi ya Jeshi Nchi nzima” Alisema Mzee Shomari, maneno yake yalileta uzito kwa Mzee Shayo alifikiria afanye nini huku Mzee Shomari akiwa anataka kubonyeza Kitufe
“Sawa!! Nakuacha uwende” Alisema Mzee Shayo huku akiweka silaha yake chini, Mzee Shomari alicheka sana kwa kuamini kila jambo linaenda kuwa sawa, alimwambia Mzee Shayo
“Itupe hiyo Bastola” Alisema kwa mkwara, Mzee Shayo aliiokota na kuitupa chini ya ghorofa hilo, hapo Mzee Shomari aliamini kuwa yupo salama kumbe nyuma ya Mgongo wa Mzee Shayo kulikuwa na Bastola aliyoificha, Mzee Shomari alipogeuka ili apande Helkopta alipigwa risasi nyingi mgongoni, hakuamini macho yake, alitamani kubonyeza kitufe ili afe na Askari wengi lakini nguvu ya kufanya hivyo ilimuisha hatimaye alianguka chini, haraka Mzee Shayo alifyetua risasi kwa dereva wa Helkopta ambaye alitaka kutoweka eneo hilo, alimpiga risasi ya shingo na kusababisha Helkopta kuruka bila uelekeo maalum hatimaye ilienda kuripuka kwenye kituo cha Mabasi ya mwendo kasi eneo la Gerezani.
Alishusha pumzi zake kisha alipiga magoti, kazi ilikuwa ngumu sana kwake, alijikuta akicheka kwa maumivu makali ndani ya nafsi yake, ngoma ilikuwa ngumu upande wa Faudhia ndani ya Chemba ya pesa, Chogo alikuwa akirudi ndani ya Benki wakati huo Faudhia akiwafuata kwa nyuma kuhakikisha hakuna atakayetoka salama eneo hilo, majibizano ya risasi yaliendelea ndani ya chemba hiyo, polisi walio juu walifanikiwa kufahamu kuwa risasi hizo zilikuwa zikifyatuliwa chini kabisa ya Ardhi hivyo waligundua huenda Magaidi wapo chini wanajibizana na askari wengine.
Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa alimpa taarifa Mkuu wa Nchi kwa kile kichokuwa kikiendelea huko Chini, Rais alimwambia asikilizie ni jambo gani lilikuwa huko chini.
Akina Chogo walijitahidi kukimbia kurudi ndani ya Benki lakini Faudhia alikuwa makini kuwawinda, alimpiga risasi mtu wa Chogo, iliamsha hasira sana kwa Chogo, alisimama kisha aliokota AK47 kisha alianza kumimina risasi nyingi mfululizo upande wa Faudhia, alifanikiwa kumfanya Faudhia alale chini huku akijificha kwenye moja ya maiti, alipomimina risasi kwa hasira hadi alipozimaliza, Faudhia alipojuwa kuwa alikuwa amemaliza Risasi alisimama akiwa na bastola yake, alipiga risasi moja mguuni kwa Chogo, alipiga nyingine kwenye bega la chogo kisha alitaka kumaliza mchezo lakini Bastola yake iliisha Risasi.
Chogo alichomoka kama Mzimu, Faudhia hakuamini kuwa Mtu aliyempiga risasi alikuwa akija kama Duma kwenye mbuga ya wanyama, alimfika Faudhia eneo la tumbo na kuumtupa pembeni, wote walikuwa na mawani maalum za kuona kwenye giza.
Chogo alikuwa kama amepagawa hivi hakutegemea kama angelikutana na upinzani wakati wa kupata kiasi hicho cha pesa, alimvaa Faudhia na kuanza kumpa mvua ya ngumi ambazo zilimrudisha tena Faudhia Chini, kabla hajakaa sawa alishindiliwa na teke tumboni zaidi ya mara tatu haidi alitema damu.
“Nani amekutuma?” Aliuliza Chogo akiwa kama kichaa, alishusha ngumi nyingine nzito kwa Faudhia na kumfanya azidi kutema damu na kuishiwa nguvu, kisha alimuacha akiwa anahema juu juu kama Mgonjwa wa presha, aliokota jiwe zito ili amshindilie Faudhia lakini alisita kufanya hivyo kisha akamwambia
“Nakuacha ufe taratibu” Chogo alilitupa jiwe hilo pembeni kisha aliokota mabegi mawili yenye pesa na kuanza kuyaburuza ili atoke nayo nje ya chemba. Japo Faudhia alikuwa katika hali mbaya sana lakini alifikiria kama jamaa huyo angeliondoka ndani ya Chemba hiyo ingekuwa kazi yote aliyoifanya ni sawa na bure tuu.
Alijivuta kwa kazi sana ili aokote AK47 ambayo ilikuwa kando yake, Chogo alikuwa akizidi kusepa huku akiikaribia ile kona ambayo kama atazama hapo basi Faudhia atamkosa Chogo na jinsi alivyo na hali mbaya asingeliweza kunyanyuka na kumfukuzia, alifanikiwa kuikota kisha aliiweka sawa, alihema kwa nguvu kisha alivuta hisia zake, akafyatua Risasi kuelekea kwa Chogo, alikuwa na hisia kali sana na kufanikiwa kumpiga Chogo kwenye kichwa, Chogo alienda Chini.
Hali ya Faudhia haikuwa nzuri alikuwa akivuja damu nyingi ndani ya Chemba hiyo yenye giza, aliona kama angeliendelea kubakia hapo basi angelikufa kwa kukosa hewa na kuvuja damu nyingi, Alijivuta kuelekea Benki ambayo ilikuwa na Askari na hakukuwa na taarifa yoyote kuwa kulikuwa na Askari wa siri wa kitengo aliyekuwa akifanya operesheni ndani ya Chemba hiyo, Askari walikuwa tayari wamefanikiwa kuona mahali walipopita akina Chogo yaani pale kwenye dali kabla ya kutokea kwenye chumba cha siri ambacho walichimba hiyo chemba.
Walianza kuhisi ujio wa Mtu kwenye Siling Board, Mkuu wa kitengo alitoa maelekezo wafyatue risasi, Ooooh!! Risasi zilifyetuliwa za kutosha hadi pale alipowaambia waache kufanya hivyo, ukimya ulitawala kwa sekunde kadhaa kisha waliona eneo hilo likibomoka, mwili wa Mtu ulianguka hadi chini ya Sakafu, ulikuwa ni mwili wa Faudhia.
Alikuwa akitema damu nyingi sana, muda huo huo aliingia Mzee Shayo, alipoangalia vizuri alimuona Faudhia, alimuona Msichana aliyemkuza kama Mtoto wake akiwa amelala chini ya sakafu akiwa anatokwa na damu nyingi huku akiwa na matundu mengi ya risasi
“Faudhiaaaaa!!!” Aliita Mzee Shayo kwa uchungu wa hali ya juu sana, alimkimbilia Faudhia
“Faudhia! Faudhia Mwanangu!! Huyu ni Askari wa kitengo na ndiye aliyekuwa akifanya operesheni hii kwa siri, mmeniulia mwanangu” Alilia Mzee Shayo wakati Faudhia akiwa anahema kwa shida sana, alifanikiwa kumuita Mzee Shayo
“Ba….baaaa” Aliita na kukata kauli yake, Faudhia alifia mikononi mwa Mzee Shayo, alilia sana Mzee Shayo, tena kwa Uchungu mkubwa sana.
“Nimekuponza Mwanangu!! Faudhiaaa, Faudhiaaaa”” alilia kwa Uchungu, Mwili wa Faudhia ulichukuliwa kupelekwa Hospitali kwa ajili ya Uchunguzi, Baadaye Mzee Shayo alitoa taarifa kwa makambi ya Jeshi kuwa Mabomu yaliyotegwa humo yaliweza kuzuiliwa, Jeshi lilitoka na kuhakikisha linakomboa Miji iliyokuwa chini ya Kundi la ESS.
BAADA YA WIKI MOJA.
Ndani ya Ndege ya Shirkika la Emirates, Mzee Shayo alikuwa anasafiri kuelekea mapunzikoni baada ya kumfyeka Mzee Shomari na kundi lake, mkononi alikuwa na picha ya Faudhia, aliibusu kisha aliiweka Mfukoni. Aliitoa simu moja ambayo aliichukua kutoka kwa Mzee Shomari, alitafakari jambo lililomshangaza sana.
Ndani ya simu ya gaidi Mzee Shomari kulikuwa na namba ya Rais wa Nchi, na namba hiyo ilionekana kuwasiliana na Mzee Shomari siku ya tukio tena kwa muda mrefu, aliwaza Rais alikuwa akiongea nini na Mzee huyo? Alivuta punzi kisha alisema
“Sitostaafu, nitahakikisha nagundua siri ambayo Rais anaificha” Aliiweka simu hiyo ndani ya Mfuko kisha aliendelea na safari yake ya kuelekea Brazil kupumzika.
MWISHO.
IFUATE RIWAYA YA AINA GANI? MAPENZI , UJASUSI , UCHAWI au MAISHA? COMMENTS ZIKIFIKA 100 Naachia Kesho MAPEMA SANA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
28 Comments
Uchawi
Mapenzi
Ujasusi
Mapenzi
Raisi alijua njama hii, Nani alimpa taarifa ya chemba ya kutunzia pesa benk kuu kuwa Ni Selina anajua?
Admin nijibu txt yangu whatsap
Ujasusi
Mapenzi
Mapenzi
Ujasusi
Uchawi kdg tuweweseke ucku
Ujasusi
ujasusi
Mapenzi
mapenzi
Mapenziii
Uchawi
Dah Faudhia kakufaaa
Mapenzi
Ujasusi! Ila io kama ingeendelea ingekuwa safi sana ili tujue siri baina ya Rais na Mzee Shomari.
Mapenzi
Mapenzi
UJASUSI IS ALWAYS THE BEST ASEEE….
BRING BACK 🔙 AGAIN LAKINI IWE MICH BETTER THAN THAT 🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
Lete kama hy mkuu
Sema kaka mkubwa anazingua katueka sana
Nimeumua kwa nin fauthia amefariki dahh
Daaah!! Kazi nzuri sana admin stay blessed, i love your work.
Ujasusii